Waislamu mjini Beijing waanza kukaribisha mwezi wa Ramadhani kwa kuandaa vyakula mbalimbali halali vya Beijing

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
Na Pili Mwinyi
VCG111189689715.jpg

VCG11400656785.JPG

Kuanzia Machi 23 yaani siku ya Jumatano, Waislamu kote duniani wanaanza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Katika kipindi hiki Waislamu huwa wanajiegemeza zaidi kwenye sala na ibada ikiwemo kujizuia mambo yote yaliyokatazwa yakiwa ni pamoja na kula na kunywa wakati wa mchana, na kuomba msamaha kwa makosa yao waliyoyafanya, lakini mbali na ibada, katika kipindi hiki pia huwa tunashuhudia wanawake wakipirikika huku na kule kuandaa mapishi ya aina mbalimbali kwa ajili ya futari.

Kawaida kila mwislamu duniani anajiandaa mapema kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Waislamu wa Beijing nao halikadhalika wana taratibu zao mbalimbali za kuukaribisha mwezi katika kipindi hiki.

Hivyo kwa kuwa nimeishi Beijing kwa muda mrefu sana na kuonja karibu mapishi mengi ya Beijing na ya miji mingine, ni vyema tu nikawafahamisha mapishi ya Beijing ama vyakula maarufu vya Beijing ambavyo Waislamu huwa wanakula katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Tukirudi nyuma na kuangalia historia ya mapishi ya Beijing, tunaona kuwa vyakula vya Beijing, ambavyo ni maarufu sana katika mji huu, ni mchanganyiko wa vyakula vya mji wa Shandong, vyakula Halali, vyakula vya malodi wa China, vyakula vya kifalme, n.k. Mbinu za kupika vyakula vya Beijing ni nyingi na vyakula hivi vina ladha ya chumvi, ni laini na vina harufu nzuri ya sosi ya soya.

Vyakula maarufu zaidi hapa Beijing ambavyo hata mgeni akifika anashauriwa kuonja japo mara moja, ni bata wa Peking, Nyama ya Kondoo wa kuchemsha, Nyama Iliyokaushwa pamoja na kutiwa sosi ya Soya, n.k. Pia kuna vitafunio maarufu ambavyo ni vitamu kama vile maini ya kukaanga, keki ya safu elfu moja, Keki ya Pea na vinginevyo.

Kama nilivyosema awali kwamba, vyakula vya Beijing ni mchanganyiko wa vyakula vingi. Katika karne ya 7, Waislamu walianza kumiminika na kuja kuishi Beijing. Kama ilivyofanyika kwa Waislamu waliokwenda maeneo mengine, Waislamu waliokuja Beijing pia walileta utamaduni wa Kiislamu na vyakula halali vya aina mbalimbali.

Tukiangalia mapishi yepi maarufu kati ya vyakula Halali, mapishi ya kifalme na mapishi ya Tan, mapishi ya vyakula Halali ndio yanapendwa zaidi na yanachukua nafasi kubwa katika vyakula vya Beijing, huku nyama ya kondoo na nyama ya ng'ombe ikichukuliwa kama nyenzo kuu.

Katika kipindi cha mwezi mzima wa Ramadhani Waislamu wenyeji na wageni huwa hawahangaiki sana kutafuta vyakula vya futari, kwa kuwa kuna masoko ya aina mbalimbali ambayo unaweza kupata bidhaa wanazotumia zaidi Wachina na pia kuna masoko ambayo hayaadimiki vyakula vya mataifa ya nje.

Kwa mfano sisi Waafrika ambao tumezoea kula futari zikiwemo mihogo, ndizi mbichi na mbivu au hata majimbi, pia tunaweza kupata vyakula vinavyoturidhi kwani China kwa muda mrefu sasa imefungua milango na kukaribisha wafanyabiashara wa nje kuleta bidhaa zao mbalimbali kwenye masoko yake ya China.

Wakati Ramadhani ya mwaka huu inabisha hodi, Waislamu wa Beijing wanaanza kujiandaa kwa futari tamu, inayoliwa wakati unapofika muda wa kufungua. Ili kuhakikisha watu wanafutari kwa wakati, mara nyingi unapokwenda kwenye misikiti mikubwa hapa Beijing kama vile Niujie, baada ya sala ya magharibi Waislamu wanaanza kufungua kwa vitafunwa vinavyopatikana kwenye msikiti huo.

Vitafunwa au futari hizi huwa zinaandaliwa na Waislamu wanaoishi karibu na misikiti na kupeleka msikitini kwa ajili ya kuwafutarisha wasafiri, watu wasiojiweza au hata waislamu wa kawaida wanaofika msikitini hapo.

Kama wewe ni mgeni uliyefika Beijing kwa mara ya kwanza tena ukiwa Muislamu, unaweza kujiuliza je katika kipindi hiki cha Ramadhani naweza kupata wapi chakula Halali?

Amini usiamini, Mji wa Beijing una idadi kubwa ya Waislamu, na wengi wao ni Waislamu wa kabila la Wahui na Wauyghur.

Kwa maana hiyo hofu ya kupata chakula halali na kitamu iondoe kabisa, kwasababu kuna migahawa mingi tu iliyotapakaa kila mahali, ambayo inatoa huduma ya vyakula Halali au vya Kiislamu, na kitu ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba wageni wengi wanapoonja huwa wananogewa na kuvipenda.
 
Na Pili Mwinyi
View attachment 2563381

View attachment 2563382

Niliwahi kupata changamoto sana. Hapo Beijing ni nyama za nguruwe nje nje. Lakini labda kwa ugeni, kwa muda niliokaa hapo Beijing, sikuwahi kuona Msikiti au Kanisa, inaonekana ni majengo adimu sana. Hivi pale Silk Market unaweza kupata futari hata jirani?
 
sijaona kanzu hapo
 
Back
Top Bottom