Wakristo hawahitaji Sensa kujua idadi Yao. Kwa sababu Ukristo wenyewe ni Hesabu

Status
Not open for further replies.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,901
WAKRISTO HAWAHITAJI SENSA KUJUA IDADI YAO. KWA SABABU UKRISTO WENYEWE NI HESABU.

Anaandika, Robert Heriel.
Mtibeli.

Moja ya mafundisho makuu katika Ukristo ni fundisho la Hesabu. Ukristo hauwezi kukamilika bila hesabu Kwa sababu hesabu ni sehemu ya Ukristo.
Jukumu kuu la Ukristo Duniani ni Utume wa kuwafanya Watu kuwa Wanafunzi wa Kristo. Utume(mission) ili ifanyike lazima hesabu ihusike ili mipango ikamilike.

Hii ni kusema kuwa Mkristo ni kuwa mtu wa mipango(utume au mmishenari).

Wakristo Kabla hawajaistablish Kanisa lazima wazingatie mambo kadhaa katika uanzishaji wa kanisa Lao. Mojawapo ni idadi ya Watu wa eneo husika, Tabia zao, maliasili kama maji, ardhi na tabia ya nchi. Hayo ni mambo ya msingi kwao.

Kwenye Ukristo kuna Imani na ushirika.
Ukristo ni ujasusi Kwa sababu taarifa za Watu na jamii kwenye Ukristo ni Jambo kubwa ambalo kanisa lazima liwe nazo.

Ibada zinaendeshwa Kwa mahesabu. Lazima kila atakayefika ijulikane amefika. Idadi ya Watu waliofika ichukuliwe. Na kama kuna Wageni watambulike kuwa wamefika Wageni wangapi. Hiyo huwa direct au indirect way.

Kila dhehebu la Kikristo linajua idadi ya waumini wake kuanzia ngazi ya familia mpaka Ulimwengu. Kwa sababu ni lazima ukiwa MTU wa dhehebu Fulani lazima usajiliwe na upewe ushirika.
Hata usipoenda Kanisani, kanisa linajua kabisa kwenye familia ya Fulani kuna Watu kadhaa na watatu sio Watu wa kuja Kanisani.

Ukristo Kwa vile misheni yake kuu NI kuongeza idadi ya Wanafunzi wa Kristo hivyo inajukumu la kujua kila Mwaka imepata ongezeko la Watu Kwa kiwango gani.

Wakristo hawajisikii vibaya pale Mkristo mwenzako akibadili dhehebu na kuhamia dhehebu jingine la Ukristo. Watalalamika lakini wanajua fika kuwa ni mti mmoja Ila matawi tofauti.

Ukristo hautegemei Sensa kujua idadi ya waumini wake na wananchi wa taifa husika.

Wakristo sio kama Dini zingine. Wao wapo in details zaidi kuliko Watu wa dini zingine.
Waposema kuwa Wakristo wapo kiasi Fulani wanamaanisha Kwa sababu wanataratibu na mifumo ya kitakwimu ya kuhesabu Watu wao. Kisha wanaona kazi waliyobakiwa nayo kuwabadilisha wengine ni kiasi gani.

Faida kubwa ya Ukristo ni kuongeza idadi ya Watu. Hiyo ndio faida namba moja. Kupitia Watu ni rahisi kuifanya jamii uishi Maisha ya Kristo ikiwa ni pamoja na upendo, neema na Wokovu.
Faida ndogo ndogo ni pamoja na biashara za kuchukua sadaka na zaka lakini pia kutoa Ajira Baada ya kuanzisha Huduma za kijamii kama Huduma za afya, elimu, kifedha n.k.

Wakristo wanamifumo ya kusomesha Watumishi wao katika ngazi za Elimu mbalimbali Kwa kuwadhamini na kuwatolea Pesa za Ada, accommodation n.k.

Ukristo ni Mungu pamoja na wanadamu.
Ukristo hauishii kwenye Ufalme wa mbinguni tuu bali ni kuushusha Ufalme WA mbinguni Duniani. Hivyo kusoma, kukusanya Mali za Ulimwengu na kumpokea Mungu vyote vinaenda sambamba.

Kristo alipewa mamlaka mbinguni na Duniani hicho ndicho Wakristo wanahangaika nacho yaani kuwa na Mamlaka mbinguni na Duniani. Jambo Hilo litawezekana na limewezekana Kutokana na hesabu, mipango na mikakati ya muda mrefu.

Ukristo ukiwatazama ni kama wapo tofauti tofauti lakini Kwa ndani ni kitu kimoja. Lakini madhehebu mengine ukiyatizama ni kama wapo pamoja lakini Kwa ndani wametengana.

Wakristo wakienda kwenye misheni huwekeana majukumu, maeneo ya kiutume, hivyo sio rahisi wao kugombana.
Kama Wakatoliki watapita ukanda huu basi Wa-KKKT watapita upande mwingine. Au Wasabato watapita upande mwingine.
Alafu watakuja Walokole wao watapiga Jambi popote huku wakijifanya wapiga kelele na wanamageuzi ya Kikristo. Lakini ukichimba Kwa ndani mizizi Yao imetoka sehemu moja.

Wakristo wanavumiliana Kwa sababu wanajua wanajenga nyumba moja. Na kusudi Lao ni lilelile ambalo ni kuongeza namba za idadi ya Wakristo.

Kuwashinda Wakristo ni Jambo lisilowezekana Kwa sababu wao ni Watu wenye mahesabu. Wanaotumia zaidi mipango na mikakati. Na mara zote Wana fanya kazi Kwa utulivu in passive ways. Hawana fujo lakini haimaanishi hawawezi kufanya fujo indirect way.

Sisi Watibeli tunambinu za kukabiliana na Wakristo Kwa sababu Wakristo ni moja ya Watoto wetu tuliowazaa wenyewe.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom