Wahitimu wa Open University tunadharaulika bila sababu, kwanini?

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
7,438
7,106
Hivi kwanini jamii ya kitanzania mmetokea kutudharau sisi wahitimu wa Chuo Kikuu Huria? Tumekosea wapi jamani?

Sisi mbona ni kama wahitimu wengine kutoka vyuo vingine vikuu? Yaani nimehudhuria interview kadhaa humo ni dharau dharau mwanzo -mwisho kisa nimesoma Open University of Tanzania?

Dharau hizi hazivumiliki asilani. Tumechoka na punde itabaki historia.

INAUMA, INAUDHI
 
kwa masters na kuendelea sawa lkn kwa kuanzia yaani bachelor, mko incompetent. sababu ni kuwa unasoma utakavyo, halafu unaweza hire mtu akakufanyia asilimia 40% ya degree yako. then we ukamalizia na pass ya 15% na ukamaliza. ndo shida iko hapo.

ni bora open ukiwa kazini ambapo mara nyingi unajiimarisha ktk eneo unalofanyia kazi
 
Mtadharaulika tu maana chuo chenu hakina hadhi hebu fikiria namna walimu/wahadhiri wenu mainly kwa kujuana, pili PROMOTION CRETERIA zenu ni kichekesho Muhadhiri akiandika makala gazetini na kutoa pamphlet(s) kama Nyangwine huyoo tayari Professor, Master/PhD presentation zenu mnafanya kisiri siri kwa hiyo hata Public haijui/haishirikishwi, Wahadhiri wenu wavivu na hawaonekani kwenye Majarida ya kitaalauma ya kimataifa (International Peer-reviewed Academic Journals) unategemea nini. Nyinyi mmekaa kisiasa kuwapatia digrii watu fulani ambao hawauwezi muziki wa UDSM. Asante.
 
Ni kukosa kujiamini tuu mbona kuna wanasheria ambao wamehitimu hapo na wanshind kesi
Kwavtaatifa tuu wanafunzi wengi wa uniz wanasomea mtihani yaani mwalimu atatoa maswali gani hii iko wazi.
 
kwa masters na kuendelea sawa lkn kwa kuanzia yaani bachelor, mko incompetent. sababu ni kuwa unasoma utakavyo, halafu unaweza hire mtu akakufanyia asilimia 40% ya degree yako. then we ukamalizia na pass ya 15% na ukamaliza. ndo shida iko hapo.

ni bora open ukiwa kazini ambapo mara nyingi unajiimarisha ktk eneo unalofanyia kazi
You are not informed. Mambo ya assignment yalishafutwa. Unasoma unaenda kufanya examination in th examination room. Mwingine atakufanyia saa ngapi and where. No research no right to allege. Ulimwengu wa leo ni wa distance learning. Mambo ya kwenda kulishwa kama kindergarten yamepitwa na wakati. Utaona mtu toka baadhi ya "vyuo vya kulishwa" hata kuandika coursework paper anashindwa kwasababu amezoezwa kulishwa kila kitu kama mtoto mdogo. Kutafuta hawezi. Open University kunafanyika research nyingi kupita chuo chochote nchini. Students are trained to search materials. Vyuo vingine mwanafunza anamaliza Masters degree hata kutumia internet hajui, library hajawai ingia. It is fanny.Open university hizo sources of doctrinal materials are core and key at all times.
 
Hivi kwa nini jamii ya kitanzania mmetokea kutudharau sisi wahitimu wa Chuo Kikuu Huria? Tumekosea wapi jamani? sisi mbona ni kama wahitimu wengine kutoka vyuo vingine vikuu? yaani nimehudhuria interview kadhaa humo ni dharau dharau mwanzo -mwisho kisa nimesoma Open University of Tanzania? Dharau hizi hazivumiliki asilani. Tumechoka na punde itabaki historia. INAUMA, INAUDHI!!

Jaribu kusoma udsm ndio ujue tofauti ya brn na true education
 
Chuo cha Kisiasa hicho yaani yeyote anaweza kupata SHAHADA hapo na ushahidi upo......wengi wa wahitimu wenu wako hoi kitaalamu hata makazini ni wachovu kupindukia...hiyo university kwenye UNIVERSITY RANKINGS Top Universities in Africa | 2015 University Web Rankings haionekani popote in short yaan ikichukuliwa SEKONDARI makini moja na chuo chenu huenda sekondari ikawashinda kwa mbali sana. JIREKEBISHENI. Kama mmoja ya mchangia mada alivyosema wahadhiri wenu wengi hawna bidii ya kuchapisha tafiti zao (kama huwa wanafanya tafiti) kwenye majarida ya kimataifa ya utafiti). Wakati fulani nilijaribu ku-Google jina Prof. mmoja hapo OUT (mmoja wa maboss hapo chuoni kwenu) nikakuta andiko lake la mwisho kitaaluma ni mwaka 2000 (miaka 15 iliyopita) hivi mwanataaluma miaka yote 15 unafanya nini kama unashindwa kuchapisha matokeo ya tafiti zako? Kufundisha chuo kikuu ni pamoja na kufanya tafiti ili kusaidia kutatua matatizo yanayoikumba jamii zetu. Open University ni Jipu la kutumbuliwa na Dr. Ndalichako (Waziri wa Elimu mpya/mteule)
 
Najivunia kusoma CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA kwanza ada ni nafuu sana, pili hamna stress za kiji.nga 3. tunafundishwa na magwiji katika taaluma husika. UDSM, UDOM, SUA wengi wenu ni vilaza mnajua kugoma tu. Fyuuuuu.................
 
Najivunia kusoma CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA kwanza ada ni nafuu sana, pili hamna stress za kiji.nga 3. tunafundishwa na magwiji katika taaluma husika. UDSM, UDOM, SUA wengi wenu ni vilaza mnajua kugoma tu. Fyuuuuu.................
Iconcur with your position. Vyuo vingine ni bla bla tu. Wanafunzi wanaambiwa na lecturer mtihani nitatoa hapa( area of cincetration). While in the Open university the whole course work is the area of concetration. Je yupi ni competant?
 
Yaani we usome open Mimi nisome udsm tuwe sawa?
Haswaaa labda jilinganishe na ustawi au cbe
 
Wewe ndio chanzo tetea kwakufanya vizur ktk eneo lako usisubili kutetewa na MTU ukifanya vizur wataluamin tu
 
Najivunia kusoma CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA kwanza ada ni nafuu sana, pili hamna stress za kiji.nga 3. tunafundishwa na magwiji katika taaluma husika. UDSM, UDOM, SUA wengi wenu ni vilaza mnajua kugoma tu. Fyuuuuu.................

Saidia basi kumuelimisha huyo mwenzio anayelalamika hapa kuwa mnadharauliwa kwenye usaili. Je, hakuna wasaili waliosoma Open university?
 
Back
Top Bottom