Itambue miezi mitukufu kwa mujibu wa uislamu. Mwezi wa Ramadhani si katika miezi mitukufu

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,219
2,825
Assalaamu àlaykum wa rahmatullaahi wa barakaatuh

Kuna watu wakiona heading kama hiyo tayari astaghfirullaah zinakuwa nyingi wakidhani labda nimepotosha. Twende pamoja kwa ufupi sana utanielewa

Kalenda wanayotumia waislamu (si kwamba mimi siyo mwislamu bali mimi na wenzangu baadhi tunaitumia ikikaribia ramadhan na ikikaribia arafa) ni kalenda ya kuhesabu siku kwa kutumia mzunguko wa mwezi mwandamo ambayo wengine wanaiita lunar calendar

Kwa mujibu wa kalenda hiyo miezi ni 12 katika mwaka na mwezi unakuwa na siku 30 au 29 basi! Nyongeza ya hilo mwaka unakuwa na siku 360 tu hazizidi.

Muḥarram (mfunguo nne)
Ṣafar (mfunguo tano)
Rabial-Awwal (mfunguo sita)
Rabial-Thāni (mfunguo saba)
Jamādal-Awwal (mfunguo nane)
Jumādal-Thāni (mfunguo tisa)
Rajab
Shaʿbān
Ramaḍhān
Shawwāl (mfunguo mosi)
Dhul-Qaʿadah (mfunguo pili)
Dhul-Ḥijjah (mfunguo tatu)


Miezi hiyo kwa Kiswahili wanaita mifunguo ambapo waswahili wanahesabu kama warabu yaani mwezi wa kwanza ni Shawwāl na wa mwisho ni Ramadhani (Kwahiyo kwa mujibu wa waswahili na waarabu ile siku ya idi baada ya ramadhan (idi ndogo) ndiyo siku ya kwanza ya mwaka yaani mwaka mpya. Kwa upande wa uislamu mwezi wa kwanza ni Muharram na wa mwisho ni Dhul Hijja (Kwahiyo ukiona mahujaji wanaenda makka vile ujue ndo tupo mwisho Mwisho wa mwaka)

Kama ilivyo kawaida mitume hawakuwa wakiondoa kila kitu tu walichokikuta bali kuna vingine waliamrishwa kuviendeleza na kuvienzi kama vilivyo ila kwa namna nzuri inayofuata sheria ya mwenyezi Mungu. Basi hata miezi Waarabu walikuwa wakiiheshimu ni minne na wakawa wanafanya ibada zao za tofauti ndipo mtume alivyokuja akaendeleza utukufu wa miezi ile kama ilivyokuwa ila kwa utaratibu wa Mwenyezi Mungu

Miezi hiyo Mitukufu ni
Dhul Qa'ada (Mfunguo pili)
Dhul Hijja (Mfunguo tatu)
Muharram (mfunguo nne)
Rajab


Ramadhan haimo!
Sikuachi hivi hivi ngoja nimwambie kwa nini watu wamezoea ramadhani ni mwezi mtukufu?

Ndani ya ramadhani kuna usiku mmoja tu (sehemu ya siku miongoni mwa siku za ramaḍhān wala si mwezi mzima wala si siku nzima) ambao usiku huo umetajwa kuwa ni bora kuliko miezi elfu. Maana yake ni kwamba mtu akifanya mema kwenye usiku huo itahesabika kama amefanya mema kwa miezi zaidi ya elfu. Vivyo hivyo kwa atakaye fanya maovu usiku huo ni sawa na aliyetumia miezi zaidi ya elfu kumuasi Mola.

Tunapata kwamba ni usiku mmoja tu ulio bora sana na hata hivyo haujaambiwa ni usiku mtukufu! Pia mwezi wa ramadhani umekuwa ni mwezi mzuri wa kufanya toba na mambo mengine ya heri kwa wingi zaidi na yakakubaliwa kwa haraka kuliko miezi mingine. Tunafundishwa kwamba mashetani ibilisi na wakubwa wenzake wanafungiwa mwezi huu (nadhani ndiyo maana hata nafsi zinamkumbuka Mola kipindi hiki kwani vishawishi vikuu vya maasi havipo)

Watu kwa kuangalia ofa hizo wakaupachika jina mwezi "mtukufu wa ramadhani" kitu ambacho kiuhalisia si kweli. Kama tutaita mtukufu kwa maana hizi hizi za Kiswahili ni sawa lakini kama mtukufu itakuwa imelenga maana ileile ya sawa na ile miezi minne basi hapo itakuwa haifai! Kiswahili saa nyingine kinakosa misamiati!

Credit kwa Shk. Dr Tawakkal Hussein wa TV Imaan
 
Ukweli kila siku ambayo Binadamu yu hai anahitaji Huruma na Baraka za Mungu. Yaani muungano wa Mtu na Mungu auna Ukomo so Kila siku ni Tukufu Mbele ya Mungu na Binadamu.
 
Ivi lile dude mnalolibusu pake maka linatofauti gani na kubusu msalaba hizi dini ni mtot wa baba mmoja
 
Ivi lile dude mnalolibusu pake maka linatofauti gani na kubusu msalaba hizi dini ni mtot wa baba mmoja
Ndani kuko hivi ! Inasemekana ndani yake hapo kabla kulikuwa na sanamu za miungu 360. Kwa sasa ndani kuna hiko kikabati, na Sehemu wanayosema Ibrahim alisali.
 

Attachments

  • IMG_5209.jpeg
    IMG_5209.jpeg
    115.9 KB · Views: 2
  • IMG_5210.jpeg
    IMG_5210.jpeg
    138.1 KB · Views: 2
  • IMG_5211.jpeg
    IMG_5211.jpeg
    152.8 KB · Views: 2
  • IMG_5207.jpeg
    IMG_5207.jpeg
    78.7 KB · Views: 2
  • IMG_5206.png
    IMG_5206.png
    156.2 KB · Views: 2
Kaanzisheni uzi wenu mimi siku hizi nimekuwa sitaki mambo hayo
Quran imechakachuliwa sana Kuna Quran inamuongelea nabii isa na mama yake Mariam ni kama watu wenye mazambi wanatakiwa kujitakasa

Kifupi nabii issa sio Yesu kama watu wengi walivyozoea
 
Back
Top Bottom