N-handsome
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,453
- 561
Watanzania wote our middle name has been Majanga kasoro wateule wachache
Dah, katika hali kama ile kweli waandishi wa habari wamefika pale wakapiga picha na kuzirusha hewani, basi? Haki ya nani watz tumechoka, kuanzia rais hadi raia wa kawaida.
Tunawapigia kelele CCM na Kikwete kwenye hili wakati waandishi wa habari na raia wengine wa kawaida waliwahi kufika eneo la tukio. Wameshindwa kweli kufanya jitihada zozote kusaidia uokoaji? Kazi yao tu ilikuwa kupiga picha na kuwafanya tamasha katika vyombo vya habari hao vijana wawili wanavyogugumia kwa maumivu makali?
Ingekuwa nchi zingine raia wa kawaida waliowahi kufika eneo la tukio wangefanya maarifa yote kwa nguvu zao zote kuhakikisha wanafanya kitu pale. Suala la kulaumu serikali halisaidii chochote katika hali kama ile.
Unamwona kabisa mtu amebanwa kabisa kwenye vyuma we kazi yako ni kunyosha mikono na kuchukua picha tu? Kweli?
Serikali inaakisi raia wenyewe tulivyo. Mijamaa imefika pale imepiga picha na kuzipeleka studio, basi.
JAMANI nimebaki najiuliza:- hivi ajali si janga la kila mtu?? sasa hapo ajali ilikotokea wenye kijiji walikuwa wapi? je serikali ya kijiji nayo ilikuwa wapi? wako wapi madiwani wa CCM, CHADEMA, CUF nk. au pale hakuna mpiga kura wa chama chochote, je makanisa na misikiti haikuwepo?? alikuwa wapi mkuu wa wilaya, na hao usalama wa taifa cheni yao inaishia wapi? walikuwa wapi wote hawa masaa kumi na sita? je wakereketwa watakaokuja kutuomba kura 2015 walishindwa kuzuia njia ili magari yote yasimame kuongezea sauti? je wajenzi walikuwa wapi ili watumie misumeno kutoboa bodi ya hiyo gari? je ndani kungekuwa na bilioni moja isingetolewa? watanzania sisi ni wanafiki wa kutupwa najuta kuzaliwa humu!! kama akili yetu ni kuihoji serikali hata pale penye janga kiai kwamba hatuwezi kujiongeza wenyewe...najuta kuzaliwa humu!!!Tatizo tumekuwa mazuzu hadi kila kitu tunategemea serikali. Tungewa na ubinadamu hao watu tungewaokoa bila kusubiri serikali ilete vifaa vyake. Ila kwa sababu kila kinachotokea tunaona serikali ndio inahusika basi sishangai kuona hao watu wamekufa bila msaada. Nina uhakika huo muda wa masaa 16 yamepita malori na matrekta ambayo yangeweza kutoa msaada kwa kiasi kikubwa, ila uokoaji ni kazi ya serikali ndio maana tumewaacha wenzetu wafe na kukimbilia kulalamika huku Jf.
Ritz,ZeMarcopolo,Mwigulu,Nape, LukoloPasco, Utaifa kwanza, Sumu, Tandale one,Mguu wa chembe etc
hao raia unaowalaumu walijitaidi kwa kadri ya uwezo wao wakamchomoa mmoja pia usiwafananishe raia wa tz na wa ulaya kule ulaya vifaa ni vingi sana na watu wana uwezo wa kuvi-operate hapa serikali haikwepi lawama wao ndo wanavifaa tunawalipa kodi kama mtanzania anaishi kwa mlo mmoja kweli ataweza kumiliki crane?pia usilaumu waandishi wamejitaidi kuonyesha matatizo ya ss maskini tusivyo dhaminiwa na hao waliokutuma uwatetee humu,ndugu yangu tafakari kabla ya kupost pia epuka kutumiwa kama ile mipira yetu ya wakubwa