Wakili Albert Msando akatwa katwa mapanga Dar

Wakili Albert Msando akatwa katwa mapanga Dar

Pole sana MAULANA atuepushe kabisa. ..dah!
 
Franklin D. Roosevelt Quotes. In politics, nothing happens by accident. If it happens, you can bet it was planned that way.
 
Ukiwa ktk gari ucku, mtu akikusimamisha, either kwa pikipiki au gari usishuke wala kufungua kioo, usijaribu hilo, kama una bastola weka standby asione, kisha ondoa gari, ukiona wanakufuata kwa kasi usisimame, elekea kituo cha karibu cha polisi, ukiona umezidiwa na bado wanataka kukushinda nguvu... DO THIS..

PARK HARAKA GARI PEMBENI YA BARABARA, TOKA, KIMBIA kwa kujibanza ukiinama karibu kama meter chache hv, au karibu na majengo ya karibu, kisha piga risasi kwa mfululizo kuwalenga na kujihami... then wahi police..!!
 
Kwani huyu Bwana hakuna kesi yenye mvutano ambayo yeye anatetea upande mmoja? Kama ipo ndiyo shughuli yenyewe
 
Mmh, Pole Wakili Msando
Something to learn about. ....
 
Mkirindi wala usisimame wala kuwasikiliza nakwambia wee chochea chombo tu mkuu. Kitendo cha kusimama tu umekwisha.

Jumamosi nimetoka zangu mbezi kwenye kwaito ya harusi ya rafiki yangu nikawa nimepakia mtu lifti nikamshusha pale mwenge ila muda mrefu kuanzia pale njia panda ya kawe kuna gari moja hivi ni saloon ilikuwa inanifuata nyuma na ilikuwa imebomoka taa moja niliona taa hiyo tukiwa kwenye taa za pale Lugalo. Ile nafika mataa ya moroco naona lile gari linaniwashia taa za honi nyingi nikajua leo ninalo nikahakikisha tu lock zote ziko vizuri baada ya mataa kuruhusu wakaendelea na honi zao na kuniwashia mataa ya kuniashiria nisimame na vile gari zilikuwa sio nyingi wakawa wanajitahidi kuniovertake na honi wanapiga mfululizo nilikanyaga mafuta huko mbele kote nilikuta green lights sikuwaona tena hadi naingia uswazi kwangu Tandika.

Ilikuwa naibiwa siku hiii na hawa ni wale wanakwambia kuwa umewagonga umewavunjia taa.kuna wanaotembea na pamber linaning'inia kuna waotembea na gari imebonyea upande mmoja yaani huu ni wizi mpya. Tuchukue tahadhari wengi inasemekana wanapark kwenye mabaa na kwenye kumbi za harusi ukitoka tu unao
Asante kwa tahadhari

Kweli mjini shule

Mbinu mpya kila kukicha
 
Tulisema akilimalizana n yule atakuja kwako akimalizana na wewe ataenda kwa wale na akimalizana na wale atakuja kwetu kama hujaelewa bwana Albert pole yako ungana na wanamabadiliko tumtoe LEMA N MAX KISHA SAA8 arudi akiwa salama
 
Hilo panga huenda lilikua na sumu. Ajipange. Asiichukulie kifacebook. Nchi ngumu hii
 
Na kweli na km wana kuandama na taa zao za hazard sehemu nzuri ya kusimaa ni kituo cha polisi au sehemu yenye mkusanyiko wa watu wengi nadhani ni suluhisho zuri tumefika pabaya kwa kweli sasa
Ila vituo vya polisi si vinafungwa usiku???? Itakuwaje??
 
Kumbe kisoma sana sio ndio kuelimika sasa wakili msomi kabisa pengine ana phd amewasaidia majambazi kumpora kisha analalamika huo ni uzembe wake kwanza inabidi achunguzwe na akikutwa alipanga huo mchezo ashitakiwe
 
Mara ya kwanza ilinitokea hii kitu, nje ya uwanja wa taifa kwenye mechi ya Tanzania vs Cameroon.. Daaah jamaa akawa analalamika nimemkanyaga, nikawa namwambia pole akaniachia, ile kupiga hatua moja tu nasikia simu yangu haipp mfukoni. Nikageuka nikakuta wanapeana ile simu nikamshika anirudishie simu akarudisha kwa aibu. WATU WA DAR HAWAKUNISAIDIA
Kuanzia siku ile nikawa nimeshajifunza, hivyo mpaka leo mtu akinizingua kwa style hiyo hawezi kunipata.

Hii ilinitokea Kariakoo mwaka 2008 wakati ndio simu za kichina zimeanza kuingia, nikawa nimenunua moja nzuri nzuri hivi.
Siku hiyo nikawa napita kando ya soko la kariakoo mara mzee mmoja kanikomalia kuwa nimemkanyaga, nikamwomba msamaha pale akaniachia, ile natembea kama hatua tano tu nikahisi mfuko wa suruali ni mwepesi simu ishachukuliwa. Naangalia pembeni naona watu wanacheka tu, nikaamua kurudi tu ubungo maana nishapoteza simu na akili ishaparanganyika!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom