Rais Magufuli, tutafutie mtu wa “Kumfufua Ruge” ili Tanzania ya viwanda iwe realized kwa haraka

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
Rugemalira Mutahaba ameaga dunia wiki jana huko “bondeni”. Ruge ali maarufu kama boss Ruge wa staff ya clouds media na watu wengine ambao hawakuwa waajiriwa wa Clouds media.

Ruge alikuwa sort of ex-officio cabinet minister kwa maana alikuwa na access na mkuu wa kaya wa sasa hata yule ambae kwa sasa yuko mapumzikoni Msoga.

Jana waziri wa Uwezeshaji Angela Kairuki kasikika kama mkuu wa Wizara ambae anamhitaji Ruge. Kuna unaccomplished jobs kati ya wizara yake mpya na Ruge.

RC wa Kagera Bridg. Gen. Gaguti amekuwa wazi kama tu anaemhitaji Ruge. Kuna mambo ya kuyafanya Kagera yamesimama kwa kuwa Ruge alikuwa mgonjwa. Sasa kaondoka kabla hawa-accomplish what he promised to do.

RC wa Mbeya ana yake, Waziri Kigwangala nae ana yake… the list goes on. Naomba nisigusie mambo ya mtu mmoja mmoja au makampuni naomba kwa leo nijikite kwa “wakubwa” ambao wana hadhi kubwa sana kwa kutmbea na magari ya bendera wanalilia Ruge kwanini kaondoka na sasa itakuwaje in his absence.

Ndiyo maana namwomba Mhe. JPM kama vile alivyoamua kwa moyo wa upendo na ubanadamu kwenda kutoa salam zake za mwisho pale Karimjee hall na kuacha shughuli chungu mzima katika desk lako, fanyafanya mambo tumfufue Ruge.

Aidha Mhe. JPM kwa kutoa ndege ya serikali kumpeleka Rugen a kumwagiza Waziri Angela Kairuki kutoa salam za serikali, ni namna gani Ruge alikuwa Mtanzania wenye vipaji vingi kwa kugusa watu mmoja mmoja, amegusa corporate world, amegusa jamii wa wanahabari, wasanii wa muziki na filamu; kila mahali Ruge Ruge Boss Ruge, aka Muzilankende.

Angekuwepo leo Yesu wa Nazareth, tungemwomba atende muujiza kama wa kumfufua Lazaro au mtoto wa kiume wa alikuwa mjane katika mji wa Nain.

Kwa kuwa Yesu hayupo kwa jinsi ya mwili na kuwa kuwa hata kama angekuwepo, ingekuwa ni discretion yake ya kutenda muujiza, bila shaka tunaweza kwenda kwenye 2nd Alternative namna gani maisha Tanzania yasonge mbele in the absence of Ruge.

Ruge alikuwa visionary na strategic leader. Amezikuta Radio nyingi Tanzania kubwa kama RTD (na sasa TBC), Radio One/ITV na Radio Free Africa ila kwa muda wa miaka 19 amepindua meza kibabe na kuwafanya Watanzania wengi kuvutiwa na Powerbreakfast; Jahazi na Clouds 360 nikitaja kwa uchache vipindi ambavyo hoja zikijadiliwa haitachukuchua muda Mawaziri na wakurugenzi kukimbia kutoa majibu au kipiga simu kama sio kwenda kabisa na kuzungumza na Watanzania. Ruge kupitia Clouds media imeibua mambo muhimu ya kijamii ambayo yamegusa vijana na wanawake kama fursa, kipepeo na malkia wa nguvu. Burudani na muziki naomba leo nisiusemee.

Nini kimemfanya wakubwa wengi wamhitaji Ruge. Ruge awe lulu kwa kuwa ana anatengeneza sustainable competitive advantage hasa kwa jamii ya vijana na wanawake hata kwa corporates.

Kuna mambo machache ambayo ntaainisha ambayo alikuwa nayo Ruge na sasa tunamhitaji afufuke ili yatimie kwa viporo ambayo kaviacha na mengine ambayo anatakiwa kuyaleta

Ruge alijua Watanzania hasa vijana wanawake na corporate world inataka nini na alikusudia kuijulisha hiyo audience yake ina potentials gani based on opportunities available in Tanzanian settings na competitive environment ya Tanzania ili tuweze ku-thrive.

Ruge kawasaidia Watanzania kujitambua who we are and where we want to go. Amekuwa na mchango wa kuhamsisha kuipenda Tanzania na ku-grab nini Watanzania wafanye katika mikoa yao kama Dodoma as our current capital city. Nini kifanyike Tanga kwenye bomba la mafuta. Ruge amekuwa msaada kwenye kuweka mikakati ya kuvutia Utalii Tanzania. Dr. Kigwangala, ameweka wazi mchango wake katika Unfogetable Tanzania Safari.

Ruge kamsaidia Mkuu wa DAWASCO Eng. Luhemeja on how to get more custmers by taking competitive advantage ya watu wanaohitaji maji Dar. Alimpa ushauri wa kibiashara wa kuwafungiwa maji wateja wapya bure na akawasaidia ku-formulate critical revenue collection strategy kwa kuwakata wateja in 12 months ile connection fee katika bill za maji. Akapata wateja wengi.

Ruge amenza kazi na Kusaga wakati Radio ikiwa unknown. Ameanza safari na wasanii wakiwa unknown. He Made their journey by translating the strategy into action kwa kutambua watu au taasisi zina uwezo gani na kuja na implementing tactics. Mengi yamefanikiwa vs machache yaliyo-fail.

Kingine, Ruge alijifunza ku-check progress ya taasisi ailiyoisimamia kama (Director of Programmes & Production) na aliendelea kuwa na tathmini ya mara kwa mara ili kuongeza effectiveness & efficiency.

Wengi wa Watanzania mmoja mmoja, jamii ya vijana na akina mama, hali kadhalika wakubwa kama Ma-RC na Mawaziri ambao Ruge kawasaidia, bila shaka wanapungukiwa na yafuatayo:

Focus: Baadhi ya Tasisi za serikali na binafsi zimekuwa hazina uongozi wenye focus na kuna baadi yao wanashindwa kuwatumia watu wao. Kwa kushindwa huko Ruge alikuwa msaada mkubwa katika “amsha amsha”.

Tactics: kama kocha wa mpira, baadhi ya watu, viongozi na idara za umma na binafsi zimekuwa na kupungukiwa na mbinu ambazo zina-aligne na Tananiania strategy kwenda kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda. Ruge alijikita katika Burundani ya muziki kama moja ya kiwanda cha kuzalisha mapato wa wanamuziki, kuwa na uhakika wa ajira endelevu. Kupitia hapo kodi ya serikali imepatikana. Aidha baadhi ya wasanii wakawa na akili yak u-diversify biashara na baadhia yao kuingia katika biashara ya vipodozi nia mitindo.

Limited range: Baadhi ya viongozi hawajui kuona mbali kwa kutengeneza short-term goals ambazo zitazaa long-term viable social investment, human capital investment anu uwekezaji wowote ule wa kibiashara. Watu wengi hasa viongozi, ni waoga wa Risk. Mtu kama Director Kipilimba anaweza kuwa na msada wa kuisadia taasisi za umma na kibiashara Tanzania isiogope risk ambazo zinaweza kuwa insured. Ikumbukwe, aliwahi kuwa Director wa risk management, The best way to mitigate risk is to know that there is a potential it can occur, so insurance cover inasidia compensation when risk becomes real.

Nini kifanyike. Tutengeneza akina Ruge wengi ambao kwa haraka sana watasambaa na kuendeleza “habari njema” ambazo Ruge alisimama na kuzihubiri. Iko haja kufanya quick indentification ya Watu ambao wapo na Serikali ifanye nao kazi ili mambo yaendelee. Otherwise watu watanendelea kumlilia na baada ya muda tutaanza kurudi nyuma badala ya kuendelea na momentum ya kuijenga Tanzania ya viwanda na kukuza uchumi wa kati kwa Watanzania wengi.

Ni kweli Ruge imeondoka. (The creative brain and innovative brain imeondoka) Tukisubiri such a daring and exposed individual to surface, huenda ikachukua muda mrefu sana Tanzania kumpata. Ruge amekuwa na competitive advantage ya kuwa na exposure ya makuzi ya wazazi wenye uelewa mkubwa na kasoma shule za ndani na nje ya Tanzania. Ukichanganya na personality yake, Ruge alikuwa MULTiTASKING PERSON.

Sasa basi, ili kuwapata akina “Ruge” wengi ku-fill the gap ya kuwapata vijana ambao watakuwa na akili za kuifadisha public sector, media, vijana kuwasaidia kuziona fursa na kuwasaidia kuibua ubunifu (creativity and innovation); tutate say a public forum ambapo watu hao wanaweza kuwa indentified. Huenda ndani ya session 3 mpaka 4 wakapatika right people to take lead. Uzoefu hasa kwa walimu, ni rahisi kumtambua akiwa mbele ya public.

Kwanini initiatives za makusudi zifanyike. Naomba kutoa mifano miwili ambayo inaweza isiwe na relevance, japo yaweza kuwa na uzito wa hoja yangu .

Rais Kikwete aliunda Tume ya kutafuta maoni ya katiba mpya wakati wa muhula wake wa pili. Tume hiyo ndiyo ilimuibua Humphrey Polepole. Ilitokea ndiyo alikuwa kijana mwenye umri mdogo, ila tokea hapo akajiongeza na leo hii kasogea kimajukumu mpaka kuaminiwa na Chama cha Mapinduzi kama Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM – Itikadi na Uenezi. Bila shaka bila ile tume ingekuwa kazi kumuibua mtu aina ya Polepole.

Kashfa ya kuchunguza UFISADI WA RICHMOND. Huu ndio wakati ambao ulimuibua Dr. Harrisaon George Mwaknyembe. Kuna wengi walikuwepo katika ila tume, ila mtu alie-ng’ara sana, ni Dr. Mwakyembe.

Ruge amekuwa ni kama Ex-officio senior government officer akiwa katika front pages za magazeti na a lot being spoken in social media and his death has come like ceremony of a “big shot” from government circles. What made him arrive there, his brain.

Mwisho nampongeza sana,tena sana Joe Kusaga. Joe amekuwa MD & CEO mzuri sana. Hakuwa na sense of insecurity kama vile Ruge anamfunika pale Clouds Media. Maana it was known huku mtaani,kuwa Ruge ndiye kila kitu pale Clouds Media. Basically, kwa mtu mwenye moyo mdogo ingeleta mafigisu sana n a labda wangeweza kusambaratika. Instead Joe, alijua nafasi yake kama MD & CEO na alimwachia Ruge “ajiachie” kwa kubuni vitu na kuibua watu Clouds Media. Clouds Radio ilihama kutoka entertainment station mpaka kuwa radio yenye “serious session” zikichanganyikana na burudani.

Mfumo wa radio kuwa hewani ikiwa supported na soundtrack ni “mfumo mpya” akina Ruge waliuleta na baadae kila FM station ikaiga.

Pengine shukurani pia zimfikie Dr. Kimei (aliekuwa MD wa CRDB Bank) kwa kutambua vision ya Joe na Ruge. Kwa maelezo ya Joe wakati Clouds inatimkiza miaka 19 (mwaka jana); mzee Kimei aliamini katika vision ya akina Joe na Ruge akawakopesha TZS 40mil bila ya kuwa na known outstanding cashflow. It was a great risk business worth of taking. Sijui le hii tuna ma-MD katika private sector wenye capacity ya fursa ya biashara mpya ambayo haina known cashflow na wakaiamini. Leo Clouds media imekuwa na group of companies yenye assets za kutosha.

Ndiyo maana narejea tena kumwomba “Mkuu wa Kaya” afanye kitu ili kuzalisha Watanzania aina ya Ruge. Ukizingatia uzalendo na assets ya imputs ambazo zitaingia katika akili na fahamu za Watanzania kwa ujumla wake. Team hu itagusa vijana, wanawake, wanaume, wanasiasa, viongozi, wasomi, wananzuoni na wenye akili ya kawaida. Niko tayari kutoa mchango wangu katika “mismatch” ya yale ambayo nafahamu Ruge alifanya husan katika eneo la kuwajengea uwezo vijana na wadau wa vijana kwa kuzidadavua fursa za biashara; namna gani ya kuwa na sustainable productive model ambazo zinaweza kuzaa matokeo yanayotarajiwa. Kwa uchache namna gani ya kukuza uchumi, kuongeza fursa za ajira rasmi, kuongeza watu wanaoingia katika mifuko ya pensheni na bima ya afya. Kupanua wigo wa biashara wanaopata fedha za uhakika kupitia mauzo ya bidhaa ndani ya Tanzania na nje ya nchi.

Nahitimisha kwa kusema, Mwl. Nyerere alikuwa na vision kubwa ya kutaka kuwa na Tanganyika huru. Bila project financing ya akina Mzee John Rupia na akina Jamal bila shaka tungechelewa sana kupata uhuru.

JPM akiwa waziri wa Ujenzi alikuwa na vision ya kuanza kujenga barabara kupitia fedha za ndani. Waziri Mkuu Sumaye na baadhi ya cabinet members walimgomea. Very fortunate, Rais Mkapa aliamini katika vision ya JPM na akatoa agizo, proposal yake itekelezwe.

Bila shaka katika mchakato wa kuwaibua akina “New Ruges” mchakato huo uendene na financing their community transforming projects. Msingi tu, uwe ni the return on investment ikipimika ina more assets kwa Watanzania. Liabilities lazima zitakuwepo, maana hata Ruge alikuwa nazo, sema tu, tunaposheherekia msiba wake, tunajivunia assets za Ruge kuliko liabilities zake.

Mhe. Rais, ukifanya hivyo, utakuwa umetengeneza human assets (known to work for public interest) ambazo zitakusaidia kuwa sehemu ya ku-neutraize our common enemies which are poverty, ignorance and diseases. These known enemies are creating new threats locally by rogue Tanzanians, same threats are potentially being used by foreign enemies.

Kama ingetokea Ruge akawa entrusted na dhamana ya Wizara ya ajira kama mshauri mwelekezi au Waziri, bila shaka angefanya makubwa. Wizara hii ina all assets to leverage into greatness, siuji kama wanajua hilo, na kama hawajaona, iko haja hoo akina “New Ruge” wakasaidia ku-fill in the gas ili wizara hii ikue sana tu. Bila shaka UVCCM na Katibu wa Uchumi na Fedha CCM, mnawahitaji akina Ruge ili nanyi muwe sehemu ya kuingia katika viwanda kama namna ya kuongeza thamani ya bidhaa, kutoa ajira endelevu na kupanua wigo wa kodi kwa serikali.

Tunaomba kwa Mungu wa Mbiguni faraja yake iwe kwa familia ya Ruge, familia ya Clouds Media na Watanzania wote.
 
umenena vyema mkuu, lakini kumbuka hakuna kiongozi wa serikali hii atakaekubali Mawazo ya Ruge yatekelezwe, wanalia kinafiki... unaambiwa baada ya kuona ushawishi wa Ruge ni mkubwa kwa vijana likatafutwa zengwe ili aharibikiwe, wakaanza na kodi wakalamba garasa, wakasema! "that is too much power for one man to have"
 
THE LOST
Boss,
Bado naendelea kuamini report ya madaktari kuwa Ruge alikuwa na shida ya figo zake kushindwa kufanya kazi na sio ini. Ila suala la kupewa sumu sina hakika hata kidogo na hiyo school of thought. Ila kama inaweza kuwa imefanyika, basi hao waliofanya watakuwa watu ambao wako very shortsighted.
He had more assets to add values vs liabilities.
Kama kuna watu wanakuwa threatened na assets za Mtanzania mwenzetu, that is a disgrace.
 
Una mada nzuri hata kama ni ndefu ina mambo mazuri. Huo ushauri unaompa Magufuli sio mbaya pia, lakini akibeba hili wazo ni rahisi kuanzisha taasisi ambayo itajaza vijana wa ccm na wenye uwezo wa kujipendekeza zaidi. Kama ni hivyo ni bora aiwezeshe tu uvccm kuliko kuunda taasisi yenye funds za serikali lakini inayoongozwa kwa utashi wa kiccm. Usishangae hiyo taasisi ikaacha lengo lake wakatumika kama kikundi cha kudhuru wapinzani nyakati za uchaguzi.
 
Ruge alifanya kazi na wana-CCM, wana-CDM, ZZK na Watanzania.
Rai yangu kuchallenge status quo ya UVCCM na sio BAVICHA, ni kwa kuwa UVCCM wana assets za kutosha in term if human, land and property. Katika Tanzania ya viwanda inayolenga kukuza uchumi, kutengeneza ajira, kuongeza thamani ya assets za Kitaasisi, UVCCM wana chance unlike wengineo.
Na kama watafanikiwa kuthubutu na ku-make investment happen, watakuwa mfano bora wa utekelezaji kwa vitendo kwa kutafsiri Tanzania ya viwanda.
Japo vyama vingine pia vinaweza ku-adopt mfumo kama huo ambao bila shaka mwisho wa siku wafaidika wanakuwa Watanzania.

Adui wakubwa wa nchi hii ni umasikini, ujinga na maradhi. Ambao wanazaa adui wapya kama rushwa, kubaguana kwa misingi ya vyama.
Utanzania wetu ni mkubwa kuliko vyama vyetu, au tofauti yoyote ile.
Bendera ya Tanzania itaendelea kupepea .
 
Ruge mlitafutiwa na Magufuli? Kuna watu mtaja mwomba Magufuli awafanyie mambo ambayo hayaandikiki kwa sababu tu ya ushabiki wenu uliopita kiasi.
 
mbona hujaweka namba ya simu?
Akina Ruge hawatengenezwi na serikali moja kwa moja kama unavyoshauri. Bali serikali ikijenga mazingira ya kukua kwa demokrasia, fikira mbadala na uhuru wa kujieleza, vipaji hivyo vinaibuka na kukua naturally. Serikali inayozuia kuibuka kwa fikira mbadala, hudumaza vipaji na ubunifu kwa vijana. Matokeo yake vijana husubiri mtukufu atoe tamko (kwa sababu ndiye ana haki ya kufikiri kwa niaba ya wengine wote) ili wapige makofi, na wanashindana kupiga makofi na kuonekana wanapiga makofi ili wapewe upendeleo wa kuteuliwa.
 
Hizi Sifa Za Ruge Ndio Tunazisikia Sasa Baada Ya Kufa.. Kipindi Yuko Hai Kitu Tulichokuwa Tunasikia Ni Malalamiko Ya Wasanii Kuhusu Kunyonywa Na Ruge Kimaslah Mpaka Ruge Kupiga Marufuku Nyimbo Zao Kupigwa Clouds! Ruge Alikuwa Mfanyabiashara Na Chochote Alichofanya Ni Kwa Masilah Yake
 
Wakina Ruge wapo wengi vijijini na mijini kwa mamilioni.
Shida ni mazingira yasio rafiki.
Ustawi wa jamii ndio jibu sahihi.
Bila hilo tutakuwa tunazidi kushangaashangaa
Wakati trend ni kuibua wajasilimali wengi kwa mamilioni,lakini serikali yenyewe inakuja na mfumo wa serikali kumiliki na kusimamia njia kuu,za kati na ndogo kiuchumi.

It seems we are reading different pages
 
Boss,
Ruge alifanya kazi na wana-CCM, wana-CDM, ZZK na Watanzania.
Rai yangu kuchallenge status quo ya UVCCM na sio BAVICHA, ni kwa kuwa UVCCM wana assets za kutosha in term if human, land and property. Katika Tanzania ya viwanda inayolenga kukuza uchumi, kutengeneza ajira, kuongeza thamani ya assets za Kitaasisi, UVCCM wana chance unlike wengineo.
Na kama watafanikiwa kuthubutu na ku-make investment happen, watakuwa mfano bora wa utekelezaji kwa vitendo kwa kutafsiri Tanzania ya viwanda.
Japo vyama vingine pia vinaweza ku-adopt mfumo kama huo ambao bila shaka mwisho wa siku wafaidika wanakuwa Watanzania.

Adui wakubwa wa nchi hii ni umasikini, ujinga na maradhi. Ambao wanazaa adui wapya kama rushwa, kubaguana kwa misingi ya vyama.
Utanzania wetu ni mkubwa kuliko vyama vyetu, au tofauti yoyote ile.
Bendera ya Tanzania itaendelea kupepea .

Hao uvccm kimewashinda nini mpaka sasa? Au walingoja mpaka ww uje na ushauri hapa jf ndio waanze?
 
mbona hujaweka namba ya simu?
Akina Ruge hawatengenezwi na serikali moja kwa moja kama unavyoshauri. Bali serikali ikijenga mazingira ya kukua kwa demokrasia, fikira mbadala na uhuru wa kujieleza, vipaji hivyo vinaibuka na kukua naturally. Serikali inayozuia kuibuka kwa fikira mbadala, hudumaza vipaji na ubunifu kwa vijana. Matokeo yake vijana husubiri mtukufu atoe tamko (kwa sababu ndiye ana haki ya kufikiri kwa niaba ya wengine wote) ili wapige makofi, na wanashindana kupiga makofi na kuonekana wanapiga makofi ili wapewe upendeleo wa kuteuliwa.
I stand to be corrected.
Ili ufanye shughuli yoyote ya kijamii, usajili unaupata Serikalini. Ikiwa Wizara ya mambo ya ndani, wizara ya afya, RITA au BRELA
Ili ufungue account kuendesha shughuli za kijamii, vibali vinapatikana katika taasisi za serikali. TIN TRA, tax clearance na Lincense katika Halmashauri uliyopo
Kama una Radio na TV lazima kupata kibali TCRA na wizara ya habari,
Ili kufanya forum za kukusanya watu hata kama ni kwa hela zako, lazima ku-liason na Mamlaka za Mikoa, Wilaya ikijumuisha wakuu wa mikoa, Police, ma-DC na Ma-DED wajue umekusudia kufanya nini na maudhui yako ni yapi.
Ili ufanikiwe huna budi kufanya kazi na Public Sector.

Kwanini Mkuu wa Kaya ni wa Muhimu sana. Sio rahisi kupata foreign donor kuunga mkono tutoke katika umasikini. Wengi wa wanaopata foreign funds, wengi ni watumwa wa fikra za hao watoa "mpunga"

Mkuu wa kaya ana hela, honestly, akipata right people waku-collaborate na vision yake, itamsaidia ku-speed up mchakato wa kubadili fikra na kuwezesha shughuli za uzalishaji.

Vinginevyo, unaweza kuwa kwenye struggle na hassles za kutosha kama public haina imani na unafanya nini na tija ya hicho unachofanya Public inafaidikaje...
 
Ruge kamgusa mkuu wa Kaya kwa sababu zao Hawa wengine wote Ni manafiq njaa yanafuata mikumbo tu hamna kitu ndani ya makichwa yao.
 
Boss,
Ruge alifanya kazi na wana-CCM, wana-CDM, ZZK na Watanzania.
Rai yangu kuchallenge status quo ya UVCCM na sio BAVICHA, ni kwa kuwa UVCCM wana assets za kutosha in term if human, land and property. Katika Tanzania ya viwanda inayolenga kukuza uchumi, kutengeneza ajira, kuongeza thamani ya assets za Kitaasisi, UVCCM wana chance unlike wengineo.
Na kama watafanikiwa kuthubutu na ku-make investment happen, watakuwa mfano bora wa utekelezaji kwa vitendo kwa kutafsiri Tanzania ya viwanda.
Japo vyama vingine pia vinaweza ku-adopt mfumo kama huo ambao bila shaka mwisho wa siku wafaidika wanakuwa Watanzania.

Adui wakubwa wa nchi hii ni umasikini, ujinga na maradhi. Ambao wanazaa adui wapya kama rushwa, kubaguana kwa misingi ya vyama.
Utanzania wetu ni mkubwa kuliko vyama vyetu, au tofauti yoyote ile.
Bendera ya Tanzania itaendelea kupepea .
Wambie ccm waache rushwa, ubaguzi na roho mbaya kwanza! Huyo Ruge alievamiwa ktk studio yao na shankupe rc makondakta mbn hatukuona wanaccm wakimlilia machozi badala yake waliothubutu kutimiza wajibu wao, akiwemo Nape Mnauye waliishia kudhalilishwa kwa bastola na kutoswa uwaziri. Nachukia sana unafiki!!!
 
Hizi Sifa Za Ruge Ndio Tunazisikia Sasa Baada Ya Kufa.. Kipindi Yuko Hai Kitu Tulichokuwa Tunasikia Ni Malalamiko Ya Wasanii Kuhusu Kunyonywa Na Ruge Kimaslah Mpaka Ruge Kupiga Marufuku Nyimbo Zao Kupigwa Clouds! Ruge Alikuwa Mfanyabiashara Na Chochote Alichofanya Ni Kwa Masilah Yake

Sijafuatilia sana tasnia ya muziki na wasanii kama kawapiga au kawainua.
Labda tujiulize, wakati Indians wakiwa middle men wa kazi za wasanii kuanzia movie mpaka muziki, ni wakati gani waasanii walifaidika ukilinganisha na alipoingia Ruge?
Nasikia huko nyuma matamasha makubwa ili kuyanogesha ilikuwa lazima kuwa na 'Wanyamwezi' au wa-Nigeria. Kijana alipiga kazi mpaka ikifikia matamasha yakawa 100% local. Kama angeiba, mbona local artists walizidi kukua?
Kama aliwaibia, ni kwa kukwapua mifukoni mwao au mikataba kama ya babu zetu akina Mangungo na Karl Peters au mikataba ya madini in exchange of 3% ya msamiati mpya wa mrahaba sijui mrabaha?

Cha msingi, kwa kuwa ashatangulia mbele ya haki na hana nafasi ya kujitetea, basi kama kuna jema moja ni busara kuli-celebrate.

So far, let's keep on focusing on how we can get rid of poverty and ignorance as our common arch threats in our communities
 
Rugemalira Mutahaba ameaga dunia wiki jana huko “bondeni”. Ruge ali maarufu kama boss Ruge wa staff ya clouds media na watu wengine ambao hawakuwa waajiriwa wa Clouds media.

Ruge alikuwa sort of ex-officio cabinet minister kwa maana alikuwa na access na mkuu wa kaya wa sasa hata yule ambae kwa sasa yuko mapumzikoni Msoga.

Jana waziri wa Uwezeshaji Angela Kairuki kasikika kama mkuu wa Wizara ambae anamhitaji Ruge. Kuna unaccomplished jobs kati ya wizara yake mpya na Ruge.

RC wa Kagera Bridg. Gen. Gaguti amekuwa wazi kama tu anaemhitaji Ruge. Kuna mambo ya kuyafanya Kagera yamesimama kwa kuwa Ruge alikuwa mgonjwa. Sasa kaondoka kabla hawa-accomplish what he promised to do.

RC wa Mbeya ana yake, Waziri Kigwangala nae ana yake… the list goes on. Naomba nisigusie mambo ya mtu mmoja mmoja au makampuni naomba kwa leo nijikite kwa “wakubwa” ambao wana hadhi kubwa sana kwa kutmbea na magari ya bendera wanalilia Ruge kwanini kaondoka na sasa itakuwaje in his absence.

Ndiyo maana namwomba Mhe. JPM kama vile alivyoamua kwa moyo wa upendo na ubanadamu kwenda kutoa salam zake za mwisho pale Karimjee hall na kuacha shughuli chungu mzima katika desk lako, fanyafanya mambo tumfufue Ruge.

Aidha Mhe. JPM kwa kutoa ndege ya serikali kumpeleka Rugen a kumwagiza Waziri Angela Kairuki kutoa salam za serikali, ni namna gani Ruge alikuwa Mtanzania wenye vipaji vingi kwa kugusa watu mmoja mmoja, amegusa corporate world, amegusa jamii wa wanahabari, wasanii wa muziki na filamu; kila mahali Ruge Ruge Boss Ruge, aka Muzilankende.

Angekuwepo leo Yesu wa Nazareth, tungemwomba atende muujiza kama wa kumfufua Lazaro au mtoto wa kiume wa alikuwa mjane katika mji wa Nain.

Kwa kuwa Yesu hayupo kwa jinsi ya mwili na kuwa kuwa hata kama angekuwepo, ingekuwa ni discretion yake ya kutenda muujiza, bila shaka tunaweza kwenda kwenye 2nd Alternative namna gani maisha Tanzania yasonge mbele in the absence of Ruge.

Ruge alikuwa visionary na strategic leader. Amezikuta Radio nyingi Tanzania kubwa kama RTD (na sasa TBC), Radio One/ITV na Radio Free Africa ila kwa muda wa miaka 19 amepindua meza kibabe na kuwafanya Watanzania wengi kuvutiwa na Powerbreakfast; Jahazi na Clouds 360 nikitaja kwa uchache vipindi ambavyo hoja zikijadiliwa haitachukuchua muda Mawaziri na wakurugenzi kukimbia kutoa majibu au kipiga simu kama sio kwenda kabisa na kuzungumza na Watanzania. Ruge kupitia Clouds media imeibua mambo muhimu ya kijamii ambayo yamegusa vijana na wanawake kama fursa, kipepeo na malkia wa nguvu. Burudani na muziki naomba leo nisiusemee.

Nini kimemfanya wakubwa wengi wamhitaji Ruge. Ruge awe lulu kwa kuwa ana anatengeneza sustainable competitive advantage hasa kwa jamii ya vijana na wanawake hata kwa corporates.

Kuna mambo machache ambayo ntaainisha ambayo alikuwa nayo Ruge na sasa tunamhitaji afufuke ili yatimie kwa viporo ambayo kaviacha na mengine ambayo anatakiwa kuyaleta

Ruge alijua Watanzania hasa vijana wanawake na corporate world inataka nini na alikusudia kuijulisha hiyo audience yake ina potentials gani based on opportunities available in Tanzanian settings na competitive environment ya Tanzania ili tuweze ku-thrive.

Ruge kawasaidia Watanzania kujitambua who we are and where we want to go. Amekuwa na mchango wa kuhamsisha kuipenda Tanzania na ku-grab nini Watanzania wafanye katika mikoa yao kama Dodoma as our current capital city. Nini kifanyike Tanga kwenye bomba la mafuta. Ruge amekuwa msaada kwenye kuweka mikakati ya kuvutia Utalii Tanzania. Dr. Kigwangala, ameweka wazi mchango wake katika Unfogetable Tanzania Safari.

Ruge kamsaidia Mkuu wa DAWASCO Eng. Luhemeja on how to get more custmers by taking competitive advantage ya watu wanaohitaji maji Dar. Alimpa ushauri wa kibiashara wa kuwafungiwa maji wateja wapya bure na akawasaidia ku-formulate critical revenue collection strategy kwa kuwakata wateja in 12 months ile connection fee katika bill za maji. Akapata wateja wengi.

Ruge amenza kazi na Kusaga wakati Radio ikiwa unknown. Ameanza safari na wasanii wakiwa unknown. He Made their journey by translating the strategy into action kwa kutambua watu au taasisi zina uwezo gani na kuja na implementing tactics. Mengi yamefanikiwa vs machache yaliyo-fail.

Kingine, Ruge alijifunza ku-check progress ya taasisi ailiyoisimamia kama (Director of Programmes & Production) na aliendelea kuwa na tathmini ya mara kwa mara ili kuongeza effectiveness & efficiency.

Wengi wa Watanzania mmoja mmoja, jamii ya vijana na akina mama, hali kadhalika wakubwa kama Ma-RC na Mawaziri ambao Ruge kawasaidia, bila shaka wanapungukiwa na yafuatayo:

Focus: Baadhi ya Tasisi za serikali na binafsi zimekuwa hazina uongozi wenye focus na kuna baadi yao wanashindwa kuwatumia watu wao. Kwa kushindwa huko Ruge alikuwa msaada mkubwa katika “amsha amsha”.

Tactics: kama kocha wa mpira, baadhi ya watu, viongozi na idara za umma na binafsi zimekuwa na kupungukiwa na mbinu ambazo zina-aligne na Tananiania strategy kwenda kwenye uchumi wa kati kupitia viwanda. Ruge alijikita katika Burundani ya muziki kama moja ya kiwanda cha kuzalisha mapato wa wanamuziki, kuwa na uhakika wa ajira endelevu. Kupitia hapo kodi ya serikali imepatikana. Aidha baadhi ya wasanii wakawa na akili yak u-diversify biashara na baadhia yao kuingia katika biashara ya vipodozi nia mitindo.

Limited range: Baadhi ya viongozi hawajui kuona mbali kwa kutengeneza short-term goals ambazo zitazaa long-term viable social investment, human capital investment anu uwekezaji wowote ule wa kibiashara. Watu wengi hasa viongozi, ni waoga wa Risk. Mtu kama Director Kipilimba anaweza kuwa na msada wa kuisadia taasisi za umma na kibiashara Tanzania isiogope risk ambazo zinaweza kuwa insured. Ikumbukwe, aliwahi kuwa Director wa risk management, The best way to mitigate risk is to know that there is a potential it can occur, so insurance cover inasidia compensation when risk becomes real.

Nini kifanyike. Tutengeneza akina Ruge wengi ambao kwa haraka sana watasambaa na kuendeleza “habari njema” ambazo Ruge alisimama na kuzihubiri. Iko haja kufanya quick indentification ya Watu ambao wapo na Serikali ifanye nao kazi ili mambo yaendelee. Otherwise watu watanendelea kumlilia na baada ya muda tutaanza kurudi nyuma badala ya kuendelea na momentum ya kuijenga Tanzania ya viwanda na kukuza uchumi wa kati kwa Watanzania wengi.

Ni kweli Ruge imeondoka. (The creative brain and innovative brain imeondoka) Tukisubiri such a daring and exposed individual to surface, huenda ikachukua muda mrefu sana Tanzania kumpata. Ruge amekuwa na competitive advantage ya kuwa na exposure ya makuzi ya wazazi wenye uelewa mkubwa na kasoma shule za ndani na nje ya Tanzania. Ukichanganya na personality yake, Ruge alikuwa MULTiTASKING PERSON.

Sasa basi, ili kuwapata akina “Ruge” wengi ku-fill the gap ya kuwapata vijana ambao watakuwa na akili za kuifadisha public sector, media, vijana kuwasaidia kuziona fursa na kuwasaidia kuibua ubunifu (creativity and innovation); tutate say a public forum ambapo watu hao wanaweza kuwa indentified. Huenda ndani ya session 3 mpaka 4 wakapatika right people to take lead. Uzoefu hasa kwa walimu, ni rahisi kumtambua akiwa mbele ya public.

Kwanini initiatives za makusudi zifanyike. Naomba kutoa mifano miwili ambayo inaweza isiwe na relevance, japo yaweza kuwa na uzito wa hoja yangu .

Rais Kikwete aliunda Tume ya kutafuta maoni ya katiba mpya wakati wa muhula wake wa pili. Tume hiyo ndiyo ilimuibua Humphrey Polepole. Ilitokea ndiyo alikuwa kijana mwenye umri mdogo, ila tokea hapo akajiongeza na leo hii kasogea kimajukumu mpaka kuaminiwa na Chama cha Mapinduzi kama Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM – Itikadi na Uenezi. Bila shaka bila ile tume ingekuwa kazi kumuibua mtu aina ya Polepole.

Kashfa ya kuchunguza UFISADI WA RICHMOND. Huu ndio wakati ambao ulimuibua Dr. Harrisaon George Mwaknyembe. Kuna wengi walikuwepo katika ila tume, ila mtu alie-ng’ara sana, ni Dr. Mwakyembe.

Ruge amekuwa ni kama Ex-officio senior government officer akiwa katika front pages za magazeti na a lot being spoken in social media and his death has come like ceremony of a “big shot” from government circles. What made him arrive there, his brain.

Mwisho nampongeza sana,tena sana Joe Kusaga. Joe amekuwa MD & CEO mzuri sana. Hakuwa na sense of insecurity kama vile Ruge anamfunika pale Clouds Media. Maana it was known huku mtaani,kuwa Ruge ndiye kila kitu pale Clouds Media. Basically, kwa mtu mwenye moyo mdogo ingeleta mafigisu sana n a labda wangeweza kusambaratika. Instead Joe, alijua nafasi yake kama MD & CEO na alimwachia Ruge “ajiachie” kwa kubuni vitu na kuibua watu Clouds Media. Clouds Radio ilihama kutoka entertainment station mpaka kuwa radio yenye “serious session” zikichanganyikana na burudani.

Mfumo wa radio kuwa hewani ikiwa supported na soundtrack ni “mfumo mpya” akina Ruge waliuleta na baadae kila FM station ikaiga.

Pengine shukurani pia zimfikie Dr. Kimei (aliekuwa MD wa CRDB Bank) kwa kutambua vision ya Joe na Ruge. Kwa maelezo ya Joe wakati Clouds inatimkiza miaka 19 (mwaka jana); mzee Kimei aliamini katika vision ya akina Joe na Ruge akawakopesha TZS 40mil bila ya kuwa na known outstanding cashflow. It was a great risk business worth of taking. Sijui le hii tuna ma-MD katika private sector wenye capacity ya fursa ya biashara mpya ambayo haina known cashflow na wakaiamini. Leo Clouds media imekuwa na group of companies yenye assets za kutosha.

Ndiyo maana narejea tena kumwomba “Mkuu wa Kaya” afanye kitu ili kuzalisha Watanzania aina ya Ruge. Ukizingatia uzalendo na assets ya imputs ambazo zitaingia katika akili na fahamu za Watanzania kwa ujumla wake. Team hu itagusa vijana, wanawake, wanaume, wanasiasa, viongozi, wasomi, wananzuoni na wenye akili ya kawaida. Niko tayari kutoa mchango wangu katika “mismatch” ya yale ambayo nafahamu Ruge alifanya husan katika eneo la kuwajengea uwezo vijana na wadau wa vijana kwa kuzidadavua fursa za biashara; namna gani ya kuwa na sustainable productive model ambazo zinaweza kuzaa matokeo yanayotarajiwa. Kwa uchache namna gani ya kukuza uchumi, kuongeza fursa za ajira rasmi, kuongeza watu wanaoingia katika mifuko ya pensheni na bima ya afya. Kupanua wigo wa biashara wanaopata fedha za uhakika kupitia mauzo ya bidhaa ndani ya Tanzania na nje ya nchi.

Nahitimisha kwa kusema, Mwl. Nyerere alikuwa na vision kubwa ya kutaka kuwa na Tanganyika huru. Bila project financing ya akina Mzee John Rupia na akina Jamal bila shaka tungechelewa sana kupata uhuru.

JPM akiwa waziri wa Ujenzi alikuwa na vision ya kuanza kujenga barabara kupitia fedha za ndani. Waziri Mkuu Sumaye na baadhi ya cabinet members walimgomea. Very fortunate, Rais Mkapa aliamini katika vision ya JPM na akatoa agizo, proposal yake itekelezwe.

Bila shaka katika mchakato wa kuwaibua akina “New Ruges” mchakato huo uendene na financing their community transforming projects. Msingi tu, uwe ni the return on investment ikipimika ina more assets kwa Watanzania. Liabilities lazima zitakuwepo, maana hata Ruge alikuwa nazo, sema tu, tunaposheherekia msiba wake, tunajivunia assets za Ruge kuliko liabilities zake.

Mhe. Rais, ukifanya hivyo, utakuwa umetengeneza human assets (known to work for public interest) ambazo zitakusaidia kuwa sehemu ya ku-neutraize our common enemies which are poverty, ignorance and diseases. These known enemies are creating new threats locally by rogue Tanzanians, same threats are potentially being used by foreign enemies.

Kama ingetokea Ruge akawa entrusted na dhamana ya Wizara ya ajira kama mshauri mwelekezi au Waziri, bila shaka angefanya makubwa. Wizara hii ina all assets to leverage into greatness, siuji kama wanajua hilo, na kama hawajaona, iko haja hoo akina “New Ruge” wakasaidia ku-fill in the gas ili wizara hii ikue sana tu. Bila shaka UVCCM na Katibu wa Uchumi na Fedha CCM, mnawahitaji akina Ruge ili nanyi muwe sehemu ya kuingia katika viwanda kama namna ya kuongeza thamani ya bidhaa, kutoa ajira endelevu na kupanua wigo wa kodi kwa serikali.

Tunaomba kwa Mungu wa Mbiguni faraja yake iwe kwa familia ya Ruge, familia ya Clouds Media na Watanzania wote.
Ruge alikuwa CCM, so hamna jipya.
Ni sawa na teuzi za juzi, ni dream team ya mechi ya 2025 na si mambo ya utendaji kama uwazavyo.
 
Back
Top Bottom