Serikali ichunguze uanzishwaji wa vyuo vikuu utitiri (holela) bila kuangalia madhara yajayo

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,379
Kwanza kabisa naanza kwa kusema Mungu ni Mtakatifu na mwenye nguvu nyingi sana, bila Yeye sisi hatuna uzima tena na uzima wetu ni pamoja na kusema ukweli mtupu bila kuficha chenga wala pumba chonganishi. Natumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 toleo la 2005, ibara ya 18 kutoa hoja yangu hapa chini ili kulinda heshima ya Shahada yangu ya ELIMU MAALUM japo ndani yake nimesoma Uongozi na Siasa.

Mimi ni mmoja wa wahanga wa Vyuo hivyo vikuu VISHIRIKI vilivyosajiliwa kutoka kwenye vyuo Vikuu na kujitegemea kuwa Vyuo vikuu huku wahitimu wakiwa hawajui walisoma vyuo gani.

Mfano mzuri kabisa mimi nimesoma Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini cha Sebastian Kolowa(SEKUCo) cha Lushoto, Tanga mwaka 2012 nikahitimu, lakini leo chuo hicho kimejitoa Tumaini na kuwa Chuo Kikuu cha kujitegemea yaani Sebastian Kolowa Memorial University(SEKOMU). Cha kushangaza leo mimi chuo nilichosoma kimefutwa yaani hakipo, tumebaki Tumaini jina ambako hakuna SEKUCO tena wala hiyo Shahada haipo tena bali imehamia SEKOMU ambako mimi sikusoma. Leo hii hata nikitambulisha kuwa nilisoma SEKUCO naonekana muongo maana chuokilichopo kwasasa siyo SEKUCO ni SEKOMU. Je, kwanini kama chuo kimebadili jina na mfumo na kujiondoa Tumaini na kufuta jina la chuo cha awali(College University),kwanini sasa tusibadilishiwe Vyeti Vyetu vya Shahada kutoka Sebastian Kolowa University College of Tumaini University kwenda Sebastian Kolowa Memorial University.

Nakumbuka wakati Chuo Kikuu Cha Mzumbe kinaanza kutoka Mzumbe IDM wale wote waliosoma Mzumbe IDM walitangaziwa kupeleka vyeti vyao Chuoni hapo na kubadilishiwa jina la chuo na pia wakabadilishiwa kutoka Advanced Diploma kwenda Bachelor Degree kulingana na mabadiliko ya chuo ya wakati huo. Ikiwa Mzumbe University waliliona hilo bado mapema na wakafanya mabadiliko ili kulinda wahitimu wao maana leo mtu ukimuuliza chuo cha Mzumbe IDM hajui bali anajua Mzumbe University.

Sasa hivi kuna Vyuo vingi tu, vishiriki ambavyo vimejitoa kwenye vyuo Vikuu vilivyokuwa na kuwa Vyuo Vikuu vya kujitegema huku kukiwa hakuna miundombinu ya kuwarekebishia Vyeti watangulizi wa vyuo hivyo,huku vyuo vikianzishwa bila kuangalia nani ana athirika, hii ni dhahiri kuwa Vyuo utitiri viko kwa ajili ya Biashara na sio kusaidia Taifa Letu Tanzania. Leo watoto wangu wakiwa watu wazima hawatajua chuo nilichosoma maana kimefutwa.

Na kumbuka pia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilikuwa Chuo Kikuu kishiriki cha Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda), lakini kilipojitegemea na kuwa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam naamini wahitimu wake walibadilishiwa Vyeti kutoka Ushiriki wa Makerere kwenda Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Mimi ni Mtaaluma tena Mwalimu nasio Mwanasiasa maana wanasiasa ni Waongoooo, hawana data bali wana kick za kutokea kifursa. Ndugu Waziri wa Elimu nakuomba wakati unachamba na kuwauumbua watendaji wa TCU angalia pia na sisi tunavyoathirika na mfumo huu maana sasa hatuna vyuo, hata vyeti vyetu sasa si vyeti tena. Kama binadamu natanguliza samahani kwa wale niliowakwaza kwa makala hii, ila tujaribu kutafakari kwa kina maana mpaka sasa tangu tumalize chuo mwaka 2012 hatujajulishwa kwa lolote lile. Tunaomba kurudishiwa vyuo Vyetu kama hawawezi kutubadilishia muundo wa vyeti kuendana na mfumo mpya.

Ndimi Mjinga Namba Moja Tanzani

DEOGRATIUS KISANDU
Mtumishi Mdogo Sana wa Mungu.
26/5/2016.
 
Hoja yako haina msingi, kweli inadhihirisha Una vyeti vya kuunga unga, nashauri urudie kusoma upya
 
...Cha kushangaza leo mimi chuo nilichosoma kimefutwa yaani hakipo, tumebaki Tumaini jina ambako hakuna SEKUCO tena wala hiyo Shahada haipo tena bali imehamia SEKOMU ambako mimi sikusoma.

Pole. Ila hata Tanganyika ilifutwa na ccm, kufutafuta jadi yao ...
 
Hilo la Mzumbe kubadilishwa kutoka institute(IDM) na kuwa University; "eti" watu waliosoma hapo zamani wakaambiwa warejeshe vyeti vyao ili viandikwe "university" na "eti" badala ya diploma viandikwe "degree", haliwezi kuwa la kweli.! Tena unaonesha umuhimu wa kutafakari upya viwango vya vyuo kikuu vilivyopo nchini, hususani vyuo vya kata kama hicho ulichosoma.
 
Kwanza kabisa naanza kwa kusema Mungu ni Mtakatifu na mwenye nguvu nyingi sana, bila Yeye sisi hatuna uzima tena na uzima wetu ni pamoja na kusema ukweli mtupu bila kuficha chenga wala pumba chonganishi. Natumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 toleo la 2005, ibara ya 18 kutoa hoja yangu hapa chini ili kulinda heshima ya Shahada yangu ya ELIMU MAALUM japo ndani yake nimesoma Uongozi na Siasa.

Mimi ni mmoja wa wahanga wa Vyuo hivyo vikuu VISHIRIKI vilivyosajiliwa kutoka kwenye vyuo Vikuu na kujitegemea kuwa Vyuo vikuu huku wahitimu wakiwa hawajui walisoma vyuo gani.

Mfano mzuri kabisa mimi nimesoma Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini cha Sebastian Kolowa(SEKUCo) cha Lushoto, Tanga mwaka 2012 nikahitimu, lakini leo chuo hicho kimejitoa Tumaini na kuwa Chuo Kikuu cha kujitegemea yaani Sebastian Kolowa Memorial University(SEKOMU). Cha kushangaza leo mimi chuo nilichosoma kimefutwa yaani hakipo, tumebaki Tumaini jina ambako hakuna SEKUCO tena wala hiyo Shahada haipo tena bali imehamia SEKOMU ambako mimi sikusoma. Leo hii hata nikitambulisha kuwa nilisoma SEKUCO naonekana muongo maana chuokilichopo kwasasa siyo SEKUCO ni SEKOMU. Je, kwanini kama chuo kimebadili jina na mfumo na kujiondoa Tumaini na kufuta jina la chuo cha awali(College University),kwanini sasa tusibadilishiwe Vyeti Vyetu vya Shahada kutoka Sebastian Kolowa University College of Tumaini University kwenda Sebastian Kolowa Memorial University.

Nakumbuka wakati Chuo Kikuu Cha Mzumbe kinaanza kutoka Mzumbe IDM wale wote waliosoma Mzumbe IDM walitangaziwa kupeleka vyeti vyao Chuoni hapo na kubadilishiwa jina la chuo na pia wakabadilishiwa kutoka Advanced Diploma kwenda Bachelor Degree kulingana na mabadiliko ya chuo ya wakati huo. Ikiwa Mzumbe University waliliona hilo bado mapema na wakafanya mabadiliko ili kulinda wahitimu wao maana leo mtu ukimuuliza chuo cha Mzumbe IDM hajui bali anajua Mzumbe University.

Sasa hivi kuna Vyuo vingi tu, vishiriki ambavyo vimejitoa kwenye vyuo Vikuu vilivyokuwa na kuwa Vyuo Vikuu vya kujitegema huku kukiwa hakuna miundombinu ya kuwarekebishia Vyeti watangulizi wa vyuo hivyo,huku vyuo vikianzishwa bila kuangalia nani ana athirika, hii ni dhahiri kuwa Vyuo utitiri viko kwa ajili ya Biashara na sio kusaidia Taifa Letu Tanzania. Leo watoto wangu wakiwa watu wazima hawatajua chuo nilichosoma maana kimefutwa.

Na kumbuka pia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilikuwa Chuo Kikuu kishiriki cha Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda), lakini kilipojitegemea na kuwa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam naamini wahitimu wake walibadilishiwa Vyeti kutoka Ushiriki wa Makerere kwenda Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Mimi ni Mtaaluma tena Mwalimu nasio Mwanasiasa maana wanasiasa ni Waongoooo, hawana data bali wana kick za kutokea kifursa. Ndugu Waziri wa Elimu nakuomba wakati unachamba na kuwauumbua watendaji wa TCU angalia pia na sisi tunavyoathirika na mfumo huu maana sasa hatuna vyuo, hata vyeti vyetu sasa si vyeti tena. Kama binadamu natanguliza samahani kwa wale niliowakwaza kwa makala hii, ila tujaribu kutafakari kwa kina maana mpaka sasa tangu tumalize chuo mwaka 2012 hatujajulishwa kwa lolote lile. Tunaomba kurudishiwa vyuo Vyetu kama hawawezi kutubadilishia muundo wa vyeti kuendana na mfumo mpya.

Ndimi Mjinga Namba Moja Tanzani

DEOGRATIUS KISANDU
Mtumishi Mdogo Sana wa Mungu.
26/5/2016.
Jina kamwe halijawa ndiyo Maarifa ayapatayo mtu. Je kabla ya hapo na sasa kuna nini kimebadilika kwa maana ya majengo, wahadhiri, na maabara(kama yapo)

Argument based on the name changed is Totally Baseless!
 
Hilo la Mzumbe kubadilishwa kutoka institute(IDM) na kuwa University; "eti" watu waliosoma hapo zamani wakaambiwa warejeshe vyeti vyao ili viandikwe "university" na "eti" badala ya diploma viandikwe "degree", haliwezi kuwa la kweli.! Tena unaonesha umuhimu wa kutafakari upya viwango vya vyuo kikuu vilivyopo nchini, hususani vyuo vya kata kama hicho ulichosoma.
Wakati fulani pale DIT ulitokea mtifuano mkubwa kati ya Wanafunzi wa iliyokua Advanced Diploma Engineering(ADE)na uongozi wa Chuo. Wahitimu wa zamani na wale ambao walikua wanamalizia mfumo huo wa ADE walidimand wabadilishiwe vyeti kutoka hiyo ADE na kupata mfumo wa Degree wa Chuo hicho yaani Bachelor in Engineering(as Opposed na Bachelor of Science in Engineering kama ile ya CoET)!

Pamoja na mvutano huo na vurumai zilizotokea wakati huo, chuo kilishikilia msimamo kuwa ADE ni ADE na BENG ni BENG,na kwamba kila mwanafunzi anapoingia chuo hujaza mkataba wa kukubali Course anayaoichukua. Sasa kama hicho chuo chenu kinaweza kubadili kinyemela mtu wa Adv Diploma apewe sawa na Bachelor Degree, kwa hakika chuo hicho kinatakiwa KIFUTWE MARA MOJA. huo ni Ubabaishaji katika kusimamia utoaji wa Elimu itolewayo!
 
Unaposema "chuo chenu" unapaswa kuwa unamwambia mleta mada. Diploma ni diploma tu(hata kama ni advanced)tena mwenye diploma siyo graduate hata siku 1
 
Jana Ndalichako alisema Kuna watu (sitaki kuwaita wanachuo) waliokuwa wsnasoma St. Joseph walikua na dvs 4.32 na hawakuwa na sifa ya kusoma hata certificate ya ualimu. Huyo hata akihitimu ataweza kupambanua nini. Mtoa mada ebu tueleze vizuri elimu yako kabla hujajiunga na chuo hicho ilikuaje. Ulikua na vigezo vya kujiunga na chuo kweli wewe? Tuanzie hapo kwanza.
 
Wakati fulani pale DIT ulitokea mtifuano mkubwa kati ya Wanafunzi wa iliyokua Advanced Diploma Engineering(ADE)na uongozi wa Chuo. Wahitimu wa zamani na wale ambao walikua wanamalizia mfumo huo wa ADE walidimand wabadilishiwe vyeti kutoka hiyo ADE na kupata mfumo wa Degree wa Chuo hicho yaani Bachelor in Engineering(as Opposed na Bachelor of Science in Engineering kama ile ya CoET)!

Pamoja na mvutano huo na vurumai zilizotokea wakati huo, chuo kilishikilia msimamo kuwa ADE ni ADE na BENG ni BENG,na kwamba kila mwanafunzi anapoingia chuo hujaza mkataba wa kukubali Course anayaoichukua. Sasa kama hicho chuo chenu kinaweza kubadili kinyemela mtu wa Adv Diploma apewe sawa na Bachelor Degree, kwa hakika chuo hicho kinatakiwa KIFUTWE MARA MOJA. huo ni Ubabaishaji katika kusimamia utoaji wa Elimu itolewayo!

nIMEKUELEWA VIZURI SANA.
 
Jana Ndalichako alisema Kuna watu (sitaki kuwaita wanachuo) waliokuwa wsnasoma St. Joseph walikua na dvs 4.32 na hawakuwa na sifa ya kusoma hata certificate ya ualimu. Huyo hata akihitimu ataweza kupambanua nini. Mtoa mada ebu tueleze vizuri elimu yako kabla hujajiunga na chuo hicho ilikuaje. Ulikua na vigezo vya kujiunga na chuo kweli wewe? Tuanzie hapo kwanza.

Elimu yangu inakuhusu nini, hata nikiwa Tanzania One kunafaida gani na mahitaji ya Nchi. Jadili kilichopo.
 
sina uhakika na suala la kubadilishwa vyeti, ila mtu anayesema kuwa mwenye Advance Diloma sio graduate nna mashaka nawe, maana Advance Diploma ni sawa na Bachelor Degree
 
Haijapata kutokea na haitatokea hata siku moja diploma (advanced) ikawa sawa na degree.! Acha kujidanganya kiasi hicho.!
 
hujawahi ona matangazo ya kazi au nafasi za masters wa
Haijapata kutokea na haitatokea hata siku moja diploma (advanced) ikawa sawa na degree.! Acha kujidanganya kiasi hicho.!
hujawahi ona nafasi za kazi au kusoma masters wakisema muombaji awe na first degree/advance diploma? First Degree ni equivalent to Advance Diploma, usichanganye na Ordinary Diploma ndugu
 
Kwanza kabisa naanza kwa kusema Mungu ni Mtakatifu na mwenye nguvu nyingi sana, bila Yeye sisi hatuna uzima tena na uzima wetu ni pamoja na kusema ukweli mtupu bila kuficha chenga wala pumba chonganishi. Natumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 toleo la 2005, ibara ya 18 kutoa hoja yangu hapa chini ili kulinda heshima ya Shahada yangu ya ELIMU MAALUM japo ndani yake nimesoma Uongozi na Siasa.

Mimi ni mmoja wa wahanga wa Vyuo hivyo vikuu VISHIRIKI vilivyosajiliwa kutoka kwenye vyuo Vikuu na kujitegemea kuwa Vyuo vikuu huku wahitimu wakiwa hawajui walisoma vyuo gani.

Mfano mzuri kabisa mimi nimesoma Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini cha Sebastian Kolowa(SEKUCo) cha Lushoto, Tanga mwaka 2012 nikahitimu, lakini leo chuo hicho kimejitoa Tumaini na kuwa Chuo Kikuu cha kujitegemea yaani Sebastian Kolowa Memorial University(SEKOMU). Cha kushangaza leo mimi chuo nilichosoma kimefutwa yaani hakipo, tumebaki Tumaini jina ambako hakuna SEKUCO tena wala hiyo Shahada haipo tena bali imehamia SEKOMU ambako mimi sikusoma. Leo hii hata nikitambulisha kuwa nilisoma SEKUCO naonekana muongo maana chuokilichopo kwasasa siyo SEKUCO ni SEKOMU. Je, kwanini kama chuo kimebadili jina na mfumo na kujiondoa Tumaini na kufuta jina la chuo cha awali(College University),kwanini sasa tusibadilishiwe Vyeti Vyetu vya Shahada kutoka Sebastian Kolowa University College of Tumaini University kwenda Sebastian Kolowa Memorial University.

Nakumbuka wakati Chuo Kikuu Cha Mzumbe kinaanza kutoka Mzumbe IDM wale wote waliosoma Mzumbe IDM walitangaziwa kupeleka vyeti vyao Chuoni hapo na kubadilishiwa jina la chuo na pia wakabadilishiwa kutoka Advanced Diploma kwenda Bachelor Degree kulingana na mabadiliko ya chuo ya wakati huo. Ikiwa Mzumbe University waliliona hilo bado mapema na wakafanya mabadiliko ili kulinda wahitimu wao maana leo mtu ukimuuliza chuo cha Mzumbe IDM hajui bali anajua Mzumbe University.

Sasa hivi kuna Vyuo vingi tu, vishiriki ambavyo vimejitoa kwenye vyuo Vikuu vilivyokuwa na kuwa Vyuo Vikuu vya kujitegema huku kukiwa hakuna miundombinu ya kuwarekebishia Vyeti watangulizi wa vyuo hivyo,huku vyuo vikianzishwa bila kuangalia nani ana athirika, hii ni dhahiri kuwa Vyuo utitiri viko kwa ajili ya Biashara na sio kusaidia Taifa Letu Tanzania. Leo watoto wangu wakiwa watu wazima hawatajua chuo nilichosoma maana kimefutwa.

Na kumbuka pia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kilikuwa Chuo Kikuu kishiriki cha Chuo Kikuu cha Makerere (Uganda), lakini kilipojitegemea na kuwa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam naamini wahitimu wake walibadilishiwa Vyeti kutoka Ushiriki wa Makerere kwenda Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Mimi ni Mtaaluma tena Mwalimu nasio Mwanasiasa maana wanasiasa ni Waongoooo, hawana data bali wana kick za kutokea kifursa. Ndugu Waziri wa Elimu nakuomba wakati unachamba na kuwauumbua watendaji wa TCU angalia pia na sisi tunavyoathirika na mfumo huu maana sasa hatuna vyuo, hata vyeti vyetu sasa si vyeti tena. Kama binadamu natanguliza samahani kwa wale niliowakwaza kwa makala hii, ila tujaribu kutafakari kwa kina maana mpaka sasa tangu tumalize chuo mwaka 2012 hatujajulishwa kwa lolote lile. Tunaomba kurudishiwa vyuo Vyetu kama hawawezi kutubadilishia muundo wa vyeti kuendana na mfumo mpya.

Ndimi Mjinga Namba Moja Tanzani

DEOGRATIUS KISANDU
Mtumishi Mdogo Sana wa Mungu.
26/5/2016.
Mtoto wa mnyonge hili la vyuo kubadili majina, hadhi, mifumo, nk, ni jambo la kawaida kabisa dunia I kote kwani ni ukuaji kitaaluma au kiutendaji kwa vyuo hivi. Lime tokens hata kwa vyuo vigumu maarufu hapa dunia. Degree yako na kubadilika kwa jina la chuo haina uhusiano wowote! Nafikiri hilo la Mzumbe kama wengi walivyolieleza umedanganywa! Degree yako uliyopata wakati chuo kikiwa ni sehemu ya chuo kiingine haina tofauti na watakayopata wenzako wa leo. Isikuumize kichwa maana inaonekana ni tatizo la ufahamu na kuwa na habari zisizo sahihi.
 
Back
Top Bottom