Wadau washauri kusiwe na Ada ya kupata Kitambulisho kipya cha Mpiga Kura iwapo cha awali kitafutika au kupotea

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
JamiiForums , Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Jukwaa la Katiba (JUKATA), Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Taasisi ya Twaweza na Centre for Strategic Litigation (CSL) wametoa maoni kwenye Miswada ya Sheria ya Uchaguzi na kushauri kusiwe na gharama za kupata Kitambulisho kipya cha Mpiga Kura.

Wadau wamebainisha kuwa hatua hiyo ni ili kuhakikisha Haki ya Kupiga Kura na pia kuhamasisha mwitikio wa Wapiga Kura kushiriki Uchaguzi

Kifungu cha 20 na 21 cha Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani vimeanisha Mtu anaweza kupata kadi nyingine ya Mpiga Kura iwapo aliyokuwa nayo imeharibika, imefutika, kupotea au akirekebisha taarifa na baada ya kulipa ada iliyoanishwa, kama ipo, ambapo Wadau wamependekeza neno 'Ada' lifutwe

Kifungu cha 20 cha Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kinasema:
20.-(1) Endapo kadi ya mpiga kura iliyotolewa kwa mtu yeyote imepotea, imefutika au imeharibika, mtu ambaye kadi hiyo ilitolewa kwake anaweza kuomba yeye mwenyewe kwa afisa mwandikishaji, mwandishi msaidizi au mtendaji mwingine yeyote kama itakavyoelekezwa na Tume kwa madhumuni ya uandikishaji wa wapiga kura kupewa kadi mpya ya mpiga kura.

(2) Baada ya maombi hayo kufanyika, afisa mwandikishaji, mwandishi msaidizi au mtendaji mwingine yeyote kama itakavyoelekezwa na Tume kwa madhumuni ya uandikishaji wa wapiga kura ikiwa atajiridhisha kuwa maombi yamefanywa ipasavyo na kwamba mwombaji bado ana sifa za kuandikishwa, atampa mwombaji kadi mpya ya mpiga kura baada ya mwombaji kulipa ada iliyoainishwa, ikiwa ipo, na iwapo maombi yatafanyika kutokana na kuharibika au kufutika kwa kadi ya mpiga kura, mwombaji atarudisha kadi hiyo iliyoharibika au iliyofutika.

Kifungu cha 21 cha Muswada huo kinabainisha kuwa:
21.-(1) Endapo taarifa zozote zilizopo katika kadi ya mpiga kura au Daftari la Awali la Wapiga Kura zitahitaji kufanyiwa marekebisho kwa sababu ya kubadilika kwa jina au mabadiliko mengine yoyote katika mazingira ambayo yatamuathiri mtu ambaye kadi ya mpiga kura imetolewa kwake tofauti na mabadiliko ya makazi kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda lingine, mtu ambaye kadi ya mpiga kura imetolewa kwake anaweza kuomba kadi mpya ya mpiga kura.

(2) Baada ya kupokea maombi na kujiridhisha kuwa maombi yamefanywa ipasavyo na kwamba mwombaji bado ana sifa ya kuandikishwa, afisa mwandikishaji, mwandishi msaidizi au mtendaji mwingine yeyote kama itakavyoelekezwa na Tume kwa madhumuni ya uandikishaji wa wapiga kura atamwandikisha mwombaji katika fomu itakayoainishwa na kumpa kadi nyingine ya mpiga kura:

Isipokuwa kwamba, kadi mpya ya mpiga kura haitatolewa chini ya kifungu hiki hadi mwombaji atakaporejesha kadi yake ya mpiga kura au atakapomthibitishia afisa mwandikishaji, mwandishi msaidizi au mtendaji mwingine yeyote kama itakavyoelekezwa na Tume kwa madhumuni ya uandikishaji wa wapiga kura kuwa kadi hiyo imepotea au imeharibika na amelipa ada iliyoainishwa, ikiwa ipo.


Maoni ya Wadau ni kama ifuatavyo:
image.png


Pia soma: Maoni ya Jumla ya Wadau Kwenye Miswada ya Sheria za Uchaguzi na Muswada wa Vyama vya Siasa - Sehemu 1

- Maoni ya Wadau kwenye Miswada ya Sheria za Uchaguzi na Muswada wa Vyama vya Siasa - Sehemu ya 2

MATOKEO.
 
Back
Top Bottom