Wahitimu wa Open University tunadharaulika bila sababu, kwanini?

Wahitimu wa Open University tunadharaulika bila sababu, kwanini?

kiukweli tunadharauliwa sana sio tu kwenye interview bali hata tukikutana na wanafunzi wenzetu huko mtaani. Waziri wa Elimu ingilia hili, hali si hali kwetu yaani tunaonekana kama MEMKWA
Wewe husomi OUT....umekuja kuchafua chuo hicho kwa malengo yako ...utafanya hata tadhimini zote humu zilizojadiliwa zidharaulike na kuonekana majungu tu ....
 
OUT ni Kichaka flani "amazing" hata ajira za pale ni ama wewe unatokea MBEYA au kama ni mpare (kwa sasa)
Unazidi kufunua malengo yako ...alafu nimeanza kushtukia hadi IDs unazotumia kuchangia humu ....
 
  • Thanks
Reactions: Ilu
Pole mkuu. Usikate tamaa. Endelea kupiga interview. Ipo day bahati itakudondokea. All the best
 
Najivunia kusoma CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA kwanza ada ni nafuu sana, pili hamna stress za kiji.nga 3. tunafundishwa na magwiji katika taaluma husika. UDSM, UDOM, SUA wengi wenu ni vilaza mnajua kugoma tu. Fyuuuuu.................
OUT hakuna rushwa, hivyo vyuo vingine vinanuka kwa rushwa.
 
Nlimaliza udom thoz yearz, nimemaliza program ingine open universty recently, mziki wa open usipime, Nlidhan open ni lelemamaa hakika sio, nlichokisomea hakijadharaulika na kimeniinua kiasi, mentality ya kudharau OUT ipo cha muhim ni kutambua malengo yako na kuyasimamia.
umeongea ukweli mtupu. OUT unapewa course content uende ukaisome yote lakini vyuo vingine wanachagua nini cha kusoma na aibu kubwa hata area of concentration kwenye mithihani wanaambiwa.
 
Duh niataka kuaoply degree next yr lkn mmenitisha
kama umezoea kutafuniwa study materials nakushauri usiende open, hata level one hutamaliza. Kule hakuna kudekezwa, kila kitu unatafuta mwenyewe.
 
kama umezoea kutafuniwa study materials nakushauri usiende open, hata level one hutamaliza. Kule hakuna kudekezwa, kila kitu unatafuta mwenyewe.
Kwanza OUT wamepandisha GPA ufaulu wa kuingia degree kitaeshimi
ka tu
 
Acheni majungu nyie hakuna chuo kinachomjenga mwanachuo kama OUT. Mtu anayemaliza hapo kwenye vitendo anakuwa jembe kwa maana amejifunza kutumia akili yake asilimia 100 tangu anasoma
 
UKABILA upo OPEN hasa kabila la WAPARE ni hatari sana kwa mustakabali wa nchi hii
 
kama chuo kikuu kimeamua kujipambanua kwa hali hii safari yetu kufikia uchumi wa kati 2025 bado sana. Tujifunze kwa wenzetu Malaysia na Korea ya kusini. Miaka ya 1960s tulikuwa tunawasaidia chakula lakini leo hii wao wamevuka kwenda dunia nyingine. Sis bado tunambwela mbwela na vyuo vyetu VIKUU.
 
kwa masters na kuendelea sawa lkn kwa kuanzia yaani bachelor, mko incompetent. sababu ni kuwa unasoma utakavyo, halafu unaweza hire mtu akakufanyia asilimia 40% ya degree yako. then we ukamalizia na pass ya 15% na ukamaliza. ndo shida iko hapo.

ni bora open ukiwa kazini ambapo mara nyingi unajiimarisha ktk eneo unalofanyia kazi

Hata Masters cyo bhana kwenye ubobezi ndy ukaharibu? Bora nikae 5 years wakati najipanga kusoma masters ya uhakika cyo za madafu.
 
tunayasema haya kiroho safi ili OUT wajirekebishe kuanzia namna wanavyoajiri Wahadhiri wao, ufundishaji na hata upandishaji vyeo kuna wakati pale Open University kulikuwa na ukabila (nyanda za juu-kusini) katika kupata ajira hasa vigogo kusukumia watoto wao hapo (majina kapuni). jifunzeni university of South Africa (UNISA) (www.unisa.ac.za) japo ni chuo kikongwe sana, wao ni kama nyie (they offer degree programmes purely by distance learning mode) na wana wanafunzi dunia nzima lakin husikii upuuz wa ukabila wala inferiority complex toka kwa wahitimu wao
 
kwa masters na kuendelea sawa lkn kwa kuanzia yaani bachelor, mko incompetent. sababu ni kuwa unasoma utakavyo, halafu unaweza hire mtu akakufanyia asilimia 40% ya degree yako. then we ukamalizia na pass ya 15% na ukamaliza. ndo shida iko hapo.

ni bora open ukiwa kazini ambapo mara nyingi unajiimarisha ktk eneo unalofanyia kazi


OUT is a public university. ....

For your information. ...

Learn to read
 
Mtadharaulika tu maana chuo chenu hakina hadhi hebu fikiria namna walimu/wahadhiri wenu mainly kwa kujuana, pili PROMOTION CRETERIA zenu ni kichekesho Muhadhiri akiandika makala gazetini na kutoa pamphlet(s) kama Nyangwine huyoo tayari Professor, Master/PhD presentation zenu mnafanya kisiri siri kwa hiyo hata Public haijui/haishirikishwi, Wahadhiri wenu wavivu na hawaonekani kwenye Majarida ya kitaalauma ya kimataifa (International Peer-reviewed Academic Journals) unategemea nini. Nyinyi mmekaa kisiasa kuwapatia digrii watu fulani ambao hawauwezi muziki wa UDSM. Asante.
kumbe chuo kikuu ni udsm,yaan elimu bado haijakukomboa, huna exposure kabisaaa, kwa taarifa yako elimu ya level yoyote ile kama kichwani hamnazo utabaki kuwa mburula.mi nakutana na barua kibao za kuomba kazi za hao waliosoma unakosema udsm, mpangilio wa barua ni shida, achana na lugha. kwa kumalizia tanzania kuna vyuo vikuu zaidi ya 50.
 
Chuo cha Kisiasa hicho yaani yeyote anaweza kupata SHAHADA hapo na ushahidi upo......wengi wa wahitimu wenu wako hoi kitaalamu hata makazini ni wachovu kupindukia...hiyo university kwenye UNIVERSITY RANKINGS Top Universities in Africa | 2015 University Web Rankings haionekani popote in short yaan ikichukuliwa SEKONDARI makini moja na chuo chenu huenda sekondari ikawashinda kwa mbali sana. JIREKEBISHENI. Kama mmoja ya mchangia mada alivyosema wahadhiri wenu wengi hawna bidii ya kuchapisha tafiti zao (kama huwa wanafanya tafiti) kwenye majarida ya kimataifa ya utafiti). Wakati fulani nilijaribu ku-Google jina Prof. mmoja hapo OUT (mmoja wa maboss hapo chuoni kwenu) nikakuta andiko lake la mwisho kitaaluma ni mwaka 2000 (miaka 15 iliyopita) hivi mwanataaluma miaka yote 15 unafanya nini kama unashindwa kuchapisha matokeo ya tafiti zako? Kufundisha chuo kikuu ni pamoja na kufanya tafiti ili kusaidia kutatua matatizo yanayoikumba jamii zetu. Open University ni Jipu la kutumbuliwa na Dr. Ndalichako (Waziri wa Elimu mpya/mteule)
nimeangalia hiyo link, kwani tanzania kuna vyuo vikuu viwili? mbona katika 100 tanzania ipo udsm tu, vingine zaid ya 50 viko wapi? au nyie mna personal conflict na hicho chuo???
by the way NACTE na TCU ndo wanaohusika kisheria kutambua vyuo vikuu, sio akina sisi na njaa zetu.
 
chuo chenyewe umeshasema ni OPEN so kila mtu anaeingia lazima amalize tena kwa GPA kuubwa lazima mtaendelea kudharaulika
umeongea uongo, watu kibao wanakimbia hichi chuo,kumbuka ni chuo cha uma hakiendeshwi na ada,so hawanaga muda wa kupetipeti wanachuo
 
Hakuna Profesa yeyote makini atakayetaka kujioanisha (associate) na Chuo kama OPEN UNIVERSITY maana huko kutamporomeshea hadhi yake. We hujiulizi chuo kikuu cha umma kinakwepa kutoa kozi za uhitaji mkubwa hapa nchini kama MEDICINE, PHARMACY na nyininezo nyingi za mrengo wa SAYANSI ANGAVU (PURE SCIENCES) wao wamekalia BBA, SOCIAL WORK, PSYCHOLOGY na TOURISM ndo ujue pale kuna tatizo!!! Poleni Open University.
1.huo utafiti umefanyia chooni ama ndotoni
hayo masomo yanahitajji vitendo zaidi kuliko blabla, wanafunzi wa open wametawanyika the whole country, waweza kuta centre flani kuna mwanafunzi mmoja wa hiyo course, je atafanya vipi practicals?
2. prof. ralph masenge yupo open ambaye ni the only prof wa mathematics in tz baada ya prof shayo kutangulia mbele ya haki
 
Back
Top Bottom