Ni rahisi sana kuzungumzia ranking za vyuo ukiwa bado unasoma ila ukimaliza utajua nini maana ya elimu, binafsi nilisoma UDSM na baadae OUT, nikiwa UDSM nilikuwa najiona wa pekee sana, nilikuwa najiuliza kwanini waajiri wasiajiri UDSM graduates tu kwanza then nafas zilizobaki wapewe wengine? Cha kunishangaza nilishuhudia wanafuzi wengi hawajui hata kujieleza, kwenye seminars ndio kulikuwa kituko na niliporud mtaani kwa mshangao mkubwa nimewakuta waliomaliza chuo kabla sijaingia mimi wapo wanasota mtaani na wapo watu wametokea vyuo nilivyovidharau wapo makazini, fikira zote zile ilikuwa ni utoto na ulimbukeni wa elimu tu na sio uhalisia wa maisha yenyewe baada ya chuo. Matatizo ya elimu yetu yapo karibia vyuo vyote na sio OUT pekee. Kwangu open imenijenga zaid kuliko UDSM, na sio kila anayesoma out kakosa UDSM, wengine wana matokeo mazur tatizo muda wao hauruhusu kusoma full time.