Siku ya Wanawake: Baada ya Watanzania Kumchagua Rais Mwanamke, 2025, Je Tumchagulie na Wabunge na Wadiwani kufikia 50/50 kisha Tufute Viti Maalum?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,605
Leo ni siku ya Wanawake duniani
Kwanza hongera kwa wanawake wote duniani kwa kuadhimisha hii siku yao.
20240310_173003.jpg

Leo kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, makala ya leo ni swali
" Baada ya Watanzania kumchagua rasmi Rais mwanamke, Uchaguzi Mkuu wa 2025, je mnaonaje kama pia tumchagulie na wabunge na madiwani wanawake wa kutosha kufikisha asawa wa kijinsia wa asilimia 50/50?. Kuelekea Usawa wa Kijinsia: Kumbe 50/50 Inawezekana!, Wanawake Hao wa 50/50 Wapo!. Hongera Sana Rais Samia Kwa Kuonyesha Njia! Je 2025 Tuwaonyeshe?

Na hiyo aslimia 50/50, ikiisha fikiwa na kupatikana, kuna haja ya kuendelea na ubunge na udiwani wa viti maalum kwa wanawake?, watakuwa ni wa nini?.

Mnaonaje au baada ya kufikiwa kwa idadi ya 50/50, na kukidhi usawa wa kijinsia, jee tuvifute viti maalum kwasababu tayari tutakuwa tumefikia usawa wa kijinsia kwa mujibu wa mkutano wa Beijing?.
ila hata Amiri Jeshi Mkuu anapokuwa Mwanamke, hapendi kuitwa Amirati ana prefers kuendelea kuitwa hivyo hivyo Amiri ambalo ni jina la kiume au chairman badala ya Chairwoman or chairperson.

Tukubali tukatae bado tuna baadhi ya watu miongoni mwetu, waliofilisika kiakili na kisiasa, ambao bado wana tatizo la kutawaliwa na mfumo dume vichwani mwao na kuamini urais wa nchi ni kazi ya kiume!, hivyo ni kweli lile tukio la March 17, lilitokea kabla ya Machi 17!, hivyo lilipotokea wakafanya siri ili kumtafuta mwanaume wa kushikilia kwa kuamimi Mwanamke hawezi!

Hivyo na mimi nauliza kuna ukweli wowote kuwa kuna kazi za kiume na za kike?, na kuna kazi za kike ambazo ni za kike tuu!, wanaume hawaziwezi kama kubeba, lakini pia kuna kazi za wanawake, wanaume wanazifanya vizuri zaidi kuliko wanawake wenyewe!. Jee kuna kazi za kiume ambazo wanawake hawawezi?

Sasa baada ya Tanzania kupata rais Mwanamke kwa kudra tuu ya Mwenyezi Mungu, natoa wito kwa Watanzania kumchagua rasmi Rais mwanamke, Uchaguzi Mkuu wa 2025, je mnaonaje kama pia tumchagulie na wabunge na madiwani wanawake wa kutosha kufikisha ile idadi ya asawa wa kijinsia wa asilimia 50/50?. +, Kuelekea Usawa wa Kijinsia: Kumbe 50/50 Inawezekana!, Wanawake Hao wa 50/50 Wapo!. Hongera Sana Rais Samia Kwa Kuonyesha Njia! Je 2025 Tuwaonyeshe?

Na hiyo aslimia 50/50, ikiisha fikiwa na kupatikana, jee bado kuna haja ya kuendelea na ubunge na udiwani wa viti maalum kwa wanawake?, watakuwa ni wa nini?.

Mnaonaje au baada ya kufikiwa kwa idadi ya 50/50, na kukidhi usawa wa kijinsia, jee tuvifute viti maalum kwasababu tayari tutakuwa tumefikia usawa wa kijinsia kwa mujibu wa mkutano wa Beijing?.

Kwa sababu wanawake wa kukidhi asilimia 50/50. Wapo, wahamasishwe, wajitokeze, na Watanzania tuwachague, na baada ya kufikiwa hiyo 50/50. Viti maalum vifutwe!.

Wasalaam.

Paskali
 
Viti maalumu nivya kufutwa, havina maana yoyote kwa ustawi wa taifa, badala yake ni matumizi mabaya ya pesa ya umma.

Kingine cha muhimu ni kwamba hatupaswi kumchagua mtu kwa misingi ya jinsia,bali kwa kuzingatia uwezo,uwajibikaji na weredi.

Jambo hili nimeandika hapa

Leo ni siku ya Wanawake duniani
Kwanza hongera kwa wanawake wote duniani kwa kuadhimisha hii siku yao.

Leo kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, makala ya leo ni swali
" Baada ya Watanzania Kumchagua Rasmi Rais Mwanamke, Uchaguzi Mkuu wa 2025, Je mnaonaje kama pia Tumchagulie na Wabunge na Wadiwani wa kutosha kufikisha asawa wa kijinsia
wa asilimia 50/50, na hiyo aslimia 50/50, ikiisha kupatikana, kuna haja ya kuendelea na viti maalum kwa wanawake, au tuvifute Viti Maalum kwasababu tayari tutakuwa tumefikia usawa wa kijinsia kwa mujibu wa mkutano wa Beijing?.

Itaendelea...

Paskali
Mkuu Paskali, unaendelea kuingia katika mtego wa kibaguzi ambao ukiendekezwa utalitafuna taifa. Unashadadia ubaguzi wa kijinsia, na tukienda mbele dini, ukabila, marika, walemavu, wakulima, wafanya biashara, wasomi, wasiosoma nk nao wataanza kugombania nafasi sawa ktk uongozi. Tunataka kiongozi kwa vigozo vya sifa si kwasababu ya jinsi yake au kundi fulani. Kuna utaratibu wa kuyafanya hayo makundi ambayo unadhani yataachwa nyuma kwenye utaratibu wa kawaida ktk uchaguzi, labda useme huo utaratibu uboreshwe pale palipo na mapungufu.

Kuna haja gani ya kufanya uchaguzi 2025 kama tayari Rais ameshapatikana?. Husije na habari za mazoea ya ndani ya chama cha mapinduzi. Hata hivyo Samia hakupatikana kwa huo utaratibu wa mazoea hivyo lolote linaweza kutokea ndani ya chama. Soma majira na alama za nyakati.
 
Leo ni siku ya Wanawake duniani
Kwanza hongera kwa wanawake wote duniani kwa kuadhimisha hii siku yao.

Leo kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, makala ya leo ni swali
" Baada ya Watanzania Kumchagua Rasmi Rais Mwanamke, Uchaguzi Mkuu wa 2025, Je mnaonaje kama pia Tumchagulie na Wabunge na Wadiwani wa kutosha kufikisha asawa wa kijinsia
wa asilimia 50/50, na hiyo aslimia 50/50, ikiisha kupatikana, kuna haja ya kuendelea na viti maalum kwa wanawake, au tuvifute Viti Maalum kwasababu tayari tutakuwa tumefikia usawa wa kijinsia kwa mujibu wa mkutano wa Beijing?.

Itaendelea...

Paskali
hakika wewe ni mchangiaji bora kuliko wote kwenye ukumbi huu,unaandika vizuri mno kwa maantiki,uteuzi mzuri wa msamiati na una mawanda mapana ya uelewa juu ya mada mbalimbali,nakuombea kwa Mungu akupe furaha,amani na mafanikio tele kwenye maisha yako
 
Fifty fifty
Leo ni siku ya Wanawake duniani
Kwanza hongera kwa wanawake wote duniani kwa kuadhimisha hii siku yao.

Leo kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, makala ya leo ni swali
" Baada ya Watanzania kumchagua rasmi Rais mwanamke, Uchaguzi Mkuu wa 2025, je mnaonaje kama pia tumchagulie na wabunge na madiwani wanawake wa kutosha kufikisha asawa wa kijinsia wa asilimia 50/50?. Kuelekea Usawa wa Kijinsia: Kumbe 50/50 Inawezekana!, Wanawake Hao wa 50/50 Wapo!. Hongera Sana Rais Samia Kwa Kuonyesha Njia! Je 2025 Tuwaonyeshe?

Na hiyo aslimia 50/50, ikiisha fikiwa na kupatikana, kuna haja ya kuendelea na ubunge na udiwani wa viti maalum kwa wanawake?, watakuwa ni wa nini?.

Mnaonaje au baada ya kufikiwa kwa idadi ya 50/50, na kukidhi usawa wa kijinsia, jee tuvifute viti maalum kwasababu tayari tutakuwa tumefikia usawa wa kijinsia kwa mujibu wa mkutano wa Beijing?.

Itaendelea...

Paskali
Ni ujinga kuwaza fifty fifty kwenye uongozi badala ya kuwaza uchapaji kazi wamtu.
Hiyo fifty tuiweke kwenye masomo/elimu sio kazi/uongozi
 
Viti maalumu vifutwe. Lakini kwakuwa katiba mpya imeota mbawa basi mabadiliko madogo ya katiba yatakayovifuta viti maalumu yaongezee idadi ya wabunge wa kuteuliwa na rais wafike hata 30.

Itamsaidia kuunda baraza la mawaziri analolitaka badala ya kuendelea ku 'recycle' hawa wa kujua kusoma na kuandika.
 
Viti maalumu ni upotevu tu wa resources, ni chanzo cha wanasiasa kujaza mahawara zao kwenye muhimili wa kutunga sheria, ni vyema kila mtu agombee, haya mambo ya viti maalumu yanahimizwa sana huku dunia ya tatu kwa walala hoi ili muendelee kuwa na matumizi yasiyo na tija muendelee kubaki kwenye lindi la umasikini. Watu wapewe nafasi sawa waingie majimboni wamwage sera then wananchi wachague. Maana hakuna mahali mjulubeng au papuchi inatumika kutunga sheria ama kufanya maamuzi ya taifa so jinsia sio issue.
Alamsiki
 
Leo ni siku ya Wanawake duniani
Kwanza hongera kwa wanawake wote duniani kwa kuadhimisha hii siku yao.

Leo kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, makala ya leo ni swali
" Baada ya Watanzania kumchagua rasmi Rais mwanamke, Uchaguzi Mkuu wa 2025, je mnaonaje kama pia tumchagulie na wabunge na madiwani wanawake wa kutosha kufikisha asawa wa kijinsia wa asilimia 50/50?. Kuelekea Usawa wa Kijinsia: Kumbe 50/50 Inawezekana!, Wanawake Hao wa 50/50 Wapo!. Hongera Sana Rais Samia Kwa Kuonyesha Njia! Je 2025 Tuwaonyeshe?

Na hiyo aslimia 50/50, ikiisha fikiwa na kupatikana, kuna haja ya kuendelea na ubunge na udiwani wa viti maalum kwa wanawake?, watakuwa ni wa nini?.

Mnaonaje au baada ya kufikiwa kwa idadi ya 50/50, na kukidhi usawa wa kijinsia, jee tuvifute viti maalum kwasababu tayari tutakuwa tumefikia usawa wa kijinsia kwa mujibu wa mkutano wa Beij

Itaendelea...

Paskali

Tanzania hakuna uchaguzi, Bali Kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura. Sasa hiyo 50/50 inatoka wapi?
 
Wasomi wa Tanganyika wasiojua ni Kwa Nini wamepata elimu.
Ukimwita Mtanganyika hakuelewi mpaka umwite Mtanzania😂.

Ila Zanzibar Iko na Icon yake mpaka leo.ina mamlaka kamili kabisa.Kiufupi ni Nchi kamiri ila Tanganyika wameamua kujiita Wabara🤔.
Nirudi kwenye hoja,hiyo 2025 tayari una matokeo🤔.
Bangi hizi jamani,wasomi mnakwama wapi?.

Tunahitaji Rais mwenye uwezo na kibari Cha wapiga kura,na sio jinsia.
Kama jinsia,basi tunaomba mkeo awe kichwa Cha familia.
Mbadili ubini wa watoto wenu waitwe jina la mkeo kwenye ubini.
Si mnaona jinsia inataka kuchukua mda ambao sio wake.
Same time msijizime data wakuu.

Mnasifia mpaka mnaboa.
Unafiki mpaka lini,eti wakifikia hiyo 50/50 ndo wataleta maisha Bora?.
Ccm janga la Taifa.
Sijawabagua wanawake,bali mnakuwa na unafiki kupitia kipimo wajameni.
 
50/50 hata mtoto atakua ni wamama na baba atakua ni rafiki tu.mwanaume ni jukumu na ni ngao ya jamii nzima.wanawake wanataka ukinzani na asili yao
 
Kwa Tanzania 50 50 ni ngumu kufanya kazi. Kenya tu hapo imeshindikana kutekelezwa, Tena wao ipo kikatiba.
 
Back
Top Bottom