Wakili Boniface Mwabukusi: Montevideo Convention na Vienna laws to Treaty hairuhusu Dubai kuingia mkataba na nchi yoyote

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
950
2,866
"Kabla sijaanza kuongea kuhusu bandari,nizungumzie mambo matatu,la kwanza,mpuuzi na mpumbavu tutamkabili kwa upuuzi na upumbavu wake" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Kabla sijaanza kuongea kuhusu bandari,nizungumzie mambo matatu,kumekuwa na tabia ya kubadili upumbavu kuwa hekima,na unapoongea ukweli unaambiwa haujaongea kwa hekima,sasa nasema mpuuzi na mpumbavu tutamkabili kwa upuuzi na upumbavu wake" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Kabla sijaanza kuongea kuhusu bandari,nizungumzie mambo matatu,la pili,unapoingia kwenye Utumishi wa Umma hauingii na faragha ya nyumbani kwako,hakuna baba,Mama,kaka,dada,unaingia kutekeleza kanuni,sheria na katiba ya nchi," Wakili Boniface Mwabukusi.

"Kabla sijaanza kuongea kuhusu bandari,nizungumzie mambo matatu,la tatu,ibara ya 34 ya katiba, Tanzania ni zao la Tanganyika na Zanzibar,tusiume ume maneno,sisi tupo Tanganyika sawa sawa na ibara ya 34,hakuna Tanzania bara hii ni Tanganyika" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Kabla sijaanza kuongea kuhusu bandari,nizungumzie mambo matatu,la tatu, Zanzibar ina bandari zake na Zanzibar ina bandari zake,tunapotaka kuingia mikataba ya Tanganyika lazima tushauliane vya kutosha na Watanganyika " Wakili Boniface Mwabukusi.

"Kabla sijaanza kuongea kuhusu bandari,nizungumzie mambo matatu,la nne,huu mkataba sio ghafla walikuwa wameuficha,wamekaa nao zaidi ya miezi tisa,mimi nimetumia dakika tano tu kuusoma nimejua mkataba huu haufai hata kuwa toilet paper ," Wakili Boniface Mwabukusi.

Wakili Boniface Mwabukusi; Mkataba wa bandari haufai hata kuwa toilet paper,hata mkataba wa Mzee Chifu Mangungo hauoni ndani hapa.

"Ndugu zangu Watanganyika mimi sina kipaji cha woga,kabla ya kuanza kuzungumzia mkataba huu wa bandari nilipiga hesabu zote,nikaiangalia Tanganyika yangu na uzao wake ndio nikatoka" Wakili Boniface Mwabukusi

"Wote waliohusika na mkataba huu wana ujasiri wa ajabu sana, hauwezi kurudi nyumbani ukawaambia watoto wako nimetoka kazini baada ya kusaini mkataba huu wa kipumbavu wa kuliuza taifa" Wakili Boniface Mwabukusi

"Waziri Mkuu,Spika na Waziri wa miundo mbinu hawafai kuchukua mshahara wa Watanzania hata muda huu tunavyoongea,hawafai hata kidogo kwa walichotufanyia kwenye mkataba huu" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Ili kuingia kwenye mkataba tunaangalia capacity to contract ile nguvu ya kisheria kuingia kwenye mkataba unayo!?Je Dubai ni nchi? is Dubai a state? Dubai sio nchi,sio state,katika sheria kuna mikataba miwili inayozungumzia kuingia kwenye mikataba,kuna Montevideo convention na Vienna laws to Treaty na kuna ,Dubai sio nchi,Ili unielewe kasome ibara ya 1,ibara ya 3,ibara 120,ibara ya 123 ya katiba ya Dubai,Dubai haina hadhi ya kuingia kwenye mkataba,huu mkataba mbovu ni wa wahuni tunao humu humu ndani na tutawajua tu"Wakili Boniface Mwabukusi

"Waziri anasema kulikuwa na tender ya kupata mwekezaji,amewahi kukwambia ni tender no ngapi,ilikuwa lini? Waziri ni muongo,fungua ukurasa wa 4 wa mkataba,unasema chanzo cha mkataba huu ni Mazungumzo ya Rais wetu Samia na Dubai Exco ya Feb 2022,Waziri hajasoma hii" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mwambieni Mbarawa awaonyeshe sehemu inayoonyesha tender kwenye mkataba huu,akiwaonyesha Mimi ninyang'anywe vyeti vyangu vyote niwe muuza parachichi" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Huu mkataba wa private company kati ya TPA na Dubai World ni kama mkataba wa dukani kuuza vitumbua,haukutakiwa kufika bungeni,lakini awa vilaza wamepeleka bungeni hili dude,kuna shida" Wakili Boniface Mwabukusi

"Mungu hawezi kushuka kutuambia mpo kwenye hali mbaya,Mungu ametupa tukio la kutuunganisha na kuungana kama taifa tutoke hapa tulipo twende mbele, viongozi wetu tunaomba mtupe ultimatum" Wakili Boniface Mwabukusi

"Ukurasa wa 9 wa mkataba huu unapingana na sheria za Umiliki wa ardhi wa mgeni,kwanini Dubai World apewe ardhi na apewe uwezo wa kuikodisha!? wakati ni kinyume na sheria ya nchi kwa mgeni!?" Wakili Boniface Mwabukusi.

"Wamewadanganya wataweka ukomo wa muda yaani time frame kwenye HGA,soma ibara ya 21 yaliyomo kwenye HGA,kuna mambo mengine kabisa hakuna ukomo wa muda,tumepigwa" Wakili Boniface Mwabukusi

"CCM is a vegetative party,ni genge la wanyang'anyi na wezi wa Mali ya Umma,bahati mbaya Watanzania ndani ya CCM ni wapole hawajui kinachoendelea ndani ya iko chama,CCM imetekwa na watu wasio waaminifu kwa Taifa la Tanzania" Wakili Boniface Mwabukusi

"ibara ya 21 ya katiba yetu inasema tutafuata sheria za Tanzania kwenye utatuzi wa migogoro ya rasilimali,IGA inatuambia tutafuata sheria za Uingereza,na HGA inatuambia tutafuata sheria za Tanzania,IGA na HGA nani yupo juu ya mwenzie,IGA na HGA zinapogongana tutamfuata nani? halafu awa mabwege wanatuambia tupo salama kwenye mkataba huu!" Wakili Boniface Mwabukusi
 
Duu hivi kumbe kweli tumeliwa mchana kweupeee kiutani utani!!!!!
Ohhh salalee Mtume simama
Tumeachiwa manyoya!!!

Ila Mungu yupo atalipa hapahapa Duniani
 
CCM is a vegetative party,ni genge la wanyang'anyi na wezi wa Mali ya Umma,bahati mbaya Watanzania ndani ya CCM ni wapole hawajui kinachoendelea ndani ya iko chama,CCM imetekwa na watu wasio waaminifu kwa Taifa la Tanzania" Wakili Boniface Mwabukusi
Huu ni ukweli
 
Ajibiwe kwa Hoja Basi siyo Polimilai.

Tenda ilitangazwa ama lah?...

IGA NA HGA zinakinzana ama lah?

Ndo vitu napenda sikia , siyo hiena hiena.
 
Back
Top Bottom