Wenzetu Kenya wameliona hili, sisi Tanzania ndio kwanza tuna mpaka wabunge viti maalum wasio na chama

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Hakika nichukue nafasi hii kumpongeza Mwanasheria Mkuu Mstaafu wa Kenya kwa kuonesha uzalendo kwa nchi yake juu ya kutaka wabunge wa viti maalum wasiwepo ili kuwapunguzia mzigo wa kodi wananchi masikini wa Kenya.

Ni imani yangu hata serikali ya Tanzania inafaa kuiga suala hili kwa kuwaondoa wabunge Viti Maalum Bungeni kwani hawana tija yoyote kwa wenye nchi ambao ni wananchi masikini wa Tanzania.

Nimekuwa nashangaa sana kuona Bunge na Serikali ya Tanzania kuendelea kuwakumbatia wabunge 19 wasio na chama badala ya kuwafukuza ili kupunguza idadi ya wabunge viti maalum huku wakijua ni uvunjifu wa Katiba.

Wabunge hao ni batili kwani upatikanaji wao haukufuata utaratibu uliopo kisheria na ndio maana wakafukuzwa na chama chao lakini bado Bunge na Serikali linawalipa mishahara na posho ambazo ni kodi na matozo yanayolipwa na masikinini.

Wabunge wa viti maalum wafutwe kuokoa fedha za walipa kodi.


1554184342.jpg
1652427482224.jpg
 
Hili ndilo tatizo kubwa la binadamu wenye ngozi nheusi. Unafiki!!!
Hayo maoni si alitakiwa ayatoe pale alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali!!

Bya the way, hata mimi kwa upande wangu siungi mkono uwepo wa hao wabunge wa viti maalum, pia siungi mkono uwepo wa wabunge 10 wa kuteuliwa na Rais! Siungi mkono uwepo wa vyeo vya kikoloni kama vile vya Wakuu wa Mikoa, Wilaya, nk.
 
Back
Top Bottom