Wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu? Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji? Wajua ubakaji unaweza kuwa alali? IGA batili yaweza kuzaa HGA halali?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,911
114,697
Wanabodi,

Hili ni bandiko la kitu kinachoitwa critical thinking, kama wewe sio critical thinker, nakushauri pita mbali na bandiko hili.

Angalizo la Uzalendo
Watanzania ni watu wa kuridhika kirahisi na sio watu wa kuhoji, hivyo unapotokea mtu kuhoji baadhi ya mambo makubwa kama haya, na kufuatia kuna baadhi ya watu wameupinga mpango huu, hivyo unawekwa kwenye kundi la wapinzani, na ukaonekana sio mzalendo, hivyo naomba nianze kwa declaration ya uzalendo na kusisitiza mimi sio mpinzani wa mpango huu, na bandiko hili limetanguliwa na mabandiko yangu matatu kuusuport mpango huu
1- Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe!. Je DPW Tunapigwa?.

2- Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!

3- Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie? hivyo nawaomba sana wasomaji wangu, msiwe na wasiwasi kabisa kuhusu uzalendo wangu kwa nchi yangu!.

Haya ni maswali critical, yanayotokana na critical thinking na critical analysis kwa lengo la kuwaelimisha Watanzania some complex issues kwa kutumia mifano rahisi ya vitu vya everyday life.
Haya ni maswali critical, yanayotokana na critical thinking na critical analysis kwa lengo la kuwaelimisha Watanzania some complex issues kwa kutumia mifano rahisi ya vitu vya everday in our life.

Maswali yenyewe ni

Je, wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu?. Vivyo hivyo kuna mikataba halali, batili na batilifu.​

IGA ya serikali yetu na DPW iliyoridhiwa na Bunge letu tukufu ni IGA halali, Batili au Batilifu?​

IGA hiyo inakwenda kuzaa ndoa ya TPA na DPW, jee ndoa hii ni halali, batili, batilifu au ni Ubakaji tuu?​

Je, wajua japo ubakaji ni kosa la jinai, lakini ubakaji unaweza kuzaa ndoa halali?.​

Jee Wajua IGA batili Inaweza kabisa kuzaa HGA halali?​

Nimekuwa nikitumia mifano hii ya ndoa kwa hoja nyingi humu baadhi yake ni hizi Ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu. Je, wajua pia kuna msamaha halali wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu? Msamaha ule ni batilifu!

Andamana nami...

1. Je, wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu?​

Ndoa ni mkataba wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata utaratibu uliowekwa na jamii. Kwa Tanzania tuna ndoa za aina tatu, za Kiserikali, Kidini na Kimila.

Sifa Kuu za ndoa ni muungano wa hiari baina watu wawili wa jinsia tofauti waliamua kuishi pamoja na kujenga familia na unaingiwa kwa ridhaa consent.

Ndoa Halali, Batili na Batilifu.
Ndoa ni mahusiano ya mapenzi kati ya watu wa jinsia tofauti ambayo huingiwa kwa hiyari na ridhaa, na kufungwa kwa mkataba wa ndoa au cheti cha ndoa, kwa jina maarufu la shahada ya ndoa.

Ndoa baada ya kufungwa kimila, kidini au kiserikali, na kukabidhiwa vyeti vyenu vya ndoa pale kanisani, msikitini , kwa DC au kwa kamishina yoyote wa ndoa, ili ndoa hiyo iwe ni ndoa halali, lazima ikamilishwe kwa performance ya kitu kinachoitwa "consummation", yaani ili ndoa iwe halali ni lazima ndoa hiyo iwe consumated.

Ikitokea kwa sababu yoyote, ndoa ile baada ya kufungwa, lakini ikashindwa kuwa performed, or consummated, ndoa ile inakuwa ni ndoa batili, yaani void marriage, hii void marriage ni ndoa cheti tuu lakini kiuhalisia ni kunakuwa ni hakuna ndoa iliyowahi kuwepo, yaani "void ab initio". Kinachotakiwa kufanywa kwenye ndoa ya aina hii, ni kuripotiwa kunakohusika na ndoa hii kuvunjwa.

Ikitokea kwa sababu yoyote, ndoa ile baada ya kufungwa, lakini ikashindwa kuwa performed, au consummated, kwa kipindi fulani, kwa panic attack, ugonjwa, njia nyembamba, etc, then ndoa ile inakuwa ni ndoa batilifu, yaani voidable marriage, hii voidable marriage sio ndoa halali, na sio ndoa batili bali batifufu. Ule ubatilifu utakapo ondolewa na performance kufanyika kwa kui consumate, inageuka ndoa halali, ikishindikana kuwa consumated then inageuka ndoa batili.

2. Vivyo hivyo kuna mikataba halali, batili na batilifu​

Kama ulivyo mkataba wa ndoa, vivyo hivyo kwenye mikataba ya Kitaifa na Kimataifa.

Kwa mujibu kifungu cha 2(1) (h) cha Sheria ya mikataba Sura ya 345 (2002) kinasema, “Mkataba ni makubaliano yanayofanyika kati ya mtu mmoja na mwingine ambayo yana lengo la kuwa na nguvu ya kisheria.” Kifungu hicho pia kinasema “mkataba ni makubaliano ya kisheria kati ya pande mbili au zaidi yanayoeleza haki na wajibu wa kila upande. Mgawanyo wa aina za mikataba unategemea na muktadha wa kimazingira. Kama tunataka tutumie maandishi kuigawanya; itaitwa mikataba ya maandishi (written) na mikataba ya maneno (oral).
Kama mtu anataka kutumia uhalali; ataita mikataba halali (legal), mikataba batili (void) na mikataba batilifu (voidable). Kama kigezo ni utekelezaji itaitwa mikataba iliyokwisha tekelezwa (executed) na mkataba utakaotekelezwa baadaye (executory), mikataba ambayo upande mmoja umeshatimiza wajibu wake (unilateral) na mikataba ambayo pande zote zinapaswa kutimiza wajibu wake baada ya kusainiwa (bilateral)

3. IGA ya serikali yetu na DPW iliyoridhiwa na Bunge letu tukufu ni IGA halali, Batili au Batilifu?​

Uhalali wa hii IGA ndio the on going debate kati supporters wa hii IGA na Wapinzani wa hii IGA.
Hapa mimi pia kama mwanasheria na wakili, nimetoa maoni yangu hapa Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
Naendelea kusisitiza ile IGA iliyoridhiwa na Bunge letu Tukufu, ni makubaliano tuu na sio mkataba!.

Jee IGA hii ni halali au batili?.
Kwa vile na mimi ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, mapungufu kisheria niliyo yaainisha kwenye hii IGA, yanaibatilisha na kuifanya ni null and void ab initio.
Hoja zangu ni hizi
.
 1. Utapeli wa kwanza mkubwa, ni hakuna mtu yoyote kati yetu aliyefanya a due diligence report ya DP World, tukaletewa, mfano mzuri ni hawa jamaa walipewa kuendesha Bandari 6 za Marekani, Bunge la Congress la Marekani lilawakatalia!. Wenzetu walipiga kura mmoja mmoja kwa majina, sisi Bunge letu limepitisha kitutusa kwa kura za gulio!. Tunaelezwa DPW ni Governmental Organisation, wakati sii kweli, it's a private company!. Kabla ya kuingia mkataba wowote, lazima kwanza kufanyike kitu kinachoitwa a due diligence process na kutolewa a due diligence report. Hili halikufanyika hivyo serikali yetu kujikuta inaingia mkataba wa kimataifa na parties to contract who has no capacity to contract international treaty hivyo ku vitiate makubaliano kugeuka void hivyo makubaliano hayo yanakuwa null and void ab initio!. NB. Mtu au kampuni, taasisi yoyote ya Kitaifa au kimataifa, inaweza kuingia mkataba na mtu, kampuni, serikali lakini sio an international Treaty, ya kuhitaji ratification ya Bunge letu, bali ni international contracts or agreements za non state parties.
 2. Mkataba wa IGA ni wa state parties inaingiwa kati ya serikali za nchi na nchi, hivyo ukisoma documents za makubaliano utaona ni kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya UAE, lakini ukija kwenye signatories kwa serikali ya Tanzania ni signatories wa serikali kweli, lakini kwa serikali ya UAE, signatories ni Mwarabu wa Dubai wa DP World na sio serikali ya UAE!. Kwenye mkataba wameandika serikali ya Dubai, Dubai is not a state, hivyo hapa kunauwezekano tunatapeliwa!. Serikali yetu inaingizwa mkenge kuingia mkataba state parties na a private company disguised as a state party or government of UAE kumbe ni kampuni binafsi!.View attachment 2653406
 3. Mikataba hii ya kimataifa inaongozwa na The Geneva Convention. Subscribes wa Geneva Convention ni state parties, Tanzania na UAE, Dubai sio subscriber wa Geneva Convention, hivyo ikitokea DPW ametukosea, sisi hatuna pa kumshitaki ila sisi tukimkosea anatushitaki!.
 4. Mkataba Kati ya serikali ya Tanzania na Dubai ni batili kwenye sheria za kimataifa. Maana Dubai sio nchi, a sovereign state kama ilivyo Tanzania, Dubai hapa inajitambulisha kama a State Party, Dubai is not a state hivyo haiwezi kuwa a state party, it has no the capacity to transact as an international state IGA, haiwezi kuingia mikataba ya kimataifa na nchi na nchi!, inaweza kuingia mkataba wa kimataifa wa nchi na kampuni au kampuni na taasisi kama ilivyoingia na mamlaka ya Bandari, taasisi kwa taasisi, kama ilivyofanya hapa View attachment 2653409ambapo DP World iliingia mkataba na Mamlaka ya Bandari TPA, mkataba ambao Rais Samia aliushuhudia ukisainiwa kule Dubai during Expo Dubai.
 5. Sasa kampuni hii ya DP World iliyoingia mkataba na mamlaka ya Bandari, sasa inajigeuza nchi, sovereign state of Dubai, imeingia mkataba wa kimataifa wa state party na serikali yetu!, huku ni kututapeli!. Dubai is not a state, it's not a nation na nchi isiyo na sovereignty!. DP World is not a state, it's a private company, hapa imejigeuza ni nchi!. Huu sio utapeli?. View attachment 2653458
 6. Mikataba ya kimataifa ya state parties, inaingiwa kati ya nchi na nchi, hapa nchi inayotambuliwa ni Falme ya Kiarabu, UAE, ndio inayotambulika kwenye sheria za kimataifa as a state, na sio Dubai ambayo ni sehemu ya UAE, sio state, hivyo hapa kuna utapeli!. Due diligence ingefanyika, hili lingeonekana!. Kwenye hii IGA, hakuna popote panapoonyesha uhusika wa UAE!.
 7. Status ya Dubai kwe UAE ni sawa na status ya Zanzibar ndani ya JMT, Zanzibar has no capacity to transact an international treaty kwasababu Zanzibar sio nchi, ni mji tuu, sio sovereign state, haina sovereignty. Dubai pia sio sovereign, hivyo mikataba yote ya kimataifa ya Zanzibar, inaingiwa na JMT kwaniaba ya Zanzibar, IGA na HGA inapaswa kuingiwa kati ya Tanzania na UAE na sio Tanzania na Dubai!.
 8. Hii IGA ya DPW na Tanzania ni fursa kwa Zanzibar kufungua macho na yeye kuwa na haki za kuingia mikataba ya kimataifa bila kuihusisha JMT!. Kama hili limewezekana kwa Dubai, linashindikana vipi kwa Zanzibar?.
 9. DPW ni kampuni kama inavyoonyesha hapaView attachment 2653462
 10. Wanasheria wanapoamua kufanya magumashi ya kisheria, wanakuzuga kwa maneno ya kweli kwenye mkataba, mfano hapa Dubai inatambulishwa kama nchi,View attachment 2653466lakini mkataba wetu hii iliyoandikwa kama nchi, sio nchi kweli bali ni kampuni ya DPW!.
 11. Kwa vile kwa upande wetu ni serikali yetu, ili kuonyesha IGA ni kati ya serikali mbili, hapa wameitaja kampuni ya kiserikali ili kuiserikalisha kampuni binafsi ya DPW kuwa ni serikali View attachment 2653471
 12. Hivyo mikataba ya HGA utaokuja kuingiwa na serikali yetu, sio mkataba wa kimataifa wa kiserikali kati ya serikali yetu na DPW, lakini hakuna chochote cha UAE bali kampuni binafsi ya DPW iliyoserikalishwa na kujifanya ni serikali!.View attachment 2653477View attachment 2653481
 13. Kwa vile mikataba ya kimataifa inahusisha state parties, HGA inayokwenda kuingiwa ni HGA kati ya nchi ya Tanzania ambayo ni state na kuingia na DPW iliyo ji stetisha kama a state ambapo huu pia sio utapeli?.View attachment 2653488
 14. Kwa Tanzania mamlaka yote ya nchi, mtu yoyote ili asaini mkataba wa kimataifa wa kuiingiza nchi, anapaswa apewe the Power of Attorney na Rais wa JMT. Hii hapa chini ni POA ya Rais Samia kumpa mamlaka Prof. Mbarawa kuingia huo mkataba kwa niaba ya Tanzania, View attachment 2653454POA hii kisheria ni defective, kwasababu japo imesainiwa na Rais Samia, lakini haina muhuri wa rais, au muhuri wa serikali, hizi documents za kisheria ikisemwa POA must be signed and stamped by the official seal, lazima iwe hivyo, not otherwise!, kama walivyofanya hawa counter parts hapa chini.View attachment 2653455
 15. Ili serikali yetu iingie kwenye mkataba wa kihalali wa kimataifa na taasisi ambayo sio nchi, kulitakiwa kuwepo POA toka UAE kuipa mamlaka Dubai kuingia mkataba wa kimataifa kwa niaba ya UAE, then ndipo Emirate wa Dubai angeweza kuwapa POA DPW kujigeuza ni nchi.
 16. Hapa Prof. Mbarawa katika kusaini almanusura . . View attachment 2653452
 17. Hakuna ubaya wowote kwa kampuni yoyote kuingia mkataba na serikali under PPP, lakini hili la kampuni binafsi iliyo serikalishwa kuingia an International treaty na serikali yetu, halikakaa vizuri!.
 18. Kwa vile Bandari iko chini ya sheria ya national wealth, sheria zetu ziko wazi kuwa kesi zote zitaamuliwa nchini kwa sheria zetu. Kitendo cha hii IGA kuzungumza usuluhishi nje ya nchi, ni kuingia illegal agreement.!. Illegality kwenye any agreement, renders this IGA illegal, hii illegality renders this IGA null and void ab initio!.

4. IGA hiyo inakwenda kuzaa ndoa ya TPA na DPW, kupitia HGA. jee ndoa hii ndoa halali, batili, batilifu au ni Ubakaji tuu?.​

Kwa vile kwa hoja zangu za kisheria, hii IGA ni null and void, hivyo HGA, inayokwenda kuzaliwa kati ya TPA na DPW ni ubakaji!.

5 Je, wajua japo ubakaji ni kosa la jinai, lakini ubakaji unaweza kuzaa ndoa halali?​

Japo ubakaji ni kosa la jinai, lakini amini usiamini, kuna mahusiano yanaanzishwa kwa ubakaji halafu yakaja kuzaa ndoa halali yenye upendo.

Ubakaji katika Mila za Kiasili za Kiafrika
Hakuna issues za consent kwenye ndoa nyingi za kimila na za kidini, ni arranged marriages hivyo ndoa hizi ni halali kisheria lakini hazina consent hivyo ni ubakaji!.

Usukumani kuna ngoma ya Chagulaga, ngoma ile ni ubakaji per se!.

Zanzibar baada ya Mapinduzi Matukufu, watwana walijitwalia mabinti wa mabwana na kuwabaka na kuwaoa kwa lazima!.

Hata katika jamii zetu nyingi, mabinti wanabakwa kila uchao, wakijikuta wamepata ujauzito, hufukuzwa kwao na kwenda kuishi na mbakaji!.

Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971, mke hawezi kubakwa na mumewe!.

6. Wajua IGA batili Inaweza kabisa kuzaa HGA halali?.​

Kwa mujibu wa hoja zangu, kuna lots of mikataba batili lakini ikazaa matunda mema!. Ubatili kwenye mikataba hiyo ni ubatili wa kisheria lakini ikahalalishwa by performance!.

Mtu aliyebakwa, akashika ujauzito wa mbakaji, akaamua kuishi na mbakaji, atahesabika anaishi kwenye dhana ya ndoa, presumption of marriage na atahesabiwa ame consent!.

Makubaliano ya muungano wetu, Articles of The Union, zimekuwa ratified upande mmoja tuu wa muungano, Bunge la Tanganyika, lakini Zanzibar, hakukufanyika ratification yoyote, Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?
hivyo ku vitiate mkataba wa muungano kwa kukosekana consent ya Zanzibar, lakini kwasababu Zanzibar ametimiza vipengele vya muungano, inahesabika Zanzibar ime consent by performance!.

Mwanamke akibakwa, halafu akaendelea kuishi na mbakaji na kutimiza wajibu wa ndoa, then atahesabika ame consent na hiyo ndoa inakuwa ni ndoa halali!.

Mtoto anayezaliwa bila ndoa ni mwanaharamu, lakini ukiamua kumuoa huyo mwanamke, then kitendo hicho kinaifuta ile haramu ya huyo mtoto na kumfanya ni mtoto halali mbele ya macho ya watu!.

Hivyo japo hii IGA ya DPW ina makasa mengi, ya kisheria yanayoipa ubatili, bila uhalali, lakini HGA itakavyo zaliwa IGA batili, inaweza kuwa ni HGA halali!.
Hitimisho
Kwa vile katika kuileta DPW, Rais Samia ana nia njema ya dhati kuisaidia nchi yetu, na hakuna mtu yoyote anayepinga uwekezaji kwenye Bandari zetu, wasaidizi wa rais na sisi Watanzania wengine wote tuna wajibu wa kumsaidia rais wetu, kuisaidia serikali yetu na kulisaidia taifa letu to do the right thing and do them right!. Huu ndio uzalendo wa kweli. Hivyo ile IGA ni IGA batili, void ab initio, lakini itazaa HGA halali kabisa!. Kitu muhimu ambacho serikali yetu itapaswa kukifanya ni kuwa very transparent ili kuwaonyesha Watanzania jinsi batili inavyoweza kugeuka halali.

Paskali
 
Wanabodi
Hili ni bandiko la kitu kinachoitwa critical thinking, kama wewe sio critical thinker, nakushauri pita mbali na bandiko hili.

Naomba usichangie kwanza hoja zinafuata....
Paskali
Pascal uzi tayari au?

Maana heading inashawishi mtu kufungua uzi asome ila uzi wenyewe ni vitisho kwa non critical thinkers.

Uzi tayari.
 
Wanabodi
Hili ni bandiko la kitu kinachoitwa critical thinking, kama wewe sio critical thinker, nakushauri pita mbali na bandiko hili.

Naomba usichangie kwanza hoja zinafuata....
Paskali
Kaka Paskali,
Fedha zilizopatikana kwa njia ISIYO halali, zikiingizwa kwenye shughuri halali, au zikatumika kuanzisha shughuri halali, tunaita utakatishaji wa fedha. Hii ina maana kuwa ili kitu kiwe halali, the entire process inatakiwa iwe halali. Kwa muktadha huu, IGA Batili HAIWEZI kuzaa HGA Halali.
 
Jee wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu?. Vivyo hivyo kuna mikataba halali, batili na batilifu.
Ndoa ambazo zimeonekana kuwa batili zinaweza kuhitaji kubatilishwa badala ya talaka! Vivyo hivyo, Mkataba unaonekana ni batili unaweza kubatilishwa.

Sasa Ndoa batili ni ipi?
Wajuvi wa Sheria za ndoa wanasema Ndoa batili ni, mpangilio wa ndoa ambao hautambuliwi kama halali na sheria....
Ndoa yetu ina Uhalali? Na uhalali huo tumeupata wapi? Na tumepata kwa kwa Sheria ipi?
Mpaka hapa tulipo Ndoa yetu(Tanzania na DPW) imepata uhalali na IGA na baada ya Bunge letu kujadili na kuridhia mkataba wa ndoa yetu?, yaani Bunge limekubali kuwa , Wazazi wetu Tanzania na DPW wamekidhi yote yanayotakikana kabla ya ndoa i.e Umri wetu,
makazi yetu, mamlaka yetu, wajibu wetu, wapi na lini tunaweza peana talaka kwenye ndoa n.k n.k Je, masuala ya uhalali wa ndoa yetu walioridhia yamewekwa bayana? Na kama hayako bayana wamehalalisha ndoa iliyo batili?

Kwa hayo tunaweza kusema Uhalali wa Ndoa ya Nchi zetu mbili una mashaka. na kukiwa kuna mashaka tunaweza peana talaka sasa Tunapeana vipi talaka ndoa ambayo tayari inaonekana ni batili?

Ubatili wa Ndoa yetu Ubatilishaji wake:

Again, wajuvi wanasema

"Ubatilishaji (wa ndoa)ni mchakato wa kisheria wa kubatilisha ndoa"
Ni nani mpaka hapa tulipofikia anaye mamlaka ya kubatilisha ndoa yetu?

Maswali ya Pascal yapo loaded kweli kweli!

Sasa kwaavile mimi sio mwanasheria nitagota hapo.
 
Wanabodi
Hili ni bandiko la kitu kinachoitwa critical thinking, kama wewe sio critical thinker, nakushauri pita mbali na bandiko hili.

Haya ni maswali critical, yanayotokana na critical thinking na critical analysis kwa lengo la kuwaelimisha Watanzania some complex issues kwa kutumia mifano rahisi ya vitu vya everday in our life.

Maswali yenyewe ni

Jee wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu?. Vivyo hivyo kuna mikataba halali, batili na batilifu.​

IGA ya serikali yetu na DPW iliyoridhiwa na Bunge letu tukufu ni IGA halali, Batili au Batilifu?​

IGA hiyo inakwenda kuzaa ndoa ya TPA na DPW, jee ndoa hii ni Ubakaji?.​

Jee wajua japo ubakaji ni kosa la jinai, lakini ubakaji unaweza kuzaa ndoa halali?.​

Wajua IGA batili Inaweza kabisa kuzaa HGA halali?.​

Nimekuwa nikitumia mifano hii ya ndoa kwa hoja nyingi humu baadhi yake ni hizi Ndoa halali, ndoa batili na ndoa batilifu. Je, wajua pia kuna msamaha halali wa kweli, msamaha batili na msamaha batilifu? Msamaha ule ni batilifu!

Andamana nami...
 1. Jee wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu?​

Ndoa ni mkataba wa kuishi pamoja kati ya mume na mke kwa kufuata utaratibu uliowekwa na jamii. Kwa Tanzania tuna ndoa za aina tatu, za Kiserikali, Kidini na Kimila.

Sifa Kuu za ndoa ni muungano wa hiari baina watu wawili wa jinsia tofauti waliamua kuishi pamoja na kujenga familia na unaingiwa kwa ridhaa consent.

Ndoa Halali, Batili na Batilifu.
Ndoa ni mahusiano ya mapenzi kati ya watu wa jinsia tofauti ambayo huingiwa kwa hiyari na ridhaa, na kufungwa kwa mkataba wa ndoa au cheti cha ndoa, kwa jina maarufu la shahada ya ndoa.

Ndoa baada ya kufungwa kimila, kidini au kiserikali, na kukabidhiwa vyeti vyenu vya ndoa pale kanisani, msikitini , kwa DC au kwa kamishina yoyote wa ndoa, ili ndoa hiyo iwe ni ndoa halali, lazima ikamilishwe kwa performance ya kitu kinachoitwa "consummation", yaani ili ndoa iwe halali ni lazima ndoa hiyo iwe consumated.

Ikitokea kwa sababu yoyote, ndoa ile baada ya kufungwa, lakini ikashindwa kuwa performed, or consummated, ndoa ile inakuwa ni ndoa batili, yaani void marriage, hii void marriage ni ndoa cheti tuu lakini kiuhalisia ni kunakuwa ni hakuna ndoa iliyowahi kuwepo, yaani "void ab initio". Kinachotakiwa kufanywa kwenye ndoa ya aina hii, ni kuripotiwa kunakohusika na ndoa hii kuvunjwa.

Ikitokea kwa sababu yoyote, ndoa ile baada ya kufungwa, lakini ikashindwa kuwa performed, au consummated, kwa kipindi fulani, kwa panic attack, ugonjwa, njia nyembamba, etc, then ndoa ile inakuwa ni ndoa batilifu, yaani voidable marriage, hii voidable marriage sio ndoa halali, na sio ndoa batili bali batifufu. Ule ubatilifu utakapo ondolewa na performance kufanyika kwa kui consumate, inageuka ndoa halali, ikishindikana kuwa consumated then inageuka ndoa batili.

Vivyo hivyo kuna mikataba halali, batili na batilifu​

Kama ulivyo mkataba wa ndoa, vivyo hivyo kwenye mikataba ya Kitaifa na Kimataifa.

Kwa mujibu kifungu cha 2(1) (h) cha Sheria ya mikataba Sura ya 345 (2002) kinasema, “Mkataba ni makubaliano yanayofanyika kati ya mtu mmoja na mwingine ambayo yana lengo la kuwa na nguvu ya kisheria.” Kifungu hicho pia kinasema “mkataba ni makubaliano ya kisheria kati ya pande mbili au zaidi yanayoeleza haki na wajibu wa kila upande. Mgawanyo wa aina za mikataba unategemea na muktadha wa kimazingira. Kama tunataka tutumie maandishi kuigawanya; itaitwa mikataba ya maandishi (written) na mikataba ya maneno (oral).
Kama mtu anataka kutumia uhalali; ataita mikataba halali (legal), mikataba batili (void) na mikataba batilifu (voidable). Kama kigezo ni utekelezaji itaitwa mikataba iliyokwisha tekelezwa (executed) na mkataba utakaotekelezwa baadaye (executory), mikataba ambayo upande mmoja umeshatimiza wajibu wake (unilateral) na mikataba ambayo pande zote zinapaswa kutimiza wajibu wake baada ya kusainiwa (bilateral

3

IGA ya serikali yetu na DPW iliyoridhiwa na Bunge letu tukufu ni IGA halali, Batili au Batilifu?​

Uhalali wa hii IGA ndio the on going debate kati supporters wa hii IGA na Wapinzani wa hii IGA.
Hapa mimi pia kama mwanasheria na wakili, nimetoa maoni yangu hapa Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
Naendelea kusisitiza ile IGA iliyoridhiwa na Bunge letu Tukufu, ni makubaliano tuu na sio mkataba!.

Jee IGA hii ni halali au batili?.
Kwa vile na mimi ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea, mapungufu kisheria niliyo yaainisha kwenye hii IGA, yanaibatilisha na kuifanya ni null and void ab initio.
Hoja zangu ni hizi
 1. Capacity ya Dubai to transact an international Treaty, Dubai sio a sovereign state, hivyo has no capacity to contract an international Treaty na Tanzania.
 2. Wenye uwezo huo ni UAE.
 3. Ile IGA imeingiwa na serikali yetu na kampuni ya DPW, hivyo hapa DPW imeji inchisha!. Hii capacity to contract ina I vitiate hii IGA na kuifanya ni null and void.
 4. Power of Attorney ya Rais Samia kumruhusu Prof. Mbarawa kusaini ile IGA, is signed, but not stamped!. Haina seal, hii inaifanya hiyo IGA kuwa voidable
 5. Kwa vile Bandari iko chini ya sheria ya national wealth, sheria zetu ziko wazi kuwa kesi zote zitaamuliwa nchini kwa sheria zetu. Kitendo cha hii IGA kuzungumza usuluhishi nje ya nchi, ni kuingia illegal agreement.!. Illegality kwenye any agreement, renders this IGA illegal, hii illegality renders this IGA null and void ab initio!.
4.

IGA hiyo inakwenda kuzaa ndoa ya TPA na DPW, kupitia HGA. jee ndoa hii ni Ubakaji?.​

Kwa vile kwa hoja zangu za kisheria, hii IGA ni null and void, hivyo HGA, inayokwenda kuzaliwa kati ya TPA na DPW ni ubakaji!.

5.

Jee wajua japo ubakaji ni kosa la jinai, lakini ubakaji unaweza kuzaa ndoa halali?.​

Japo ubakaji ni kosa la jinai, lakini amini usiamini, kuna mahusiano yanaanzishwa kwa ubakaji halafu yakaja kuzaa ndoa halali yenye upendo.

Ubakaji katika Mila za Kiasili za Kiafrika
Naomba usichangie kwanza kwa sasa, subiria hoja za kushiba zinafuata....
Paskali
Mtajirudi mdogo mdogo tu kikubwa uzima!!
 
Katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu rais kuongoza mihula miwili (2) mfululizo ya urais kwa maana ya miaka 10.. ila ikiwapendeza wabunge wetu wanaweza wakafanya namna kurekebisha hicho kifungu ili kukidhi mahitaji yetu kwa sasa.. Mama Samia aongoze hadi 2040.
 
Back
Top Bottom