Wakristo, waislam, walevi, maDJ na wezi muwe watulivu wakati NEMC wakifanya kazi yao halali

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,859
18,277
Nimefurahi sana kusikia NEMC wameanza kuwashughulikia wapiga kelele wanaosababisha zogo mtaani na kuwafanya raia wengine wakose raha na utulivu. Kipekee kabisa naomba NEMC wamulike zaidi makanisa, misikiti, vigodoro na wauza muziki (wezi wa kazi za wasanii) kwani hawa ndio wamekithiri kwenye uchafuzi wa hewa kwa kelele, hivyo kupelekea raia wasiishi kwa raha na amani katika maskani yao.

Hivi ninavyoandika uzi huu kuna nyumba moja ya ibada hapa karibu na nyumbani kwangu wamefungulia maspika yao wanatoa mawaidha kwa sauti ya juu hadi mtaa mzima umechafuka kwa kelele. Na maspika yako maanne na yamefungwa kuelekea upande zote nne za dunia. Na utaratibu huu sio wa siku moja tu bali ni wa kila siku. Inakuwa vigumu watu kusikilizana na wagonjwa kupumzika kwa amani kwa kuwa kelele ni kubwa sana.

Jirani na nyumbani kwangu kuna nyumba ya ibada ambamo kila siku lazima wawashe mispika wakati wa kuswalisha na mawaidha. Na pamoja na kuwa spika husaidia kukuza sauti lakini hata mswalishaji mwenyewe huongea kwa sauti hadi mishipa inakaribia kukatika.

Kuamsha watu asubuhi sasa ndio usiseme. Kiongozi wao huanza kuwaita wenzake na kuimba nyimbo kwa sauti kubwa tangu saa 9 alfajili hadi saa 11 swala inapoanza. Yaani tunakomaje hapa mtaani! Kuanzia saa 9 hadi saa 11 alfajili huwezi kulala hata ukiwa na usingizi mwingi kiasi gani. Ni KERO kubwa sana kwa kweli. Hivi kwanini kila muumini asiweke alarm kwenye saa au simu yake iwe inamuamsha badala ya kukera mtaa mzima kwa mikelele ya maspika? Ustaarabu uko wapi? Hapa ndipo nampendea Rais Kagame. Nchini kwake amepiga marufuku matumizi ya maspika.

Pamoja na kero ya kelele kutoka misikitini, pia kuna hizi kelele za maspika ya walokole na kengele za wakatoliki zinazopigwa kwa sauti ya juu hadi kukaribia kupasua ngoma za masikio ya raia. Utakuta muumini wa kilokole anaishi nyumba ya kupanga na kila wiki wenzake wanakuja kwake kukesha wakinena kwa lugha, kupiga vinanda na kuimba kwa sauti kiasi cha kuwa kero kwa wapangaji wengine. Kuabudu ni jambo zuri lakini isiwe kero kwa wenzako. Hata Mungu hapendi. Kuwakera wenzako kwa kelele za ibada kunaondoa baraka zote ambazo ungepata kutokana na kumuabudu Mungu wako.

Kelele nyingine za kuudhi hutoka kwenye mabaa, kwa kisingizio cha kuwaburudisha walevi. Pombe ikishakolea, usikivu wa mlevi hupungua, hivyo kuwalazimu maDJ kupiga muziki wa juu ili walevi wafurahi. Matokeo yake ni kuwakera raia wengine wasiolewa. Kero hii hupelekea wananchi na wafanyakazi kushindwa kulala usingizi mzuri, hivyo kupunguza utendaji kazi na kushusha uchumi wa taifa. Serikali isipokuwa makini kuzuia kelele hizi, uchumi wa nchi utashuka bila sababu za msingi.

Kero nyingine ya kelele hutoka kwa wauza CD, ambao wengi wao ni wezi wa kazi za wasanii. Ukipita kila mtaa, maeneo kama Kariakoo, kelele za wezi wa muziki zinakuwa kubwa kiasi cha kuondoa utulivu na kusababisha wafanyabiashara kushindwa kusikilizana na wateja wao. Kitendo hiki pia kinashusha uchumi wa nchi na kupunguza mapato ya serikali. Hapa uchumi wa nchi hushuka kwa namna mbili – namna ya kwanza ni kushusha mapato ya kodi na namna ya pili ni kupitia wizi wa sanaa za wanamuziki.

Kero ya mwisho kutokana na kelele, hasa maeneo ya uswahilini, ni vigogoro. Kuna mitaa ambayo kila wiki hukosi kusikia muziki wa kutisha kutoka kwenye maspika makubwa ya vigodoro. Unaambiwa kwamba hiyo ni never miss. Usiombe ukajenga au kupanga maeneo hayo. Hukawii kutelekeza nyumba yako uliyoijenga kwa mikono yako mwenyewe ukaenda kupanga mitaa ya mbali. Kelele za vigodoro ni kero zaidi hasa katika maeneo ya ukanda wa pwani na uswazi.

MAONI YANGU
Naunga mkono juhudi za NEMC kuwashughulikia wapiga kelele kwani kelele hizi, kama ilivyoainishwa hapo juu, zinasababisha ghasia kwa umma na kuvuruga uchumi wa taifa. Shime watanzania wote tushikane mikono kuhakikisha kwamba tunatoa ushirikiano wa kutosha kwa NEMC wakati wanapofanya juhudi za kuondoa kelele hizi kwenye mitaa yetu ili wananchi tuishi kwa amani na furaha.

Nawasilisha.
Pia soma:
 
NEMC wasiwaache walokole aisee na hawa wenye viharusi vya mtaani , wanakesha wakipiga mziki sku moja kabla ya harusi hawa jamaa hawafai kabisa
 
Mimi hapa jirani pana mtu anakemewea mapepo hii ni siku ya nne kelele nipo njiani naenda kulala guest KWA afya ya akili yangu Mimi na kelele tofauti, talala guest hadi pepo litakapotoka.
Unajiita Mkristo hali unateswa na wachawi na majini. Ngoja nikalale guest
 
NEMC wasiwaache walokole aisee na hawa wenye viharusi vya mtaani , wanakesha wakipiga mziki sku moja kabla ya harusi hawa jamaa hawafai kabisa
Kweli kabisa mzee. Huku uswazi tunaishi kwa taabu sana; utakuta siku moja kuna vigodoro zaidi ya 10 kwenye mtaa mmoja. Yaani inakuwa vurugu kweli kweli. Siku moja niliwahi kuhama nyumbani nikaenda kulala lodge kwa sababu ya kukwepa kelele za vigodoro.
 
Mimi hapa jirani pana mtu anakemewea mapepo hii ni siku ya nne kelele nipo njiani naenda kulala guest KWA afya ya akili yangu Mimi na kelele tofauti, talala guest hadi pepo litakapotoka.
Unajiita Mkristo hali unateswa na wachawi na majini. Ngoja nikalale guest
Haya usiku mwema mkuu :D :D :D :D
 
NEMC wasiwaache walokole aisee na hawa wenye viharusi vya mtaani , wanakesha wakipiga mziki sku moja kabla ya harusi hawa jamaa hawafai kabisa
Hawa jamaa yaani wanatusumbua sana na mikelele yao hapa mtaani. Serikali isipowachukulia hatua, wananchi tutajichukulia wenyewe sheria mkononi. Tumechoka.
 
hakika ni jambo la msingi sana vigodoro sijui visherehe uchwara vya mtaani wanakodi mziki unakesha kama ni majirani zako unakoma

nakumbuka mwaka jana kuna siku sijalala usiku mzima kulikuwa na kitu gani sijui cha kiislamu basi walikesha mpaka asubuhi na kelele za kufa mtu hakika ilikuwa mbaya sana sana haielezeki nikawa nafikiria kuhusu wagonjwa na watu wenye shida mbalimbali walivyoadhirika na kelele hizo
 
Kinara wa hilo boga Ni dhehebu gan?
Walokole ndio kinara mkuu. Wanatuimbia mapambio hapa mtaani usiku kucha hatulali. Afadhali waislamu wao hupiga kelele kwa muda mfupi tu kuliko hawa wanenaji kwa lugha wanaokesha wakicharaza vinanda na kukemea mapepo.
 
hakika ni jambo la msingi sana vigodoro sijui visherehe uchwara vya mtaani wanakodi mziki unakesha kama ni majirani zako unakoma

nakumbuka mwaka jana kuna siku sijalala usiku mzima kulikuwa na kitu gani sijui cha kiislamu basi walikesha mpaka asubuhi na kelele za kufa mtu hakika ilikuwa mbaya sana sana haielezeki nikawa nafikiria kuhusu wagonjwa na watu wenye shida mbalimbali walivyoadhirika na kelele hizo
Nakuambia hao jamaa wakiamua kupiga kelele zao lazima utamhamisha mtaa mgonjwa wako, la sivyo watampasua ngoma za masikio na mispika yao.
 
Mimi hapa jirani pana mtu anakemewea mapepo hii ni siku ya nne kelele nipo njiani naenda kulala guest KWA afya ya akili yangu Mimi na kelele tofauti, talala guest hadi pepo litakapotoka.
Unajiita Mkristo hali unateswa na wachawi na majini. Ngoja nikalale guest
Tunza risiti ili wakishamaliza hiyo shughuli yao sumbufu uwape risiti wakupe reimbursement.
 
Pole sana jomba ndio maana NEMC wamelichukua hilo na kuanza kulifanyia kazi ipasavyo. Muda si mrefu mambo yatakuwa shwari.
Mungu asaidie wasije ishia katikati mambo yakabaki kama yalivyo especially mitaani vipazasauti misikitini na makanisa ya walokole sehemu za makazi kuwe na utaratibu na kuhakikisha kinachoendelea ndani sisi wa nje ambao hakituhusu tusisikie

mfano azana sijui waite watu then baada ya hapo mijadala yao haituhusu

na makanisa ya kilokole watoane pepo ndani kwa ndani sisi nje hatupaswi kusikia mahubiri yao
 
Back
Top Bottom