Wabunge Dr. Slaa na Dr. Tarab wafanyiwa umafia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge Dr. Slaa na Dr. Tarab wafanyiwa umafia!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Feb 5, 2009.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Feb 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Kuna taarifa zinatinga mezani kwetu zinadai kuwa kuna mchezo mchafu kafanyiwa mpambanaji Dr. Slaa kwa kuwekewa vinasa sauti chini ya godoro lake na tayari polisi wanaelekea chumbani kwake na watu wa usalama na kuthibitisha tukio hilo.

  Jopo la waandishi wameelekea chumbani kwa Dr. Slaa na watatufahamisha kinachoendelea.

  Hapo ni Dodoma - Hotel 56.
   
  Last edited by a moderator: Feb 6, 2009
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Feb 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Nuh uuuhhhh...that ain't right...
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mmewahi kusikia msemo wa 'mcheza huchezwa" au "mwosha huoshwa".. ni sehemu ya mapambano.. !
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,503
  Trophy Points: 280
  hao wanaoenda 'kuangalia' na hao walioviweka wanatofautianaje?
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Feb 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Hii kitu binafsi nilishaihisi.

  Nimeongea na mtu wa karibu na Dr. Slaa kanihakikishia kuwa kitu hicho kimetokea na akaniambia kwa sasa Slaa hatoweza kuongea kwakuwa ni kitu ambacho hakutarajia angeweza kufanyiwa. Naambiwa alikuwa anapaamini sana chumbani kwake. Katibu wa Bunge yuko njiani kuelekea huko ili polisi na wana usalama wetu watekeleze wajibu wao.

  This' Bongo!
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Feb 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Na nyinyi mnaopenda kuongea ovyo ovyo kwenye simu shauri yenu....
   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ....Icadon, kamanda wetu wa security... hii changamoto kwetu sote

  ....sasa ni kifaa gani cha kisasa kilichopo ambacho ni affordable kinachofaa Mh. Slaa awe nacho kwa ajili ya kukabiliana na ma-invaders wa privacy kama hao?!
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Feb 5, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Hii kitu wanafanyiwa wengi lakini kushtukia ni rahisi. Ndo maana huwa sina makazi maalum!
   
 9. M

  Mkuu Senior Member

  #9
  Feb 5, 2009
  Joined: Jan 1, 2007
  Messages: 127
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mapinduzi yatalindwa kwa haliyoyote
  Mafisadi watalindwa kwa haliyoyote
  Tukitumia ari mpya na kasi mpya
   
 10. share

  share JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,295
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  Siasa za Tanzania ni siasa za kutegeana. Tulidhani bunge lipo kazini kwa maslahi ya Taifa, kumbe kaa yao Dodoma ni sehemu ya kutegana! Mwenye data za uhakika dhidi ya ujambazi wa serikali ndiye anayetegwa!! Badala ya serikali kujirekebisha, inamtega mrekebishaji!!! Siamini kama mtu wa kawaida anaweza kutenda hili hotelini bila ya kutumwa na wenye dhamana. Tutafika kweli?
   
 11. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Walikuwa wanamvizia kuona kama anaingiza kimada nini?
  Bug Sweeping ndio jibu. Lakini inategemea na aina ya bug waliyoweka kama ni zile zinakuwa remotely controlled kuna kazi ya kuzidetect(controllers wanaweza kuswitch on and off), nyingine zinabadirisha mawimbi kila mara na ofcourse kuna kuishiwa betri so huwezi kudetect. Mwisho deadly bugs ni zile zisizo emit RF.

  **Vile vile huwezi kusahau kuwa mtu anaweza kuactivate microphone ya simu yako remotely ata kama umezima simu. Kazi kwenu
   
  Last edited: Feb 5, 2009
 12. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  Where are we going ?
   
 13. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hapo cha kunasa ni siri za kamati ya Bunge sio? kama nihivo inaonekana hata mh. Sauti nae alikua anajua dili maana onyo kalitoa tu jana na leo wamekamata mmoja! duh TZ yetu kaazi kwelikweli! kwa maana hiyo na ile skendo ya id ndio imeshagubikwa na hili watu wanaendelea kupeta!
  Tutafika tu..!
   
 14. share

  share JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,295
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  Dr. Slaa jana alimwaga data za uhakika kwenye kamati ya bunge inayomjadili Masha. Wengi wa wajumbe walistushwa na hali hiyo. Hii ni kawaida ya Dr. Slaa, ni mtu makini. Halisemi jambo bila ya kuwa na data zinazojitosheleza. Na anakerwa kidhati na hali hiyo. Kumuwekea vinasa sauti kitandani ni moja ya njia za kutapatapa kwa mafisadi ili kujua anapataje habari hizi nyeti. Wasiwasi wangu ni kuwa hao wanaenda sasa chumbani kwake kuchunguza wana tofauti gani na walioviweka vyombo hivyo chumbani!
   
 15. Machiavelli

  Machiavelli Member

  #15
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Huyu hana sera toka alivyondolewa kwenye kura za maoni CCM. Sasa hivi anatafuta umaarufu kwa njia zozote zile na watu wameshashtuka. Hana lolote ni sawa na Mengi. Wanapenda Misafa.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Feb 5, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  KLHN/JF Exclusive:

  Na. Mwandishi Wetu

  Wabunge wawili wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dr. Wilbroad Slaa na Dr. Ali Tarab Ali wamekuta vyumba vyao vimetegeshwa vyombo ambavyo vinaamini kuwa kuwa ni vya kunasa mawasiliano bila ya wao wenyewe kujua. Habari kutoka Dodoma ambazo zimethibitishwa na Dr. Slaa zimesema kuwa ugunduzi huo umefuatia taarifa za kijasusi ambazo zilipenyezwa kwa waheshimiwa hao kutoka "vyanzo vya kuaminika" kuwa vyumba vyao vimetegeshwa vyombo hivyo na watu ambao KLHN inasita kuwataja kwa sasa.

  Taarifa hizo ambazo zilipenyezwa mapema leo zilidokeza kuwa vyumba vya wabunge hao na bila ya shaka baadhi yao wengine viko katika uchunguzi katika jitihada ya kupata taarifa za nini waheshimiwa hao wanapanga, nani wanakutana nao na wanazungumza nini. Vyanzo vya udokezi huo wa habari za kijasusi ambavyo vimezungumza na KLHN kwa masharti ya kutotajwa jina, wadhifa au idara vinasema kuwa vifaa hivyo vya kielektroniki viliingizwa humo kwa njia za kiufundi wa hali ya juu na ilikuwa ni vigumu kugundulika.

  Baada ya kupata taarifa hizo Dr. Slaa (Karatu- CHADEMA) hakuzipa uzito mkubwa sana hadi aliporudi hotelini (Hotel 56 iliyoko upande wa Mashariki wa Bunge - Geti la wageni) majira ya saa 12:30 za jioni. Baada ya kufuatilia na kuulizia wahudumu Dr. Slaa aliomba msaada wa kupekua pekua chumba hicho ili kuona kama taarifa alizopewa zina ukweli wowote. Hata hivyo wakiwa wamekata tamaa waliamua kuangalia chini ya godoro/kitanda na kwa sekunde chache walishangazwa na kukuta kifaa ambacho hawakukitambua kikiwa kinamulikamulika taa nyekundu.

  Mara moja taarifa ilitolewa kwa Katibu wa Bunge, Polisi, na waandishi wa habari ambao waliwahi kufika hotelini hapo. Wakati hilo linafanyika Dr. Slaa alitaka kuona kama kati ya wabunge wanne waliopo pale ambao wako karibu naye kama wengine nao wamekabiriwa na kitu kama hicho. Wabunge wawili wa CCM ambao majina yao hayajafahimika hawakukuta kitu kama hicho isipokuwa Dr. Ali Talib Ali (CUF - Konde) anayepakana chumba na Dr. Slaa. Hivyo taarifa hizo nazo zilizidi kuwashtua wabunge hao na hasa lengo na madhumuni ya vitu hivyo.

  Hadi hivi sasa vyombo mbalimbali vya usalama vilikuwa vinasubiriwa kufika hotelini hapo ili kuhakikisha kuwa vifaa hivyo ni vitu gani, vya nani, na vimewekwa kwa madhumuni gani.

  Endapo itagundulika na kuthibitishwa kuwa vifaa hivyo ni vya kunasia sauti au kunasa mawasiliano itakuwa ni mara ya kwanza kwa kugundulika hadharani kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametegeshwa namna hiyo na zaidi ya yote itatishia uhuru wa wao kuzungumza, kukutana, au kuwasiliana na mtu yeyote kama raia huru. Zaidi ya yote wataalamu wa kisheria wameidokeza KLHN kuwa endapo hilo ni kweli "basi yeyote atakayekuwa amefanya hivyo atakuwa amevunja Katiba Ibara 18:1" inayotambua uhuru wa mtu binafsi na kukataza mawasiliano yake kuingiliwa nje ya sheria.

  Kwa muda mrefu hata hivyo Dr. Slaa amekuwa akilalamikiwa kuvujisha siri za serikali na amewahi kutishiwa kukamatwa na Polisi kutokana na kudai kuwa anazo nyaraka mbalimbali za serikali. Hivi juzi baadhi ya viongozi wa serikali wameoneshwa kuchukizwa na kukerwa na Dr. Slaa kupata taarifa ya barua ya Waziri wa Mambo ya Ndani (anayesimamia Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji, Uokoaji) kwenda kwa Waziri Mkuu kuhusiana na suala la mradi wa Vitambulisho.

  Hata hivyo haijulikani kama vifaa hivi vinahusiana kwa namna yeyote na shughuli za Dr. Slaa katika kuibua kashfa mbalimbali za ufisadi. Ikumbukwe kuwa ni Dr. Slaa na viongozi wengine wa upinzani walioibua ile orodha maarufu ya vitendo vya Aibu ambayo hadi hivi sasa baadhi ya walioatajwa wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na kashfa mbalimbali.

  Katika kijarida chetu cha Cheche toleo la wiki hii na katika Mtandao wa JamiiForum, Dr. Slaa aliandika kuwapiga mkwara wale wote watakaojaribu kuficha au kuvuruga masuala mbalimbali ambayo wamekuwa wakiyafanyia kazi.

  Juhudi za kupata uongozi wa Polisi zinaendelea na tutawapa taarifa pindi tukijua nini kinachoendelea mjini Dodoma.
   
 17. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nategemea kupata taarifi ya kwanza kuwa waliokuwa zamu hotelini wote wanashikiliwa na polisi, pili ndani ya saa 5 aliye husika kutajwa, tatu ndani ya siku 2 mhusika/wahusika kuwa washakamatwa. nje ya hapo wananchi watatakiwa kufanya uchunguzi wenyewe na kutoa adhabu kwawatakaye mkamata
   
 18. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #18
  Feb 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Baada ya ripoti ya Polisi ndipo naweza kuona kama kweli hana sera ama anayo.

  Mwanakijiji nimekukubali...
   
 19. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #19
  Feb 6, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nategemea kupata taarifi ya kwanza kuwa waliokuwa zamu hotelini wote wanashikiliwa na polisi, pili ndani ya saa 5 aliye husika kutajwa, tatu ndani ya siku 2 mhusika/wahusika kuwa washakamatwa. nje ya hapo wananchi watatakiwa kufanya uchunguzi wenyewe na kutoa adhabu kwawatakaye mkamata
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Feb 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mtaambiwa kuwa "vyombo hivyo si vya kunasa sauti bali ni kwa ajili ya kuhakikisha joto la magodoro linabakia kuwa constant"! Atakayesema hivyo atakuwa Waziri Mkuu tena kwa uchungu wote na machozi yakimlenga "Dr. Slaa ni mtu muhimu sana, tumechoshwa kuona anatishiwa tishiwa hivyo kwa kutumia mbinu za kisasa tumemuongezea ulinzi na usalama. Sasa kama Watanzania wanafikiri sisi kumlinda Dr. Slaa ni kosa kubwa kulinganisha na yeye kuja kurudhika fine! Mungu atanisamehe na ninaomba mtusamehe"... atasema Waziri Mkuu..

  Wabunge watasimama na kumpigia makofi. Vyombo vya habari vitaandika "Waziri Mkuu azikoga nyoyo za wabunge"
   
Loading...