PostGE2025 Jaji Chande: Matukio ya Oktoba 29 yalipangwa na kufadhiliwa na watu waliopata mafunzo

PostGE2025 Jaji Chande: Matukio ya Oktoba 29 yalipangwa na kufadhiliwa na watu waliopata mafunzo

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,125
Reaction score
3,611
Wakuu,

Anazungumza Jaji Chande leo wakati anakabidhi anakabidhi Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani Yaliyotokea Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025, tarehe 23 Aprili, 2026, Dar es Salaam

Pasipo na shaka, kuwa matukio ya ghasia ya tarehe 29 Oktoba yalipangwa, yaliratibiwa, yalifadhiliwa na kutekelezwa na watu waliopata mafunzo.

Waratibu walitumia mbinu mbalimbali, ikiwemo kuwatumia watu wasio na ufahamu wa kina na vijana waliokata tamaa, huku wakihakikisha kuwa vitendo vya ghasia vinafanyika kwa wakati mmoja kufikia maeneo tofauti ili kuwachanganya na kuwatawanya Jeshi la Polisi.

mzee kapita kwenye mwongozo alio pewa

daah kalamba posho kuandika maneno yale aliyo ambiwa kabla yaan hata kauli ya hakuna nnywinywi wala nywinywinywi hataki iona kabisa ye anaona ilikuwa sawa kabisa
 
"Pasipo na shaka, kuwa matukio ya ghasia ya tarehe 29 Oktoba yalipangwa, yaliratibiwa, yalifadhiliwa na kutekelezwa na watu waliopata mafunzo.

Waratibu walitumia mbinu mbalimbali, ikiwemo kuwatumia watu wasio na ufahamu wa kina na vijana waliokata tamaa, huku wakihakikisha kuwa vitendo vya ghasia vinafanyika kwa wakati mmoja kufikia maeneo tofauti ili kuwachanganya na kuwatawanya Jeshi la Polisi.

Mheshimiwa Rais, taarifa na ushahidi unathibitisha kuwa watu waliokuwa wakizunguka katika maeneo mbalimbali kama vile mitaani, vyuoni, kwenye masoko, na stendi za mabasi, wakishawishi na kuwaandikisha watu mbalimbali kushiriki katika ghasia za wakati na baada ya uchaguzi mkuu.

Mfano, watoto wanaoshi katika mazingira magumu, waendesha pikipiki, na wajasiriamali wadogo walieleza kuwa walipewa fedha kati ya Shilingi elfu kumi hadi Shilingi elfu hamsini, na waliahidiwa ajira na maisha bora.

Ilielezwa zaidi kuwa kuanzia tarehe 12 Oktoba mwaka 2025 hadi tarehe 28 Oktoba, waliwekwa pamoja kupewa mafunzo, kuandaliwa na kuhamasishwa kuwa sehemu ya kuanzisha na kushiriki ghasia siku hiyo". Jaji Chande
 
Hata mimi nililipwa na ccm kufanya namna
 
Tume imetoa yaleyale yaliyodhaniwa kutolewa. Ni kinyume na matarajio ya walio wengi
 
Tunaomba mtupe muda tufanye upelelezi sasa
Mwanzo tulifanya uchunguzi tu
 
Tume ilitakiwa iwe tume huru ndio ingeweza kuja na majibu murua. Ni ngumu tume kuja na majibu ya kumsagia kunguni aliyeiunda. Tume ilitakiwa ijitegemee, kama kupiga ipige pande zote mbili, kama ni makosa hata upande wa pili nao ulikosea kutenda vitendo vile vya kijinai
 
Tuseme ndivyo japo sivyo. Ila ingekua ndvyo kama asemavyo jaji chande ni dhahiri kuwa ni tusi kubwa kwa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi. Kwamba tukio la ghasia kubwa lipangwe, mafunzo yafanyike, malipo ya pesa yafanyike bado vyombo vya dola visiwe na hizo taarifa. Hili ni tusi kwa vyombo.
 
Tume ilitakiwa iwe tume huru ndio ingeweza kuja na majibu murua. Ni ngumu tume kuja na majibu ya kumsagia kunguni aliyeiunda. Tume ilitakiwa ijitegemee, kama kupiga ipige pande zote mbili, kama ni makosa hata upande wa pili nao ulikosea kutenda vitendo vile vya kijinai
Samia ulitaka awe mjiga aunde tume ya kumsagia kunguni.
 
Huyu babu nimemdharau sana kuanzia leo heshima yake will be reduced to zero, he is pleasing his mistress, at his age he has to remain faithful and trustworthy but what he has done is the same like mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, these two old tumbocrat may never live longer.
 
Hivi inakuwaje wanapiga makofi kupokea ripoti? Kwamba wanatoa pongezi kwa vifo au? Its so evil!!!
 
Tume ingekuwa huru leo pangekuwa hapatoshi wote waliomo ndani wamehusika
 
Back
Top Bottom