Wahitimu wa Open University tunadharaulika bila sababu, kwanini?

Wahitimu wa Open University tunadharaulika bila sababu, kwanini?

Mna utoto sana, hata mleta hoja huna akili...na naamini hata kama ungesoma harvard wewe ni kiazi tu huwezi kuuzika kwa fikra zako hizo. Mambo ya vyuo bora ni ushamba kubishania. Njooni sokoni tupambane sio chuo, kwani wa udsm wote wameajiliwa? Au udom wote wana ajira....je, out wote hawajawahi kupata ajira? Mie nimesoma open undergraduate na nafanya kazi kwenye moja ya tasisi kubwa kwenye hii nchi ambayo ni ya muhimu kwenye uchumi wa nchi yenu na na enjoy life kitaa. Ninausafiri wangu, siwazi ntakula nini, najenga na familia yangu inaishi fresh kwa kipato changu halali, namshukuru Mungu. Sasa nyie endeleeni kubishana na vyuo mtajikuta imefika jioni hamna lolote, na sasa hivi nafanya MBA udsm na wale waliosoma udsm wakakosa ajira wakaamua kuliunga master na wako wepesi sana kwenye darara. Kwa hali hii tatuna wasomi, eti ndo hawa wanao zalishwa na udsm ni mnahizi hoja!poleni sana. Halafu pia malecture wanaonifundisha ud ndo hao hao wa open ndo pia hao hao wa cbe, mzumbe n.k. acheni zarau, akina prof Bisanda wa open si ni product za ud. Shauri yenu, sisi acha tule maisha na open zetu

Na mwanao akiuliza ulis6a wapi unasema OUT over my dead body bora udom
 
kwa masters na kuendelea sawa lkn kwa kuanzia yaani bachelor, mko incompetent. sababu ni kuwa unasoma utakavyo, halafu unaweza hire mtu akakufanyia asilimia 40% ya degree yako. then we ukamalizia na pass ya 15% na ukamaliza. ndo shida iko hapo.

ni bora open ukiwa kazini ambapo mara nyingi unajiimarisha ktk eneo unalofanyia kazi

Mkuu kama umekurupuka hivi....uwe unauliza kwanza Out ni mziki maana hakuna ushindi wa Mezani.....Najivunia kusoma Open University of Tanzania........
 
Najivunia kusoma CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA kwanza ada ni nafuu sana, pili hamna stress za kiji.nga 3. tunafundishwa na magwiji katika taaluma husika. UDSM, UDOM, SUA wengi wenu ni vilaza mnajua kugoma tu. Fyuuuuu.................

Chuo cha waliopata division five hicho ka elimu ni ghali basi jaribu ujinga
 
Mtadharaulika tu maana chuo chenu hakina hadhi hebu fikiria namna walimu/wahadhiri wenu mainly kwa kujuana, pili PROMOTION CRETERIA zenu ni kichekesho Muhadhiri akiandika makala gazetini na kutoa pamphlet(s) kama Nyangwine huyoo tayari Professor, Master/PhD presentation zenu mnafanya kisiri siri kwa hiyo hata Public haijui/haishirikishwi, Wahadhiri wenu wavivu na hawaonekani kwenye Majarida ya kitaalauma ya kimataifa (International Peer-reviewed Academic Journals) unategemea nini. Nyinyi mmekaa kisiasa kuwapatia digrii watu fulani ambao hawauwezi muziki wa UDSM. Asante.
Hawa wanaoona udsm ni kila kitu ni wachovu wa kufikiri. Ukiwa pale wanafunzi wanasoma handouts,slides, vitabu vya miaka ya 90 wanarithishana, kwenye zile theatre na Nkrumah wanadesa vibaya. Kwenda chuo ni msingi tu, you can better yourself whatever the background you have. Ndio maana magufuli anang'ang'ania watu wasome bongo because that's his only exposure.
 
You are not informed. Mambo ya assignment yalishafutwa. Unasoma unaenda kufanya examination in th examination room. Mwingine atakufanyia saa ngapi and where. No research no right to allege. Ulimwengu wa leo ni wa distance learning. Mambo ya kwenda kulishwa kama kindergarten yamepitwa na wakati. Utaona mtu toka baadhi ya "vyuo vya kulishwa" hata kuandika coursework paper anashindwa kwasababu amezoezwa kulishwa kila kitu kama mtoto mdogo. Kutafuta hawezi. Open University kunafanyika research nyingi kupita chuo chochote nchini. Students are trained to search materials. Vyuo vingine mwanafunza anamaliza Masters degree hata kutumia internet hajui, library hajawai ingia. It is fanny.Open university hizo sources of doctrinal materials are core and key at all times.

Ndio Mkuu kabisa 100%... uku tunakomaa unacheza na course outline tu,,,unajitafutia material alafu mtu unakuwa na uwezo mkubwa,,,tofaut na hawa wa ushindi wa Mezani
 
Chuo cha waliopata division five hicho ka elimu ni ghali basi jaribu ujinga



Ah ah ah diva .... Hatari. Ila njoo kwenye practice . Vigezo vya OUT vinatolewa na TCU sio chuo.
Mfano Mwaka huu kuna binti ana diploma kaomba LLB out kakosa October tulienda pale centre dar wakasema hana vigezo coz kafeli fomu four.
Tukaomba batch 2 TCU ila tukaomba udsm. Ninavoongea apa kapata udsm na cha ajabu kapata mkopo juu. Kaeni mnajidanganya !!
 
Fikra zangu hapa ni kwamba, kwanza kuna tatizo la kujiamini kwa mtoa hoja, if you are doubting yourself no one else will believe in you. It does not matter umesomea chuo gani, hata hivyo vinavyofananishwa hapo. Mamlaka pekee yenye uwezo wa kuhalalisha au kuharamisha chuo na taasisi zingine za elimu ni NACTE, ambayo bila shaka imejiridhisha kwamba taasisi zote zinazotoa elimu ya juu vinao uwezo huo, pia, kuna tume ya vyuo vikuu, ambayo huhakiki utendaji wa vyof vyo, na inatoa uhakika (assurance) kwa watumiaji kuhusu ubora. Kumbukeni chuo cha KIU kilivyoingia matatani na siyo open university. Mimi sijasoma huko lakini naamini wanajitosheleza otherwise wangefutwa,

Pili, dhana ya wachangiaji wingi ati ukisoma UD ndo una guarantee ya kuwa bora ilipitwa na wakati miaka mingi iliyopita, wakati kikiwa chuo pekee, kwa sasa kuna wanafunzi wengi na vyuo vilevile. Ubora wa mtu siyo chuo ulichosoma bali una content gani ndani yako, sorry to say, wengi hamtendei haki mjadala kwa kutoa kasfa ambazo ni baseless.

Ukweli ni kwamba ubora wa elimu umeshuka sana nchini hasa kwa takwimu za UDSM wenyewe na la msingi ni kufikiria ku improve siyo kukebehiana, no one is better than others in this.
 
Goood,Out haina degree za sketi kama uds na Udom,nimesoma masters barchelor msuli wake nilikili kuwa elimu ni ghalama.Nimesoma kiswahili ila mtu wa uds na udom nampiga lecture anakubali mwenyewe.Ukiwa open karibia kila kitabu makin kinachohusu koz yako utakisoma lakn vyuo kama uds watu wanatembea na summary mfukon na anafaulu.

Kwa jinsi unavoandika we we ni empty set hata udom hujaikanyaga we we
 
Ah ah ah diva .... Hatari. Ila njoo kwenye practice . Vigezo vya OUT vinatolewa na TCU sio chuo.
Mfano Mwaka huu kuna binti ana diploma kaomba LLB out kakosa October tulienda pale centre dar wakasema hana vigezo coz kafeli fomu four.
Tukaomba batch 2 TCU ila tukaomba udsm. Ninavoongea apa kapata udsm na cha ajabu kapata mkopo juu. Kaeni mnajidanganya !!

Bora umewaambia,......ukweli safi sana mkuu
 
Kujcfia chuo au fan fulan uliosoma wakat huna kaz ni ulimbuken na umaskin wa kimawazo unaowakumba wasom weng tz, watu mnashindwa kukadil jins ya kuibua fursa za kujiajil kwa kutumia taaluma zen mnabak kujicfu chuo
 
Sijui mnabishana madudu gani, mimi degree yangu ya kwanza BA. Economics nimesomea OPEN UNIVERSITY, nakumbuka kwenye group discussion yetu tulikuwa 5 tu, wote tulifanikiwa kumaliza ndani ya kipindi cha miaka 3. Tuliamua kwa umoja na mshikamano wetu tuliokuwa nao tufanye MBA Mzumbe. Kule tukakutana na wanafunzi wa kutoka vyuo mbali mbali na hata waliosoma soma vyuo vya nje ya nchi. Darasa lilikuwa na jumla ya wanafunzi 25 na kwenye test yoyote the best 5 tulikuwa ni sisi kutoka Open university, wale wanafunzi wengine walikuwa wanapata sana shida kufahamu kwanini tuko bora zaidi na tumetoka chuo kimoja.

Acheni upumbavu kudharau vyuo vingine wakati ninyi ni MASANGWINE

Hahaha kweli nyie mlisoma open University mpk mmeenda kwenye vyuo vya watu mnaleta mambo eti "top 5" ya wanaofanya vzr kwenye test, hahah so sad aisee
 
Ah ah ah diva .... Hatari. Ila njoo kwenye practice . Vigezo vya OUT vinatolewa na TCU sio chuo.
Mfano Mwaka huu kuna binti ana diploma kaomba LLB out kakosa October tulienda pale centre dar wakasema hana vigezo coz kafeli fomu four.
Tukaomba batch 2 TCU ila tukaomba udsm. Ninavoongea apa kapata udsm na cha ajabu kapata mkopo juu. Kaeni mnajidanganya !!

Wa udsm walipotia diploma wengi wamekosa hata waliotoka fomu six wengi wamekosa nafasi competition ni kubwa mno. OUT warekebishe mapungufu yao ni mengi ndo mana Chuo kinakimbiliwa na wapenda short cut, nilipitia baadhi ya proposal na dissertations zao majanga wabadilike kiukweli.
 
Yaani we usome open Mimi nisome udsm tuwe sawa?
Haswaaa labda jilinganishe na ustawi au cbe

Hatuwezi kulingana kwa sababu wewe unapewa ushindi wa mezani,,,,,unaambia wa na lecture sehemu ambayo atatunga mtihani....sasa utakuwa bora kweli....we wa udsm
 
Iconcur with your position. Vyuo vingine ni bla bla tu. Wanafunzi wanaambiwa na lecturer mtihani nitatoa hapa( area of cincetration). While in the Open university the whole course work is the area of concetration. Je yupi ni competant?

Angalia hata kuandika tu kiingereza cha kawaida huwezi...huwa mnafundishwa kwa kiswahili nini?
 
Tatizo vijana wengi wanaona udsm ndo chuo bora kuliko vyote hapa tanzania, wengi vijana wa udsm wanakua na GPA kubwa ila kichwani ni ufutio kabisa, ndo maana wanaishia kua mabank teller
 
Back
Top Bottom