Wale 'Team Mungu Mtu Chama' niambieni leo amecheza nini dhidi ya Coastal Union FC kwa Mkapa?

Najua Kocha Mgunda ni Muoga na aliogopa Lawama Kumtoa ila kama kuna Wachezaji ambao leo wamecheza hovyo / vibaya na najua Kocha wangu Mkuu, Fundi na Mtaalam Roberto Olivieira angekuwepo angewatoa hata dakika ya 15 tu ya Mchezo walikuwa ni Clatous Chama na Pape Ousmane Sakho.

Ni mpaka uujue vyema Mpira na mtizamo wako kuhusu Soka uwe ni wa Kiwango Kikubwa, Umewahi Kuucheza na ni Mfuatiliaji hasa ndipo Utanielewa na Utakubaliana nami GENTAMYCINE kuwa Clatous Chama kwa Mpira wa sasa hafai na hapati Namba labda tu aonewe Huruma na Kocha.

Uchezaji wa Chama una umuhimu pale tu Timu ikiwa imeshapata Matokeo yake na inahitaji sasa Kuyalinda ndipo Umuhimu wake Chama utaonekana ili kupoteza muda.

Na leo nairudia tena hii Kauli kuwa namuomba sana Mwenyezi Mungu huko mbeleni katika CAFCL Simba SC yetu ikutane na Klabu ya Mamelodi Sundowns ambapo ninavyowapenda walivyo na Mpira wa Kasi na Nguvu muda Wote huyu Mungu Mtu Wenu Clatous Chama akipangwa mtakataa Wenyewe na ninavyowajua msivyo na Uvumilivu kama hiyo Mechi tutafungwa mtamtukana Matusi yote yaliyoko duniani na hata Chupa za Mikojo mtamrushia.

Nikimkosoa Mtu huwa namaanisha!!!
Umeongea kweli aisee!!! Ila wachache wanaoujua mpira ndio watakuelewa
 
Hapa unataka kuaminisha jamii mtazamo wako dhidi ya kocha robetinho ila tambua Kila timu lazima iwe key player iwe ameamka vzr au vibaya uwepo wake tu ni ushindi tosha, chama atabaki km alivyo na aina ya uchezaji wake ni taratibu ila aina ya pasi zake na upunguzaji wake presha uwanjan ndio muhimu zaidi,
 
Kuleta makocha katikati mwa musimu wa ligi athari zake ndizo hizi. Tusimlaumu Chama peke yake . Angalia timu nzima walivyocheza . Ni utumbo mtupu

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom