Wakili Masha alinufaikaje na Deep Green Finance? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wakili Masha alinufaikaje na Deep Green Finance?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mzalendo, Mar 11, 2008.

 1. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #1
  Mar 11, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  This is what IMMMA Advocates had to say in regards to MwanaHalisi's publications including its article published on Wednesday, March 5th.This was according to the DAILY NEWS, Monday, March 10, 2008; Please see attachment of the article unaltered, Asante.
   

  Attached Files:

 2. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mzalendo,

  Asante sana kwa hiyo attachment, hivi ni kwa mazingira gani hao lawyers wawili waliweza kuwa na hizo 1% shares kwenye hiyo kampuni? Je hilo ni jambo la kawaida?

  Hili jambo haliwezi kuisha mpaka Deep Green imechunguzwa mpaka mwisho. Inaelekea makampuni mengi makubwa ya sheria Tanzania ni ya kitapeli sawa tu na viongozi wetu.

  Kuna kila harufu ya ufisadi kwenye hili suala la Deep Green.
   
 3. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mafisadi ni mafisadi na wataalamu sana kwa kujitetea, Ndugu zangu MwanaHalisi wala msitishike na kauli hizo fanyeni kazi zenu za uchunguzi bila woga.
   
 4. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Jamaa hawana nyimbo, bila shaka wanahusika na huo ufisadi na ndio maana hakuna maombi ya msamaha kwa kuharibiwa jina. Kusema kuwa wameagiza wanasheria kuangalia uwezekano wa kushitaki gazeti kwa kudhadhalishwa na kuaribiwa jina, inaonyesha ni jinsi gani wanajua ukweli wa jambo lenyewe. Ningetegemea jamaa watoe siku kadhaa na kuombwa radhi na kwenda mahakamani.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huko mahakamani waende kweli maana isije ikawa changa la macho kama wakina Rutabanzibwa na Karamagi ambao mpaka leo jiiiiii!!!!!! toka walituahidi kwenda huko.........
   
 6. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Haendi mtu mahakamani, kwani IMMMA wanajua huko mengi yatajulikana. Kina Mgonja na Mkono hawakuwa wajinga kutokwenda. Wanajua wanachokifanya. Ila ushauri wa bure, kama hawatakwenda wenyewe basi siku si nyingi watapelekwa mahakamani pamoja na hao wanaowatetea.
   
 7. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nani aende mahakamani? IMMMA? Thubutu! Hiyo tisha toto tu! Wanajua wakienda tu itabidi soo lote libumburuke details zote za Deep Green, Tangold na wenzao itabidi zianikwe sasa mnadhani waliojichotea BOT kupitia makampuni hayo wataunga mkono jambo hilo?
   
 8. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Mwakilishi, I have liked your signature..."Dr Watson was right".
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mafisadi wameshaanza kutapatapa
   
 10. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Jamani its high time hawa wanasheria wetu wajue kwamba we are also Tanzanians and that most of the things happening in our country we know them. wasifikiri sisi tunaishi kwenye sayari ya Mars!

  Huyo Stella is just a junior Officer who graduated from UDSM just in 2003 na alikuwa ni Legal Officer pale..labda kama amepandishwa na kuwa associate juzi juzi. So it doesnt ring kwamba a junior Legal Officer ambaye amepewa kazi juzi kwamba angekuwa Director (though kisheria its possible, but reality transcends the statements made).wa Deep Green....These guys should know that we are better informed than what they think.

  Yes Ridhiwani can practice law like any other citizen. No doubt about that. What we contest however is to use his name and proximity to his father who happens to be the President of the Republic for scrupulous advantanges. They should stop. wasiibe resources zetu kwa kutumia mgongo wa siasa na majina yao. Thats what we object.

  Reading that press release one can easily know...ni lugha ya mfa maji..these people have nothing to contest. Kama wanajiamni waende mahakamani. Ukweli ni kwamba IMMMA kama wako clean basi waende mahakamani waone kama hawajafungua pandora`s box! (though najua iko siku litafunguka!

  Watanzania sio vichaa we know some of these dubious deals sema nyinyi mnafikiri kwamba wote ni akina Kalumanzira ambao hatujui kitu!

  But I am dissapointed kuona vijana kama akina Masha ambao wamejitahidi kwenye shughuli zao wanajiingiza kwenye deal chafu chafu kama hizi...do they really need kuiiba wafanikiwe? Well sitaki kumhukumu Masha so far, but really his involvement (through his law firm) Leaves many questions unanswered.
   
 11. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Naona IShengoma kapata kiburi sasa na ameanza vitisho bubu. Nenda mahakamani kama unaweza ili angalau watanzania wajue huu mzimu wa Deep Green na Tangold ni nini na ni nani wako behind it. Tumechoshwa na majibu ya serikali kuwa huu ni mradi wa usalama wa taifa wakati inajulikana kabisa kuwa top brass ya ccm inahusika hapa.

  Countdown imeanza sasa kwa IMMMA kwenda mahakamani kulishtaki gazeti la mwanahalisi...

  tik tak tik tak tik tak tik tak.......
   
 12. M

  Msavila JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 404
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Nani anaajiliwa au anaungana na IMMMA ni swala la strategic positioning for any business entity ambayo inania ya kuendelea na kupata faida. Hii ni kampuni binafsi hivyo tusiulize kwa nini wamemuajili au wanashirikiana na fulani. Swala je IMMMA licha ya kutoa huduma za kawaida za kisheria kwa Deep Green, je kuna sheria za nchi zilivunjwa? Je, ethically may be, unaweza kufacilitate kuanzishwa kwa kampuni yenye/ au itakayokuwa na mwenendo wa mashaka kama Deep Green halafu ujitetee ulikuwa ukitoa huduma tu? Hao mawakili wawili walioazimwa share moja ilikufanikisha uundwaji wa Deep green ni accomplices. Hebu fikiria unamwazima mtu bunduki ukijua anakwenda kuua, anaua, anakulipa na kukurudishia bunduki, bado si muhusika katika mauaji hayo. Offering legal service to shaddy companies does not put IMMMA in good limelight. Kwa utetezi huu kama unakubalika, Segerea na Ukonga etc. inabidi ziwe tupu, waliomo wanaonewa.
   
 13. canaan

  canaan Member

  #13
  Mar 11, 2008
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwa utetezi huu, ni sawa na kukiri makosa, umepewa hisa kwenye kampuni iliyohusika na ufisadi, utaacha kuwa mtuumiwa kweli?
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hawa sasa wana mwangusha mzee ES maana nilidhani watakuja na kukataa kwa kasi ile ile ya FMES kumbe wanasuausua wanampa wakati mgumu mtetezi wao na Masha jwa ujumla wake .
   
 15. d

  dwnmtz Member

  #15
  Mar 11, 2008
  Joined: Dec 18, 2007
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mimi nina wasiwasi kidogo hawa IMMMA wanaweza kwenda mahakamani kweli kwa sababu wana resource zote.

  Waziri aliyewatetea hata kabla hawajaenda huko mahakamai kwenyewe

  Jaji Mkuu

  Watoto wa Marais 2

  Na Mheshimiwa Muungwana mwenyewe

  Ni Bora Mwanahalisi wajiandae kwa hili mapema. Ila tupo pamoja
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wote ulio wataja wanazijua nguvu za Umma zilivyo na hasira ya Umma ikiamua kuwaangukia hawataweza. Unajua MwanaHalisi hawabahatishi wanajua wanacho kiandika hawawezi kungia kichw akichwa .Kama wao wanataka basi waende uone kama mahakama haitakuwa inajaa kusikia hoja maana mawakili wa kumwaga watajitokeza .
   
 17. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hawa wamekiri wenyewe kuwa ni MAFISADI.

  1. Wamesema wamefungua kampuni ya Deep Green mwaka 2004. ( Masha alitudanganya kuwa hajui chochote kuhusu deep green kwa kuwa yeye hakuwepo.)- UKWELI NI KUWA 2004 ALIKUWEPO IMMA NA ALIJUA KUHUSU SUALA HILI

  2. Wamesema Masha yuko likizo(Masha mwenyewe alisema amejiuzulu ukurugenzi- WATU WANAOJICHANGANYA NI ISHARA YA UWONGO NA KUFICHA MAMBO

  3. Wanasema walianzisha kampuni 2004. Hawazungumzi kwa kina kuhusu legal services walizozitoa baada ya kuanzishwa kwa kampuni hususani mwaka 2005. Wanataka umma udhani tu walianzisha wakaondoka. Kumbe walianzisha, wakajificha, wakarudi baadaye tena hadharani kuifilisi kampuni ambayo walijua kabisa ni ya KIFISADI

  4. WAMEKIRI KUPOKEA MALIPO TOKA KAMPUNI YA KIFISADI.

  Sasa kama wao ni kampuni ambayo inafuata maadili kweli kweli wajitokeze hadharani, wameseme wanajua nini kuhusu Deep Green na wenzake? Deep Green wako wapi? Kampuni ya mawakili ikiombwa kufanya representation lazima iwe na imani na inayemwakilisha, lazima imjue.

  Ama waseme waliwajua MAFISADI hao au HAWAKUFUATA TARATIBU ZA TAALUMA YAO NA KUTUMIWA NA MAFISADI

  Waziri wa Usalama wa Raia anaposhiriki kuwatapeli raia!

  Asha
   
 18. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #18
  Mar 12, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Wakati Rais akipigia kelele uhuru wa vyombo vya habari na maadili yake yafanye kazi kwa haki na upendo , kuna baadhi ya waandishi na wamiliki wa hivi vyombo vya habari viko mstari wa mbele katika kuhakikisha maadili hayafuatwi na hakuna uhuru wowote ule wanataka waendelee kudangana umma wa watanzania kwa kutumia vyombo hivyo wanavyoandikia au kuvimiliki .

  Kwa njia hiyo hakuna atakaye kaa kimya kungoja mpaka hawa waandishi na wamiliki wa vyombo hivi waendelee kuonea wananchi kwa kutumia taaluma au vyombo vyao hivi vyombo hivi na waandishi hawa wakemewe na ikiwezekanwa wafungiwe au kunyanyanywa leseni zao za kazi hizi .

  Ni wiki mbili sasa baada ya mimi binafsi kuanza kumtafuta Suedi Kubenea niweze kufanya nae mahojiano pamoja na kutengeneza kipindi maalumu kwa ajili ya mambo mbali mbali anayoandika katika gazeti lake la mwanahalisi .

  Nimemtafuta kwa njia ya simu , hiyo simu muda mwingi inaita tu haipokelewi kama ikipokelewa basi utasikia niko busy au katoka nashangaa jamani hivi mwanahabari anakuwaga busy asiweze kupokea simu zingine ? au ndio jeuri na nyodo zenyewe hizi ?

  Kwa kuwa nimemtafuta kwa muda mrefu ili aweze kuelezea baadhi ya mambo anayoandika katika magazeti yake na sisi tutengeneze makala kwa ajili ya wasomaji wengine kwa njia ya mtandao na kumkosa .

  Naamini moja kwa moja sasa Kubenea pamoja na gazeti lake la mwahalisi na Mseto wamekuwa wanacheza michezo ya kuigiza kwa muda mrefu sasa , umma wa watanzania inabidi iwaangalie kwa macho mengi zaidi kuliko yale yaliyokuwa yanawaangalia hapo mwanzo .

  Huwa nashangaa anajiamini nini kuandika vitu vya uzushi katika magazeti yake kisha anashindwa kuja mbele ya jamii husika kuelezea au hata pale anapopigiwa simu hataki kujibu kitu anakata au anasema ana kazi nyingi ?

  Kwa maana hiyo tukubali Sued Kubenea wafanyakazi wa mwanahalisi pamoja wengine wote anaoshirikiana nao kwa njia mbali mbali ni waongo na wazushi wanachonganisha watu kwa masilahi yao wao wenyewe .

  Taarifa iliyotolewa na kampuni ya IMMA and Advocates inadhibitisha hilo kwa zaidi ya asilimia moja nategemea IMMA and advocates watafikisha suala hili katika vyombo husika ili sheria ichukuwe mkondo wake .

  Mwisho kabisa napenda kumwomba Kubenea , gazeti la mwanahalisi , mseto waandishi wa magazeti hayo pamoja na wale wote anaoshirikiana nao katika kueneza chuki na uwongo katika jamii ya watanzania iliyojaa amani na upendo toka uhuru wake waombe radhi ya yale waliyoyafanya na wanayotarajia kufanya katika magazeti yao au vyombo vingine wanavyoshirikiana navyo mara moja watakaposoma ujumbe huu .

  La sivyo suala hili lifikishwe mbele ya vyombo vya sheria ili waitwe kuja kudhibitisha madai yao waliyoandika katika magazeti yao pamoja na yale wanayoshirikiana nao ili ummah watanzania wapate kujua ukweli .
   
 19. Ibambasi

  Ibambasi JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2008
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 6,634
  Likes Received: 2,445
  Trophy Points: 280

  Shy huhitaji kuwapigwa mkwara mbuzi MwanaHalisi na Kubenea wala pia huhitaji kuwa msemaji wa mafisadi.IMMMA wameshatoa press release yao na wanadai wamewaelekeza wanasheria wao what cause of action to follow.Pia hueleweki unataka nini kwa Kubenea,je hasira zako ni kumkosa Kubenea tu ndo utake kutoa vitisho?Mwenzio kweli yuko busy akifanya reseacrh ya habari za gazeti lake,hana muda na wapambe wa mafisadi kama wewe.if the story on IMMMA imekudistrub sana well take the lwad and put their defense i katika Habari Corp mafisadi wenzao.
   
 20. Mkanya

  Mkanya JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2008
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 600
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  HIVI JAMANI KWANI HAKUNA MTU ANAYE MFAHAMU HUYU SHY JINA KAMILI???
  LIWEKENI WAZI BASI MAANA ANATUVULUGIA UTARATIBU NA KUKASHFI CHOMBO CHETU CHA NEWS HUMU JF,KUBENEA ,NA WENGINE WATANZANIA WOTE WANA MUUNGA MKONO KAPONGEZWA BUNGENI ALAFU WEWE UNALETA POLOJO ZAKO HUMU,

  WEWE UTAKUWA UMEPEWA PESA NYINGI MNO.

  HUU SASA NI MSIMAMO WA WANA JF KUWA TUSISOME POST ZA HUYU JAMAA KATUMWA NA MAFISADI.SHAME ON YOU.
   
Loading...