Wahitimu wa Open University tunadharaulika bila sababu, kwanini?

Wahitimu wa Open University tunadharaulika bila sababu, kwanini?

Chuo kikuu chochote hakiko kivyakevyake. Maarifa yanathibitishwa na external examiners kuthibitisha viwango.
Mtu wa Out anayesoma kwa uaminifu yuko vizuri hasa katika kuandika na ku create knowlege. Ushahidi upo wa waliosoma degree ya kwanza open na walipoenda Udsm wakafanya vizuri tu degree ya pili na ya tatu
 
Unasema kweli hakika ingetokea exams kwa graduantes wa vyuo vyote(Udsm, Mzumbe,Open, IFM, SAUT,TIA) after 3 yrs of experience Hakika naamin matokeo ya OUT watu hawataamini
Hahakika OUT itawaacha midomo wazi
 
OUT ni chuo cha KUKIFUTA kabisa!! ukabila, upendeleo wa wazi katika ajira ndio sifa kuu pale pia umefanya wahitimu wake kuwa dhaifu katika soko la ajira/kujiajiri
Rais alikuwa pale juzi na amekisifia kweli kweli....
 
Marks za kuingia open zinafanana na za kuingia udsm? Mzumbe?
 
Rais alikuwa pale juzi na amekisifia kweli kweli....
Wana cover material mengi kutokana na kozi outline waliyopewa,tofauti na full time ya vyuo vingine mitihani huishia pale lecture alipoishia kufundisha.Wanaosoma open na Ku graduate wako fit asilimia kubwa kwa general knowledge tofauti na ukasuku wa kukariri. Hii nimethibitisha kwa marafiki zangu waliopitia hapo.Hata test na mitihani yao wakipewa wa vyuo vingine wa full time kwa level ya master na graduate kuwapima wanachemsha.Na walimu wanaofundisha hapo ni wale waliokuwa wanafundisha vyuo vingine mnavyoita nguli.KINACHOANGALIWA NI PERFOMANCE KAZINI NA MAISHA KWA WAHITIMU,UNAWEWZA UKAWA UMESOMA HARVAD LAKINI PERFORMANCE NA LIFE IKAPIGA CHENGA TOFAUTI NA ALIYESOMA OUT,LIFE NA PERFOMANCE IKAWA JUU.NI SAWA NA KUKANDIA SHULE ZA KATA,WAKATI CHA MUHIMU NI UELEWA NA KUTOA MATOKEO CHANYA KATIKA JAMII.
 
Ila nimeshalipa ada ya masters, waseme tu nitamaliza na hatutalingana na wengi wanaosema hovyo.
 
kumbe chuo kikuu ni udsm,yaan elimu bado haijakukomboa, huna exposure kabisaaa, kwa taarifa yako elimu ya level yoyote ile kama kichwani hamnazo utabaki kuwa mburula.mi nakutana na barua kibao za kuomba kazi za hao waliosoma unakosema udsm, mpangilio wa barua ni shida, achana na lugha. kwa kumalizia tanzania kuna vyuo vikuu zaidi ya 50.

ubishani wenu umenifanya nikumbuke kipindi kile tunabishana kati ya
la tatu A na la tatu B ipi ni bora.

sasa hivi ndio tunajua kuwa hamna cha la tatu A wala la tatu B,
Hahahaa kweli fact
 
Hivi kwanini jamii ya kitanzania mmetokea kutudharau sisi wahitimu wa Chuo Kikuu Huria? Tumekosea wapi jamani?

Sisi mbona ni kama wahitimu wengine kutoka vyuo vingine vikuu? Yaani nimehudhuria interview kadhaa humo ni dharau dharau mwanzo -mwisho kisa nimesoma Open University of Tanzania?

Dharau hizi hazivumiliki asilani. Tumechoka na punde itabaki historia.

INAUMA, INAUDHI
Ukiona mtu anakudharau tambua huyo hamnazo yaani elimu aliyonayo haijamkomboa.
 
Back
Top Bottom