Wabunge Dr. Slaa na Dr. Tarab wafanyiwa umafia!

Wabunge Dr. Slaa na Dr. Tarab wafanyiwa umafia!

Kitakachofuta sasa ni kuwa wekea Polonium kwenye miswaki yao ama chakula, nadhani mnakumbuka murder of Alexander Litvinenko.....jamani wapinzani na wale wenye nia njema na nchi yetu kuweni makini. Hii siwezi kutoamini kama waziri kijana mwenye scandal ya national ID hahusiki. God bless Dr Slaa, God Bless Tanzania

Masa
 
Ama kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Hii itaigharimu sana serikali na CCM...

Hata hivyo iwe somo kwa wanasiasa wetu kwa umoja wao.....Maana ni wengi wataumia kwa style hii.

Kuhusu kukamwatwa sijui ni sheria gani itatumika maana nijuavyo hadi sasa hatuna sheria ya kulinda siri za mtu binafsi....

Tanzanianjema
 
Criminal!

Smells like Watergate.

Now ask yourself this question, who stands to gain the most from this intel?

It is either the CCM establishment or it's mafisadi, what am I talking about, like they are two different things.

I see masha's hand in this.
 
Usalama wa wabunge upo wapi Dodoma! Kama inawezekana kuweka vinasa sauti chumbani, kwanini isiwezekane kuweka sumu au dawa yeyote ya "kill slowly" kwenye mashuka na hata air freshner! Hoteli hizi zina credibility yeyote tena!?!
 
Walikuwa wanamvizia kuona kama anaingiza kimada nini?
Bug Sweeping ndio jibu. Lakini inategemea na aina ya bug waliyoweka kama ni zile zinakuwa remotely controlled kuna kazi ya kuzidetect(controllers wanaweza kuswitch on and off), nyingine zinabadirisha mawimbi kila mara na ofcourse kuna kuishiwa betri so huwezi kudetect. Mwisho deadly bugs ni zile zisizo emit RF.

**Vile vile huwezi kusahau kuwa mtu anaweza kuactivate microphone ya simu yako remotely ata kama umezima simu. Kazi kwenu

..... ki-rf jammer kimoja na ki-sweeper kinamfaa. pia anaweza kuongeza ki-cheap metal detector ili kukamilika kiu-full masinondo. iwapo simu kama ulivyoainisha zinakuwa chanzo (kitu ambacho nadhani kwa hapa bongo bado maana ni manufacturer/network provider controlled), basi atumie zile za mwaka 1998 hivi pale anapokuwa katika maongezi sensitive. nyingi za wakati huo zilikuwa na basic functions tu - simu, pager na sms.
 
Hao ni usalama wa taifa, badala ya kuwafuatilia akina Chenge wanahangaika na akina Dr. Slaa.

Dr. Slaa atakuwa mjinga kwenye kukutana na informers wake kwenye chumba anacholala au kupigiwa simu akiwa kwenye hicho chumba.

Ukiwa na deal lolote ni kwenda kwenye park.

Mwulize Annan, Wamarekani kila siku walikuwa wananasa mazungumzo yake.
 
Huyu hana sera toka alivyondolewa kwenye kura za maoni CCM. Sasa hivi anatafuta umaarufu kwa njia zozote zile na watu wameshashtuka. Hana lolote ni sawa na Mengi. Wanapenda Misafa.

Mwenye lolote nani? Wewe!
 
men! this sounds quite spooky.it's nothing new really, i guess many more outspoken critics of the regime are under the same bugging patch.or worse.what were they trying to achieve?

still it only demonstrates how divided the operatives in the system are, for Dr Slaa to find out and actually retrieve the gadgets, i won't be surprised if the culprits are named within a short time.question is, will they be prosecuted?

shame on the government, it spends more time fighting accusations than it does on planning and moving our nation forward in development.the ultimate winner here will the innocent Tanzanian whose usingizi wa muda mrefu is being disturbed by the activities of walafi.
 
Hao ni usalama wa taifa, badala ya kuwafuatilia akina Chenge wanahangaika na akina Dr. Slaa.

Dr. Slaa atakuwa mjinga kwenye kukutana na informers wake kwenye chumba anacholala au kupigiwa simu akiwa kwenye hicho chumba.

Ukiwa na deal lolote ni kwenda kwenye park.

Mwulize Annan, Wamarekani kila siku walikuwa wananasa mazungumzo yake.

.... funny in a way but it's sadly true, mithili ya akina osama . ikishindikana, awe na kiredio kimoja kwa ajili ya ku-play mazungumzo yenye variation ya sauti yake mwenyewe ili ku-confuse bugs kama zinakuwepo.
 
mtaambiwa kuwa "vyombo hivyo si vya kunasa sauti bali ni kwa ajili ya kuhakikisha joto la magodoro linabakia kuwa constant"! Atakayesema hivyo atakuwa Waziri Mkuu tena kwa uchungu wote na machozi yakimlenga "Dr. Slaa ni mtu muhimu sana, tumechoshwa kuona anatishiwa tishiwa hivyo kwa kutumia mbinu za kisasa tumemuongezea ulinzi na usalama. Sasa kama Watanzania wanafikiri sisi kumlinda Dr. Slaa ni kosa kubwa kulinganisha na yeye kuja kurudhika fine! Mungu atanisamehe na ninaomba mtusamehe"... atasema Waziri Mkuu..

Wabunge watasimama na kumpigia makofi. Vyombo vya habari vitaandika "Waziri Mkuu azikoga nyoyo za wabunge"

Sawa mkuu. Ndivyo tunavyotarajia. Itakuwa kichekesho kweli. Yaani ni chombo cha kuongeza joto! tena Dodoma!
 
1. Hadi hivi sasa vyombo mbalimbali vya usalama vilikuwa vinasubiriwa kufika hotelini hapo ili kuhakikisha kuwa vifaa hivyo ni vitu gani, vya nani, na vimewekwa kwa madhumuni gani.

2. Endapo itagundulika na kuthibitishwa kuwa vifaa hivyo ni vya kunasia sauti au kunasa mawasiliano itakuwa ni mara ya kwanza kwa kugundulika hadharani kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametegeshwa namna hiyo na zaidi ya yote itatishia uhuru wa wao kuzungumza, kukutana, au kuwasiliana na mtu yeyote kama raia huru.

3. Zaidi ya yote wataalamu wa kisheria wameidokeza KLHN kuwa endapo hilo ni kweli "basi yeyote atakayekuwa amefanya hivyo atakuwa amevunja Katiba Ibara 18:1" inayotambua uhuru wa mtu binafsi na kukataza mawasiliano yake kuingiliwa nje ya sheria.


1. mtaambiwa kuwa "vyombo hivyo si vya kunasa sauti bali ni kwa ajili ya kuhakikisha joto la magodoro linabakia kuwa constant"!

2. Atakayesema hivyo atakuwa Waziri Mkuu tena kwa uchungu wote na machozi yakimlenga "Dr. Slaa ni mtu muhimu sana, tumechoshwa kuona anatishiwa tishiwa hivyo kwa kutumia mbinu za kisasa tumemuongezea ulinzi na usalama.

4. Sasa kama Watanzania wanafikiri sisi kumlinda Dr. Slaa ni kosa kubwa kulinganisha na yeye kuja kurudhika fine! Mungu atanisamehe na ninaomba mtusamehe"... atasema Waziri Mkuu..

5. Wabunge watasimama na kumpigia makofi. Vyombo vya habari vitaandika "Waziri Mkuu azikoga nyoyo za wabunge"

- There we go again, tafadhali tuwapeni nafasi wanausalama wafanye kazi yao kwanza ndio turushe hukumu, mbona mbio mbio hivi kwani viongozi wa upinzani wote wanampenda Dr. Slaaa? Vyama vyote vya upinzani wanamepnda Dr. Slaa? Je viongozi wote wa Chadema wanampenda Dr. Slaaa?

- Ninamtakia heri shujaa wangu Dr. Slaa, ila ajue tu kua haiwezekani kwamba hii ikawa ni mara ya kwanza, na sio yeye tu maana siasa ni mchezo mchafu sana maana na yeye hatujui njia anazotumia kupata dataz za serikali, lakini tunamshangalia anyways kwa sababu anazitumia dataz hizo kwa manufaa ya sisi wananchi wanyonge na taifa letu, siamini hawa waliomtegea walitaka kuzitumia habari zake nyeti kwa manufaa ya taifa na sisi wananchi.

Tusirushe hukumu bila ukweli, tupate kwanza habari za pande zote mbili na wanasualama pia, ingawa hatuwaamini sana hasa tukikumbuka jinsi
Chenge alivyokwenda kutafuta kiti chake bungeni usiku wa manane bila kikao cha bunge.


Hadi hivi sasa vyombo mbalimbali vya usalama vilikuwa vinasubiriwa kufika hotelini hapo ili kuhakikisha kuwa vifaa hivyo ni vitu gani, vya nani, na vimewekwa kwa madhumuni gani.
 
klhnsiren.gif

KLHN/JF Exclusive: Na. Mwandishi Wetu

Wabunge wawili wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dr. Wilbroad Slaa na Dr. Ali Tarab Ali wamekuta vyumba vyao vimetegeshwa vyombo ambavyo vinaamini kuwa kuwa ni vya kunasa mawasiliano bila ya wao wenyewe kujua. Habari kutoka Dodoma ambazo zimethibitishwa na Dr. Slaa zimesema kuwa ugunduzi huo umefuatia taarifa za kijasusi ambazo zilipenyezwa kwa waheshimiwa hao kutoka "vyanzo vya kuaminika" kuwa vyumba vyao vimetegeshwa vyombo hivyo na watu ambao KLHN inasita kuwataja kwa sasa.[ ..........
Wow !! Hii kali.....JF where people dare ? - wenzio tuna njaa.

Hadi hivi sasa vyombo mbalimbali vya usalama vilikuwa vinasubiriwa kufika hotelini hapo ili kuhakikisha kuwa vifaa hivyo ni vitu gani, vya nani, na vimewekwa kwa madhumuni gani.............
Hmm sijui - are they one and the same ? - haiwezekani kukata mti ulokalia.

Zaidi ya yote wataalamu wa kisheria wameidokeza KLHN kuwa endapo hilo ni kweli "basi yeyote atakayekuwa amefanya hivyo atakuwa amevunja Katiba Ibara 18:1" inayotambua uhuru wa mtu binafsi na kukataza mawasiliano yake kuingiliwa nje ya sheria.
Katiba ya wapi ? hii yetu mbona inavunjwa kila leo ? si kuna kinga.

Juhudi za kupata uongozi wa Polisi zinaendelea na tutawapa taarifa pindi tukijua nini kinachoendelea mjini Dodoma.
Et tu Brutus ? - nothing new, it's all just a change of scene - bora tusubiri.
 
Jamani kama ni kweli, hii ni kali!. Tulizoea kusoma hivi vidubwana kwenye spy novels enzi za cold war kumbe ni kweli tena enzi hizi cold war imeisha!. Lets not speculate any more and wait for more facts to unfold. Na kama ni 'waziri kijana' tena, itakuwa ni laana ya Mangi!.
 
- hasa tukikumbuka jinsi
Chenge alivyokwenda kutafuta kiti chake bungeni usiku wa manane bila kikao cha bunge.

Mkulu unapiga Ikulu kabisa huogopi kitu hahahah umenifurahisha .....kikao cha bunge saa nane hahahahah haya mtu wangu tupo pamoja kwa hili. Ila waziri kijana ana hali mbaya kama ni mgonjwa anapumulia mashine

Masa
 
- There we go again, tafadhali tuwapeni nafasi wanausalama wafanye kazi yao kwanza ndio turushe hukumu, mbona mbio mbio hivi kwani viongozi wa upinzani wote wanampenda Dr. Slaaa? Vyama vyote vya upinzani wanamepnda Dr. Slaa? Je viongozi wote wa Chadema wanampenda Dr. Slaaa?

Tusirushe hukumu bila ukweli, tupate kwanza habari za pande zote mbili na wanasualama pia, ingawa hatuwaamini sana hasa tukikumbuka jinsi
Chenge alivyokwenda kutafuta kiti chake bungeni usiku wa manane bila kikao cha bunge.

Mimi nadhani pamoja na kuwa makundi yote yaliyotajwa wapo wasiompenda Dr Slaa, lakini bado ukweli unabaki kuwa masilahi ya hayo makundi hayako sana mashakani ukilinganisha na kundi kubwa la wasiopenda mabadiliko, na ambao bahati mbaya wengi wao wamo ndani ya mfumo. Hivyo waacheni watu wacheu, ukweli ukitoka, nao watapata nafasi ya kupima kulingana na yale waliyokuwa wanayahisi.

Lakini kubwa zaidi hapa, ni kupeana habari, na kumbuka kuwa habari zinasema kuwa Dr Slaa alipata habari za kuwepo vifaa hivyo kabla hata ya kufika chumbani, hivyo hawa hawa unaotaka wasiseme sasa, wapo wenye habari za uhakika na sio sahihi kuwasitisha wasitufikishie hapa jamvini! La msingi wenye taarifa za uhakika watumwagie hapa kama unavyotumwagia.
 
Hao ni usalama wa taifa, badala ya kuwafuatilia akina Chenge wanahangaika na akina Dr. Slaa.

Dr. Slaa atakuwa mjinga kwenye kukutana na informers wake kwenye chumba anacholala au kupigiwa simu akiwa kwenye hicho chumba.

Ukiwa na deal lolote ni kwenda kwenye park.

Mwulize Annan, Wamarekani kila siku walikuwa wananasa mazungumzo yake.

mwongo wewe.........
 
..... ki-rf jammer kimoja na ki-sweeper kinamfaa. pia anaweza kuongeza ki-cheap metal detector ili kukamilika kiu-full masinondo. iwapo simu kama ulivyoainisha zinakuwa chanzo (kitu ambacho nadhani kwa hapa bongo bado maana ni manufacturer/network provider controlled), basi atumie zile za mwaka 1998 hivi pale anapokuwa katika maongezi sensitive. nyingi za wakati huo zilikuwa na basic functions tu - simu, pager na sms.

Say the bug used haitransmit radio waves lakini inarecord tuu?
Ebu niulize swali, Mh. Slaa aliona mabadiriko yoyote ya sauti kwenye simu ya ndani(kama alikuwa nayo), Radio na TV kupata interference kila mara?
Kwa zaidi search Technical Surveillance Counter-Measures.

Kwenda kwenye park kwenye sio safe vile vile angalia Enemy Of The State, mwendo ni kutumia old school methods.
 
Last edited:
Mpaka vifaa viwekwe chumbani kwa mtu, ina maana lazima mlango ulifunguliwa. Na wenye funguo ni wamiliki wa Hoteli, sasa kitu cha kwanza viongozi na wahudumu wa hiyo hoteli wanatakiwa kuisaidia polisi. Lakini kama ni watu wa usalama/serikali ndio walioweka hivyo vifaa, hata hao viongozi na wahudumu wa hiyo hoteli hawatatoa ushahidi utakaomsaidia Dk. Slaa.

Lakini pia kama tuna uchunguzi huru, hivyo vifaa vingeweza onesha alama za vidole (finger prints), ila huenda waliovitoa walivishika bila kutumia gloves.

Kwa kuwa siasa nao ni mchezo wa kuviziana, na kwakuwa Dk. Slaa alisema alitumiwa habari, na alipofika chumbani kwake aliomba na majirani zake waangalie vyumba vyao. Ikakutwa tena kwa Mbunge wa CUF kuna hicho kifaa. Yawezekana pia vifaa wameviweka wenyewe ili kuonesha wanafuatiliwa na wapate huruma toka kwa wananchi. Nakubaliana na Dk. Slaa na wapinzani kwa kazi wanayoifanya kwa Taifa letu, lakini bado siasa yaweza tumika vibaya.

Ingekuwa vyombo vyetu vya uchunguzi viko huru, tungejua mbaya ama mkweli nani?.
 
Walikuwa wanamvizia kuona kama anaingiza kimada nini?
Bug Sweeping ndio jibu. Lakini inategemea na aina ya bug waliyoweka kama ni zile zinakuwa remotely controlled kuna kazi ya kuzidetect(controllers wanaweza kuswitch on and off), nyingine zinabadirisha mawimbi kila mara na ofcourse kuna kuishiwa betri so huwezi kudetect. Mwisho deadly bugs ni zile zisizo emit RF.

**Vile vile huwezi kusahau kuwa mtu anaweza kuactivate microphone ya simu yako remotely ata kama umezima simu. Kazi kwenu

Kaka umenigusa hapo hebu tuelekeze inakuwaje mtu ana-activate microphone ya simu yako hata kama umezima na nini kifanyike kuzuia hili maana ni muhimu wanaJF kujua mbinu hizi. Umesema pia ''Mwisho deadly bugs ni zile zisizo emit RF'' sijakupata naomba ufafanue mkulu hoja yako muhimu sana.
 
Back
Top Bottom