Wakili Mwabukusi: Tulichokuwa tunalalamikia ni IGA sio HGA. Serikali imewadanganya Wananchi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,054
49,742
Kwamba Katiba(IGA) ndio Ina shida sio kanuni(HGA) hivyo Serikali imedanganya Wananchi,asisitiza Maandamano.

--
"Sasa Juzi (Oktoba 22.2023) Serikali inasema imesikia maoni ya Wananchi na kurekebisha Mkataba (Mkataba wa Bandari), Serikali imewadanganya Wananchi kwa sababu moja IGA ndio iliyokuwa inalalamikiwa na tuligusa vipengele vyenye mapungufu ikiwemo uwezo wa Dubai, kukiukwa sheria za ndani (Tanzania), kutwaa au kuweka mali chini ya mikono ya kigeni bila ukomo unaoeleweka nk, Sasa leo Serikali inazungumzia Host Government Agreement (HGA) halafu inawadanganya Wananchi kana kwamba imerekebisha IGA hiyo si kweli IGA na HGA ni vitu viwili tofauti na HGA haiwezi kukiuka masharti ya IGA kwasababu IGA ndio Mkataba Mama, IGA ni Katiba na HGA ni kanuni sasa ukitwambia HGA ina miaka 30 je IGA ina miaka mingapi" -Mwabukusi Wakili wa Kujitegemea Boniface Mwabukusi amezungumza alipokuwa akifanya Mahojiano maalumu na Jambo TV Ofisini kwake Jijini Mbeya Leo, Jumanne Oktoba 24.2023.

Nini maoni Yako?
 
Kuchamba kwingi kuondoka na Mavi!!
 
Huyu naye anywe maji akalale.
 
Viongozi mnapoambiwa kwenye suala la maendeleo hakuna kuchekacheka na kima ndo kama hivi,.....wapuuzi wa namna hii wakiendelewa kuachiwa tu bila 'pyuu pyuu' za hapa na pale hakuna chochote serikali itafanya.

.." pyuu pyuu " wapewe wanaoingiza nchi hasara.

..kwa mfano, kuna watu walimdanganya Jiwe kuhusu mikataba na sasa tumeshindwa makesi na kupigwa faini bilioni 75, billion 300, na nyingine zinakuja.
 
Kwa hiyo wewe huwezi kufikiria unasubiri mtu aongee na umfuatishe?

Kweli vilaza wengi sana nchi hii
Sio Kila mtu ni mwanasheria, ni sawa na kumpeleka mgonjwa hospital, ni wazi utawasikiliza wataalamu na sio kwamba wewe ni kilaza, bali ni mambo ya professionalism.
 
.." pyuu pyuu " wapewe wanaoingiza nchi hasara.

..kwa mfano, kuna watu walimdanganya Jiwe kuhusu mikataba na sasa tumeshindwa makesi na kupigwa faini bilioni 75, billion 300, na nyingine zinakuja.
Aliyedanganywa na alidanganya wawajibike.
 
Ukweli ni kwamba Rais Samia amefanya hila na udanganyifu wa hali ya juu.

Atoke hadharani, aseme ni nini kwenye IGA kilichorekebishwa kwa kuzingatia maoni ya umma.
 
Hivi ninyi hamna Mungu? Mungu akiombwa vizuri anaweza mfyagia huyu maza kizimkazi na timu yake yote kutoka Ofisini. Tuombe tuache kupiga kelele. Mnayo mamlaka na Mungu anawasikiliza
 
Kama unaweza, kuwaamini CCM, inabidi uperekwe milembe, upimwe kichwa!
Tangu kwenye sakata LA Escrow, waliposema pesa za escrow sio za serikali, niliwachoka ccm
 
Back
Top Bottom