profftobe
JF-Expert Member
- Sep 12, 2017
- 906
- 940
Kuolewa sio kwamba unamuendesha au unammiliki ishu ni kwamba na yeye ni mtu binafsi!
Ni mtu binafsi na ana vitu vyake,huwezi m-control mkuu,yule sio your personal property!
Cha msingi ajue muda wa kurudi home na kuondoka,otherwise itakua ugomvi big time!
Hapo ni uelewa tu na attitude ya mhusika,ndio maana malezi ni ishu kubwa!
My school of thought ni kwamba,hela zake ni zake,za baba ndio za kila kitu,akiamua kusaidia vitu fulani fulani ni yeye kwa hiyari yake na kwangu mimi asiniambie chochote akiwa anafanya hivyo!
Nachojua mwanaume ndio anatakiwa ku-provide kila kitu kwa familia regardless!
Hii “saidiana” ina costs zake,kama unaweza zivumilia sawa,endelea “kusaidiana” ila kwa mimi “saidiana” ni totally no,forever!
Labda nife a-take over yeye!Nina miguu miwili mzee,hilo ni no kabisa!
Mtumishi, nakushukuru kwa kushare hiyo "school of thought" yako. Kimsingi, huko sahihi kabisa, kuolewa hakumfanyi mtu mke hapoteze utu wake na hivyo kuwa chini ya mme wake. Hili nalikubali asilimia zote.
Na pia sijakataa kuwa hela siyo zake, ni za kwake maana yeye ndiye anafanya kazi.
Utata huko kwenye hili eti "Mwanaume ndio anatakiwa ku-provide kila kitu kwa familia regardless". Hapa mtumishi, utanisamehe, sikubaliani na wewe hata kidogo. Hii ilikuwa sahihi zamani wakati wamama wengi walipokuwa wanaitwa mama wa nyumbani (housewife), wanakaa nyumbani kulea watoto na kufanya kazi za pale nyumbani zisizo kuwa na kipato. Hivyo, hata kwa sasa itaendelea kuwa sahihi tu endapo mtu mke atakuwa hatumii mda wa familia kujitafutia kipato, kwa maana nyingine kama ni mama wa nyumbani na/au labda ana kipato chake binafsi kama vile fedha zake za uridhi n.k. lakini mda wake mwingi yuko pale home. Ninachopinga ni hawa ke wa siku hizi wanaomilikisha watoto/familia zao kwa ma-housemaids alafu eti ni sawa tu watafute fedha zao binafsi kisha mme a-provide kila kitu na kumlipa hadi huyo housemaid. Kama ni hivyo kwa nini nisioe kabisa huyohuyo housemaid, kwani hanakosa nini kama mke mwenyewe ndiyo wa hivyo unayemsema wewe maana huyo mke wa hivyo faida yake ni sex na kuzaa ambavyo hata house-girl (above 18yrs) anaweza kufanya hayo.
Mimi sikatai mwanaume ku-provide kila kitu kwa familia, ila iwe katika mazingira yasiyo ya kinyonyaji ambapo wote mme na mke mnaondoka kila siku asbh nyumbani na kurudi jioni alafu eti mme anatafuta fedha za familia na mke atafute za kwake binafsi. Hapo si bora ahache tu kazi ili mme a-provide kila kitu akiwa anajua mke wake anasaidia kulea watoto hapo nyumbani na siyo house-girls. Kwanza kama siyo kwenye familia huyo mke atakuwa anazitumia wapi hizo fedha?
Mwisho kama huyo mke hajazoea kuchangia walao kidogo kwenye famila, hata mme bahati mbaya akinyamaza huyo mke hataweza ku-take over kama ulivyosema, familia itamshinda kesho yake, na kuna possibility kubwa ya kuwatelekeza watoto/familia akiangaika kutafuta mabwana ili aendelee na ubinafsi wake.
Hacha bana wanawake wanye-ndoa (siyo wale ma side chicks) na wana kipato wachangie maendeleo ya familia zao walao kidogo kwa hiari yao lakini!!