Wale mliooa wanawake wanaofanya kazi

Wale mliooa wanawake wanaofanya kazi

Mwanaume mwenye ajira nzuri kipato kizuri fuata njia zangu tafuta mwanamke mwenye kipato cha chini yako ikiwezekana mfungulie biashara ,pia angalia na tabia zake kama mtaendana...utaishi maisha mazuri sana na Mungu atawabatiki sana...ila kama amekuzidi vipato usitarajie amani ndani ya nyumba

Classic and most honest opinion so far!
 
Utatembea na wanaume wangapi au ndiyo hulka kutembea na kila anaekufaa kwa muda huo......huwa majibu yako siku zote huwa ni ya mtindo huu kwenye nyuzi nyingi hasa maswala ya vipato na mwenza wako, huwa sipatagi majibu mnaishije mwanamke kutunisha kifua mbele ya mume wake ni dhana ya ushindani na kujitia uanaume ilihali wewe ni mwanamke
Ndugu kama kulinda kihela changu kidogo nachokitafuta dhidi ya marioos ni kushindana na mwanaume anayetaka tunzwa na mwanamke so be it,jion njema hahahah
 
Mkuu wewe kazi za nyumbani huwa unamsaidia?
Mrejesho.........Badala ya kwenda mbele ndo narudi nyuma!

Huyu mwenzangu ye kaajiriwa na serikali na mwisho wa mwezi sio haba. Tunakaa mikoa tofauti, Usiku wa kuamkia leo nikampa maneno matamtam sana ili nianze kuandaa mazingira ya kumuomba aniongezee laki na 10 ili niagizie vifaranga vipya kwenye mradi wangu maana bado haujaanza kutoa matunda. Nilipomwambia tu akaanza kuniambia ooh hela sina na wakati najua juzi kapokea mshahara.
Akiwa katikati ya mwezi hali mbaya huwa nafanya kila niwezalo nimtumie hata 50 ya matumizi kwa wiki ila yeye laki tu karuka viunzi.
Hapa najiona kama nimeruka stage kwenye maisha yangu, kutokana na kuoana na yeye now nashindwa hata kujilipua kwenda mbali kutafuta maisha, nakaa karibu nae ili niwajibike kama mwanaume kwake na kwa mtoto wetu lakini mwenzangu akipata hela anajiangalia sana yeye tu.
Sioni faida ya hii ndoa soon naongeza idadi ya single mothers mtaani.
 
Wanaume mngekuwa mnalijua hili basi pia hata kufanya kazi za ndani mngechukulia ni kama jukumu lenu pia
Ungelitazama kwa mtazamo tofauti usingeona kama unamhudumia mwanaume (kama mmeoana). Ungeona ni kama unajihudumia mwenyewe (coz mmeshakuwa mwili mmoja). Utaionaje sehemu ya mwili wako kuwa mzigo?
 
Wanaume mngekuwa mnalijua hili basi pia hata kufanya kazi za ndani mngechukulia ni kama jukumu lenu pia
Kazi za ndani, ni neno pana siyo kupika, kufua na vyombo tu. Kuna kazi za ndani wanaume tunafanya mfano: kuhudumia mifugo kama ipo, bustani, matengenezo ya hitirafu mbalimbali zinapojitokeza kama za nyumba, umeme, magari n.k. Hizi zote ni kazi za nyumbani ila wanawake kwa sababu ya ubinafsi wao hawaoni kama hizo ni kazi za ndani mpaka ufanye kazi ndogo ndogo kama kufua na kupiga deki ndo watarizika umefanya kazi za ndani. Ujinga tu!!
 
Haya

Kwanza usomi sio pesa, mbili udhaifu/insecurity ni kudhani kusaidiana kimawazo ama kiuchumi kunaleta kupoteza madaraka yako kama baba wa nyumba. Ndio maana ndoa zenu zinakuwa ngumu, hamna pa kugeukia ama hata kupata msaada,, sio Hata kwa wenzi wenu! Huu usiri sijui wa vipato na matumizi na kutokutaka kusaidiana ni hulka ya Uchoyo tu, hakuna kingine. Changu changu chako changu, maendeleo mtayasikia tu, badilikeni. Mahusiano hutengenezwa, na hakuna raha ya ndoa kama pale mnaposhirikiana maana maisha yanakuwa ahueni. Hakuna mtu mwenye pesa zikamtosha, poleni Sana
Kwanza kabisa sihitaji pole yako hata kidogo, mimi na wewe ni dhairi tunaishi dunia mbili tofauti. Kama ambavyo unashangaa na kuona mawazo yangu ni ya kijima au ya kipumbavu hivyo hivyo pia hata mimi naona mawazo yako ni kipuuzi sana. Kwa kusoma tu hii comment yako wewe huko kwenye ile 80% ya wanaume wote(sihitaji kuelezea hapa maana huitaji kuambiwa maana).

Mwanaume mzima kabisa unahitaji ushirikiano wa kiuchumi kutoka kwa mkeo hili maisha yawe ahueni, halafu eti unaiita mimi dhaifu? eboo!!

Wewe una safari ndefu sana, tena sana ya kuwajua wanawake, hapo ulipo wewe mimi nilikuwepo miaka kadhaa nyuma
 
Tunaomba mrejesho kwa wale ambao mmeoa wanawake wanaofanya kazi ili muweze kusaidiana maisha
MREJESHO ni kwamba:

Waliooa wanawake wenye kufanya kazi sasahivi wana stress na hawana Amani ilihali mwanamke anaingiza kipato

Waliooa wanawake wamama wa nyumbani tu wana Amani tele ingawa mwanamke haingizi pesa ndani.

Tafakari.....Chukua hatua!
 
Kwanza kabisa sihitaji pole yako hata kidogo, mimi na wewe ni dhairi tunaishi dunia mbili tofauti. Kama ambavyo unashangaa na kuona mawazo yangu ni ya kijima au ya kipumbavu hivyo hivyo pia hata mimi naona mawazo yako ni kipuuzi sana. Kwa kusoma tu hii comment yako wewe huko kwenye ile 80% ya wanaume wote(sihitaji kuelezea hapa maana huitaji kuambiwa maana).

Mwanaume mzima kabisa unahitaji ushirikiano wa kiuchumi kutoka kwa mkeo hili maisha yawe ahueni, halafu eti unaiita mimi dhaifu? eboo!!

Wewe una safari ndefu sana, tena sana ya kuwajua wanawake, hapo ulipo wewe mimi nilikuwepo miaka kadhaa nyuma
Siyo kweli mtumishi. Hivi mwanamke anayeaga nyumbani kila siku na kwenda kazini. Wakati mwingine anaondoka saa 11 asbh na kurejea saa 3 usiku. Kisha mwisho wa mwezi asichangie chochote, ada ya watoto asichangie chochote, hadi matumizi yake binafsi na mshahara wa housemaid anaomba apewe kweli!. Huyo wa hivyo ana faida gani katika familia? Si anakuwa sawa na malaya tu? Hayo unayosema yataeleweka ikiwa mke ni mama wa nyumbani, au ana kibiashara kidogo tu pale nyumbani, vinginevyo siyo sawa.
 
Teh...maendeleo ni suala mtambuka.

Wengine kitokupitwa na mitindo mipya ndiyi maendeleo yenyewe. Kwanini ugombane na my wife wako bila sababu acha ajinafasi.

Dawa my wife wa hivyo unamchukulisha mkopo kisha huulizi pesa inakoelekea...
Kila fashion isipite, kazi ipo
 
Siyo kweli mtumishi. Hivi mwanamke anayeaga nyumbani kila siku na kwenda kazini. Wakati mwingine anaondoka saa 11 asbh na kurejea saa 3 usiku. Kisha mwisho wa mwezi asichangie chochote, ada ya watoto asichangie chochote, hadi matumizi yake binafsi na mshahara wa housemaid anaomba apewe kweli!. Huyo wa hivyo ana faida gani katika familia? Si anakuwa sawa na malaya tu? Hayo unayosema yataeleweka ikiwa mke ni mama wa nyumbani, au ana kibiashara kidogo tu pale nyumbani, vinginevyo siyo sawa.

Mtumishi kama utakuwa ulinisoma tangu kwenye comment yangu ya awali nadhani ungekuwa umenielewa ni wapi nasimamia na kwanini nimemjibu hivyo huyo jamaa hapo!

Nakubaliana na wewe kabisa mwanamke anayechakalika sawa na wewe ni wajibu wake kuchangia mkate mezani, lakini sasa hicho kisiwe kigezo kikuu cha wewe kutafuta mkee eti awe na kazi hili msaidiane.. binafsi mimi siafikiani na hilo bali niko kinyume na hapo!

Kilichonikera kwenye hiyo comment ya jamaa niliye maquote ni kuniambia eti kumkataa mwanamke wa aina hii ni insecurity na udhaifu wakati ukiiangalia kwa mapana hiyo kauli yake yeye ndio dhaifu maana anaonesha wazi hawezi kutumia akili yake mwrnyewe kuendesha familia mpaka aunganishe na ya mke wake ndio maendeleo yataonekana!! si uzwazwa huo wa kiwango cha mwisho.
 
Ni mwaka wa nne huu na bado sijutii. Tunasaidiana kwa mengi, kuanzia matumizi ya nyumbani mpaka kwenye investments. Na hata bahati mbaya nikitangulia mbele za haki, Niko na confidence of more than 60% kwamba mtoto (watoto) wangu are in good hands.

Hongera, nimependa ulichoandika. Mungu abariki ndoa yenu.
 
Mrejesho.........Badala ya kwenda mbele ndo narudi nyuma!

Huyu mwenzangu ye kaajiriwa na serikali na mwisho wa mwezi sio haba. Tunakaa mikoa tofauti, Usiku wa kuamkia leo nikampa maneno matamtam sana ili nianze kuandaa mazingira ya kumuomba aniongezee laki na 10 ili niagizie vifaranga vipya kwenye mradi wangu maana bado haujaanza kutoa matunda. Nilipomwambia tu akaanza kuniambia ooh hela sina na wakati najua juzi kapokea mshahara.
Akiwa katikati ya mwezi hali mbaya huwa nafanya kila niwezalo nimtumie hata 50 ya matumizi kwa wiki ila yeye laki tu karuka viunzi.
Hapa najiona kama nimeruka stage kwenye maisha yangu, kutokana na kuoana na yeye now nashindwa hata kujilipua kwenda mbali kutafuta maisha, nakaa karibu nae ili niwajibike kama mwanaume kwake na kwa mtoto wetu lakini mwenzangu akipata hela anajiangalia sana yeye tu.
Sioni faida ya hii ndoa soon naongeza idadi ya single mothers mtaani.

Pole sana. Ngoja nikupe ujanja [emoji16], wanawake wanapenda wakitoa hela waone matumizi yake na faida atakayoipata. Ukimuomba pesa unatakiwa ujieleze ya nini na kwa Kazi ipi, ikiwezekana mshirikishe na faida mpatie kidogo. Ukifanya hivyo utapewa bila shida.

Ukiomba then haoni matunda yake. Hutopewa tena na hii ni kutoka na asili yetu, sisi wanawake ni wazalishaji huwa tunapenda kuona ongezeko.
 
Back
Top Bottom