Wahitimu wa Open University tunadharaulika bila sababu, kwanini?

Wahitimu wa Open University tunadharaulika bila sababu, kwanini?

Hivi kwa nini jamii ya kitanzania mmetokea kutudharau sisi wahitimu wa Chuo Kikuu Huria?

Tumekosea wapi jamani? sisi mbona ni kama wahitimu wengine kutoka vyuo vingine vikuu? yaani nimehudhuria interview kadhaa humo ni dharau dharau mwanzo -mwisho kisa nimesoma Open University of Tanzania?

Dharau hizi hazivumiliki asilani. Tumechoka na punde itabaki historia. INAUMA, INAUDHI!!
duu pole, wanaokudharau ni akina nani, angalia hiyo link Best Universities in Tanzania 2015 - Latest Rankings
but what matter is what you have in your head.na sio chuo chako cha ngapi ubora/ kama ni kichwa popo hata ukisoma chuo bora duniani utaendelea kuwa jingajinga flani hivi kama hao wanaokucheka.
 
Hakuna Profesa yeyote makini atakayetaka kujioanisha (associate) na Chuo kama OPEN UNIVERSITY maana huko kutamporomeshea hadhi yake. We hujiulizi chuo kikuu cha umma kinakwepa kutoa kozi za uhitaji mkubwa hapa nchini kama MEDICINE, PHARMACY na nyininezo nyingi za mrengo wa SAYANSI ANGAVU (PURE SCIENCES) wao wamekalia BBA, SOCIAL WORK, PSYCHOLOGY na TOURISM ndo ujue pale kuna tatizo!!! Poleni Open University.

Kuwa chuo kikuu cha umma sio
lazima kitoe kozi ulizotaja hapo juu,ili kozi ianzishwe katika chuo kuna mahitaji yake.
Mbona MZUMBE chuo kikuu cha umma na hakitoi MEDICINE?!
 
Ninachojua lecturers wa open university sometimes ndo hao hao wa Udsm, Mzumbe, udom etc. tatizo la open university ni kudekezwa tu na wahadhiri wao ili wasionekane kwamba hawafundishi na hawafaulishi, ukienda chuo kama Mzumbe ambapo nimesoma pale hawakubembelezi ukifeli umefeli na supplementally utafanya tu hutaki acha, ukidisco ndo bye bye...sisi mwaka wetu mtoto wa kigogo wa CCM alidisco Mzumbe pamoja na baba yake kufanya juhudi kubwa kumuokoa mwanaye wapiii!!! hata kaka yake ambaye leo ni waziri wa wizara ile ya M..u..u..n..g..a..n..o alifanya juhudi wapiiiiii......!! lakini ingekuwa open ....????
nyie (mzumbe) si ndio mnaoongoza kwa kutoa shahada feki?
 
Huwa nawakonsida watu wa open university as fake.....everything is fake....

Kuna vitu vingi mnakosa sana! Waulizeni waliosoma Udsm, Ardhi university, DIT , na SUA...na vyuo vingine pia...

Hamuwezi kuwa level moja hata siku moja!
 
Dhana ya open universty sawasawa na shule ya kata iliyokosa maaabara huku ikiwa na majengo mazur lkn vitendo hamna yaan si ajabu hata mouth hawaiijui dah
 
You are not informed. Mambo ya assignment yalishafutwa. Unasoma unaenda kufanya examination in th examination room. Mwingine atakufanyia saa ngapi and where. No research no right to allege. Ulimwengu wa leo ni wa distance learning. Mambo ya kwenda kulishwa kama kindergarten yamepitwa na wakati. Utaona mtu toka baadhi ya "vyuo vya kulishwa" hata kuandika coursework paper anashindwa kwasababu amezoezwa kulishwa kila kitu kama mtoto mdogo. Kutafuta hawezi. Open University kunafanyika research nyingi kupita chuo chochote nchini. Students are trained to search materials. Vyuo vingine mwanafunza anamaliza Masters degree hata kutumia internet hajui, library hajawai ingia. It is fanny.Open university hizo sources of doctrinal materials are core and key at all times.
Una hoja lakini..

Kiuhalisia,nchinii kwetu, Tanzania,hakuna miundombinu bora kuwezesha "e-learning".Hivyo hata quality ya elimu ya OUT inatia mashaka sana.
 
Huwa nawakonsida watu wa open university as fake.....everything is fake....

Kuna vitu vingi mnakosa sana! Waulizeni waliosoma Udsm, Ardhi university, DIT , na SUA...na vyuo vingine pia...

Hamuwezi kuwa level moja hata siku moja!
..vitu vingi km nini? area of concentration ryt?!
 
Ni kukosa kujiamini tuu mbona kuna wanasheria ambao wamehitimu hapo na wanshind kesi
Kwavtaatifa tuu wanafunzi wengi wa uniz wanasomea mtihani yaani mwalimu atatoa maswali gani hii iko wazi.

mkuu hiyo stori ya Mwalimu atatoa kitu fulani imemfanya rafiki yangu apate disco ya Masters. Mfumo huo ktk chuo fulani umeisha, tulikutana na maswali mapya yote zaidi ya nusu ya darasa ilipata sup.
 
Hivi kwa nini jamii ya kitanzania mmetokea kutudharau sisi wahitimu wa Chuo Kikuu Huria?

Tumekosea wapi jamani? sisi mbona ni kama wahitimu wengine kutoka vyuo vingine vikuu? yaani nimehudhuria interview kadhaa humo ni dharau dharau mwanzo -mwisho kisa nimesoma Open University of Tanzania?

Dharau hizi hazivumiliki asilani. Tumechoka na punde itabaki historia. INAUMA, INAUDHI!!

kampuni huwa zinataka wajue wewe una nini kwa ajili yao, siyo umesomea kitu gani.
 
mapungu ktk out ni mengi mno..can u imagine nilikua namtafutia mjomba course oulines za linguistic sikuzipata hata course moja halafu anategemea kufanya test mwezi wa kwanza..jamani ni halali mzalaulike...kuapload to course ouline ni shida sasa mtu atasomaje?
Sasa wewe unatafuta course outline ya Linguistic wakati wao wanafundisha Linguistics sasa ungeiona wapi wakati hiyo course uliyokuwa unatafuta haipo
 
Mwaka 2007 nilijiunga OUT kwa LLB. Nikawa ninapiga shule kama sina akili nzuri. Mwak 2008 wakati wa mahafali, nikawaona baadhi ya ambao tulikuwa tukisoma nao wanagraduate. Nikamwuliza mama mmoja tuliyekuwa tukifanya pamoja kazi lakini yeye akisoma BBA hii inawezekanaje? Akaniambia kama una mkwanja umafanya makaratee unagraduate. Akasema yeye alichelewa tu kushtukia huo mchongo angekuwa amekwishakata mkwanja apate digrii yake ili apande cheo ofisini. Lile jambo lilinivunja moyo sana. Nikaona hiki si chuo kinifaacho. Siku chache baadaye nikaacha. Nikajipanga upya. Miaka miwili baadaye nikaacha Kazi na kwenda kusoma chuo kikuu kwa kuketi darasani.

Baada ya hapo, nami nimekuwa sina imani na graduates wa OUT
 
Sina uhakuka saana na hilo!!
 
Ni rahisi sana kuzungumzia ranking za vyuo ukiwa bado unasoma ila ukimaliza utajua nini maana ya elimu, binafsi nilisoma UDSM na baadae OUT, nikiwa UDSM nilikuwa najiona wa pekee sana, nilikuwa najiuliza kwanini waajiri wasiajiri UDSM graduates tu kwanza then nafas zilizobaki wapewe wengine? Cha kunishangaza nilishuhudia wanafuzi wengi hawajui hata kujieleza, kwenye seminars ndio kulikuwa kituko na niliporud mtaani kwa mshangao mkubwa nimewakuta waliomaliza chuo kabla sijaingia mimi wapo wanasota mtaani na wapo watu wametokea vyuo nilivyovidharau wapo makazini, fikira zote zile ilikuwa ni utoto na ulimbukeni wa elimu tu na sio uhalisia wa maisha yenyewe baada ya chuo. Matatizo ya elimu yetu yapo karibia vyuo vyote na sio OUT pekee. Kwangu open imenijenga zaid kuliko UDSM, na sio kila anayesoma out kakosa UDSM, wengine wana matokeo mazur tatizo muda wao hauruhusu kusoma full time.
 
Huwa nawakonsida watu wa open university as fake.....everything is fake....

Kuna vitu vingi mnakosa sana! Waulizeni waliosoma Udsm, Ardhi university, DIT , na SUA...na vyuo vingine pia...

Hamuwezi kuwa level moja hata siku moja!
ungetaja hivo wanavovikosa,wewe umesoma kipi mbona unasema waulizeni??
hivi wewe ukipewa course outline utashindwa kujitafutia? mpaka utafutiwe?
ndo maana elimu zetu mtu ana masters au phd lakini anasubiri kuajiliwa. elimu tegemezi mpaka kwenye application.pole sana tanzania, wanachuo wako wanaishia kujisifia vyuo walivosoma wakati wanashindwa hata kutumia taaluma yao kujiajili
 
Ni rahisi sana kuzungumzia ranking za vyuo ukiwa bado unasoma ila ukimaliza utajua nini maana ya elimu, binafsi nilisoma UDSM na baadae OUT, nikiwa UDSM nilikuwa najiona wa pekee sana, nilikuwa najiuliza kwanini waajiri wasiajiri UDSM graduates tu kwanza then nafas zilizobaki wapewe wengine? Cha kunishangaza nilishuhudia wanafuzi wengi hawajui hata kujieleza, kwenye seminars ndio kulikuwa kituko na niliporud mtaani kwa mshangao mkubwa nimewakuta waliomaliza chuo kabla sijaingia mimi wapo wanasota mtaani na wapo watu wametokea vyuo nilivyovidharau wapo makazini, fikira zote zile ilikuwa ni utoto na ulimbukeni wa elimu tu na sio uhalisia wa maisha yenyewe baada ya chuo. Matatizo ya elimu yetu yapo karibia vyuo vyote na sio OUT pekee. Kwangu open imenijenga zaid kuliko UDSM, na sio kila anayesoma out kakosa UDSM, wengine wana matokeo mazur tatizo muda wao hauruhusu kusoma full time.
no coment zaid ya like kibaaao
 
lazima mkumbuke kuwa Chancellor (wa sasa) OUT alishawahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa so ndo uone OUT si ya kuokota okota tu. Ni chuo makini Barani Afrika na kwingineko. Pia tuna matawi duniani mfano Rwanda, Kenya, Namibia na Dubai (Falme za Kiarabu).
 
OUT ingepata uongozi makini ingekuwa chuo makini mithili ya UNISA (www.unisa.ac.za) ambazo kinafanana kwa namna ya uendeshaji. OUT imekosa uongozi makini tu
 
Back
Top Bottom