Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt Samuel Gwamak
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt Samuel Gwamaka awataka wamiliki wote wa baa na kumbi za burudani kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake wakati wakiendesha shughuli zao za burudani ili kuepusha bugudha kubwa kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.
Amelitoa agizo hilo leo Septemba 12, 2023 katika Ukumbi wa mikutano wa NEMC alipokutana na vyombo vya habari kuzungumzia hali iliyopo kwa sasa katika jamii kufuatia kukithiri kwa sauti zilizozidi viwango na kusababisha athari kubwa.
Amesema kuna ongezeko la malalamiko ya uchafuzi wa mazingira kwa njia ya kelele ndani ya wiki mbili zilizopita.
Amebainisha kuwa baada ya kutoa adhabu ya faini na kuwafungia baadhi ya wahusika ikiwemo kumbi za starehe, baadaye wakafunguliwa, ndipo wahusika wameanza kujisahau na kuanza kupiga kelele.
Ametosema “Baraza tunawakumbusha Sheria bado ipo na inafanya kazi, kelele ni kero hasa zinapowagusa wasiohusika.
“Kuna watu wanaumwa na wanahitaji utulivu hasa wakati wa usiku, hivyo unapofanya sherehe au tukio kumbuka kuna raia wengine wanahitaji muda wa kupumzika na wanastahili haki hiyo.
“Naomba kutoa tahadhari kwa wote wanaoendesha vyombo vya starehe, si vema tukarudi tulipotoka, zoezi lile lilikwisha na elimu ilishatolewa."