Wafanyabiashara Arusha wafunga maduka kwa muda usiojulikana

Naamini Kama CDM wangekuwa wanaongoza serikali haya mambo ya kodi zisizoeleweka zisingekuwepo kwa wananchi,hebu fikiri mara kodi mara tozo za miamala mara kodi za majengo kwenye luku mara bei ya mazao ya petroli hazieleweki mara bei ya mafuta ya kula haieleweki,hata haijulikani kama kuna bunge such wacko likizo
 
Sijui ni mwandishi wa aina gani wewe ,Hujasema Kodi gani imepandishwa pango,leseni,au TRA???

Pia Hujasema awali ilikuwa shilinngi ngapi na Sasa imepanda ngapi ?

Ujinga mwingine ni kuoanisha wafanya biashara na Chadema duh! Akili hizi!
 
Wamachinga kusema ukweli walikuwa wanaichafua miji badala ya kuleta muonekano wa usafi na ustaarabu. Wanapika juu ya mitaro na wanamwaga mabaki ya chakula katikati ya miji.

Ni sawa wanajikimu kimaisha lakini mpangilio wa mji unapotea kabisa.
 
Baada ya wafanyabiashara na Chadema kushangilia mateso ya kufungiwa biashara kwa wamachinga hatimae zamu yao imefika, kuanzia leo kodi ya maduka kwenye jiji la Arusha imepandishwa kwa 100% na kupelekea wenye maduka kugoma kwa muda usiojulikana.

Wafanyabiashara wafunga maduka kisa kupandishiwa kodi | Mwananchi - Wafanyabiashara wafunga maduka kisa kupandishiwa kodi
Kwani wamelazimishwa kulipa kodi? Halmashauri ya jiji ni mwenye nyumba kwa maana ya kwamba yeye ndiye anayechukua kodi anayoona kwamba itamlipa am kumrudishia gharama za uwekezaji aliouweka katika kuyajenga maduka hayo na kupande mwingine wafanyabiadhara ni mpangaji ambaye anapaswa kumlipa mwenye nyumba kodi yake ili na yeye awe huru kuifanya biashara yake

sasa hapa kufunga ama kugoma kugungua biashara ili umlazimishe mwenye nyumba akukubalie ulipe kodi unayotaka wewe siyo sawa cha msingi ni kwwmba ikiwa mwenye nyumba ama chumba unachofanyia biashara amekutoza kodi ya pango kubwa na ikawa wewe inakushinda kwa sababu unazoona kwamba haitakulipa basi unapaswa kuiacha nyumba hake ili wewe ukapange kwa mwenye nyumba mwingine na ambaye kodi yake itakuwa na ahueni na hapo mwenye nyumba naye amtafute mpangaji mwingine ambaye atakubaliana na kodi yake ama ikimshinda nyumba yake kumpata mpangaji mwenye kumlipa kodi anayoitaka basi pengine anaweza kuwa na hiyari ya kushusha kodi ama vinginevyo bila yankulazimishwa na mpangaji

Hapa hawa wapangaji wanadeka na kuigomea serikali kwa sababu ni serikali kwa sababu kwa watu binafsi huwa wanalipa kodi ama wanaacha pango wazi ili mwenye nyumba atafute wmpangaji hivyo na huku kwenye halmashauri ifanyike hivyo hivyo maana hii ni biashara kama biashara nyingine yeyote.
 
Wamachinga kusema ukweli walikuwa wanaichafua miji badala ya kuleta muonekano wa usafi na ustaarabu. Wanapika juu ya mitaro na wanamwaga mabaki ya chakula katikati ya miji.

Ni sawa wanajikimu kimaisha lakini mpangilio wa mji unapotea kabisa.
USafi wa miji unaendana na uchumi wa mtu Moja moja kuondoa machinga mtaa ni ngumu sana watarudi wote
 
Kodi ni kodi hata ukijua ni kodi gani itakusaidia nini?
Aliyeleta hii habari kaileta ili itusaidie nini ?

Ili kujua kama Sheria imekiukwa au kama kuna haki imepindishwa lazima ujue aina ya Kodi, Kama ni TRA (hii haiwezekani ipande kinyemela) kama ni Kodi kulingana na bylaws za sehemu husika au kama ni Kodi ya Pango ? na limepanda kulingana na sehemu husika / majirani wengine wanalipaje na demand ipo vipi...

Bila kujua hayo habari haijakamilika (Kodi ya Maduka hii sentensi haileti maelezo yaliyokamilika)
 
Ukishajua utaindoa?
 
Baada ya wafanyabiashara na Chadema kushangilia mateso ya kufungiwa biashara kwa wamachinga hatimae zamu yao imefika, kuanzia leo kodi ya maduka kwenye jiji la Arusha imepandishwa kwa 100% na kupelekea wenye maduka kugoma kwa muda usiojulikana.

Wafanyabiashara wafunga maduka kisa kupandishiwa kodi | Mwananchi - Wafanyabiashara wafunga maduka kisa kupandishiwa kodi

Wewe kimba! Kama kodi ya maduka imepanda kwa 100% je ni kwa Chadema tu?? CCM au vyama vingine imebaki ilipokuwa? Na ni nani hasa aliyewaondoa wamachinga na kupandisha kodi husika, Chadema???

Nina masikitiko kwa mumeo na wanao kuwa na mke na mama wa aina hii!! Kwa hakika hutazalisha wana bora kuliko mwenyewe!!
 
Baada ya wafanyabiashara na Chadema kushangilia mateso ya kufungiwa biashara kwa wamachinga hatimae zamu yao imefika, kuanzia leo kodi ya maduka kwenye jiji la Arusha imepandishwa kwa 100% na kupelekea wenye maduka kugoma kwa muda usiojulikana.

Wafanyabiashara wafunga maduka kisa kupandishiwa kodi | Mwananchi - Wafanyabiashara wafunga maduka kisa kupandishiwa kodi
Labda maduka ya mumeo ndio yamefungwa,bladifaken wahed
 
Arusha wafanyabiashara zaidi ya 100 wa maduka katikati ya Jiji la Arusha wamefunga maduka yao bila kikomo wakipinga kupandishiwa mara dufu kodi na halmashauri ya Jiji la Arusha kutoka Sh150,000 hadi Sh300,000 kinyume na utaratibu.

Aidha wamemwomba Rais Samia Suluhu na Waziri Ummy Mwalimu kuingilia kati ili kuondoa unyanyasaji huo unaosababisha washindwe kufanya biashara zao kwa uhuru.

Wakiongea na waandishi wa habari leo Desemba 10, wafanyabiashara hao katika eneo la Ranger Safari, wamedai kuwa kitendo cha halmashauri hiyo kupandisha kodi ya pango kinyemela hakikuwa na makubaliano bali halmashauri hiyo imetumia ubabe wakati mwafaka ulikuwa bado.

Baadhi ya wafanyabiashara hao Godluck Alick na Amani Mollel wamedai kuwa usiku wa siku ya kusherehekea miaka 60 ya uhuru wa Tanzania ,baadhi ya maofisa wa jiji wakiwa na mgambo kadhaa walivamia katika maduka hayo na kuwakamata viongozi wa wafanyabiashara hao na kuwapelekea polisi wakidai wanashinikiza wafanyabiashara wasilipe Kodi.

"Hili suala lilishazungumziwa na mkuu wa wilaya aliyepita Mbele ya mkurugenzi wa jiji na kufikia mwafaka kwamba wafanyabiashara hao waendeleee kulipa kodi ya zamani ya shilingi laki moja na nusu ,lakini tumeshangaa hapo jana jambo hili limeibuka upya"alisema Mollel.

Naye mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara hao,Loken Masawe na Katibu wake,Hamidur Jamari wamemwomba Mkurugenzi wa Jiji la Arusha kukaa na Wafanyabiashara hao ili kuondoa sintofahamu inayojitokez kwa kuwa msuguano huo umekuwa wa muda mrefu unaosababisha adha kwa wananchi.

Hawa wafanyabiashara ndio waliojenga haya maduka wanamchagia wao ni mkubwa kwa Serikali. Huyu mkurugenzi akutane na wafanyabiashara na awaheshimu kwa mchango wao kitendo cha kuwatumia mgambo siku ya uhuru na kuwakamata viongozi wao awaombe radhi sio cha uungwana"alisema Masawe.

Aidha mwenyekiti huyo amedai kuwa wafanyabiashara hao hawatafungua maduka yao katika muda usiojulikana ili kushinikiza halmashauri hiyo kukaa kitako ili kufikia mwafaka.

Katika hatua nyingine wafanyabiashara waliopanga katika maduka mapya ya halmashauri hiyo yaliyopo eneo la Disemba nao wamegoma kufungua wakidai kiwango cha kodi wanachoyozwa na halmashauri hiyo ni kikubwa.

Mmoja ya wapangaji wa maduka hayo, Modester Kapinga alidai kuwa kodi wanayolipa kwa sasa ni kati ya ya Sh,300,000 na Sh600,000, ambayo haiwapi faida na kwamba maduka hayo ni madogo sana..

Akijibu hoja za wafanyabiashara hao mstahiki meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranghe alisema uamuzi wa kupandisha Kodi ni uamuzi uliotolewa na baraza la madiwani baada ya kujiridhisha kuwa wafanyabiashara hao wanalipwa kiasi kidogo cha kodi .

"Haya maamuzi yametolewa na baraza la madiwani halmashauri ni watekelezaji tu, hao wafanyabiashara wanalipa kodi ndogo sana"alisema Meya.

Awali mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Dkt John Pima alidai kuwa suala hilo litazungumziwa na Meya wa Jiji la Arusha kwa sababu maamuzi ya kupandisha kodi yalifikiwa na baraza lake la madiwani.

View attachment 2039570
Madiwani wa mchongo viti maalum,baraza la mchongo
 
Baada ya wafanyabiashara na Chadema kushangilia mateso ya kufungiwa biashara kwa wamachinga hatimae zamu yao imefika, kuanzia leo kodi ya maduka kwenye jiji la Arusha imepandishwa kwa 100% na kupelekea wenye maduka kugoma kwa muda usiojulikana.

Wafanyabiashara wafunga maduka kisa kupandishiwa kodi | Mwananchi - Wafanyabiashara wafunga maduka kisa kupandishiwa kodi
Simlikuwa mnasema Magufuri aliua biashara kwa kubambika watu kodi,sasa imekuwaje tena? Kweli Magufuri alisingiziwa kwa mengi sana
 
Back
Top Bottom