Mimi binafsi nafikiri umefika muda sisi Watanzania kuwa responsible na maisha yetu na mambo yanayotuhusu kwenye jamii zetu. Tunalalamika sana bila kupata suluhisho la Matatizo yanayotukabili katika maisha yetu ya kila siku.
Tumeweka ushabiki katika mambo ya Mipira...Big Brothers n.k na kusahahau mambo muhimu kwenye maisha yetu ya kila siku.
Asilimia 90 ya ajali zinazotokea na maafa hapa Tanzania zinatokana na UZEMBE uliopitiliza. Halafu sisi Watanzania tunabaki tukilalamika bila kuwa na mipango fasaha ya kutatua matatizo yetu.
Tusitegemee Serikali ikafanya kila kitu. Kwa sababu hao Viongozi/WanaSiasa wameshalewa na madaraka.
Tuacheni kulalamika Watanzania na tuchukue hatua madhubuti ili kujikomboa na haya MAJANGA.
Hii kazi ni yangu mimi...wewe na kila Mtanzania anayetaka mabadiliko na Maendeleo.
Tuache Ushabiki na lawama za kutupiana mipira. CHUKUA HATUA.
RIP MAREHEMU....POLENI SANA WAFIWA NA WATANZANIA WOTE MLIOGUSWA NA HILI JANGA.
kama walikua wamebaniwa kwenye cabin ,si kwamba kilitakiwa kifaa cha kukatia vyuma ili kuwanasua na si crane?.Hapo akwenye blue,
Tuchukue hatua gani ??
Tununue crane kubwa ili zikae standby ??
Maana katika tukio lile, ilihitajika crane ya kunyanyua magari mazito ili kunusuru maisha ya watu wale.
Crane iliyohitajika ni kama hii hapa kwenye picha...
![]()
msimu wa maembe ukifika vichaa wanakuwa wengi kwahiyo ukikutana na simba porini utakimbia kujioka au utasubiri mpaka askari game aje kukuokoa sasa hao wapigapicha walipatawapi vifaa vya kupigia picha wakashindwa kutafuta njia ya kuwasaidia hilo eneo linawatu au ndio msimuwao kama kicha mirembe amechorewa mlanga anasema anafunguo kilakitu tutasubiri serikali ata ukiingia chooni utasubiri serikali
Waandishi badala ya kusaidia uokoaji wanapiga picha tu.
Mkuu Elungata heshima mbele,Ufisadi nyuma. Nashukuru sana kwa kumjibu Huyo mdau.kama walikua wamebaniwa kwenye cabin ,si kwamba kilitakiwa kifaa cha kukatia vyuma ili kuwanasua na si crane?.
Kama wangekua wameangukiwa na cabin au bodi ndo nadhani ingetakiwa crane.
Mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa husika waachie ngazi haraka sana kwa ujinga huu.
Mbona siwaoni akina Ritz & co kwenye huu uzi? Nawapa pole sana familia za wafiwa na watanzania kwa ujumla
Nenda kasubiri mkeo na wanao wabanwe ndipo utajua kati ya mimi na wewe na mjinga.
mwisho SERIKALI IMEJIPANGA TUKIO KAMA HILI HALITATOKEA TENA!Majibu ya kesho yatakuwa ni kama ifuatavyo:
Ndugu wananchi serikali ingependa kutoa tamko kuhusu ajali mbaya ya magari ya mzigo ambapo watu watatu walifariki, baada ya serikali kupata taarifa hizo utaratibu wa kuwakwamua majeruhi ulianza kufanyika mara moja. Serikali kupitia kitengo cha maafa chini ya ofisi ya waziri mkuu iliwasiliana na mkuu wa mkoa wa Pwani wakawa eneo la tukio muda wote wakijaribu kuwanasua majeruhi. Ndugu wananchi wakati mipango ya kuwanasua ikiendelea kufanyika mitambo mikubwa ilibainika kutakiwa kuwepo kutokana na ukubwa wa tatizo lenyewe, tuliwasiliana na makampuni makubwa ya ujenzi jijini Dar es Salaam ambao kulingana na taratibu zao mitambo hiyo lazima ipate vibali ili kuruhusiwa kutoka eneo la kazi, wakati huo ni takribani saa kumi na moja zilikuwa zimepita tangu tuanze kufanya harakati kuwa nasua majeruhi. Safari ya kwenda ilanza ambapo kutokana na ukubwa wa mitambo uharaka wa kuwasili eneo latukio iliweza kuchelewa na kuweza kusababisha vifo hivyo.
Hii ndiyo itakuwa ni maneno yako kujinasua na kadhia hii ya serikali yetu kujali watu wake kulingana na NAFASI ZAO. SERIKALI INAYOBAGUA WANANCHI WAKE NI SAWA NA NYUMBA ILIYOGAWANYIKA YENYEWE KWA YENYEWE NA HAIWEZI KUSIMAMA KAMWE.
na bado watanganyika nagombania mipaka, mnataka watu zaidi mpate kuwatesa. Leo malawi kesho zanzibar halafu mlima kilimanjaro ili mradi shida tuinauma sana kaka! Utaskia imesababishwa na chadema,ngoja tusubiri.
yaani katika mambo yalioniaribia siku ni taarifa ya habari ya ITV kuhusu majeruhi waliobanwa na lori.sijui hii ni serikali ya namna gani,watu wanakufa wanajiona kabisa kisa hakuna vyombo vya kuwaokoa!!! Mpaka saiv ile picha bado inanijia kichwani jinsi walivyokuwa kwenye mavyuma huku wakiomba msaada.pumzikeni kwa amani ndugu zangu!
wewe hapo kwenye red