Waliobanwa katika ajali wafariki

Waliobanwa katika ajali wafariki

Mkuu wa nchi alipokuwa anasoma matokeo ya sensa alitoa kauli kuwa Watanzania tumekuwa wengi mno!! Hii kauli ni ya kusikitisha sana. Kupunguza wingi wa watu sio kwa kuwaua au kutokuwasaidia pale wanapopatwa na majanga.
 
Mkuu machozi yamenitoka watu walivyokuwa wanarusha miguu na mikono kuashiria wako hai na mwingine sehemu ya uso inaonekana ila katikati kabanwa. Wakuu ni simanzi, sijui tunaelekea wapi kwa kushuhudia ndugu zetu wanakufa kwa kukosa huduma
 
Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi na awape nguvu na faraja wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu kwao~AMEN
 
Mwenyezi Mungu nisamehe kwa haya niyasemayo ni ubinadamu naomba niandike kama binadamu na kiumbe chako.

Mwenyezi Mungu nauliza hii serikali ya awamu hii imekuja kutufundisha nini au unatupitisha jangwani? hivi ni haki kuanzia afisa mtendaji wa eneo la tukio hadi mkuu wa mkoa @#$%^&*()_(*&^%$ zao hawakuona au kuambiwa watu wanateseka kwa zaidi ya masaaa 10 kwa maumivu wamekalisha ------ yao ofisini wanatumbua hela zetu na vingora mabarabarani kweli?????????????????

Hivi afisa usalama na kamanda wa mkoa MOD tafadhari hawa watu ni ------- nashindwa niandikeje nieleweke kwa hisia na maumivu niliyonayo kwa waliyowakuta wananchi wenzangu.

Jifikirie wewe hata ukibanwa na mlango maumivu yake then jiweke wewe ndo umebanwa na vyuma, mwenyezi Mungu kama unaweza naomba mafuriko yaanzie magogoni plz sir GOD inaumaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Hata kauli ya waziri wa mambo ya ndani jana sikuisikia YA kuwa HAWA MAJERUHI WAOPOLEWE HARAKA SANA!
 
Hii ndiyo hali halisi ya ccm haiwezi kubadilika! utapewa kofia kabla ya uchaguzi na baada ya hapo ????????????????
 
....hiyo ndo hali halisi ya Nchi yetu; haki ya kuishi kwa wananchi especially wa hali ya chini ni mwiko.
 
Hii imenisikitisha sana tena sana,ktk jambo lililoniuma ni hili,maana wale jama niliwaona jana wakiongea tena na nguvu zao na wala hawakuwa wadhoofu na nilitegemea kuwa wale si watu wa kufa,kwani kama waandishi wa habari waliwahi kufika eneo husika iweje vifaa vya uokozi vichelewe hadi watu wale kupoteza uhai.
Hapana,hii haikubaliki
 
Mi ccm inakimbilia kufungua kampuni za kifisadi Jitegemee huku raia tunakufa bila sababu
 
inaniuma kujikuta nachangia JF tuuuuuu.... bila mchango wowote wa kimatendo dhidi Majamaa kadhaa wa wanaoifaidi hii Nchi. It pains mazee!
 
Hii habari imenitoa machozi.
Poleni wafiwa wote.

*Bahati mbaya sana Tanzania kwa sasa hatuna serikali madhubuti wala Rais madhubuti bali tuna genge la Wahuni linaloitwa CCM likiongozwa na Mwendawazimu mmoja anaitwa Mkwele.
Kwa hali iliyopo huenda tukaendelea kushuhudia vifo hivi zaidi na Zaidi.

*Wito wangu kwa watanzania popote pale mlipo tuanze kuchukua hatua zifuatazo;
1/Kuwazomea na kuwadhihaki viongozi wote wa Serikali na CCM wanapojitokeza hadharani.

2/Kuhakikisha kuanzia SASA CCM na serikali yake vianze kujiandaa vinaondoka madarakani na hitimisho liwe 2015.
 
so sad
kwani mkoa hauna vifaa vya kuokoa majeruhi?
walikosa vifaa vya kukatia yale machuma?
kamanda wa polisi mkoa ana kazi gani au kusubiri maandamano na majambazi?
 
Mimi binafsi nafikiri umefika muda sisi Watanzania kuwa responsible na maisha yetu na mambo yanayotuhusu kwenye jamii zetu. Tunalalamika sana bila kupata suluhisho la Matatizo yanayotukabili katika maisha yetu ya kila siku.
Tumeweka ushabiki katika mambo ya Mipira...Big Brothers n.k na kusahahau mambo muhimu kwenye maisha yetu ya kila siku.

Asilimia 90 ya ajali zinazotokea na maafa hapa Tanzania zinatokana na UZEMBE uliopitiliza. Halafu sisi Watanzania tunabaki tukilalamika bila kuwa na mipango fasaha ya kutatua matatizo yetu.
Tusitegemee Serikali ikafanya kila kitu. Kwa sababu hao Viongozi/WanaSiasa wameshalewa na madaraka.

Tuacheni kulalamika Watanzania na tuchukue hatua madhubuti ili kujikomboa na haya MAJANGA.
Hii kazi ni yangu mimi...wewe na kila Mtanzania anayetaka mabadiliko na Maendeleo.
Tuache Ushabiki na lawama za kutupiana mipira. CHUKUA HATUA.

RIP MAREHEMU....POLENI SANA WAFIWA NA WATANZANIA WOTE MLIOGUSWA NA HILI JANGA.
 
ITV jana ilifanya kazi yake km chombo cha habari kwa kutoa taarifa ya kina iliyojaa simanzi ya hali ya juu kwa wale waliotazama watakiri kwa hili yani mpaka mtangazaji studio alionyesha sura ya masikitiko makubwa wahanga kwa sauti zenye majonzi ziliomba msaada kwa serekali yao sikivu kuwasaidia kuwaokoa kwenye mauti lakini masikini ya Mungu hakuna msaada wowote toka serekalini inauma sana,wangekuwa wageni weupe toka ngambo serekali ingefunga ofisi kwenda kunusuru maisha yao
 
hivi ni kweli wale aliowahi eneo la tukio walishindwa kuokoa?
 
Hakuna kitu kilichonitia huzuni kama kifo cha hawa wenzetu watu wamekoswa msaada kwa zaidi ya saa16 nchi hii tunakwenda wapi?,hivi kweli wangesikia chadema wanamaandamano eneo lili ingeliwachukua sekunde ngapi kufika pale?
 
Hivi kweli kuna mtu bado anafikiria kuwa tuna serikali? Yaani inauma balaa bandugu.
 
Mimi naamini watanzania wengi hatufi kwa mapenzi ya mungu bali ni kwauzembe wa watuwachache

ila kama ingesikika kunamaandamano ya chadema vifaa vya kutuliza maandamano vingekuja on spot

r.i.p watanzania wenzangu#
 
Back
Top Bottom