Wale mliooa wanawake wanaofanya kazi

Wale mliooa wanawake wanaofanya kazi

Mimi sitaki mke akwepe kazi zake za nyumbani, regardless anatafuta pesa au hatafuti. Na kama inamuwia ngumu na hio kazi aache. Afanye majukumu yake ya nyumbanu hatutakufa njaa
Sasa mbona ndo unalalamika kuwa haupendi mwanamke golikipa?
 
Wanawake wa kibongo wengi choka mbaya halafu wana roho za kimaskini sana...hio ndio shida [emoji1787][emoji1787][emoji1787]!!!

Mapenzi ni kutoa na kupokea ila kadri unavyojitahidi kuwa upande wa kutoa kuliko kupokea ndipo thamani yako inapokuwa maradufu. Always strive to be more giving than recieving, kuna baraka tele katika hilo hata kiimani. Ubinafsi uliopo kwa ke wengi wa kibongo eti mwanaume agharamikie kila kitu ni wa kizamani na ndio umesababisha tatizo la udangaji kutamalaki badala ya watu kufanya kazi kujipatia vipato vya halali.

Kwa jamii zilizostaarabika huo upuuzi haupo. Wadada mbona mnachagua vya kuiga, igeni na hilo kwa wanawake wa kizungu sio mnaiga vitu vya kijinga tu kama kuchora tatoo, kuweka kope, nyusi, kucha na matako bandia.

Mi naona cost sharing inasaidia sana kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa haraka zaidi, simlazimishi mtu kuadopt huo mfumo ila nimeongea kwa mtazamo wangu binafsi.
Thats true men
 
Hiki ndicho wengi hutarajia kwa wapenzi ambao mmefanikiwa kuwa mke na mume. Sijui ugumu wa kulielewa hili uko wapi. Mke akiamua kushirikiana na mumewe kujiletea maendeleo ni dhambi wazee?[emoji2] Mliooa ma slay queen msitupe tabu jamani.

Mwanamke mwenye hekima ndio hufanya hayo usemayo.
Sasa wewe unataka mkeo afanye majukumu mengi kuliko wewe? Hivi nini maana ya usaidizi?
 
Khaa sasa kwani pia ni maana ya mume ikiwa na mke ameolewa na huku anatafuta pesa na anahudumia familia? Yaani huyo msaidizi ndo umtwishe majukumu yote wewe ufanye machache? Hivi unajua maana ya msaidizi?
Kwani majukumu ya mke ni yapi? Tuanzie hapo!
 
Ukweli huu hapa
Screenshot_20190529-102744.jpg
 
Mrejesho.........Badala ya kwenda mbele ndo narudi nyuma!

Huyu mwenzangu ye kaajiriwa na serikali na mwisho wa mwezi sio haba. Tunakaa mikoa tofauti, Usiku wa kuamkia leo nikampa maneno matamtam sana ili nianze kuandaa mazingira ya kumuomba aniongezee laki na 10 ili niagizie vifaranga vipya kwenye mradi wangu maana bado haujaanza kutoa matunda. Nilipomwambia tu akaanza kuniambia ooh hela sina na wakati najua juzi kapokea mshahara.
Akiwa katikati ya mwezi hali mbaya huwa nafanya kila niwezalo nimtumie hata 50 ya matumizi kwa wiki ila yeye laki tu karuka viunzi.
Hapa najiona kama nimeruka stage kwenye maisha yangu, kutokana na kuoana na yeye now nashindwa hata kujilipua kwenda mbali kutafuta maisha, nakaa karibu nae ili niwajibike kama mwanaume kwake na kwa mtoto wetu lakini mwenzangu akipata hela anajiangalia sana yeye tu.
Sioni faida ya hii ndoa soon naongeza idadi ya single mothers mtaani.
Pole sana mkuu.

Kula like upunguze machungu
 
Hivi na kazi za ndani huwa mnawasaidia wake zenu kwa mtazamo huo huo kuwa mnafanya kwa ajili yenu wote au kazi za ndani ni za mke peke yake?
Mimi kwangu hata kuogesha watoto naogesha kasoro kupiga deki tu, jumapili zote kupika zamu yangu na watoto wanafurahi sana wakiniona jikoni mana wanajua kitu nachokitoa huko si mchezo.
 
Sasa nini maana ya mke kama mie nimeoa ili hizo kazi afanye mke. Haingii akilini niweke msaidizi kisha nifanye hizo kazi tena.
Mwisho wa siku ukichunguza sana, siku hizi wanawake wengi hasa wale waliojaliwa kazi za kipato/mshahara hata hizo kazi za ndani anazosema hawazifanyi. Na ki-ubinadamu rahisi kuelewa kwa nini hawafanyi, kwa sababu hizo kazi za mshahara nyingine ni ngumu na zinawachosha, kama zinavyowachosha wanaume. Lakini sasa wanatafuta na kuwaachia kazi zote ma-housemaids. Na kibaya zaidi hata mshahara wa hao housemaids wanataka me ndiyo walipe. Sasa unajiuliza nini maana ya mke kufanya kazi za kipato, maana kazi za ndani hafanyi tena, na faida ya kazi anazofanya huko nje anasema haina uhusiano na matumizi ya familia maana ni jukumu la mme kuitafutia familia yake. Kama ni hivyo nini hasa maana ya kuwa na mke kama huyo hapo nyumbani!! Wanawake wengine ni shida, they are too selfish & greedy
 
Mimi kwangu hata kuogesha watoto naogesha kasoro kupiga deki tu, jumapili zote kupika zamu yangu na watoto wanafurahi sana wakiniona jikoni mana wanajua kitu nachokitoa huko si mchezo.
Najua unatania brother G.Jacob. Kama kweli unayafanya hayo, usijisifisie utakuwa umelishwa limbwata la grade A+
 
Sitanii na wala sijalishwa hilo mbwata hata kidogo, ni mfumo wa maisha tuliishi nikiwa nyumbani kwetu na sasa nimeuhamishia kwangu.

Haya bwana, hongera kwa hilo, nakubali sana ya kuwa kila mtu aishi na familia yake kama atakavyo ili mradi wanafurahia hayo maisha waliojipangia. Lakini kwa mtazamo wangu na kwa traditions nyingi za kiafrica nazani siyo vizuri mme kusonga ugali, kumenya ndizi na/au kukuna nazi jikoni kwenye kigoda wakati mke anaangalia TV sebureni na watoto.

Mimi hata nikiwa na nia ya kufanya hayo wife atanifukuza jikoni, japo kwakweli hata mimi siongopi najua sana kupika maana nyumbani nilikokulia, nilikuwa napika kila aina ya vyakula na ninaweza hata kumenya ndizi hadi za watu 20 mpaka 50. Lakini baada ya kuanzisha mji wangu kwa kweli sipiki tena hata nikiingia jikoni mara kwa mara wife ananifukuza, unless kama kuna challenge kama vile gas imeisha, nikachue mtungi kwenda kununua au kuna kitu cha muhimu nahitajika kusaidia jikoni.

Labda, nikuulize, your wife alilichukuliaje hilo swala la wewe kuhamishia nyumbani kwake huo utaratibu wa wewe kupika?
 
Ah, that situation you are talking about is full of nothing rather than an undisputed hypocrisy.

And why do you assume handshaking by those two political figures has to do with hypocrisy? haujui kwamba mmoja ni msema kweli na tena mpenzi wa Mungu.
 
Wataelewa tuu , tukikaa kikao cha wanaume kuwajadili umekula kwako
Mrejesho.........Badala ya kwenda mbele ndo narudi nyuma!

Huyu mwenzangu ye kaajiriwa na serikali na mwisho wa mwezi sio haba. Tunakaa mikoa tofauti, Usiku wa kuamkia leo nikampa maneno matamtam sana ili nianze kuandaa mazingira ya kumuomba aniongezee laki na 10 ili niagizie vifaranga vipya kwenye mradi wangu maana bado haujaanza kutoa matunda. Nilipomwambia tu akaanza kuniambia ooh hela sina na wakati najua juzi kapokea mshahara.
Akiwa katikati ya mwezi hali mbaya huwa nafanya kila niwezalo nimtumie hata 50 ya matumizi kwa wiki ila yeye laki tu karuka viunzi.
Hapa najiona kama nimeruka stage kwenye maisha yangu, kutokana na kuoana na yeye now nashindwa hata kujilipua kwenda mbali kutafuta maisha, nakaa karibu nae ili niwajibike kama mwanaume kwake na kwa mtoto wetu lakini mwenzangu akipata hela anajiangalia sana yeye tu.
Sioni faida ya hii ndoa soon naongeza idadi ya single mothers mtaani.
 
kwa upande wangu mm sioni shida kushare mshahara wang na mume wang tena mm ndio nnapokea mshahara mkubwa kuliko mme wang na hutasikia hata siku moja naanza maneno maneno kwa mme wang, nampenda sana na kumuheshimu mume WANG na najua tunachofanya ni kwaajili ya WATOTOT wetu na FAMILIA yetu kiujumla yani mie kumwambia mme wang acha mwezi huu ntafanya kila kitu ww mshahara wako nunua chochote unachotaka sioni shida kabisaaaaaa,, NB: KUPANGA NI KUCHAGUA...
 
Congratulations. Keep up that good habit, you are one among a few understand women! I guess that your man is also an understanding person. So I pray may you two make a strong and happily united family in God's name
 
Back
Top Bottom