Wako wapi mabinti waliotajwa na FA kwenye wimbo wa “Mabinti”?

Forest Hill

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
767
1,000
Tusaidie kuuweka hapa chief

Pia kama unazo nyingine za kwenye album ya 'Toleo Lijalo' tuwekee

Nyimbo kama;-

Ungenambia ft Stara
Aminia ft Alberto & Inspector
Wakati umelala ft Jose Mtambo & Suka
Demu wangu wa kwanza unaipata??
 
Mzigua90

JF-Expert Member
Sep 23, 2014
36,175
2,000
Huu ndio ulikua mziki.Nakumbuka nilitoloka shule Kibaha Secondary nikaja Dar kihudhuria show ya FA pale Chuo kikuu Mlimani.Nani kama FA,nilikua namkubali sana kuliko madogo wanavyomkubali Mondi.
Mimi nikiwaona kina FA Jay Mo,Solo huwa nafurahi sana coz hicho ndio kizazi chetu cha muziki.
Nilinunua albamu zote za FA nilikua nazo hadi leo makava ya zile kanda ninazo.Mara ya mwisho nilihangaika sana kupiga picha na FA pale mabibo hostel it was 2003.
Ngoma ya mabinti ni kweli inafanana na ya Jay Mo ile ya kama unataka demu zilikua moto sana zote mbili,na tumecheza sana club hizo ngoma. FA katolewa kimziki na produza Boniluv hadi leo FA hawezi kutaja historia yake career wise bila ku mention jina la Boniluv.
MADEMU KWENYE WIMBO
1.Seven...alikua meneja wa Kiba,alikua pini sana enzi hizo na aliwahi msimamia kimziki Jay dee pia
2."Kisese mithili ya Radhia"....hawa walikua wawili walikua wanaunda kundi la Unique sisters alikuwepo Radhia na Radhina
3.Happy Magese alikua Miss for now anajulikana kama Millen Magese
4.Zay b,Ray C, wote walikua wanamziki.
5.Shose alikua pini sana,now nadhani yupo jela kwa ile case yao pale Stanbic
6.Mboni Mhita alikua mbunge enzi hizo nasikia alikua pini balaa
Enzi hizo ndio Pfunk alikua anammendea Kajala nadhani kwenye wimbo wa Jay mo katajwa kama sijakosea.
Sijawahi ona wimbo mbaya wa mwanafa hadi leo.kwenye laptop yangu nina nyimbo zake zote toka nipo chuo nazitunza.
Kuna ngoma moja yupo na lady jayde inaitwa "siku nikianguka" inahusu kifo usipime kali sana na ina touch sana,kuna mistari hua naipenda inasema
(nihodhi makazi yangu kando ya ufukwe wa bahari,
mke mzuri aliepambwa nyumbani na watoto walionawiri,
mikono yangu izungushe usukani wa motokari,
tupia macho takwimu,mimi mwana wa adamu kwani kasi inatisha,
maisha yangu yatakatika,
nafsi itabaki na tamaa lakini kamwe mwili hautoamka")
Nani kama MwanaFa hiki kizazi cha iyoooo Laizaaaaa haikuji mambo haya.
Shose yuko uraiani. Kesi yao ilikwisha.
 
Duke Tachez

JF-Expert Member
Mar 28, 2018
5,447

habari za p funk na kajala mlikuwa mnazipata wapi maana kulikuwa hamna YouTube na Instagram
 
Harry Mapande

Senior Member
May 18, 2020
109
500
habari za p funk na kajala mlikuwa mnazipata wapi maana kulikuwa hamna YouTube na Instagram
Magazeti ya udaku,vijiweni,shuleni, kwenye matamasha nk. humo kote stori za watu maarufu zinapigwa na zinasambaa kwa kasi.
Unaweza kukuta mtu 1 kaenda kwenye tamasha mf.Diamond jubilee akikuta stori ya umbea au akimuona star na demu wake akirudi mtaani anawakusanya watu anawapigisha stori ,huyo ndiye anaonekana mjanja wa mtaa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom