Ahukumiwa kunyongwa kwa kuua watu saba wa familia moja

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Mahakama Kuu kanda ya Kigoma imemuhukumu Mkazi wa Mlole, Kigoma Ujiji Peter Moris Mwandelema (34) kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya Watu saba wa familia moja. ( sita usiku mmoja na mmoja alifariki baadae )

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Kigoma Agostine Rwizile amesema Mahakama imefanya maamuzi hayo kwa kuzingatia kifungu cha 26 kifungu kidogo cha kwanza cha kanuni ya adhabu ya mashitaka ambapo imekubaliana na maelezo ya Mashahidi baada ya kupima mnyonyoro wa vielelezo na vipimo vya sampuli za vinasaba vya damu zilizokutwa katika nguo za mshitakiwa pamoja na panga lilotumika katika mauaji.

Jaji Rwizile pia amsema Mahakama imejiridhisha kuwa maelezo ya ungamo yaliyotolewa na upande wa mashitaka ni sahihi na kwamba Mshitakiwa alikiri kutenda kosa kwa Mlinzi wa amani katika Kata lilipotokea tukio hilo na vilevile Mahakama imejiridhisha kuwa simu aliyokutwa nayo Mshitakiwa baada ya kukamatwa ni mali ya mmoja wa Marehemu hao ambayo aliondoka nayo baada ya mauaji.

Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa Peter Moris Mwandelema alitenda kosa hilo Julai 03, 2022 kwa kuwauwa Tilifera Toyi (70), Januari Mussa (34) Sara Dunia (28) ,Joel Mussa (40), Christina Lazaro (9) James Joel (7) na Mtoto mchanga wa miezi mitatu James January ambaye alifia Morogoro akipelekwa Dar es salaam kwa matibabu.

Mwandishi wetu wa Kigoma amesema ilielezwa siku za awali kuwa chanzo cha Peter kufanya mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya kugundua Mmoja wa Wanaume wa familia hiyo ana uhusiano wa kimapenzi na Mwanamke wake ambapo siku ya tukio wakati anatekeleza mauaji ya Mwanaume huo alilazimika kuua Watu wengine waliobaki ili kupoteza ushahidi baada ya kuamka na kuanza kupiga kelele huku wengine wakiwa wamemgundua.

Source - AyoTv
 
Ukatili wa namna hiyo siyo mrundi kweli huyo?

Cha kujiuliza alitembezaje mapanga kikomando namna hiyo bila ya wahanga vijana kuweza kujitetea?
 
Lipumbavu kweli lililojaa laana. Kupoteza ushahidi ndo linashambulia hadi mtoto wamiezi mitatu!

Huyo anyongwe hadharani, na utekelezaji wa hukumu usicheleweshwe
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kila nikisema tuanze kutekeleza hukumu ya kunyonga hadi kufa sijui huwa naonekana katili?
 
ACHA hasira mkuu,bado mshtakiwa ana haki ya kukata rufaa Kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 na marekebisho yake.
Hii kauli yako inakua ni tamu sana kama wwe siyo victim, ila ukiwa Victim au ni ndg yako ndiyo katendewa huo uhalifu,hii kauli yako inaonekana ni ya kijing sana!!
 
Hii habari naikumbuka yaani kama jana tu
 
Back
Top Bottom