Wageni wa 'ghafla' majumbani mwetu.....

RR kuna watu wengine wanafanya hii kuwa ni tabia yao kila mara hufanya hivi labda kwa mwezi mara tatu au nne (hasa weekend na siku za sikukuu) , watu kama hawa ni lazima kuwafahamisha kwamba hali hii haikubaliki lakini kama inatokea mara moja moja sana basi hakuna ubaya hata kuongeza chakula (kama kipo) ili nao wapate msosi.
Kama wanajifanya ni tabia yao basi for every visit at your place make two at theirs, wataelewa shidya ya unexpeted visits. Au waambie next time wakupigie maana 'almost wangekukosa'. ila changia msosi tu, usiwanyime. Wakija tena you say the same and unajifanya kutania but ndio unamaanisha: hivi nyinyi kutoa taarifa mmeshindwa kabisa? shauri zenu ipo siku mtafika mnakuta fridge nyeupeeee, hata cha kuwakaribisheni sina. Hapo lazima wataelewa tu. Mbona tunaelewa visomo vya kanga jamani, ndio message kama hii tushindwe?
 
Hivi na nyinyi mshawahi kufeki kama unaongea kwenye simu pale umwonapo kwa mbali mtu ambaye unayemfahamu anakuja eneo ulipo wewe?

Ile umwonapo tu unachomoa simu yako halafu unaiweka sikioni kama vile uko bize kwenye maongezi....lol

Hii yote ni katika kum-avoid tu huyo mtu maana akisimama kuongea na wewe itachukua forever na wewe huna muda ama hujisikii kumsikiliza na mistori yake.
Kuna mngine anakija kabisa na anasubiri umalize. alafu tatizo ni wakati umesha jifanya unaongeaaaaa, alafu sim inalia ukweli sasa, bado ipo sikioni!
 
Hivi na nyinyi mshawahi kufeki kama unaongea kwenye simu pale umwonapo kwa mbali mtu ambaye unayemfahamu anakuja eneo ulipo wewe?

Ile umwonapo tu unachomoa simu yako halafu unaiweka sikioni kama vile uko bize kwenye maongezi....lol

Hii yote ni katika kum-avoid tu huyo mtu maana akisimama kuongea na wewe itachukua forever na wewe huna muda ama hujisikii kumsikiliza na mistori yake.


hiyo ya simu hiyo naona kila mtu 'amewahi tumia' lol
 
inakera sana, ugeni wa kijima umepitwa na wakati, inabidi mtu atoe taarifa ili mwenyeji amjulishe nafasi yake na aweze kujitayarisha na kama ni dharura iwe ni dharura kweli na hata hivyo mawasiliano yapo!
 
Wageni wa ghafla wakati wa sikukuuu sina shida nao maana hata mimi nakuwa nimejiandaa. Ila hao wa kuja siku nyingine tu za weekend bila taarifa, kama nna mipango yangu watanisamehe, siwezi kuahirisha kwa ajili yao.
 
au umekimbia chumbani umesema waseme 'haupo'
mgeni anaamua 'kukusubiri' sebuleni lol
Mi hiyo hainipi shida. Kama nina sababu za msingi za kutotaka kumuona, namwambia mwanangu L aseme hivi: mama Kafurahi kweli kuskia umekuja kumsabahi. anasema atachelewa sana kuja, ila anaomba umkute XXX, anakusubiri hapo. alafu 30 min later, hata hajapata time ya kufina namtumia msg kusema: mbona umechelewa sana, naondoka basi, tuonane kesho (or whatever time is convinient). For extreme desiease use extreme cure.
But under normal circumstances sijifichi, nikipata mgeni nampokea tu, hata kama ni kwa muda mfupi kuliko alivo panga.
 
au umekimbia chumbani umesema waseme 'haupo'
mgeni anaamua 'kukusubiri' sebuleni lol
Mimi nadhani ni bora mtu umwambie ili aelewe..hii ya kuumia rohoni huku mwenzio ananenepa inaudhi..just be transparent..njoo kwangu kwa taarifa ..akimaind..to hell!
 
Wageni wa ghafla wakati wa sikukuuu sina shida nao maana hata mimi nakuwa nimejiandaa. Ila hao wa kuja siku nyingine tu za weekend bila taarifa, kama nna mipango yangu watanisamehe, siwezi kuahirisha kwa ajili yao.
I think na mimi ni hivo hivo. kwa sikukuu sawa, ila isiwe tabia ya kuja bila kutoa taarifa sasa. bora hata uje jioni during week days ila please, please, usije weekend!!!
 
In fact hao wageni sio wajinga, wanaenda kwa yule ndugu ambae wanamuona kajiweza kidogo na mara nyingi huyo ndugu mwenyewe atakua na kitu for sikukuu. Kama huna kabisa kabisa basi inabidi na wewe uanze safari ya kwenda nao kwa next ndugu. lol

Wanalenga siyo?! Nimependa sana ufumbuzi wako...
 
Nafikiri ni utamaduni wetu hasa vijijini and this is what keep people together. Tofauti na watu wa West huwa hatutoi notice kabla ya kwenda kumtembelea mtu. Binafsi sina tatizo na hili and like it when mtu ambaye sijaonana nae kwa muda kuniibukia home ghafla. Kitu ambacho sipendi ni mtu kuniibukia kazini bila notice na anategemea mpige story
 
Kiganda sio suala la kuwa watatosheka na watakachokikuta. Kuna ubaya gani wa kutoa taarifa mapema tu kidogo kuwa sisi tunakuja huko pia.

Kwa sababu kwa experience yangu, wageni mkiwa wingi wa ghafla chakula kitabidi tu kiongezwe. Kwa hiyo bora watu wahangaike mapema kupika ili nao waenjoy company yako

Duh kwa hiyo mipango yako, kama wangepiga simu hata wasingekupata.
Hata kwenye basi kama una nauli pungufu eti konda anataka umwambie kabla hujapanda. Kama ana moyo wa kukusaidia basi hakuna tofauti ya huo msaada whether safari imeanza au lah.
RR kasema kama hali yako nawe mbaya basi unga tela nendeni kwa ndugu mwingine, huyo akiwa hana pia naye aunge, hivyo hivyo mpaka mumpate ambaye yuko fresh...
 
Unajua mimi huwa sielewi kabisa. Sasa sijui sielewi kwa vile mimi siko hivyo...

Kwangu ni common sense. Mtu huwezi tu kwenda kwa mtu (ukiondoa shida au haja ya dharura) pasipo kumtaarifu. Kwangu ni jambo rahisi sana na wala halihitaji tafakuri. Lakini unakuta mijitu mingine inaona ni jambo la kawaida tu.

Naam NN, nakubaliana nawe kabisa na watu wenye tabia hizi ukiwaendekeza wanachonga mzinga. Kila Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu wanazuka tena bila hata kutoa taarifa mapema ,tena siku zote timing yao huwa nzuri sana, karibu na saa za msosi.
 
hatusemi wageni wasije au wakija tukasirike
tunasema kama simu zipo
si upige mapema kuwa unakuja?????
kuliko kwenda kwa mtu ghafla????

ishu sio chakula hapa,ishu ni mgeni na mahitaji yake hata kama 'ni kupiga story tu'
je wewe ukijua mapema kuna mtu anakuja kupiga story si better? kuliko unajiandaa kutoka au kulala
mara watu hao...

Simu haina credit, lol...
 
Upo nyumbani kwako umepumzika,ni wikiendi au sikukuu
kama leo.una mipango yako binafsi
labda unataka kulala tu siku nzima
au kutoka na mkeo/mumeo bf/gf so mnavuta vuta mda hivi....

ghafla bin vuu wanaibuka 'wageni ' pengine ndugu zako au wa mwenzio
au tu marafiki na jamaa, wamekuja 'kukutembelea' au
'kusheherekea sikukuu' labda wamekuja na 'watoto wao'
na muelekeo wao ni kushinda hadi jioni ndo warudi makwao.....

dah jamani mimi hili huwa linanikera mno....
siku hizi si kuna simu????inakuwaje jamani??????

nyinyi ikiwatokea mnafanya nini?????????

Boss, kwangu mimi wageni wanakaribishwa anytime. Wakija kwangu na kama nina muda wa kuwaentertain nitafanya hivyo. Kiafrika naona ni poa. Wageni ni baraka. Mgeni awezakuwa malaika. Kwa ughaibuni ndio sitaki mtu aje kwangu bila taarifa. Ila nikiwa bongo, wageni karibuni sana anytime mnipe baraka zenu.
Shukran
 
Jee mtu kupiga simu tu bila mpango, "kupiga story"?

Mimi hata simu sitaki, mtu akipiga simu hana sababu ya msingi ananirusha stimu ile mbaya.

Gaijin sorry wewe ni me au ke? Sijawahi kupigiwa simu na mwanamke akaongea less than 5 minutes. Ataongea weeeeeeeeeee halafu atakuambia the actual reason ya kukupigia simu at the end. Kwa wanaume, tunaweza kuongea kwenye simu less than a minute unless its football. lol
 
hatusemi wageni wasije au wakija tukasirike
tunasema kama simu zipo
si upige mapema kuwa unakuja?????
kuliko kwenda kwa mtu ghafla????

ishu sio chakula hapa,ishu ni mgeni na mahitaji yake hata kama 'ni kupiga story tu'
je wewe ukijua mapema kuna mtu anakuja kupiga story si better? kuliko unajiandaa kutoka au kulala
mara watu hao...

Labda in urban areas lakini vijijini mtu akupigie simu eti anakuja kukutembelea? Sidhani. Kwanza kama hajakuona kama siku tatu lazima akuzukie home kama ni mzima. Vijijini bado wana ile sense ya community. Mijini tunapenda sana individualism, private life, privacy, etc tunazodesa toka West.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom