Wale 'Team Mungu Mtu Chama' niambieni leo amecheza nini dhidi ya Coastal Union FC kwa Mkapa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,052
107,530
Najua Kocha Mgunda ni Muoga na aliogopa Lawama Kumtoa ila kama kuna Wachezaji ambao leo wamecheza hovyo / vibaya na najua Kocha wangu Mkuu, Fundi na Mtaalam Roberto Olivieira angekuwepo angewatoa hata dakika ya 15 tu ya Mchezo walikuwa ni Clatous Chama na Pape Ousmane Sakho.

Ni mpaka uujue vyema Mpira na mtizamo wako kuhusu Soka uwe ni wa Kiwango Kikubwa, Umewahi Kuucheza na ni Mfuatiliaji hasa ndipo Utanielewa na Utakubaliana nami GENTAMYCINE kuwa Clatous Chama kwa Mpira wa sasa hafai na hapati Namba labda tu aonewe Huruma na Kocha.

Uchezaji wa Chama una umuhimu pale tu Timu ikiwa imeshapata Matokeo yake na inahitaji sasa Kuyalinda ndipo Umuhimu wake Chama utaonekana ili kupoteza muda.

Na leo nairudia tena hii Kauli kuwa namuomba sana Mwenyezi Mungu huko mbeleni katika CAFCL Simba SC yetu ikutane na Klabu ya Mamelodi Sundowns ambapo ninavyowapenda walivyo na Mpira wa Kasi na Nguvu muda Wote huyu Mungu Mtu Wenu Clatous Chama akipangwa mtakataa Wenyewe na ninavyowajua msivyo na Uvumilivu kama hiyo Mechi tutafungwa mtamtukana Matusi yote yaliyoko duniani na hata Chupa za Mikojo mtamrushia.

Nikimkosoa Mtu huwa namaanisha!!!
 
Leo mechi ya tatu sasa simba inacheza mpira mbaya sana japo tunapata matokeo
Performance ya mechi ya leo na za hivi karibuni inafikirisha sana. Inawezekana wachezaji hawalali masaa ya kutosha. Leo wachezaji wengi walikuwa wanashindwa kabisa hata kutuliza mpira tu hasa kuanzia katikati kwenda mbele, back passes zimerudi, hawakabi, wanatembea tu uwanjani.
 
Haya kusanya hao utopolo hapo juu mjipigie makofi chama kacheza chini ya kiwango umeingiza pesa ngapi?
 
Ninachojua ni kuwa Chama anampira wa taratibu sana na hana mbio ila ana akili na utulivu mkubwa sana wa mpira na muda wowote anakupa matokeo yeye binafsi au anasababisha timu ipate matokeo na ameshafanya hivyo mara kadhaa wala hili halina ubishi. Mafundi wa mpira kama Zidane, Pilo,Ronaldo Delima, Ronaldinho, Xavi wala hawakuwa na mbio kama za Mpape.

Mchezaji kama Kibu au Sakho ni wachezaji wenye kasi sana na papara muda mwingi hawana utulivu hivyo kutokuwa na impact kubwa uwanjani mda mwingi ni kukumbia kumbia na mpira bila sababu.

Binafsi mimi nimeshuhudia mechi nyingi za Simba kama Chama hayupo tumekuwa tukipata ushindi kwa tabu sana na mpira tunaocheza huwa ni wabutua butua. Kifupi Simba mbadala wa Chama kwa sasa hayupo, hata kama kuna siku atacheza chini ya kiwango mashabiki sio wajinga wampende mchezaji bila sababu kwani kawapa rushwa?
 
Mgunda anasema wanatumia Falsa ya Robertinho.
Labda ndio maana.
Utakuwa ni ukweli maana kabla ya ujio wa huyu kocha Simba ilikuwa inasakata kabumbu safi Boko na Saidoo walikuwa moto wa kuotea mbali sasa hivi wamefifia.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom