Wakili Albert Msando akatwa katwa mapanga Dar

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
0b258c8f1ba3c0c8c2701acb17f49612.jpg

Haya ndio aliyoandika baada ya tukio!

Ndugu zangu, nawashukuruni wote mliojaribu kunitafuta na kunipa pole toka jana. Sikuwa napatikana kwa sababu walionivamia waliiba simu pamoja na vitu vingine.

Kilichotokea: Usiku wa saa tano siku ya Alhamisi (juzi) nilisimamishwa na gari baada kupigiwa honi na kuwashiwa taa na gari iliyokuwa nyuma yangu. Niliposhusha kioo driver akawa anaongea haraka haraka kwamba nimewagonga wakati narudi nyuma parking na nakimbia. Nikamjibu kwamba sijamgonga.

Akaniambia umetugonga angalia bampa. Kweli bampa lilikuwa limelegea. Ila sikuwa nimewagonga hivyo nikaendelea kubisha. Akaniambia shuka uangalie hata pembeni. Alikuwa amevaa smart tu so nikashuka. Wakati naangalia anaposema nimemgonga wakashuka wengine wawili kutoka kwenye gari na kunishika. Wakaanza kunishambulia huku wakinipora wallet, saa nk. Then wakanikata panga kichwani na kupekua gari wakaondoka na laptop na simu pamoja na funguo wa gari.

Kwa sasa naendelea vizuri baada ya kupata matibabu. Nawashukuru wote.

Albert Msando
 
Daaah police wetu huwezi wasikia wamewakamata watu kama hawa interijensia yao ipo kwa Lema na Max.....

Mungu mkubwa kama umepona kwanza shukuru kuna wakili mmoja wa Kenya miezi miwili iliyopita alitekwa na wateja wake na dereva wake wakauawa na kuwekwa kwenye mifuko na kutupwa kwenye mto uku wakiwa wamakatwa katwa na mapanga

Huyu hapa............
9a5704d84cb72d034af97d21b243db51.jpg


Very sad pole sana wakili....
 
0b258c8f1ba3c0c8c2701acb17f49612.jpg

Haya ndio aliyoandika baada ya tukio!

Ndugu zangu, nawashukuruni wote mliojaribu kunitafuta na kunipa pole toka jana. Sikuwa napatikana kwa sababu walionivamia waliiba simu pamoja na vitu vingine.

Kilichotokea: Usiku wa saa tano siku ya alhamisi (juzi) nilisimamishwa na gari baada kupigiwa honi na kiwashiwa taa na gari iliyokuwa nyuma yangu. Niliposhusha kioo driver akawa anaongea haraka haraka kwamba nimewagonga wakati narudi nyuma parking na nakimbia. Nikamjibu kwamba sijamgonga.

Akaniambia umetugonga angalia bampa. Kweli bampa lilikuwa limelegea. Ila sikuwa nimewagonga hivyo nikaendelea kubisha. Akaniambia shuka uangalie hata pembeni. Alikuwa amevaa smart tu so nikashuka. Wakati naangalia anaposema nimemgonga wakashuka wengine wawili kutoka kwenye gari na kunishika. Wakaanza kunishambulia huku wakinipora wallet, saa nk. Then wakanikata panga kichwani na kupekua gari wakaondoka na laptop na simu pamoja na funguo wa gari!!

Kwa sasa naendelea vizuri baada ya kupata matibabu. Nawashukuru wote.

Albert Msando
Ndio nani huyo tutambulishe mkuu
 
Nampa pole ndugu Albert, huu ni dhahiri ujambazi wa aina mpya kabisa. Tumepata fundisho, mtu akijaribu kukusimamisha na kavaa vizuri , usikubali mwambie tuongozane mpaka kituo cha polisi karibu na hapo. Na mwambie chukua nbr ya gari kama anafikiri utakimbia.

Kwa wale wapendao kuzusha mambo na kuwachonganisha watanzania haya fursa hiyo, njooni muitumie kujenga hoja zenu za kinafiki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom