Wakili Masha alinufaikaje na Deep Green Finance?

Mkuu FMES,

Huyu Masha ukisoma tu ile hotuba yake pale ubalozi wa USA, unapata majibu yote kwamba alikuwa na mission ambayo alikuwa tayari kutumia kila njia kuitimiza.

Bahati nzuri Watanzania wameanza kuamka na wanamjua nani mkweli na nani anadanganya.

Huyu mheshimiwa ana maswali mengi ya kujibu. Mimi nakushauri mlete hapa JF, yeye ni kijana, anajua vizuri kutumia mtandao, ajitambulisha hata kwa siku moja ili kujibu maswali ya wana JF. Kama hana cha kuficha wala hawezi kuogopa kuja JF.
 
Mkuu FMES Sauti ya Umeme,
Kumbe vita dhidi ya ufisadi ni ngumu.Unafikiri wewe unavyokuwa unamwaga data zako kuhusu kina lowasa et al ulikuwa huumizii baadhi ya member hapa JF??HIVYO HIVYO NA KWA DATA HIZO HIZO LEO MASHA WANAMKOMA NYANI...ULICHONICHEKESHA WEWE UZALENDO UMEKUSHINDA UKAMKINGIA MASHA KIFUA.Mkuu usije ukawa umesahau hebu soma hapo juu ya screen yako kwenye maneno yaliyopambwa na kusomeka JAMIIFORUMS kuna vijimaneno chini yake vinavyoanza na "Where we Dare to..........."
 
Kiongozii FMSE, Heshima mbele Mkuu;

Ni vema tukajifunza uvumilivu hasa pale watu wanapoongea facts badala ya wewe kuwa dissapointed pale watu wanapohoji mambo ya kimsingi au wanataka kusema ya kweli.

Uliongea mengi sana kuwa wewe uko close naye na ukajenga mazingira halisi kuwa uko karibu sana na familia ile. Ukajibu hoja nyingi sana lakini ulipoulizwa katika hayo masuala mawili ukashindwa kujibu na kudai hutaongelea hilo. Kama hutaki kuwa dissapointed tuletee majibu ya mswali hayo kuwa alikwepaje JKT na aliingiaje UDSM bila kuwa na cheti cha JKT. I will be OK.

Kama kuna kiongozi yeyote unayemjua hata humu JF ambaye hapendi kufuata utaratibu na unamjua, jibu ni kumtaja na kumsaidia wapi alikosea na wala si kuwa na wasiwasi kuwa tutaibua mengi. Tumechoka sasa na haya mambo ambayo ndiyo yametufikisdha hapa tulipo miaka 47 baada ya uhuru ingawa tuna rasilimali zote za kuleta maendeleo. Inatia uchungu sana.

FMSE mimi ni moja kati ya watu wanaokuheshimu sana hasa kwa kuleta datas. Na nakuhakikishia kuwa post zako zote nimekuwa nikizisoma. Hunijui ni nani na wala mimi sikujui ni nani. Mhusika pia ni namfahamu kiasi japo inaweza kuwa si karibu sana kama wewe. Lakini inapokuja suala la ukweli na maslahi ya taifa, wengine sasa tumechoka na tumeamua kujitoa mhanga kwa ajili ya taifa hilia come what may. Just wait and see. Call a spade spade. Black balck and white white.

Katika uongozi historia na tabia ya mtu has something to do with the future. Hasa kama mhusika hataki kujisahihisha. Its is the history which shapes the future. Nina imani wahusika walikuwa wanajua ni nini kinaendelea katika suala la Deep Green hasa ukiangalia facts zote ambazo Dr. Slaa alizitoa bungeni.

Nakusihi na kukuomba kuwa, wakati huu ni wa kusimama pamoja na kuwa wakweli bila kujali kama mhusika mna uhusiano naye kivipi. Ni kwa kufanya hivyo mimi, wewe na wote tutalirekebisha taifa. Dawa ya jipu ni kulitumbua na kutoa usaha. Japo litauma lakini utapona. Sisi ni watu wazima, kubali kiungwana kuwa yatupasa tuwajibike.

Duh! Allien napenda kweli unavyoshusha vitu. Hebu kaa ulimwenguni kwa muda kidogo tunufaike na busara na hekima zako. Usirudi kule kwa Maallien wenzio maana hukawii kupotea tena kwa kipindi kirefu.
 
- Mkuu Allien nilifkiri you are for real, kumbe ni yale yale I am very dis-apponted! Mana kama ni tabia ya mtu kutofichika basi tutaibua wengi sana kuanzia humu JF! na hizi madas!

Ila kwenye hili ninaamini kuwa wakili wa Masha atasiamama mwenyewe kwa miguu yake na patakua patamu sana hapo na hii habari.

Sssssssssssss eti huyu ndiye FMES sauti ya mafisadi. Hivi kweli bado mnaamini data zake mpaka kumuita mzee wa madataz?
Huyu ni mmoja wao wala nchi na sasa ameguswa hasa na Masha wake. Hapa hana hoja labda matusi tu. Na naanza kumuamini kuhani kuwa anaandamwa sana na jamaa huyu kwa sababu alishagundua ni mbabaishaji tu hapa.
Nahisi Masha amemuahidi kwamba atagombea urais 2010 kwa hiyo atampa uwaziri mkuu, na kwa sababu hiyo anadhani naye atarudi hapa tz kutoka US aje kuwa kwenye cabinet. Atamtetea weeeeeeeeeee Masha wake hata kama mgeleta evidence zote.
Achaneni naye huyu!
 
Waziri Masha kwa umri ni mdogo (kulinganisha na timu ya baraza la mawaziri).

Inakubalika na wengi hapa kuwa kiutendaji Waziri Masha hana credibility yenye nguvu. Ingekuwa vema iwapo mwenye data akatudaidia kujua ni nani aliyempa nguvu ya kisiasa kufika hapo alipo kwa kasi (Naibu waziri na kuwa waziri katika kipindi cha miaka 3). Iwapo hakuna mtu yoyote nyuma yake kisiasa, nini ulikuwa mchango wake kwenye Chama Cha Mapinduzi kilichopelekea JK kumpa nafasi hii?
 
Duh! Allien napenda kweli unavyoshusha vitu. Hebu kaa ulimwenguni kwa muda kidogo tunufaike na busara na hekima zako. Usirudi kule kwa Mallien wenzio maana hukawii kupotea tena kwa kipindi kirefu.

Kiongozi Bubu;

Nimekusoma na tuko pamoja Mzee wa Ma-Breaking News.

Mkuu sina uhakika nina hekima na busara kiasi gani. Nasukumwa tu na uzalendo na uchungu wa nchi yangu.

Vijana wenzetu ambao tulifikiri wangekuwa mfano mzuri na kutoa changamoto kwa vijana wengine kuingia katika siasa wametuangusha. Tumepiga kelele miaka mingi vijana tupewe nafasi, baada ya kupewa tunasahau kupigania maslahi ya nchi. Inasikitisha sana.

Sipotei tena Mkuu, napiga Kambi hapa mpaka kieleweke. Nikishindwa hapa JF, natoka public kichwa kichwa . . . . Potelea pote, kama noma na iwe noma.
 
wana JF naomba kusisitiza kuuliza hili swali limeulizwa hapo juu. Hivi ni kitu gani Lau Masha kakifanya ambacho ni kizuri wakati bado hajawa kiongozi (Naibu/waziri) na kitu chochote kizuri ambacho amekifanya akiwa kiongozi? maana labda nasoma habari zake hapa JF tuu na hakuna lolote zuri linalosemwa juu yake.!? ni swali tuu
 
Kiongozi Mwanakijiji;

Huenda akawa ni mtu asiyependa kufuata utaratibu

Alikacha kupitia JKT

Aliingia UDSM kinyume na kigezo cha kupitia JKT

Unategemea nini? Tabia ya mtu haifichiki kwa muda mrefu.

Inapokuja suala la Opportunity na Maslahi ya taifa, chaguo liko wazi.

...Masha its time sasa....umekalia vitisho tuu na majungu na huna idea namna ya kuendesha Wizara bora utoke tuu sasa,at this age Waziri mzima bado una operate kwa vitisho vya siku saba....aibu saaaaaana!
 
Kila mara fedha za kifisadi zina laana na hazikawii kumtafuna kila aliyefaidika nazo kwa namna moja au nyingine. Tutashuhudia mengi kadri tunavyozidi kuwabana wahusika na punde si punde, kila utetezi kutoka kwao na washirika wao utazidi tu kuwafunua na kuweka wazi maovu yao. Kila watakapojaribu kujikwamua ndivyo watakavyozidi kudidimia kwenye shimo la tope kwa sababu tutahakikisha hakuna pa kushika. Vilio vyao vitakuwa kama muziki kwenye masikio yetu na mali walizokwapua kwenye hazina zetu ziwe chungu kama pilipili na wazirudishe wenyewe.

Kidogo kidogo washirika wao watajitokeza kwa umbo tofauti tofauti lakini hata wakijibadili kama kinyonga, harufu yao haifichiki - la kuvunda halina ubani. Kwa sasa bado wanakimbizana tu na vivuli vyao lakini tunaanza kuwamulika kutoka kila kona na vivuli vinaanza kupotea na hawana tena pa kuficha nyuso zao. Tuhakikishe tu kwamba tuna'charge' hizo betri tochi zetu ziendelee kutoa mwanga mkali mpaka mvunguni mwa vitanda vyao. Kamwe tusikubali nchi hii yenye milima na mabonde, maziwa na asali, dhahabu na almasi itafunwe na mchwa usiku na mchana.

This is the time to separate the men from the boys. A luta continua.......
 
Masha inadaiwa kuwa anasemea pembeni kuwa "haijui Deep Green Finance" kwa undani na kuwa alikuwa hajui kuwa fedha walizotumia DGF kuwalipa IMMMA zimechotwa Benki Kuu!! Na kuwa yeye hajaonja hata senti moja! Anasema watu wanamtafuta tu kwa sababu ya wivu na majungu!
 
Wivu na majungu ndiyo catch phrase ya wafamaji nini? Hata Lowasa naye alisema hivyo hivyo.
 
- Tik tak tik tak kweli JF tumeingiliwa sasa where is our credibility masikini wa Mungu sisi, what is the agenda? Yaani na sisi tumeingia vita vya urasi wa CCM?

Mungu atupishilie mbali sana haya mabalaaa!

Mzee ES kuna kitu unataka kutueleza sisi ambao tuko huku mbali ?Hebu sema usikike
 
Kama kuna vita vya urais CCM shauri zao.

Lakini usitegemee hata siku moja Masha ajipige risasi mguuni mwenyewe kama Plaxico Buress kwa kutoa siku saba kama Mzee wa Kiraracha halafu watu wakakaa kimya.
 
Masha inadaiwa kuwa anasemea pembeni kuwa "haijui Deep Green Finance" na kuwa alikuwa hajui kuwa fedha walizotumia DGF kuwalipa IMMMA zimechotwa Benki Kuu!! Na kuwa yeye hajaonja hata senti moja! Anasema watu wanamtafuta tu kwa sababu ya wivu na majungu!

Mzee Mwanakijiji;

Hapa nadhani si suala la majungu bali ni suala la uwajibikaji.

Inawezekana kweli alikuwa hajui, lakini maadamu sasa IMMMA imehusishwa na yeye wakati huo alikuwa kazini kama mmoja wa wamiliki, let him stand up and be a man!

Ajiuzulu na kuvipisha vyombo husika vifanye uchunguzi, baada ya hapo ukweli utajulikana. Shida ni kuwa, hawa wanasiasa wetu huwa hawakubali kirahisi hata wakiundiwa tume au evidence kupatikana mf. Karamagi, Msabaha, EL, Mramba, Yona, Chenge nk.

It is time now they take the responsibility.
 
Kiongozi Bubu;

Vijana wenzetu ambao tulifikiri wangekuwa mfano mzuri na kutoa changamoto kwa vijana wengine kuingia katika siasa wametuangusha. Tumepiga kelele miaka mingi vijana tupewe nafasi, baada ya kupewa tunasahau kupigania maslahi ya nchi. Inasikitisha sana.
SIZE]

Duh, kweli mzee. Masha ametuangusha mnooooooooooo. Nilipita mtaani nikasikia vijana wanamtosa eti "chinga jinga" !.
 
Masha ni fisadi na kuhusika kwake na ufisadi ni jambo ambalo nimekuwa nalisema toka wakati ule wa issue ya mwanahalisi na pia wakati wa issue ya Ridhiwani Kikwete na kampuni la kifisadi la IMMA (IMMMA).

Ugomvi wa Masha dhidi ya Mengi ni kwa sababu Thisday na Kulikoni wameendelea kushika bango ufisadi (wa deep green, kagoda nk) wakati ambapo Masha na serikali walitegemea watanzania kukaa kimya baada ya Mramba na Yona kupelekwa mahakamani.

Masha wewe ni fisadi, tena umeanza kutisha na hizi amri zako za siku saba. Kama bado unabisha basi unaweza kunipa mimi siku saba ili tukutane mahakamani. Nadhani mimi na wewe tunajuana vizuri sana na unajua kuwa najua kuwa unajua kuwa ninajua kile ambacho unajua kuwa ninakijua.

Msitari wa kuwaogopa mafisadi ulichorwa pale mlipoanza kutuma watu kuja US ili kujua wana JF..... nenda mahakamani kama hukupenda nilichoandika.
 
Mzee ES kuna kitu unataka kutueleza sisi ambao tuko huku mbali ?Hebu sema usikike

Lunyungu,

Ndugu yangu mfa maji haachi kutapatapa. Kidogo tunaanza kuwajua wabaya wetu - a man is judged by the company he keeps. Kuna wakuu ukiwagusa tu basi utabatizwa kila jina - kisa ushikaji. Wengine tumeshtuka zamani - birds of a feather fly together. Wengine tumeamua kumkoma nyani hata akivaa sura gani - hatuiangalii. Hakuna undugu, urafiki, ushikaji n.k. Tunatanguliza nchi yetu tunayoipenda kwanza - hayo mengine baadaye. Tik tak tik tak - time and tide waits for no man.
 
Masha ni fisadi na kuhusika kwake na ufisadi ni jambo ambalo nimekuwa nalisema toka wakati ule wa issue ya mwanahalisi na pia wakati wa issue ya Ridhiwani Kikwete na kampuni la kifisadi la IMMA (IMMMA).

Ugomvi wa Masha dhidi ya Mengi ni kwa sababu Thisday na Kulikoni wameendelea kushika bango ufisadi (wa deep green, kagoda nk) wakati ambapo Masha na serikali walitegemea watanzania kukaa kimya baada ya Mramba na Yona kupelekwa mahakamani.

Masha wewe ni fisadi, tena umeanza kutisha na hizi amri zako za siku saba. Kama bado unabisha basi unaweza kunipa mimi siku saba ili tukutane mahakamani. Nadhani mimi na wewe tunajuana vizuri sana na unajua kuwa najua kuwa unajua kuwa ninajua kile ambacho unajua kuwa ninakijua.

Msitari wa kuwaogopa mafisadi ulichorwa pale mlipoanza kutuma watu kuja US ili kujua wana JF..... nenda mahakamani kama hukupenda nilichoandika.

We dare talk openly here, hebu mwaga kuku kwenye mchele wengi tujue na sisi, tehe tehe tehe teh.
 
Masha ni fisadi na kuhusika kwake na ufisadi ni jambo ambalo nimekuwa nalisema toka wakati ule wa issue ya mwanahalisi na pia wakati wa issue ya Ridhiwani Kikwete na kampuni la kifisadi la IMMA (IMMMA).

Ugomvi wa Masha dhidi ya Mengi ni kwa sababu Thisday na Kulikoni wameendelea kushika bango ufisadi (wa deep green, kagoda nk) wakati ambapo Masha na serikali walitegemea watanzania kukaa kimya baada ya Mramba na Yona kupelekwa mahakamani.

Masha wewe ni fisadi, tena umeanza kutisha na hizi amri zako za siku saba. Kama bado unabisha basi unaweza kunipa mimi siku saba ili tukutane mahakamani. Nadhani mimi na wewe tunajuana vizuri sana na unajua kuwa najua kuwa unajua kuwa ninajua kile ambacho unajua kuwa ninakijua.

Msitari wa kuwaogopa mafisadi ulichorwa pale mlipoanza kutuma watu kuja US ili kujua wana JF..... nenda mahakamani kama hukupenda nilichoandika.

Bi. Mdogo, nilidhani hutomtolea uvivu; sasa kesho nadhani watanunua magazeti yotemaana kesho EPA itawekwa pembeni kidogo na watu kudili na ndugu yetu huyu. Natumaini watu wenye hekima watakuwa wamemkalisha chini kumpa ushauri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom