Walimu wengi wa ndoa ni wachonganishi wa familia: Pesa zote zinapaswa kusalimishwa kwa Mume kichwa cha familia

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,699
15,655
Mwanaume ameaminiwa na Mungu na kuwekwa kuwa kichwa cha familia.
Kichwa ndio Injini ndio ubongo wa familia. Kwa mtazamo huu Rasilimali na vipato vyote vya familia vinapaswa kuwasilishwa kwa kichwa mara tu vinapopatikana.

Mwanamke hata uwe CEO wa Google(kampuni inayoongoza kwa kulipa mishahara minono duniani) na mme wako ni mishenTown au Dalali unapaswa kusalimisha mishahara, malipulupu, Per Diem etc kwa mumeo ili apange maendeleo ya familia kwa kutumia ukichwa wake.

Shetani ili kufuta ndoa anatumia waseminishaji kuhimiza wanawake wamiliki fedha nyingi, huku wakiponda wanaume kutokupwa na pesa au kuwa nazo chache. Wanatumiwa kuwazodoa wanaume bila kujali chanzo cha ukosefu wa pesa na harakati za mwanaume huyo ambazo bado hazijatoboa.


Kabla ya semina hizi kushamiri makanisani (maana zamani hazikuwepo), zilianza kutanguliwa na jamii kumkuza mtoto wa kike na kumfungulia fursa nyingi kwa mgongo wa kumtetea asinyanyasike. Hilo zoezi limepelekea mtoto wa kiume kutelekezwa. Leo hata ukienda interview mwanamke akilingana na wanaume wawili atapata hiyo kazi sio kwa sababu ya uwezo bali uanamke wake.

Jamii inaandaliwa vurugu zisizo za lazima. Mke mwema aliyeelezewa Mithali 31, ni mchapakazi anatafuta hadi mishahara ya mabekitatu wake, nguo za watoto lakini yeye ndio chanzo cha mwanaume wake kuheshimiwa mtaani. Maana yake anamfanya aonekane yuko vizuri na provider hata kama yuko kipindi cha mpito wa kiuchumi. Wanachohamasisha watu wa kisasa kinavunja hii kanuni na badala yake wanahamasisha umalaya na uvunjwaji ndoa kisirisiri.

Huu uanamke unaotengenezwa sasa kupitia mimbari, harakati za kimagharibi na wasemaji na washauri wa ndio ni bomu jipya ambalo litagharimu familia zijazo.


Ni hayo tu...
Nini maoni yako.
 
Mwanaume ukifeli kwenye majukumu yako ya msingi tegemea lolote likupate, na huna haki yoyote.

Akikustahi sema Alhamdulillah ila akiifuata asili yake akapita na zote sema pia Inshallah.

Hakuna haki bila wajibu.
 
Ngoja nikwambie ndugu yangu. Wanaume mmeharibiana wenyewe kwa wenyewe. Wenzenu washenzi (laanakum), walinyanyasa na wanaendelea kunyanyasa wake zao (na watoto) financially na kupelekea movement ya sisi wanawake kujilimbikizia pesa.

Huko nyuma wanawake wengi hawakuwa wachoyo wala wabinafsi.
 
Back
Top Bottom