NEMC wekeni utaratibu wa ibada; huku mtaani leo hakukaliki kwa sababu ya kelele!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,799
18,224
Hata kama serikali haina dini lakini hapa tulipofika sasa kuna haja ya serikali kuingilia kati. Hapa mtaani kwangu leo hakukaliki kwa sababu ya kelele za maspika ya ibada. NEMC walisema wataweka utaratibu wa kufanya ibada lakini sijui wanakwama wapi mpaka sasa hawajachukua hatua zozote. Hadi natamani niuze nyumba hii nihamie mkoa mwingine.

Kuna nyumba nne za ibada kuzunguka makazi yangu na kila nyumba ina spika nne – kila spika imetazama upande mmoja wa dunia (kusini, kaskazini, magharibi na mashariki). Jumla ya maspika ni 16 na wote wanahubiri kwa wakati mmoja, tena kwa sauti kubwa sana. Wewe fikiria maspika 16 yamekuweka kati na yote yanaunguruma kwa wakati mmoja! Kuna kusikilizana hapo?

Halafu leo ni kama vile wameamua kuongeza sauti kwa makusudi ili kutukomesha. Nipo hapa nafanya kazi zangu za kujenga taifa lakini nahisi kichwa kinawaka moto. Sasa kama watu wanaohubiriwa wapo ndani ya nyumba ya ibada kuna haja gani ya kuning’iniza maspika juu ya paa kama sio ukorofi?

Na hapo bado kesho na keshokutwa wenzetu watakapoungurumisha mavinanda na kuimba mapambio. Na wao nyumba zao za ibada zipo hapa hapa jirani. Ni kero kubwa sana kwa kweli, hasa unapokuwa unafanya kazi inayohitaji utulivu.

Naomba NEMC waingilie kati mara moja kwa kuweka utaratibu wa ibada wa kiistarabu badala ya huu utaratibu wa ovyo wa kuhanikiza kelele mtaa mzima.
Pia soma:
 
Aisee hapa kwetu pua na mdomo na nyumba za ibada tatu ni mseto,,,,,,jamani jamani ni kero kero
Baa zikipiga kelele mnasema mnaburudika pombe haipandi bila kelele

Kutesa kwa zamu baa walevi wanapigia kelele walokole wakinyamaza walokole wanapigia kelele walevi sababu na wao Roho. Wa Mungu hashshukii bila kelele Kelele ni burudani kwao ya kiroho

Ngoma draw
 
Baa zikipiga kelele mnasema mnaburudika

Kutesa kwa zamu baa walevi wanapigia kelele walokole wakinyamaza walokole wanapigia kelele walevi

Ngoma draw
Mkuu baa nazo zinakera sana, hasa hizi ambazo zimepakana na makazi. Nazo NEMC watazishughulikia kwa wakati wake.
 
Baa zikipiga kelele mnasema mnaburudika

Kutesa kwa zamu baa walevi wanapigia kelele walokole wakinyamaza walokole wanapigia kelele walevi

Ngoma draw
Hahahaha hapana siwezi burudika na kelele za bar,,,,
 
Hao nemc na wapange ibada za aia zote wakifika kupanga ibada za waislamu nadhani na sheria ndio itavunjikia hapo
 
Mbona vijana kibao wako kitaa hata hawajala bado?
Wapeni hela wakayabomoe mbona kazi rahisi
Au mnajua kuwachoma moto waizi wa yebo tu
Kuyabomoa utakuwa uchokozi mkuu. Tunataka NEMC waweke utaratibu laini wasije wakachokoza nyuki tukakosa mahali pa kujificha.
 
Kuyabomoa utakuwa uchokozi mkuu. Tunataka NEMC waweke utaratibu laini wasije wakachokoza nyuki tukakosa mahali pa kujificha.
Hao NEMC hawana makali yoyote
Ukiona sheria iliyotungwa inapondwa na kina Msukuma na chala unategemea kuna kitu hapo?

Tuna tatizo la kutokufuata sheria kwa sababu mengi ni matamko tu

Mkuu wa mkoa mpya kaletwa ili awadhibiti hakuna kingine na vile ana mdomo
 
Hao NEMC hawana makali yoyote
Ukiona sheria iliyotungwa inapondwa na kina Msukuma na chala unategemea kuna kitu hapo?

Tuna tatizo la kutokufuata sheria kwa sababu mengi ni matamko tu

Mkuu wa mkoa mpya kaletwa ili awadhibiti hakuna kingine na vile ana mdomo
Hata mimi NEMC nawashangaa kwanini wanachukua muda mrefu kuweka utaraibu wakati ni suala la kutamka tu na kumaliza kazi. Wawaelekeze wenzetu wawe wanatumia alarm kuwambusha muda wa ibada unapofika badala ya kutupigia mikelele yao kila alfajiri tunashindwa kulala.
 
Back
Top Bottom