Wabunge wa Viti Maalum na wale wa kuteuliwa na Rais wana faida gani katika Taifa?

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Mimi naomba kushangaa, nchi inapokua uchumi wa chini ni heri kujitahidi kuzuia mianya ya ufujaji na upotevu mkubwa wa pesa za serikali.

Licha ya kwamba bunge la Tanzania lina wabunge wengi kutokana na majimbo kuwa mengi, bado pia wanaongeza wabunge wa viti maalumu na wabunge wa kuteuliwa tu na Rais, hawana majimbo wala hawana ofisi.

Hii ni kama vile hatujitambui wabunge wasio na majimbo wanakua zaidi ya 100, hivi kwa mwezi tunapoteza kiasi gani hapa?

Baaada ya miaka mitano wanapewa na viinua migongo kabisa.

Aisee hiii nchi inahitaji mabadiliko makubwa sana, hii hela inayopotea kwa hawa wabunge wasio na majimbo ingeweza kujenga zahanati ngapi kila mwaka?

Basi kama tumeshindwa kubadilisha katiba kwa ujumla, inabidi tubadilishe baadhi ya vipengele, tuna matumizi makubwa sana yasiyo na tija.
 
Kama ulivyosema awali! Hivyo ni vitu maalumu! Kipi hukijui! Vile ni vyakula vya maofisa wa CCM. Angalia tofauti ya vitu maalumu wanaotokea ccm na wale wa viti maalum wanaotokea upinzani. Hawa wa upinzani(sio covid 19) wapo very strong, no mipasho, hoja hoja! Tofauti na kina lucy mayenga, vick kamata taarabu na kuvaa vikuku tu.
 
Mimi naomba kushangaa, nchi inapokua uchumi wa chini ni heri kujitahidi kuzuia mianya ya ufujaji na upotevu mkubwa wa pesa za serikali...

Hawana faida zaidi ya mzigo wa posho na mishahara
 
Wale viti maalumu hua ni kuleta uwiano wa 50 50 kwa wanawake na wanaume bungeni.

Katika maswala ya gender equality inabidi wote tuonekane tupo katika ngazi za kufanya maamuzi na hili siyo ombi ni lazima ili kupata mikopo.

Kwahivyo viti maalumu vilibuniwa kwaajili hiyo.

Hawa wa kuteuliwa kuna scenarios nyingi;
- Mfano rais akaona kuna mtu anafaa kua waziri ila siyo mbunge atatumia hiyo nafasi.

- Anataka tu kuongeza idadi ya watakaompa kura za ndio bungeni.

- kulipa fadhila.

- Kuhonga n.k.
 
Back
Top Bottom