Jembe Ulaya
JF-Expert Member
- Oct 27, 2008
- 456
- 104
Waokoaji wako ikulu wanakunywa chai na mkulu.
Dah, katika hali kama ile kweli waandishi wa habari wamefika pale wakapiga picha na kuzirusha hewani, basi? Haki ya nani watz tumechoka, kuanzia rais hadi raia wa kawaida.
Tunawapigia kelele CCM na Kikwete kwenye hili wakati waandishi wa habari na raia wengine wa kawaida waliwahi kufika eneo la tukio. Wameshindwa kweli kufanya jitihada zozote kusaidia uokoaji? Kazi yao tu ilikuwa kupiga picha na kuwafanya tamasha katika vyombo vya habari hao vijana wawili wanavyogugumia kwa maumivu makali?
Ingekuwa nchi zingine raia wa kawaida waliowahi kufika eneo la tukio wangefanya maarifa yote kwa nguvu zao zote kuhakikisha wanafanya kitu pale. Suala la kulaumu serikali halisaidii chochote katika hali kama ile.
Unamwona kabisa mtu amebanwa kabisa kwenye vyuma we kazi yako ni kunyosha mikono na kuchukua picha tu? Kweli?
Serikali inaakisi raia wenyewe tulivyo. Mijamaa imefika pale imepiga picha na kuzipeleka studio, basi.
Tatizo tumekuwa mazuzu hadi kila kitu tunategemea serikali. Tungewa na ubinadamu hao watu tungewaokoa bila kusubiri serikali ilete vifaa vyake. Ila kwa sababu kila kinachotokea tunaona serikali ndio inahusika basi sishangai kuona hao watu wamekufa bila msaada. Nina uhakika huo muda wa masaa 16 yamepita malori na matrekta ambayo yangeweza kutoa msaada kwa kiasi kikubwa, ila uokoaji ni kazi ya serikali ndio maana tumewaacha wenzetu wafe na kukimbilia kulalamika huku Jf.
ITV jana ilifanya kazi yake km chombo cha habari kwa kutoa taarifa ya kina iliyojaa simanzi ya hali ya juu kwa wale waliotazama watakiri kwa hili yani mpaka mtangazaji studio alionyesha sura ya masikitiko makubwa wahanga kwa sauti zenye majonzi ziliomba msaada kwa serekali yao sikivu kuwasaidia kuwaokoa kwenye mauti lakini masikini ya Mungu hakuna msaada wowote toka serekalini inauma sana,wangekuwa wageni weupe toka ngambo serekali ingefunga ofisi kwenda kunusuru maisha yao