Wachungaji wa Kilokole hamuoni hili?

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,488
19,286
Naomba kuongea na wachungaji wa kilokole hapa, nadhani hii itapunguza na makelele ya watu kulalamika kuwa mnapiga mno kelele kwenye makanisa yenu. kuna tabia mnazifumbia macho ila sio za Kimungu zimeenea sana makanisani. Mimi ninayeongea ni mlokole, sio wa mitume na manabii, hao huwa nawahesabu ni matapeli na wezi. mimi nimeokoka na ninasali kanisa la kipentecost. tunaingia mwaka mpya, naomba Mungu atusaidie, atusamehe pale tulipokosea, atuoshe kwa Damu yake, tuishi maisha matakatifu, tuache kupoteza muda, tuukomboe wakati kwasababu muda tuliobaki nao ni mchache sana, Yesu Kristo yuaja kulichukua kanisa lake. angalia usijecheleweshwa na mambo ya dunia, ukaachwa.

Kwanza niwapongeze watu wote waliookoka, kwasababu wamechagua fungu lililo jema, ukiokoka wewe ni mtoto wa Mungu, wakati wale ambao hawajaokoka wao ni wana wa Mungu. wewe hata ukikosea, utashughulikiwa kama mtoto wa nyumbani, tofauti na mwana ambaye hakai nyumbani. Yesu Kristo ni advocate wetu kwa kupitia Damu yake, Damu yake inanena mema kwa wale waliompokea. ninyi ambao hamjampokea, hamna mwombezi/advocate, hamna Damu ya kuwaokoa, mtajiokoa wenyewe na hamtaweza. hivyo kwa hiki nitakachokiandika hapa msifikiri nawasema walokole hapana, hawa ni heri kuliko ninyi msiookoka, nataka kuwajenga tu ili waendelee na wokovu. nanyi msiookoka nawakaribisha kwa Bwana katika Mwaka hu mpya, anza na Bwana, ishi na Bwana. hakuna aliyemkimbilia akaaibika.

1. KUSIFU NA KUABUDU: kipindi hiki, mnakiweka cha muda mfupi sana, kuna dakika chache za kusifu, na dakika chache zaidi za kuabudu. kwenye kusifu mnatuwekea vijana wahuni wanaotupotezea muda, mtu umeacha kazi zako unaenda kusali unafika pale kakijana kanavaa kisharobaro kahuni tu mnakaweka pale kaabudishe, ibada inakuwa kavu tunarudi hivyo hivyo. tunataka wale mnaotuletea kusifu na kuabudu wawe wamejiandaa, wamefunga, wameutafuta uso wa Mungu akisimama pale Nguvu za Mungu ziwepo, hatuji kanisani kukutana na ninyi, tunakuja kukutana na Nguvu za MUngu.

2. AINA ZA NYIMBO: Biblia inasema "wala msiifuatishe namna ya dunia hii"..vijana mnaotuwekea kutuabudishia au kusifu na kuabudu, wanacopy namna ya nyimbo za duniani wanaleta huku, wanabadilisha maneno tu, wanacopy namna ya kucheza duniani wanaleta madhabahuni. wapo vijana madhabahuni wanacheza sebene, ndomboro, wengine wanacheza kama Diamond na hamonize kabisa, vilevile. na aina hiyo ya uchezaji ikianza, utakuta wanawake wengi wameinuka wanacheza kama wapo disco, ni kama wameamsha lile shetani la disco walilokuwa nalo zamani, wanakumbushia na kutoa stress pale, na wanaamini wanamchezea Mungu. huu ni uhuni na Mungu hawezi kuonekana mazingira hayo. Ina maana Roho Mtakatifu ameshindwa kuwatafutia tyuni, au maneno ya kuweka kwenye wimbo, au namna ya kucheza? hadi muige uchezaji na lafudhi za kina Diamond? kweli? aokoaye ni Mungu wala sio uwezo wenu wa kucheza au kuimba, kama uimbaji wenu au uchezaji wenu hauna Mungu ni kujilisha upepo.

3. MAHUBIRI: mnatumia muda mchache wa kuhubiri, muda mwingi mnautumia kwenye matangazo na michango. kama hamjui, ukihubiri kwa Nguvu za Mungu hauhitaji kutangaza tangazo la michango au kuhudhuria ibada za katikati kwa nguvu, watu wenyewe watajiongoza kwasababu wameona kuna Mungu. kama hakuna Mungu ndio mtakamuanaaa hadi michango midogo tu. nawashauri tafuteni Mungu, Mtafuteni MUngu na Nguvu zake, mkifanikiwa kwenye hilo vingine hivyo ni vitu vidogo sana mkiwa na Mungu.pia tumeacha shughuli zetu mfano jumapili, tumeiweka wakfu kwa ajili ya Mungu, mnaweka ibada fupi mnataka twende wapi, mnakimbilia wapi, wiki nzima tupo bise, tunataka kuabudu hadi stress zote zitoke, na mtufundishe hadi tuchoke. Roho aongoze, sio ratiba zenu. hatutaki kuabudu dini, tunataka kumwona Mungu halisi wa kitabu cha Matendo ya Mitume.

4. KUABUDU: wafundisheni watu wenu kwamba, Mungu hapatikani wakati unapopayukapayuka, Mungu anapatikana kwenye utulivu, basi hata kama unaimba kwa nguvu basi uwe wimbo wa kuabudu mzuri, sio mandombolo na masebene ya kicongo hapa. hayo manyimbo ya kicongo mnaimba kwa kunengua viuno utafikiri mnazini, mnaruka kimasai nini na nini sijui, wala Mungu hapatikani. Mungu hupatikana kwenye utulivu, hapo ndipo mahali pa siri yaani ndaniii kule rohoni sio huku mwilini unaruka kwa kutumia ugali. hata wale ambao walishawahi kumwona Mungu maishani mwao, ni wale waliofanya maombi ya kufunga mfano, wakasoma Neno la Mungu na kutafakari, wakaingia chumbani, wakafung amlango, wakafunga simu na kila kitu, wakamwabudu Mungu kidogo, wakaingia kwenye kuomba then kutafakari kwa ndaniiiii kwenye ulimwengu wa Roho, hapo ndipo Roho Mtakatifu mwenyewe huamua kuomba kwa kukusadia wewe ndani yako. Maombi pekee yenye uhakika wa kujibiwa ni Maombi ya Roho, ya kimwili hayana uhakika. wengi mtasema mbona tukiwa tupo semina au maombi ya wengi Roho Mtakatifu huwa anashuka, ndio anaweza kushuka yeye hapangiwi hana sheria atashuka wakati wowote na popote, ila mimi nilikuwa nashauri wale ambao wamepanga kwamba nataka kuongea na Mungu na Mungu aongee na mimi kabisa, hilo ni mara chache linatokea kwenye jumuiya, na hao wanaonena public kwenye jumuia wengine ni mapepo though weingine pia ni wananena kwa Roho.

DAUDI ALICHEZA HADI NGUO ZIKADONDOKA; wengi wanachukua mstari huu wakisema hata watu makanisani wacheze kwa namna zozote zile kwasababu Daudi alifanya hivyo. Ukiangalia, utakuta kwa desturi za kipindi kile, hata Daudi alikosea ndio maana watu walimshangaa, imekuwaje, na pia wale walikuwa wanaabudu Mungu kimwili, sisi tunaabudu kiroho, leteni nyimbo tulivu za kuabudu na waabudishaji wasiwe wadhaifu wa imani/wazinzi na ambao hawajajiandaa, hawatatusaidia. na nyimbo hizo za kuabudu ziwe muda mrefu watu wazame, sio mnaimbisha kidogo tu kama mnafukuzwa na nini sijui, tayari mmeshasimama mnaleta neno kidogo tu ibada imeisha. jaribuni kuweka nyimbo za staha kwa muda mrefu, hivi tukiabudu hata kwa masaa mawili au hata matatu watu wanazama tu Mungu hatashuka? au mnataka Mungu asiwe anashuka tunaabudu kwa kulipua na mchungaji umekaa hapo unasubiri sadaka. ndio maana wanatoa kidogo. hata kama Biblia inasema tunaweza kucheza tunapomsifu Mungu (Zaburi 149:3) haimaanishi tucheze kama kina awilo, kunengua viuno kuigiza kuzini hadi watu wanaamshana hisia au kuifuata dancing ya kidunia hii.

5. UJAZO WA ROHO MTAKATIFU: Uzima wa kanisa ni Roho Mtakatifu, Yesu alisema siwezi kuwaacha peke yenu, nitawaachia msaidizi, huyo Roho atokaye kwa Baba, ndiye anayetutia kwenye kweli yote. huyu ndiye Roho anayetusaidia kuomba, analia Aba yaani Baba, kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, na yeye anaijua nia ya roho na hutusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ukiomba kwa akili utaomba kwa kuomba mahitaji ya mwili bila hata kujua impact yake, unaomba gari kumbe hujui kama gari hiyo inaweza kukuua mwenyewe, ila ukiomba kwa Roho utaomba kwa yale tu yaliyo mapenzi ya Mungu. ni furaha kubwa namna gani kuomba na kupata yale tu yaliyo mapenzi ya Mungu, kuliko yale yaliyo mapenzi yetu sisi wanadamu! hivyo, HAMASISHENI WATU WENU WAJAZWE ROHO, hapo ndipo mtakuwa na kanisa. bila Roho mtakatifu hata maombi yatakuwa mzigo, kutoa sadaka na michango au kuinjilisti itakuwa mzigo, ila wakiwa na Roho Mtakatifu watafanay bila kuambiwa na ninyi, Roho atawaongoza tena maeneo sahihi. waambieni wafunge, wasome Neno, watafute uso wa Mungu na kuacha njia mbaya hadi pale watakapojazwa na kutembea na Roho Mtakatifu, hao ndio wakristo hai. wengine wote ni mizigo na mtakuwa mnaogoza watu ambao hamna uhakika kama wataenda mbinguni, kwasababu wale wenye Roho tu ndio watu wa Mungu. na Yesu atakapokuja kunyakua atanyakua wale wenye Roho tu, wasio na Roho wa Mungu hatawanyakua. WALAKINI AWAYE YOTE ASIPOKUWA NA HUYO ROHO WA KRISTO, HUYO SIO WAKE. mkristo yeyote ambaye hana Roho Mtakatifu, huyo hana Mungu, na kuwepo kwa Roho hat akama wengi mnajifariji kwamba unaweza kuwa naye bila kunena, ila aliye naye anajijua anaye, na kunena ni ishara ya udhihirisho. ukienda kanisa ukaona mwezi wa kwanza, wapili hawahubiri na kuhamasisha ujazo wa Roho Mtakatifu, hapo kimbia, hakuna Mungu, kuna dini. msingi wa kwanza wa mpentecost ni ujazo wa Roho tena kunena kwa lugha kama kitabu cha matendo ya mitume. na ndilo agizo la Yesu.

6. SEMINA NA MAFUNDISHO; mnazidiwa na manabii na mitume wa uongo wanaouza mafuta kwasababu hamfundishi Neno, wekeni semina, fundisheni watu, na wakati unafundisha, usiende iviivi, jiandae kiroho ili ukiwa pale usihubiri wewe, bali Roho aongee kupitia wewe, hayo ndio mahubiri na mafundisho yanayookoa, elimu yenu ya chuo haiokoi, hata kama mmesoma theologia hadi PHD. ila tone moja tu la Roho wa Bwana linatosha kubadilisha Roho. Roho Mtakatifu ni mhuri, akikufikia tu ni kama amekupiga mhuri, kama ni wimbo au Neno hilo utalikumbuka. au kama ndoto kama ni ya Kimungu utaona ni kama umepigwa mhuri, hautaisahau. maishani mwangu kuna ndogo na maono niliyaona miaka 20 iliyopita, ila hadi sasa nakumbuka kila kitu ni kama nimeota au kuona jana. huyo ndiye Mungu. na huwezi kusema labda havikutoka kwa Mungu, Nooo, msidanganyike, labda kama haujawahi kukutana na Mungu au kusikia sauti yake, Yesu alisema Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nao wanifuata. akija mwizi wakiita kondoo wanajua huyo sio mchungaji, ila akija mchungaji akiita sauti moja tu unajua huyo ndiye. ndivyo ilivyo, Mungu anajulikana kwetu kama tumejitoa kwake.

nimetoa haya machache, wengine watasema kwanini nimetolea hapa naaibisha kanisa, hapana, nimeona bora niweke hapa ili ifikie wachungaji wengi, kwasababu wapo humu. Mungu aliokoe kanisa lake.
 
DAUDI ALICHEZA HADI NGUO ZIKADONDOKA; wengi wanachukua mstari huu wakisema hata watu makanisani wacheze kwa namna zozote zile kwasababu Daudi alifanya hivyo. Ukiangalia, utakuta kwa desturi za kipindi kile, hata Daudi alikosea ndio maana watu walimshangaa, imekuwaje, na pia wale walikuwa wanaabudu Mungu kimwili, sisi tunaabudu kiroho, leteni nyimbo tulivu za kuabudu na waabudishaji wasiwe wadhaifu wa imani/wazinzi na ambao hawajajiandaa, hawatatusaidia. na nyimbo hizo za kuabudu ziwe muda mrefu watu wazame, sio mnaimbisha kidogo tu kama mnafukuzwa na nini sijui, tayari mmeshasimama mnaleta neno kidogo tu ibada imeisha. jaribuni kuweka nyimbo za staha kwa muda mrefu, hivi tukiabudu hata kwa masaa mawili au hata matatu watu wanazama tu Mungu hatashuka? au mnataka Mungu asiwe anashuka tunaabudu kwa kulipua na mchungaji umekaa hapo unasubiri sadaka. ndio maana wanatoa kidogo.

5. UJAZO WA ROHO MTAKATIFU: Uzima wa kanisa ni Roho Mtakatifu, Yesu alisema siwezi kuwaacha peke yenu, nitawaachia msaidizi, huyo Roho atokaye kwa Baba, ndiye anayetutia kwenye kweli yote. huyu ndiye Roho anayetusaidia kuomba, analia Aba yaani Baba, kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, na yeye anaijua nia ya roho na hutusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ukiomba kwa akili utaomba kwa kuomba mahitaji ya mwili bila hata kujua impact yake, unaomba gari kumbe hujui kama gari hiyo inaweza kukuua mwenyewe, ila ukiomba kwa Roho utaomba kwa yale tu yaliyo mapenzi ya Mungu. ni furaha kubwa namna gani kuomba na kupata yale tu yaliyo mapenzi ya Mungu, kuliko yale yaliyo mapenzi yetu sisi wanadamu! hivyo, HAMASISHENI WATU WENU WAJAZWE ROHO, hapo ndipo mtakuwa na kanisa. bila Roho mtakatifu hata maombi yatakuwa mzigo, kutoa sadaka na michango au kuinjilisti itakuwa mzigo, ila wakiwa na Roho Mtakatifu watafanay bila kuambiwa na ninyi, Roho atawaongoza tena maeneo sahihi. waambieni wafunge, wasome Neno, watafute uso wa Mungu na kuacha njia mbaya hadi pale watakapojazwa na kutembea na Roho Mtakatifu, hao ndio wakristo hai. wengine wote ni mizigo na mtakuwa mnaogoza watu ambao hamna uhakika kama wataenda mbinguni, kwasababu wale wenye Roho tu ndio watu wa Mungu. na Yesu atakapokuja kunyakua atanyakua wale wenye Roho tu, wasio na Roho wa Mungu hatawanyakua. WALAKINI AWAYE YOTE ASIPOKUWA NA HUYO ROHO WA KRISTO, HUYO SIO WAKE. mkristo yeyote ambaye hana Roho Mtakatifu, huyo hana Mungu, na kuwepo kwa Roho hat akama wengi mnajifariji kwamba unaweza kuwa naye bila kunena, ila aliye naye anajijua anaye, na kunena ni ishara ya udhihirisho. ukienda kanisa ukaona mwezi wa kwanza, wapili hawahubiri na kuhamasisha ujazo wa Roho Mtakatifu, hapo kimbia, hakuna Mungu, kuna dini. msingi wa kwanza wa mpentecost ni ujazo wa Roho tena kunena kwa lugha kama kitabu cha matendo ya mitume. na ndilo agizo la Yesu.

6. SEMINA NA MAFUNDISHO; mnazidiwa na manabii na mitume wa uongo wanaouza mafuta kwasababu hamfundishi Neno, wekeni semina, fundisheni watu, na wakati unafundisha, usiende iviivi, jiandae kiroho ili ukiwa pale usihubiri wewe, bali Roho aongee kupitia wewe, hayo ndio mahubiri na mafundisho yanayookoa, elimu yenu ya chuo haiokoi, hata kama mmesoma theologia hadi PHD. ila tone moja tu la Roho wa Bwana linatosha kubadilisha Roho. Roho Mtakatifu ni mhuri, akikufikia tu ni kama amekupiga mhuri, kama ni wimbo au Neno hilo utalikumbuka. au kama ndoto kama ni ya Kimungu utaona ni kama umepigwa mhuri, hautaisahau. maishani mwangu kuna ndogo na maono niliyaona miaka 20 iliyopita, ila hadi sasa nakumbuka kila kitu ni kama nimeota au kuona jana. huyo ndiye Mungu. na huwezi kusema labda havikutoka kwa Mungu, Nooo, msidanganyike, labda kama haujawahi kukutana na Mungu au kusikia sauti yake, Yesu alisema Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nao wanifuata. akija mwizi wakiita kondoo wanajua huyo sio mchungaji, ila akija mchungaji akiita sauti moja tu unajua huyo ndiye. ndivyo ilivyo, Mungu anajulikana kwetu kama tumejitoa kwake.

nimetoa haya machache, wengine watasema kwanini nimetolea hapa naaibisha kanisa, hapana, nimeona bora niweke hapa ili ifikie wachungaji wengi, kwasababu wapo humu. Mungu aliokoe kanisa lake.
Una hoja.
 
Urokole ni uzezeta mpya hapa duniani

Makanisa yote ya kirokole yananuka uzinzi kuanzia kwa wachungaji mpaka kwa waumini.
sikubaliani na wewe, walokole sio malaika, na wengi wanaokoka lakini bado wachanga wa imani kama walivyo watoto tu wanaweza kucheza na matope kwasababu ya uchanga wa imani ila haimaanishi sio watoto wako. walokole wanazini, ila sio kwa hali ya juu kama wengine. ni chuki zako tu. pia, hiyo kauli kwamba ulokole ni uzezeta, unataka wawe wakatoliki? wawe watu gani sasa? wawe wafuasi wa papa? wasali kwa litulgia kwa kusoma vitabu na kuomba kwa maria? unataka wasalije? kuna siku utawatafuta walau wakuombee ila hutawapata, Mungu akurehemu na kukusaidia.
 
Yani unakaa unamtazama muhubiri pale mbele anacho kizungumza mpaka unakufuru kwa kujiwazia "hiv hiki ndio kilichonileta hapa leo au??"
 
Ni muhimu wachungaji waamke na wawe serious. Mimi cha kwanza ambacho ni kero, ni pale kipindi cha kusifu na kuabudu kinaanza, afu kanapanda kakijana fulani hivi, kwasababu tu ni katoto ka mchungaji au ndugu au kamaarufu, hakajajiandaa kiroho kuabudisha au kusifu, kanaanza kutuletea manyimbo ya kucheza kwa kunengua na step za watu wa duniani, na kanasisistiza cheza cheza umchezee Mungu, utafikiri kanamjua Mungu vizuri. na mchungaji yupo anawaangalia tu. wananengua viuno, wanaruka kama wanacheza bongoflavour, manyimbo makavuuu, hivi kweli nimepoteza muda wangu wote niende pale niabudu Mungu roho isuuzike, afu nakutana na kitu cha ajabu, wanatuchukuliaje lakini? kwenye mahubiri, ukiona umegombana na mkeo, mpe mtu mwingine ahubiri, pia usihubiri kwa akili yako, jiandae ili Roho wa Mungu akutumie kama chombo, kukona siku hio haupo kiroho mpe mwingine ahubiri au alika hata mchungaji mwenzio tu kuliko kutupotezea muda.
 
yaani wakianza kucheza na kunengua viuno utafikiri wamepagawa na mapepo ya ngono. jirekebisheni nyie vijana, sio wote tuliokuja kanisani tuna utoto kama ninyi. jueni kwenye congragation kuna watu wazima na heshima zao na wapo pale sio kwenye show, wapo kutafuta uso wa Mungu, dunia hii wameshaiishi wameichoka kwasababu wamepita kila angle, sio ninyhi mpo kanisani na bado mnaitaka dunia hii.
 
Naomba kuongea na wachungaji wa kilokole hapa, nadhani hii itapunguza na makelele ya watu kulalamika kuwa mnapiga mno kelele kwenye makanisa yenu. kuna tabia mnazifumbia macho ila sio za Kimungu zimeenea sana makanisani. Mimi ninayeongea ni mlokole, sio wa mitume na manabii, hao huwa nawahesabu ni matapeli na wezi. mimi nimeokoka na ninasali kanisa la kipentecost. tunaingia mwaka mpya, naomba Mungu atusaidie, atusamehe pale tulipokosea, atuoshe kwa Damu yake, tuishi maisha matakatifu, tuache kupoteza muda, tuukomboe wakati kwasababu muda tuliobaki nao ni mchache sana, Yesu Kristo yuaja kulichukua kanisa lake. angalia usijecheleweshwa na mambo ya dunia, ukaachwa.

Kwanza niwapongeze watu wote waliookoka, kwasababu wamechagua fungu lililo jema, ukiokoka wewe ni mtoto wa Mungu, wakati wale ambao hawajaokoka wao ni wana wa Mungu. wewe hata ukikosea, utashughulikiwa kama mtoto wa nyumbani, tofauti na mwana ambaye hakai nyumbani. Yesu Kristo ni advocate wetu kwa kupitia Damu yake, Damu yake inanena mema kwa wale waliompokea. ninyi ambao hamjampokea, hamna mwombezi/advocate, hamna Damu ya kuwaokoa, mtajiokoa wenyewe na hamtaweza. hivyo kwa hiki nitakachokiandika hapa msifikiri nawasema walokole hapana, hawa ni heri kuliko ninyi msiookoka, nataka kuwajenga tu ili waendelee na wokovu. nanyi msiookoka nawakaribisha kwa Bwana katika Mwaka hu mpya, anza na Bwana, ishi na Bwana. hakuna aliyemkimbilia akaaibika.

1. KUSIFU NA KUABUDU: kipindi hiki, mnakiweka cha muda mfupi sana, kuna dakika chache za kusifu, na dakika chache zaidi za kuabudu. kwenye kusifu mnatuwekea vijana wahuni wanaotupotezea muda, mtu umeacha kazi zako unaenda kusali unafika pale kakijana kanavaa kisharobaro kahuni tu mnakaweka pale kaabudishe, ibada inakuwa kavu tunarudi hivyo hivyo. tunataka wale mnaotuletea kusifu na kuabudu wawe wamejiandaa, wamefunga, wameutafuta uso wa Mungu akisimama pale Nguvu za Mungu ziwepo, hatuji kanisani kukutana na ninyi, tunakuja kukutana na Nguvu za MUngu.

2. AINA ZA NYIMBO: Biblia inasema "wala msiifuatishe namna ya dunia hii"..vijana mnaotuwekea kutuabudishia au kusifu na kuabudu, wanacopy namna ya nyimbo za duniani wanaleta huku, wanabadilisha maneno tu, wanacopy namna ya kucheza duniani wanaleta madhabahuni. wapo vijana madhabahuni wanacheza sebene, ndomboro, wengine wanacheza kama Diamond na hamonize kabisa, vilevile. na aina hiyo ya uchezaji ikianza, utakuta wanawake wengi wameinuka wanacheza kama wapo disco, ni kama wameamsha lile shetani la disco walilokuwa nalo zamani, wanakumbushia na kutoa stress pale, na wanaamini wanamchezea Mungu. huu ni uhuni na Mungu hawezi kuonekana mazingira hayo. Ina maana Roho Mtakatifu ameshindwa kuwatafutia tyuni, au maneno ya kuweka kwenye wimbo, au namna ya kucheza? hadi muige uchezaji na lafudhi za kina Diamond? kweli? aokoaye ni Mungu wala sio uwezo wenu wa kucheza au kuimba, kama uimbaji wenu au uchezaji wenu hauna Mungu ni kujilisha upepo.

3. MAHUBIRI: mnatumia muda mchache wa kuhubiri, muda mwingi mnautumia kwenye matangazo na michango. kama hamjui, ukihubiri kwa Nguvu za Mungu hauhitaji kutangaza tangazo la michango au kuhudhuria ibada za katikati kwa nguvu, watu wenyewe watajiongoza kwasababu wameona kuna Mungu. kama hakuna Mungu ndio mtakamuanaaa hadi michango midogo tu. nawashauri tafuteni Mungu, Mtafuteni MUngu na Nguvu zake, mkifanikiwa kwenye hilo vingine hivyo ni vitu vidogo sana mkiwa na Mungu.pia tumeacha shughuli zetu mfano jumapili, tumeiweka wakfu kwa ajili ya Mungu, mnaweka ibada fupi mnataka twende wapi, mnakimbilia wapi, wiki nzima tupo bise, tunataka kuabudu hadi stress zote zitoke, na mtufundishe hadi tuchoke. Roho aongoze, sio ratiba zenu. hatutaki kuabudu dini, tunataka kumwona Mungu halisi wa kitabu cha Matendo ya Mitume.

4. KUABUDU: wafundisheni watu wenu kwamba, Mungu hapatikani wakati unapopayukapayuka, Mungu anapatikana kwenye utulivu, basi hata kama unaimba kwa nguvu basi uwe wimbo wa kuabudu mzuri, sio mandombolo na masebene ya kicongo hapa. hayo manyimbo ya kicongo mnaimba kwa kunengua viuno utafikiri mnazini, mnaruka kimasai nini na nini sijui, wala Mungu hapatikani. Mungu hupatikana kwenye utulivu, hapo ndipo mahali pa siri yaani ndaniii kule rohoni sio huku mwilini unaruka kwa kutumia ugali. hata wale ambao walishawahi kumwona Mungu maishani mwao, ni wale waliofanya maombi ya kufunga mfano, wakasoma Neno la Mungu na kutafakari, wakaingia chumbani, wakafung amlango, wakafunga simu na kila kitu, wakamwabudu Mungu kidogo, wakaingia kwenye kuomba then kutafakari kwa ndaniiiii kwenye ulimwengu wa Roho, hapo ndipo Roho Mtakatifu mwenyewe huamua kuomba kwa kukusadia wewe ndani yako. Maombi pekee yenye uhakika wa kujibiwa ni Maombi ya Roho, ya kimwili hayana uhakika. wengi mtasema mbona tukiwa tupo semina au maombi ya wengi Roho Mtakatifu huwa anashuka, ndio anaweza kushuka yeye hapangiwi hana sheria atashuka wakati wowote na popote, ila mimi nilikuwa nashauri wale ambao wamepanga kwamba nataka kuongea na Mungu na Mungu aongee na mimi kabisa, hilo ni mara chache linatokea kwenye jumuiya, na hao wanaonena public kwenye jumuia wengine ni mapepo though weingine pia ni wananena kwa Roho.

DAUDI ALICHEZA HADI NGUO ZIKADONDOKA; wengi wanachukua mstari huu wakisema hata watu makanisani wacheze kwa namna zozote zile kwasababu Daudi alifanya hivyo. Ukiangalia, utakuta kwa desturi za kipindi kile, hata Daudi alikosea ndio maana watu walimshangaa, imekuwaje, na pia wale walikuwa wanaabudu Mungu kimwili, sisi tunaabudu kiroho, leteni nyimbo tulivu za kuabudu na waabudishaji wasiwe wadhaifu wa imani/wazinzi na ambao hawajajiandaa, hawatatusaidia. na nyimbo hizo za kuabudu ziwe muda mrefu watu wazame, sio mnaimbisha kidogo tu kama mnafukuzwa na nini sijui, tayari mmeshasimama mnaleta neno kidogo tu ibada imeisha. jaribuni kuweka nyimbo za staha kwa muda mrefu, hivi tukiabudu hata kwa masaa mawili au hata matatu watu wanazama tu Mungu hatashuka? au mnataka Mungu asiwe anashuka tunaabudu kwa kulipua na mchungaji umekaa hapo unasubiri sadaka. ndio maana wanatoa kidogo. hata kama Biblia inasema tunaweza kucheza tunapomsifu Mungu (Zaburi 149:3) haimaanishi tucheze kama kina awilo, kunengua viuno kuigiza kuzini hadi watu wanaamshana hisia au kuifuata dancing ya kidunia hii.

5. UJAZO WA ROHO MTAKATIFU: Uzima wa kanisa ni Roho Mtakatifu, Yesu alisema siwezi kuwaacha peke yenu, nitawaachia msaidizi, huyo Roho atokaye kwa Baba, ndiye anayetutia kwenye kweli yote. huyu ndiye Roho anayetusaidia kuomba, analia Aba yaani Baba, kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, na yeye anaijua nia ya roho na hutusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ukiomba kwa akili utaomba kwa kuomba mahitaji ya mwili bila hata kujua impact yake, unaomba gari kumbe hujui kama gari hiyo inaweza kukuua mwenyewe, ila ukiomba kwa Roho utaomba kwa yale tu yaliyo mapenzi ya Mungu. ni furaha kubwa namna gani kuomba na kupata yale tu yaliyo mapenzi ya Mungu, kuliko yale yaliyo mapenzi yetu sisi wanadamu! hivyo, HAMASISHENI WATU WENU WAJAZWE ROHO, hapo ndipo mtakuwa na kanisa. bila Roho mtakatifu hata maombi yatakuwa mzigo, kutoa sadaka na michango au kuinjilisti itakuwa mzigo, ila wakiwa na Roho Mtakatifu watafanay bila kuambiwa na ninyi, Roho atawaongoza tena maeneo sahihi. waambieni wafunge, wasome Neno, watafute uso wa Mungu na kuacha njia mbaya hadi pale watakapojazwa na kutembea na Roho Mtakatifu, hao ndio wakristo hai. wengine wote ni mizigo na mtakuwa mnaogoza watu ambao hamna uhakika kama wataenda mbinguni, kwasababu wale wenye Roho tu ndio watu wa Mungu. na Yesu atakapokuja kunyakua atanyakua wale wenye Roho tu, wasio na Roho wa Mungu hatawanyakua. WALAKINI AWAYE YOTE ASIPOKUWA NA HUYO ROHO WA KRISTO, HUYO SIO WAKE. mkristo yeyote ambaye hana Roho Mtakatifu, huyo hana Mungu, na kuwepo kwa Roho hat akama wengi mnajifariji kwamba unaweza kuwa naye bila kunena, ila aliye naye anajijua anaye, na kunena ni ishara ya udhihirisho. ukienda kanisa ukaona mwezi wa kwanza, wapili hawahubiri na kuhamasisha ujazo wa Roho Mtakatifu, hapo kimbia, hakuna Mungu, kuna dini. msingi wa kwanza wa mpentecost ni ujazo wa Roho tena kunena kwa lugha kama kitabu cha matendo ya mitume. na ndilo agizo la Yesu.

6. SEMINA NA MAFUNDISHO; mnazidiwa na manabii na mitume wa uongo wanaouza mafuta kwasababu hamfundishi Neno, wekeni semina, fundisheni watu, na wakati unafundisha, usiende iviivi, jiandae kiroho ili ukiwa pale usihubiri wewe, bali Roho aongee kupitia wewe, hayo ndio mahubiri na mafundisho yanayookoa, elimu yenu ya chuo haiokoi, hata kama mmesoma theologia hadi PHD. ila tone moja tu la Roho wa Bwana linatosha kubadilisha Roho. Roho Mtakatifu ni mhuri, akikufikia tu ni kama amekupiga mhuri, kama ni wimbo au Neno hilo utalikumbuka. au kama ndoto kama ni ya Kimungu utaona ni kama umepigwa mhuri, hautaisahau. maishani mwangu kuna ndogo na maono niliyaona miaka 20 iliyopita, ila hadi sasa nakumbuka kila kitu ni kama nimeota au kuona jana. huyo ndiye Mungu. na huwezi kusema labda havikutoka kwa Mungu, Nooo, msidanganyike, labda kama haujawahi kukutana na Mungu au kusikia sauti yake, Yesu alisema Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nao wanifuata. akija mwizi wakiita kondoo wanajua huyo sio mchungaji, ila akija mchungaji akiita sauti moja tu unajua huyo ndiye. ndivyo ilivyo, Mungu anajulikana kwetu kama tumejitoa kwake.

nimetoa haya machache, wengine watasema kwanini nimetolea hapa naaibisha kanisa, hapana, nimeona bora niweke hapa ili ifikie wachungaji wengi, kwasababu wapo humu. Mungu aliokoe kanisa lake.
Umesema vema mtumishi, watu siku hizi hawaendi kusali Bali kuitika numba kama shule siku za nyuma, aonekane yuko bila kujali amepokea nini ktk ibada...
Mim binafsi baada ya kugundua system nzima imeharibika, yaani sifa, kuabudu na mahubiri... Nimeona ili kuleta mabadiliko... Ni kuingia ktk uongozi na kujitolea kuwa kama mfano kwa kile nacho taka... Ukweli vita ni kubwa kiroho na kimwili... Ila. Naona wawili watatue wananielewa... Hata mchungaji yuko kinyume ila natumia influence yangu vema kumrekebisha..... Na vile anafurahia visadaka yangu... Sio rahisi kunichomoa... Nimepanga hadi mambo yake Sawa ndio nakaa bench... Maana kila niliko enda kusali tatizo lile lile... Nikasema hapa nitahama mpaka lini.. Let me be the change agent... Huku nilimwomba Mungu Sana kwa kila ibada mapenzi yake asimame... Sasa naona vijana wakimaanisha kidogo... Ukiona inafaa... Iga na wewe ili sote tuujenge mwili wa Kristo ktk ubora🙏🙏
 
sikubaliani na wewe, walokole sio malaika, na wengi wanaokoka lakini bado wachanga wa imani kama walivyo watoto tu wanaweza kucheza na matope kwasababu ya uchanga wa imani ila haimaanishi sio watoto wako. walokole wanazini, ila sio kwa hali ya juu kama wengine. ni chuki zako tu. pia, hiyo kauli kwamba ulokole ni uzezeta, unataka wawe wakatoliki? wawe watu gani sasa? wawe wafuasi wa papa? wasali kwa litulgia kwa kusoma vitabu na kuomba kwa maria? unataka wasalije? kuna siku utawatafuta walau wakuombee ila hutawapata, Mungu akurehemu na kukusaidia.
Nilitaka nishangae nisikukute umewataja hawa watu?ktk chochote mnachokihubiri hamuwezi kuacha kuwataja hao watu seems ticket zenu za peponi wamezishikilia wao.

Hongera sana,wewe mbingu ni yako 100% wewe huna cha kukuzuia.
 
shida ni kwamba, ukipambana na shetani sana rohoni, yeye huwa anaona moto unawaka, hivyo anapandikiza watu mle mle kanisani, wengine wanapandikizwa ni wachawi kabisa, wengine ni wale wakristo wenye michanganyo ambao wanatambulika kuwa wameokoka kumbe ni vuguvugu, shetani huwa anaingia ndani yao halafu anawatumia kama chombo kuvuruga ibada. ndio maana unaweza kukuta kijana alikuwa ameokoka vizuri, ataenda kuzini huko shetani anamwingia alafu anakuwa ndio mvurugaji wa ibada, na ukute ndio wanampa aendeshe sifa na kuabudu pale ndani yake linaloimba ni shetani na hauwezi kuona uwepo wa Mungu hata siku moja. cha muhimu ni kanisa kuweka principles za maana kwa mujibu wa Biblia, sio kuwa fanatic, ni kufundisha watu kwenye semina n.k hadi waelewe, wale wanaoleta mambo ya dunia madhabahuni unawapumzisha kwanza wautafuta uso wa Mungu wakiupata watapanda tena. very simple. ila kwa ufupi, shetani huwa anawaingia watu afu wanakuwa maajenti ndani ya kanisa ambao kazi yao ni kunyonya usafi wa kanisa kidogokidogo hadi inafika wakati watu wanaona kawaida tu kucheza kama diamond na koffi olomide kwenye madhabahu.
 
Nikusahihishe, ondoa neno mlokole, hilo neno si sahihi kwa wakristo waliookoka/born again. Ni neno lililokuwa ni kejeli, dhihaka na dharau kwa wakristo waliojitenga na dhambi, likitokea uganda. Hili neno limezoeleka kuelezea wakristo wa makanisa ya kipentekoste na wale wa faraghani wanaojiita fellowship walioko katika makanisa ya kilutheri, kianglikani, moravian na mengine yanayofanana na hayo. Wale walokole wa kikatoliki wanajulikana kama karithmatiki. Wapentekoste hawalikubali neno mlokole, wanaona kuwa mlokole ni kuwa vuguvugu huna msimamo na unachoamini. Wapentekoste ambao ndio walengwa wa neno hilo hawalikubali, wanaona ni la kejeli na mzaha
 
nashindwa kukuelewa ni wapentecost gani hao unaowazungumzia, na pia inawezekana wewe ni mtu wa Bukoba ndio maana unaamini neno ulokole lilitokea Uganda. mimi nilizaliwa mkoa fulani wa mbali kabisa na kagera na kwa kabila langu mtu anayeokoka tunaita amelokoka, maana yake halisi ni kwamba ametapika uchafu/dhambi sasa ni msafi, hata katika maisha ya kawaida tu mtoto akitapika au mgonjwa akitapika kwa lugha yetu tunaita "amelokola", hivyo hatujawahi kulipokea kama ni kudharauliwa hata siku moja na ukienda mikoa nilikokulia ukaongea hili watakushangaa sana kwasababu ndio lugha yao na haimaanishi dharau. tangu nimepata akili nikiwa na miaka 17 sasaivi nakaribia 45 nipo kwenye makanisa ya kipentecost. kutokana na kuhamahama mikoa kikazi na kwa shule, nimesali karibia yote. nimesali awali kabisa Elim Pentecost, nikasali Pentecost Holyness, nikasali Evangelical Assemblies of God ya Kulola, nikasali Tanzania Assemblies of God ya Lazaro, nikasali PAG na ujanani nilishajaribiwa kusali hayo makanisa ya manabii wa uongo Mungu akanifunulia ukweli nikayakimbia. kwenye makanisa yote hayo ya kilokole sijawahi kusikia hicho unachokisema.

hata hivyo, hii haisaidi lolote kwa wokovu. ukiitwa mlokole kwa dharau au kwa sifa kwamba umetapika kama lilivyo kabila langu, cha muhimu ni kwamba uwe umesafishwa dhambi, umeziacha na unatembea na Yesu maishani mwako.

kwa habari ya wana fellowship au karithmatic n.k, nikutoa tu hofu kwamba, watu wote waliowahi kukutana na Mungu rohoni wameshashuhudiwa kwamba "Mungu hana dini", ukienda kwa Mungu dini yako haioni. though hii haimaanishi kwamba unaweza kusali popote, dini ni utaratibu tu ambao wanadamuw amejiwekea na kukubaliana namna gani wamwabudu Mungu, kuna taratibu zingine zipo kwenye misingi ya kimungu na zingine hazipo kabisa kwenye misingi ya kimungu. taratibu zile zilizoko kwenye misingi ya Kimungu huwa zinakusaidia kukuguide na utamwona Mungu kama ukitia bidii, na zile zingine za kuabudu masanamu na wafu, katu hautakuja kumwona Mungu. hivyo uchaguzi wa dini ya kusali ni muhimu. ndio maana hao fellowship na carithmatic wanapigwa vita sana na wachungaji na mapadre.

walutheran na anglican wanawapigaga sana vita, ukija kwa carithmatic ya wakatoliki, baadhi ya makanisa yameandika kibao kabisa "haturuhusu kerithmatic hapa". why? kwasababu wao wamestuka, wameamua kusali kwa misingi ya rohoni sio kufuata katekisimo au litulgia. katika yote, waabuduo halisi huwabudu Mungu katika Roho na kweli, kumwabudu Mungu katika Roho ni pale unapomhusisha Roho Mtakatifu akakupeleka rohoni kukutana na Mungu. hilo ndilo kanisa la Matendo ya Mitume, lazima ukubali ujazo wa Roho Mtakatifu ambaye Yesu alisema hatuwezi bila yeye, na udhihirisho wake kuanzia kitabu cha Matendo utaona ni kunena kwa lugha ambako ni muhimu sana. hao fellowship na karithmatic na wapentecost hujaribu kumwendea Mungu kwa namna hiyo na huwa wanamwona maishani mwao regardless of differences ya madhehebu.

kila unayesoma hapa Nakutakia mwaka mpya mwema wenye baraka kwa Jina la Yesu.
 
Kina kulola wenyewe walikuwa hawalipendi neno hili mlokole, waliona ni mtu ambaye hajaokoka vizuri, ni vuguvugu, hana msimamo wa imani
 
basi linatafsiriwa tofautitofauti kulingana na mazingira kile mtu alipo. binafsi nafurahi kuitwa mlokole kwasababu nilikuwa nimejaa uchafu, Yesu akanitapisha, nikautapika.
 
Naomba kuongea na wachungaji wa kilokole hapa, nadhani hii itapunguza na makelele ya watu kulalamika kuwa mnapiga mno kelele kwenye makanisa yenu. kuna tabia mnazifumbia macho ila sio za Kimungu zimeenea sana makanisani. Mimi ninayeongea ni mlokole, sio wa mitume na manabii, hao huwa nawahesabu ni matapeli na wezi. mimi nimeokoka na ninasali kanisa la kipentecost. tunaingia mwaka mpya, naomba Mungu atusaidie, atusamehe pale tulipokosea, atuoshe kwa Damu yake, tuishi maisha matakatifu, tuache kupoteza muda, tuukomboe wakati kwasababu muda tuliobaki nao ni mchache sana, Yesu Kristo yuaja kulichukua kanisa lake. angalia usijecheleweshwa na mambo ya dunia, ukaachwa.

Kwanza niwapongeze watu wote waliookoka, kwasababu wamechagua fungu lililo jema, ukiokoka wewe ni mtoto wa Mungu, wakati wale ambao hawajaokoka wao ni wana wa Mungu. wewe hata ukikosea, utashughulikiwa kama mtoto wa nyumbani, tofauti na mwana ambaye hakai nyumbani. Yesu Kristo ni advocate wetu kwa kupitia Damu yake, Damu yake inanena mema kwa wale waliompokea. ninyi ambao hamjampokea, hamna mwombezi/advocate, hamna Damu ya kuwaokoa, mtajiokoa wenyewe na hamtaweza. hivyo kwa hiki nitakachokiandika hapa msifikiri nawasema walokole hapana, hawa ni heri kuliko ninyi msiookoka, nataka kuwajenga tu ili waendelee na wokovu. nanyi msiookoka nawakaribisha kwa Bwana katika Mwaka hu mpya, anza na Bwana, ishi na Bwana. hakuna aliyemkimbilia akaaibika.

1. KUSIFU NA KUABUDU: kipindi hiki, mnakiweka cha muda mfupi sana, kuna dakika chache za kusifu, na dakika chache zaidi za kuabudu. kwenye kusifu mnatuwekea vijana wahuni wanaotupotezea muda, mtu umeacha kazi zako unaenda kusali unafika pale kakijana kanavaa kisharobaro kahuni tu mnakaweka pale kaabudishe, ibada inakuwa kavu tunarudi hivyo hivyo. tunataka wale mnaotuletea kusifu na kuabudu wawe wamejiandaa, wamefunga, wameutafuta uso wa Mungu akisimama pale Nguvu za Mungu ziwepo, hatuji kanisani kukutana na ninyi, tunakuja kukutana na Nguvu za MUngu.

2. AINA ZA NYIMBO: Biblia inasema "wala msiifuatishe namna ya dunia hii"..vijana mnaotuwekea kutuabudishia au kusifu na kuabudu, wanacopy namna ya nyimbo za duniani wanaleta huku, wanabadilisha maneno tu, wanacopy namna ya kucheza duniani wanaleta madhabahuni. wapo vijana madhabahuni wanacheza sebene, ndomboro, wengine wanacheza kama Diamond na hamonize kabisa, vilevile. na aina hiyo ya uchezaji ikianza, utakuta wanawake wengi wameinuka wanacheza kama wapo disco, ni kama wameamsha lile shetani la disco walilokuwa nalo zamani, wanakumbushia na kutoa stress pale, na wanaamini wanamchezea Mungu. huu ni uhuni na Mungu hawezi kuonekana mazingira hayo. Ina maana Roho Mtakatifu ameshindwa kuwatafutia tyuni, au maneno ya kuweka kwenye wimbo, au namna ya kucheza? hadi muige uchezaji na lafudhi za kina Diamond? kweli? aokoaye ni Mungu wala sio uwezo wenu wa kucheza au kuimba, kama uimbaji wenu au uchezaji wenu hauna Mungu ni kujilisha upepo.

3. MAHUBIRI: mnatumia muda mchache wa kuhubiri, muda mwingi mnautumia kwenye matangazo na michango. kama hamjui, ukihubiri kwa Nguvu za Mungu hauhitaji kutangaza tangazo la michango au kuhudhuria ibada za katikati kwa nguvu, watu wenyewe watajiongoza kwasababu wameona kuna Mungu. kama hakuna Mungu ndio mtakamuanaaa hadi michango midogo tu. nawashauri tafuteni Mungu, Mtafuteni MUngu na Nguvu zake, mkifanikiwa kwenye hilo vingine hivyo ni vitu vidogo sana mkiwa na Mungu.pia tumeacha shughuli zetu mfano jumapili, tumeiweka wakfu kwa ajili ya Mungu, mnaweka ibada fupi mnataka twende wapi, mnakimbilia wapi, wiki nzima tupo bise, tunataka kuabudu hadi stress zote zitoke, na mtufundishe hadi tuchoke. Roho aongoze, sio ratiba zenu. hatutaki kuabudu dini, tunataka kumwona Mungu halisi wa kitabu cha Matendo ya Mitume.

4. KUABUDU: wafundisheni watu wenu kwamba, Mungu hapatikani wakati unapopayukapayuka, Mungu anapatikana kwenye utulivu, basi hata kama unaimba kwa nguvu basi uwe wimbo wa kuabudu mzuri, sio mandombolo na masebene ya kicongo hapa. hayo manyimbo ya kicongo mnaimba kwa kunengua viuno utafikiri mnazini, mnaruka kimasai nini na nini sijui, wala Mungu hapatikani. Mungu hupatikana kwenye utulivu, hapo ndipo mahali pa siri yaani ndaniii kule rohoni sio huku mwilini unaruka kwa kutumia ugali. hata wale ambao walishawahi kumwona Mungu maishani mwao, ni wale waliofanya maombi ya kufunga mfano, wakasoma Neno la Mungu na kutafakari, wakaingia chumbani, wakafung amlango, wakafunga simu na kila kitu, wakamwabudu Mungu kidogo, wakaingia kwenye kuomba then kutafakari kwa ndaniiiii kwenye ulimwengu wa Roho, hapo ndipo Roho Mtakatifu mwenyewe huamua kuomba kwa kukusadia wewe ndani yako. Maombi pekee yenye uhakika wa kujibiwa ni Maombi ya Roho, ya kimwili hayana uhakika. wengi mtasema mbona tukiwa tupo semina au maombi ya wengi Roho Mtakatifu huwa anashuka, ndio anaweza kushuka yeye hapangiwi hana sheria atashuka wakati wowote na popote, ila mimi nilikuwa nashauri wale ambao wamepanga kwamba nataka kuongea na Mungu na Mungu aongee na mimi kabisa, hilo ni mara chache linatokea kwenye jumuiya, na hao wanaonena public kwenye jumuia wengine ni mapepo though weingine pia ni wananena kwa Roho.

DAUDI ALICHEZA HADI NGUO ZIKADONDOKA; wengi wanachukua mstari huu wakisema hata watu makanisani wacheze kwa namna zozote zile kwasababu Daudi alifanya hivyo. Ukiangalia, utakuta kwa desturi za kipindi kile, hata Daudi alikosea ndio maana watu walimshangaa, imekuwaje, na pia wale walikuwa wanaabudu Mungu kimwili, sisi tunaabudu kiroho, leteni nyimbo tulivu za kuabudu na waabudishaji wasiwe wadhaifu wa imani/wazinzi na ambao hawajajiandaa, hawatatusaidia. na nyimbo hizo za kuabudu ziwe muda mrefu watu wazame, sio mnaimbisha kidogo tu kama mnafukuzwa na nini sijui, tayari mmeshasimama mnaleta neno kidogo tu ibada imeisha. jaribuni kuweka nyimbo za staha kwa muda mrefu, hivi tukiabudu hata kwa masaa mawili au hata matatu watu wanazama tu Mungu hatashuka? au mnataka Mungu asiwe anashuka tunaabudu kwa kulipua na mchungaji umekaa hapo unasubiri sadaka. ndio maana wanatoa kidogo. hata kama Biblia inasema tunaweza kucheza tunapomsifu Mungu (Zaburi 149:3) haimaanishi tucheze kama kina awilo, kunengua viuno kuigiza kuzini hadi watu wanaamshana hisia au kuifuata dancing ya kidunia hii.

5. UJAZO WA ROHO MTAKATIFU: Uzima wa kanisa ni Roho Mtakatifu, Yesu alisema siwezi kuwaacha peke yenu, nitawaachia msaidizi, huyo Roho atokaye kwa Baba, ndiye anayetutia kwenye kweli yote. huyu ndiye Roho anayetusaidia kuomba, analia Aba yaani Baba, kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, na yeye anaijua nia ya roho na hutusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ukiomba kwa akili utaomba kwa kuomba mahitaji ya mwili bila hata kujua impact yake, unaomba gari kumbe hujui kama gari hiyo inaweza kukuua mwenyewe, ila ukiomba kwa Roho utaomba kwa yale tu yaliyo mapenzi ya Mungu. ni furaha kubwa namna gani kuomba na kupata yale tu yaliyo mapenzi ya Mungu, kuliko yale yaliyo mapenzi yetu sisi wanadamu! hivyo, HAMASISHENI WATU WENU WAJAZWE ROHO, hapo ndipo mtakuwa na kanisa. bila Roho mtakatifu hata maombi yatakuwa mzigo, kutoa sadaka na michango au kuinjilisti itakuwa mzigo, ila wakiwa na Roho Mtakatifu watafanay bila kuambiwa na ninyi, Roho atawaongoza tena maeneo sahihi. waambieni wafunge, wasome Neno, watafute uso wa Mungu na kuacha njia mbaya hadi pale watakapojazwa na kutembea na Roho Mtakatifu, hao ndio wakristo hai. wengine wote ni mizigo na mtakuwa mnaogoza watu ambao hamna uhakika kama wataenda mbinguni, kwasababu wale wenye Roho tu ndio watu wa Mungu. na Yesu atakapokuja kunyakua atanyakua wale wenye Roho tu, wasio na Roho wa Mungu hatawanyakua. WALAKINI AWAYE YOTE ASIPOKUWA NA HUYO ROHO WA KRISTO, HUYO SIO WAKE. mkristo yeyote ambaye hana Roho Mtakatifu, huyo hana Mungu, na kuwepo kwa Roho hat akama wengi mnajifariji kwamba unaweza kuwa naye bila kunena, ila aliye naye anajijua anaye, na kunena ni ishara ya udhihirisho. ukienda kanisa ukaona mwezi wa kwanza, wapili hawahubiri na kuhamasisha ujazo wa Roho Mtakatifu, hapo kimbia, hakuna Mungu, kuna dini. msingi wa kwanza wa mpentecost ni ujazo wa Roho tena kunena kwa lugha kama kitabu cha matendo ya mitume. na ndilo agizo la Yesu.

6. SEMINA NA MAFUNDISHO; mnazidiwa na manabii na mitume wa uongo wanaouza mafuta kwasababu hamfundishi Neno, wekeni semina, fundisheni watu, na wakati unafundisha, usiende iviivi, jiandae kiroho ili ukiwa pale usihubiri wewe, bali Roho aongee kupitia wewe, hayo ndio mahubiri na mafundisho yanayookoa, elimu yenu ya chuo haiokoi, hata kama mmesoma theologia hadi PHD. ila tone moja tu la Roho wa Bwana linatosha kubadilisha Roho. Roho Mtakatifu ni mhuri, akikufikia tu ni kama amekupiga mhuri, kama ni wimbo au Neno hilo utalikumbuka. au kama ndoto kama ni ya Kimungu utaona ni kama umepigwa mhuri, hautaisahau. maishani mwangu kuna ndogo na maono niliyaona miaka 20 iliyopita, ila hadi sasa nakumbuka kila kitu ni kama nimeota au kuona jana. huyo ndiye Mungu. na huwezi kusema labda havikutoka kwa Mungu, Nooo, msidanganyike, labda kama haujawahi kukutana na Mungu au kusikia sauti yake, Yesu alisema Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nao wanifuata. akija mwizi wakiita kondoo wanajua huyo sio mchungaji, ila akija mchungaji akiita sauti moja tu unajua huyo ndiye. ndivyo ilivyo, Mungu anajulikana kwetu kama tumejitoa kwake.

nimetoa haya machache, wengine watasema kwanini nimetolea hapa naaibisha kanisa, hapana, nimeona bora niweke hapa ili ifikie wachungaji wengi, kwasababu wapo humu. Mungu aliokoe kanisa lake.
Aliyekuongoza kuyaandika haya,ameamsha ari ya kuifanya kazi ya Mungu kwa bidii zangu zote. Muda uliotenga kuandika bandiko hili haujapotea bure kuna kitu kikubwa kinakwenda kufanyika. Jina la BWANA libarikiwe sana!
 
Umesema vema mtumishi, watu siku hizi hawaendi kusali Bali kuitika numba kama shule siku za nyuma, aonekane yuko bila kujali amepokea nini ktk ibada...
Mim binafsi baada ya kugundua system nzima imeharibika, yaani sifa, kuabudu na mahubiri... Nimeona ili kuleta mabadiliko... Ni kuingia ktk uongozi na kujitolea kuwa kama mfano kwa kile nacho taka... Ukweli vita ni kubwa kiroho na kimwili... Ila. Naona wawili watatue wananielewa... Hata mchungaji yuko kinyume ila natumia influence yangu vema kumrekebisha..... Na vile anafurahia visadaka yangu... Sio rahisi kunichomoa... Nimepanga hadi mambo yake Sawa ndio nakaa bench... Maana kila niliko enda kusali tatizo lile lile... Nikasema hapa nitahama mpaka lini.. Let me be the change agent... Huku nilimwomba Mungu Sana kwa kila ibada mapenzi yake asimame... Sasa naona vijana wakimaanisha kidogo... Ukiona inafaa... Iga na wewe ili sote tuujenge mwili wa Kristo ktk ubora
Aisee hongera Sana. Mimi niliona nikae benchi tu mwaka wa 15 huu. Kuna mambo kuyavumilia nilishashindwa kabisa!
 
Naomba kuongea na wachungaji wa kilokole hapa, nadhani hii itapunguza na makelele ya watu kulalamika kuwa mnapiga mno kelele kwenye makanisa yenu. kuna tabia mnazifumbia macho ila sio za Kimungu zimeenea sana makanisani. Mimi ninayeongea ni mlokole, sio wa mitume na manabii, hao huwa nawahesabu ni matapeli na wezi. mimi nimeokoka na ninasali kanisa la kipentecost. tunaingia mwaka mpya, naomba Mungu atusaidie, atusamehe pale tulipokosea, atuoshe kwa Damu yake, tuishi maisha matakatifu, tuache kupoteza muda, tuukomboe wakati kwasababu muda tuliobaki nao ni mchache sana, Yesu Kristo yuaja kulichukua kanisa lake. angalia usijecheleweshwa na mambo ya dunia, ukaachwa.

Kwanza niwapongeze watu wote waliookoka, kwasababu wamechagua fungu lililo jema, ukiokoka wewe ni mtoto wa Mungu, wakati wale ambao hawajaokoka wao ni wana wa Mungu. wewe hata ukikosea, utashughulikiwa kama mtoto wa nyumbani, tofauti na mwana ambaye hakai nyumbani. Yesu Kristo ni advocate wetu kwa kupitia Damu yake, Damu yake inanena mema kwa wale waliompokea. ninyi ambao hamjampokea, hamna mwombezi/advocate, hamna Damu ya kuwaokoa, mtajiokoa wenyewe na hamtaweza. hivyo kwa hiki nitakachokiandika hapa msifikiri nawasema walokole hapana, hawa ni heri kuliko ninyi msiookoka, nataka kuwajenga tu ili waendelee na wokovu. nanyi msiookoka nawakaribisha kwa Bwana katika Mwaka hu mpya, anza na Bwana, ishi na Bwana. hakuna aliyemkimbilia akaaibika.

1. KUSIFU NA KUABUDU: kipindi hiki, mnakiweka cha muda mfupi sana, kuna dakika chache za kusifu, na dakika chache zaidi za kuabudu. kwenye kusifu mnatuwekea vijana wahuni wanaotupotezea muda, mtu umeacha kazi zako unaenda kusali unafika pale kakijana kanavaa kisharobaro kahuni tu mnakaweka pale kaabudishe, ibada inakuwa kavu tunarudi hivyo hivyo. tunataka wale mnaotuletea kusifu na kuabudu wawe wamejiandaa, wamefunga, wameutafuta uso wa Mungu akisimama pale Nguvu za Mungu ziwepo, hatuji kanisani kukutana na ninyi, tunakuja kukutana na Nguvu za MUngu.

2. AINA ZA NYIMBO: Biblia inasema "wala msiifuatishe namna ya dunia hii"..vijana mnaotuwekea kutuabudishia au kusifu na kuabudu, wanacopy namna ya nyimbo za duniani wanaleta huku, wanabadilisha maneno tu, wanacopy namna ya kucheza duniani wanaleta madhabahuni. wapo vijana madhabahuni wanacheza sebene, ndomboro, wengine wanacheza kama Diamond na hamonize kabisa, vilevile. na aina hiyo ya uchezaji ikianza, utakuta wanawake wengi wameinuka wanacheza kama wapo disco, ni kama wameamsha lile shetani la disco walilokuwa nalo zamani, wanakumbushia na kutoa stress pale, na wanaamini wanamchezea Mungu. huu ni uhuni na Mungu hawezi kuonekana mazingira hayo. Ina maana Roho Mtakatifu ameshindwa kuwatafutia tyuni, au maneno ya kuweka kwenye wimbo, au namna ya kucheza? hadi muige uchezaji na lafudhi za kina Diamond? kweli? aokoaye ni Mungu wala sio uwezo wenu wa kucheza au kuimba, kama uimbaji wenu au uchezaji wenu hauna Mungu ni kujilisha upepo.

3. MAHUBIRI: mnatumia muda mchache wa kuhubiri, muda mwingi mnautumia kwenye matangazo na michango. kama hamjui, ukihubiri kwa Nguvu za Mungu hauhitaji kutangaza tangazo la michango au kuhudhuria ibada za katikati kwa nguvu, watu wenyewe watajiongoza kwasababu wameona kuna Mungu. kama hakuna Mungu ndio mtakamuanaaa hadi michango midogo tu. nawashauri tafuteni Mungu, Mtafuteni MUngu na Nguvu zake, mkifanikiwa kwenye hilo vingine hivyo ni vitu vidogo sana mkiwa na Mungu.pia tumeacha shughuli zetu mfano jumapili, tumeiweka wakfu kwa ajili ya Mungu, mnaweka ibada fupi mnataka twende wapi, mnakimbilia wapi, wiki nzima tupo bise, tunataka kuabudu hadi stress zote zitoke, na mtufundishe hadi tuchoke. Roho aongoze, sio ratiba zenu. hatutaki kuabudu dini, tunataka kumwona Mungu halisi wa kitabu cha Matendo ya Mitume.

4. KUABUDU: wafundisheni watu wenu kwamba, Mungu hapatikani wakati unapopayukapayuka, Mungu anapatikana kwenye utulivu, basi hata kama unaimba kwa nguvu basi uwe wimbo wa kuabudu mzuri, sio mandombolo na masebene ya kicongo hapa. hayo manyimbo ya kicongo mnaimba kwa kunengua viuno utafikiri mnazini, mnaruka kimasai nini na nini sijui, wala Mungu hapatikani. Mungu hupatikana kwenye utulivu, hapo ndipo mahali pa siri yaani ndaniii kule rohoni sio huku mwilini unaruka kwa kutumia ugali. hata wale ambao walishawahi kumwona Mungu maishani mwao, ni wale waliofanya maombi ya kufunga mfano, wakasoma Neno la Mungu na kutafakari, wakaingia chumbani, wakafung amlango, wakafunga simu na kila kitu, wakamwabudu Mungu kidogo, wakaingia kwenye kuomba then kutafakari kwa ndaniiiii kwenye ulimwengu wa Roho, hapo ndipo Roho Mtakatifu mwenyewe huamua kuomba kwa kukusadia wewe ndani yako. Maombi pekee yenye uhakika wa kujibiwa ni Maombi ya Roho, ya kimwili hayana uhakika. wengi mtasema mbona tukiwa tupo semina au maombi ya wengi Roho Mtakatifu huwa anashuka, ndio anaweza kushuka yeye hapangiwi hana sheria atashuka wakati wowote na popote, ila mimi nilikuwa nashauri wale ambao wamepanga kwamba nataka kuongea na Mungu na Mungu aongee na mimi kabisa, hilo ni mara chache linatokea kwenye jumuiya, na hao wanaonena public kwenye jumuia wengine ni mapepo though weingine pia ni wananena kwa Roho.

DAUDI ALICHEZA HADI NGUO ZIKADONDOKA; wengi wanachukua mstari huu wakisema hata watu makanisani wacheze kwa namna zozote zile kwasababu Daudi alifanya hivyo. Ukiangalia, utakuta kwa desturi za kipindi kile, hata Daudi alikosea ndio maana watu walimshangaa, imekuwaje, na pia wale walikuwa wanaabudu Mungu kimwili, sisi tunaabudu kiroho, leteni nyimbo tulivu za kuabudu na waabudishaji wasiwe wadhaifu wa imani/wazinzi na ambao hawajajiandaa, hawatatusaidia. na nyimbo hizo za kuabudu ziwe muda mrefu watu wazame, sio mnaimbisha kidogo tu kama mnafukuzwa na nini sijui, tayari mmeshasimama mnaleta neno kidogo tu ibada imeisha. jaribuni kuweka nyimbo za staha kwa muda mrefu, hivi tukiabudu hata kwa masaa mawili au hata matatu watu wanazama tu Mungu hatashuka? au mnataka Mungu asiwe anashuka tunaabudu kwa kulipua na mchungaji umekaa hapo unasubiri sadaka. ndio maana wanatoa kidogo. hata kama Biblia inasema tunaweza kucheza tunapomsifu Mungu (Zaburi 149:3) haimaanishi tucheze kama kina awilo, kunengua viuno kuigiza kuzini hadi watu wanaamshana hisia au kuifuata dancing ya kidunia hii.

5. UJAZO WA ROHO MTAKATIFU: Uzima wa kanisa ni Roho Mtakatifu, Yesu alisema siwezi kuwaacha peke yenu, nitawaachia msaidizi, huyo Roho atokaye kwa Baba, ndiye anayetutia kwenye kweli yote. huyu ndiye Roho anayetusaidia kuomba, analia Aba yaani Baba, kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, na yeye anaijua nia ya roho na hutusaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Ukiomba kwa akili utaomba kwa kuomba mahitaji ya mwili bila hata kujua impact yake, unaomba gari kumbe hujui kama gari hiyo inaweza kukuua mwenyewe, ila ukiomba kwa Roho utaomba kwa yale tu yaliyo mapenzi ya Mungu. ni furaha kubwa namna gani kuomba na kupata yale tu yaliyo mapenzi ya Mungu, kuliko yale yaliyo mapenzi yetu sisi wanadamu! hivyo, HAMASISHENI WATU WENU WAJAZWE ROHO, hapo ndipo mtakuwa na kanisa. bila Roho mtakatifu hata maombi yatakuwa mzigo, kutoa sadaka na michango au kuinjilisti itakuwa mzigo, ila wakiwa na Roho Mtakatifu watafanay bila kuambiwa na ninyi, Roho atawaongoza tena maeneo sahihi. waambieni wafunge, wasome Neno, watafute uso wa Mungu na kuacha njia mbaya hadi pale watakapojazwa na kutembea na Roho Mtakatifu, hao ndio wakristo hai. wengine wote ni mizigo na mtakuwa mnaogoza watu ambao hamna uhakika kama wataenda mbinguni, kwasababu wale wenye Roho tu ndio watu wa Mungu. na Yesu atakapokuja kunyakua atanyakua wale wenye Roho tu, wasio na Roho wa Mungu hatawanyakua. WALAKINI AWAYE YOTE ASIPOKUWA NA HUYO ROHO WA KRISTO, HUYO SIO WAKE. mkristo yeyote ambaye hana Roho Mtakatifu, huyo hana Mungu, na kuwepo kwa Roho hat akama wengi mnajifariji kwamba unaweza kuwa naye bila kunena, ila aliye naye anajijua anaye, na kunena ni ishara ya udhihirisho. ukienda kanisa ukaona mwezi wa kwanza, wapili hawahubiri na kuhamasisha ujazo wa Roho Mtakatifu, hapo kimbia, hakuna Mungu, kuna dini. msingi wa kwanza wa mpentecost ni ujazo wa Roho tena kunena kwa lugha kama kitabu cha matendo ya mitume. na ndilo agizo la Yesu.

6. SEMINA NA MAFUNDISHO; mnazidiwa na manabii na mitume wa uongo wanaouza mafuta kwasababu hamfundishi Neno, wekeni semina, fundisheni watu, na wakati unafundisha, usiende iviivi, jiandae kiroho ili ukiwa pale usihubiri wewe, bali Roho aongee kupitia wewe, hayo ndio mahubiri na mafundisho yanayookoa, elimu yenu ya chuo haiokoi, hata kama mmesoma theologia hadi PHD. ila tone moja tu la Roho wa Bwana linatosha kubadilisha Roho. Roho Mtakatifu ni mhuri, akikufikia tu ni kama amekupiga mhuri, kama ni wimbo au Neno hilo utalikumbuka. au kama ndoto kama ni ya Kimungu utaona ni kama umepigwa mhuri, hautaisahau. maishani mwangu kuna ndogo na maono niliyaona miaka 20 iliyopita, ila hadi sasa nakumbuka kila kitu ni kama nimeota au kuona jana. huyo ndiye Mungu. na huwezi kusema labda havikutoka kwa Mungu, Nooo, msidanganyike, labda kama haujawahi kukutana na Mungu au kusikia sauti yake, Yesu alisema Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nao wanifuata. akija mwizi wakiita kondoo wanajua huyo sio mchungaji, ila akija mchungaji akiita sauti moja tu unajua huyo ndiye. ndivyo ilivyo, Mungu anajulikana kwetu kama tumejitoa kwake.

nimetoa haya machache, wengine watasema kwanini nimetolea hapa naaibisha kanisa, hapana, nimeona bora niweke hapa ili ifikie wachungaji wengi, kwasababu wapo humu. Mungu aliokoe kanisa lake.
Pumbavu hakuna kitu ulokole hapa ulimwenguni mnajisafisha tu kuficha utumwa na ujinga mliobeba vichwani mwenu.

Umeokoka nini wakati bado umezungukwa na matatizo kibao unayoyasababisha wewe mwenyewe hasa UJINGA.
 
Back
Top Bottom