Wakristo wenzangu hebu tuacheni tabia hizi!

Wakristo wenzangu hebu tuacheni tabia hizi!

Hii kitu nimekuwa nikiiona na ikawa inanifanya nijiulize maswali mengi huku ikinikera sana na leo nimeona nitoe " nyongo " hasa kwa Wakristo wenzangu. Nilichokiaona leo Ibadani ndiyo kabisa " imenitibua ". Hivi kweli Mkristo na Mcha Mungu wa kweli umeamua mwenyewe kwenda Ibadani Kanisani unaweza kuthubutu kuyafanya haya yafuatayo?

  1. Kutoa Sadaka na kuomba chenji kwa Mashemasi tena bila hata aibu?
  2. Muda wote Ibada inaendelea Wewe unasinzia huku " udenda " ukikutoka " ndomoni? "
  3. Nyimbo ya kusifu inapigwa " Jitu " linapiga makofi huku " limenuna " mwanzo mwisho.
  4. Mtu mzima kabisa muda wa kutoa Sadaka unatoa Tsh 500/ huku umevalia Suti.
  5. Ibada inaendelea unachati na muda mwingine kuinama na kuongea na Simu.
  6. Mwanamke mzima unakaa Ibadani na " unajipanua panua " miguu yako hovyo hovyo.
  7. Unajitayarisha kutoa Sadaka yako " lijitu " linakuangalia " kodo " unatoa Tsh ngapi.
Ibada ya leo imenikera sana na haya yasipofanyika au kurekebishwa haraka katika Makanisa yetu ya Kikristo / Kiroho nadhani itabidi tu niwe nasalia Chumbani kwangu. Kuna Watu na matendo yao yanakufanya kabisa ukereke Ibadani hadi kupelekea kubadili Sala / Maombi yako ya siku hiyo.

Jamani hamjalazimishwa kwenda Kusali Kanisani kama unaona siku hiyo haupo vizuri vinginevyo mnapokuja Kusali na hayo Matendo yenu mnatukera mno Sisi Wakristo wa kweli na tunaomjua Mungu kisawasawa.

Ewe Mwenyezi Mungu nawaomba uwalaani vikali hawa Wakristo wenzangu wenye hizo tabia saba ( 7 ) hapo juu kwani wanatuharibia Imani yetu iliyotukuka kwako.
Naunga mkono hoja Ila hapo kwenye kulaani nakupinga
 
ni vyema ungeshare nao huu ujumbe hao waumini unaosali nao hapo kanisani kwenu sio kuja huku haijasaidia kitu bado
 
Ukristo ni mfumo wa maisha. Ila wengi hawakubaliani na huu mfumo maana unapitia kwenye njia nyembamba. Wamegeuza makanisa vijiwe saccoss madanguro sehemu za maonyesho na viwanja vya maigizo. Yote haya hayakufanyi usiende kanisani maana hufuati watu unamfuata Mungu.
Mkuu naomba unisaidie kirefu cha SACCOS
 
Hii kitu nimekuwa nikiiona na ikawa inanifanya nijiulize maswali mengi huku ikinikera sana na leo nimeona nitoe " nyongo " hasa kwa Wakristo wenzangu. Nilichokiaona leo Ibadani ndiyo kabisa " imenitibua ". Hivi kweli Mkristo na Mcha Mungu wa kweli umeamua mwenyewe kwenda Ibadani Kanisani unaweza kuthubutu kuyafanya haya yafuatayo?

  1. Kutoa Sadaka na kuomba chenji kwa Mashemasi tena bila hata aibu?
  2. Muda wote Ibada inaendelea Wewe unasinzia huku " udenda " ukikutoka " ndomoni? "
  3. Nyimbo ya kusifu inapigwa " Jitu " linapiga makofi huku " limenuna " mwanzo mwisho.
  4. Mtu mzima kabisa muda wa kutoa Sadaka unatoa Tsh 500/ huku umevalia Suti.
  5. Ibada inaendelea unachati na muda mwingine kuinama na kuongea na Simu.
  6. Mwanamke mzima unakaa Ibadani na " unajipanua panua " miguu yako hovyo hovyo.
  7. Unajitayarisha kutoa Sadaka yako " lijitu " linakuangalia " kodo " unatoa Tsh ngapi.
Ibada ya leo imenikera sana na haya yasipofanyika au kurekebishwa haraka katika Makanisa yetu ya Kikristo / Kiroho nadhani itabidi tu niwe nasalia Chumbani kwangu. Kuna Watu na matendo yao yanakufanya kabisa ukereke Ibadani hadi kupelekea kubadili Sala / Maombi yako ya siku hiyo.

Jamani hamjalazimishwa kwenda Kusali Kanisani kama unaona siku hiyo haupo vizuri vinginevyo mnapokuja Kusali na hayo Matendo yenu mnatukera mno Sisi Wakristo wa kweli na tunaomjua Mungu kisawasawa.

Ewe Mwenyezi Mungu nawaomba uwalaani vikali hawa Wakristo wenzangu wenye hizo tabia saba ( 7 ) hapo juu kwani wanatuharibia Imani yetu iliyotukuka kwako.
Unaonyesha wewe hujaenda kusali... bali kuchunguza watu... mana mda wote wa ibada wewe umafatile yupo kapanua paja.. uyi anadai chenji ya sadaka
 
ni vyema ungeshare nao huu ujumbe hao waumini unaosali nao hapo kanisani kwenu sio kuja huku haijasaidia kitu bado

Kwa hili bandiko lako tu nimeshagundua aina ya ubovu wa Ubongo wako. Nani aliyekuambia kuwa Members wa JF hawapatikani katika hilo Kanisa langu? Huwa sipendi KUWADHARAU ila kuna Watu wa mfano wako hakika huwa mnanilazimisha NIWADHARAU na hakika NITAWADHARAU hadi muwe na AKILI au FIKRA kubwa mnapokuwa humu jamvini. Kwa kukusaidia tu JF imeteka makundi yote ya Watu wa kila kada na kila mahala hapa Tanzania na nje ya nchi hivyo IMPACT yake katika jambo fulani huwa ni very positive na Jamii kupitia Mtu mmoja mmoja imeweza kubadilika kwa matendo au miendendo yao baada ya mambo fulani kuwekwa humu na nikuhakikishie tu kuwa UZI wangu haujasaidia tu hapo ninaposali Mimi ila umeweza kusomwa na Watu wengine wenye kupata Kero kama hizi na nina uhakika kuwa haya mapungufu katika nyumba zetu za Ibada yatafanyiwa kazi na kubadilika hivyo kupelekea Mimi kuwa Mshindi wa kile nilichokileta humu.

Usiponijua au kunizoea vizuri waweza kuniona kama vile nina masihara fulani na napoteza tu muda hasa kupitia mabandiko yangu ila mwenyewe najijua kuwa nimeweza kubadili mambo kadha wa kadha hasa kwa yale ninayoyaibua humu na style yangu itabaki kuwa hii hii ya kikomedi komedi lakini nafikisha ujumbe panapotakiwa na Jamii inabadilika. Usidhani Watu tunapo log in humu JF tumekuja tu kupoteza muda bali fahamu kuwa We're on the serious business of transforming the Society and taking it to the next level of ideological development.
 
Unaonyesha wewe hujaenda kusali... bali kuchunguza watu... mana mda wote wa ibada wewe umafatile yupo kapanua paja.. uyi anadai chenji ya sadaka

Niliamua kuwa " Mdukuzi " wa Kiroho na Kiiamani kwa leo Kanisani.
 
Ufahamu wako unakuambia ibada ni nini na unaenda kanisani kufanya nini? Maana unayoyaandika mtandaoni na unavyotukana watu nikajua huna dini kabisa.
 
Eti wanakukera wewe unamjua Mungu sawasawa na Mungu awalaani wanofanya hivo.Unauhakika gani Mungu hataanza na wewe unayejiona mwema
 
Nasoma huu uzi, lakin akili inagoma kabisa kuamin, si ungeenda kuwaambia wanaofanya hivyo ili wakupe sababu za wao kufanya hivyo halafu mwisho wa siku unakuja hapa jukwaan kutupa somo, sio kulaan huku hujafanya hata research ndogo
 
Kwanza tungeelewa kwann sadaka?
Mungu hana shida na coin wala noti ya muumini, lkn kanisa kama taasisi inahitaji pesa kwa ajili ya kujiendesha kwnye mambo mbali mbali, kwa hiyo unachikitoa kanisani ni msaada km ilivyo misaada mingine hivyo hupangiwi utoe kiasi gani.
 
Mwenye Afya haitaji Daktari, hao wenzio wapo mahali sahihi, ilibidi uwaombee Mungu awabadilishe izo tabia,. Mkristo WEWE unapataje nguvu yakuwaombea wenzio walaaniwe??.Jitoe kwanza kibanzi kilichopo jichoni mwako Ndio upate uwezo wakumtoa mwenzio Boriti jichoni mwake. Namba saba inaonesha kuwa WEWE pia unatatizo Ndio mana Ukaliona hilo la Namba nne.
 
Si wamelazimishwa kusali.. Kwani ukristo umeandikwa na nani na tuwekee masharti ya Mungu yanasemaje.
 
Wataacha wewe utakapoacha upuuzi wa kufuatilia watu Kanisani na kuacha kumsikiliza Mungu.
Unataka kufikiri kila aliyepo kanisani ni mtakatifu au ni lazima iwe hivyo na lama ndivyo mbona shetani hujihudhutisha nao mara kwa mara?
 
Yesu kasema usihukumu usije na wew ukahumiwa,,

Hiyo kazi uliyofanya ya kutafuta makosa ya wenzio mule Ibadani haikuwa yako bali ni yake mwenyewe Mungu Baba,,
 
Wasamehe saba mara sabiini imekushinda!!
 
Back
Top Bottom