Wabunge Dr. Slaa na Dr. Tarab wafanyiwa umafia!

Wakuu

Ni kweli nimesikia kwenye Radio kwamba vitu kama Flash Disk vimekutwa kwa Dr Slaa Na Dr Taarab. Polisi wamesema wanachunguza ili waweze kutoa taarifa kamili.

Swali kwa Dr Slaa na mwenzake Tunataka kujua nani alimwambia kuwa kuna vitu vimewekwa kwenye vyumba vyao?

Kama ni kweli Haya mambo yanatisha?? Tusubiri tuone kinachofuata

Dr. Slaa atakuwa ameambiwa na wale jamaa wa Iaitivee tu coz wao ndiyo hwua wanarekodi mazungumzo ya watu.Plus Boss wao yeye huwa analetewa tu habari kuhusiana na vikao vya siri!
 
Hii ishu bila shaka imetokea jana.
Lakini tumeishia kupata habari kuwa wanausalama wanakwenda hotelini.
Vp wakuu wanausalama toka jana hawajafika chumbani??Tunaomba more dataz.
 
Watanzania ambao kwa muda huu mmelala fofofo, muda huu ni Saa saba Usiku, Dodoma hali sio nzuri usiku wa leo, Dr, wilbrod Slaa na Tarab Ally wamewekewa vitu vinavyosadikiwa kuwa ni vifaa vya kuwarekodi kwenye vyumba vyao vya kulala, kwenye sehemu za uvungu wa vitanda. hatujajua lengo la watu hao kuweka vifaa hivyo, ila ninachoweza kusema ni wabunge ambao wamekuwa na changamoto Bungeni, huenda kuna njama za Wabunge hao kuhujumiwa. Nchi yetu sijui inaenda wapi tuiombee.
 
Mzee Mwanakijiji na wengine hasa Invisible tuwe waangalifu sana katika Masuala kama haya na tusipende kutoa maamuzi mapema sana.
Duh,

Mkuu wangu unaua bendi... Hapana, nadhani ukiangalia maandishi yangu sijamhukumu yeyote.

Taarifa hizi nilipewa na mtu ambaye ni wa TISS na yuko Dodoma na kwa bahati nzuri (au mbaya) TBC1 mida ya saa 6 usiku waligusia suala hili "Live" japo kwa sauti tu. Binafsi access ya kuangalia TBC1 sina kwa hapa nilipo lakini kwa walio Bongo wanaweza kuthibitisha hilo.

Nisingependa kumwonea yeyote katika suala hili, siasa ni mchezo na wachezaji wenyewe wanajua namna ya kuucheza kisawasawa... Sipendi kuegemea kwa Slaa ama the opposite, ni vema kuwa fair na kufikisha ujumbe kwa jamii ili ichambue pumba na mchele.

BTW: Nafanya mawasiliano na watu wengine hapo Dodoma nitarejea punde
 
Watanzania ambao kwa muda huu mmelala fofofo, muda huu ni Saa saba Usiku, Dodoma hali sio nzuri usiku wa leo, Dr, wilbrod Slaa na Tarab Ally wamewekewa vitu vinavyosadikiwa kuwa ni vifaa vya kuwarekodi kwenye vyumba vyao vya kulala, kwenye sehemu za uvungu wa vitanda. hatujajua lengo la watu hao kuweka vifaa hivyo, ila ninachoweza kusema ni wabunge ambao wamekuwa na changamoto Bungeni, huenda kuna njama za Wabunge hao kuhujumiwa. Nchi yetu sijui inaenda wapi tuiombee.

Vp hao wanausalama walienda kukagua jana vp imeshia wapi?Maana toka jana tunaona kuwa wanausalama wanaenda hotelini hatujui kama wameviona hivyo au lah?
 
Wakuu

Ni kweli nimesikia kwenye Radio kwamba vitu kama Flash Disk vimekutwa kwa Dr Slaa Na Dr Taarab. Polisi wamesema wanachunguza ili waweze kutoa taarifa kamili.

Swali kwa Dr Slaa na mwenzake Tunataka kujua nani alimwambia kuwa kuna vitu vimewekwa kwenye vyumba vyao?

Kama ni kweli Haya mambo yanatisha?? Tusubiri tuone kinachofuata

Sina hakika kama hilo swali ni muhimu sana katika hatua za awali za uchunguzi. Ukishajua halafu??
 
Wakulu Heshima Mbele,

Mpaka sasa sijapata Taarifa ambazo zinridhisha kuamini Dr. Slaa aliwekewa vifaa vivyo vya kurekodi sauti.Mambo mawili ambayo nasikitika tumeingia kwa mkumbo kwa mawazo ya kulia tu ni haya.

1.Kwanini tunashikilia Dr. slaa ndiyo amewekewa vifaa hivyo na watu ambao hawatuwafahamu ili khali inawezekana kabisa Dr. Slaaa na CHADEMA wakawa wameweka vifaa hivi kama kujitafutia Umaarufu.Hilo Linawezekana na ni moja ya mbinu za kisiasa ili watu waendelee kuamini kuwa unaweza kuleta Mabadiliko. Tusubiri uchunguzi na iiwezekana Mzee Mwanakijiji na Bongo Radio any mahojiano na wale wahudumu wa ile Hotel.

2. Kuanza kuhisi kuwa ni Masha ndiyo kafanya jambo hili, ama waziri kijana. Huu ni upotoshaji tena kwa hoja kwamba Masha alilipuliwa na Dr. Slaa. Kama tumefika katika siasa za chuki kama alivyosema Mzee Mkapa basi 2010 uchaguzi utakuwa ni wa aina ya ajabu kutokea katika Nchi hii.

Mzee Mwanakijiji na wengine hasa Invisible tuwe waangalifu sana katika Masuala kama haya na tusipende kutoa maamuzi mapema sana. Mpaka sasa niko kwenye msimamo wangu kuwa vile vifaa havijawekwa na mtu yeyote na nitafanya jitihada za kuongea na Mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Dodoma kujua ukweli.!

yeah yeah yeah.. soma habari yangu kwa kina utaona haimhusu Dr. Slaa peke yake! Vyanzo vyangu vya ndani kabisa vya kiusalama vinadokeza kuwa Dr. Slaa amekuwa bugged karibu mara nne (chombo kinarekodi na kujaa na kubadilishwa) na Dr. Tarab karibu mara ya pili. Pia inadokezwa kuwa siyo wao peke yao bali kuna wabunge kadhaa ambao na wenyewe walikuwa kwenye rada hiyo!


Sitoshangaa kikiitishwa kikao cha "Wabunge wa CCM" - Caucus very soon.
 
Wakulu Heshima Mbele,

Mpaka sasa sijapata Taarifa ambazo zinridhisha kuamini Dr. Slaa aliwekewa vifaa vivyo vya kurekodi sauti.Mambo mawili ambayo nasikitika tumeingia kwa mkumbo kwa mawazo ya kulia tu ni haya.

1.Kwanini tunashikilia Dr. slaa ndiyo amewekewa vifaa hivyo na watu ambao hawatuwafahamu ili khali inawezekana kabisa Dr. Slaaa na CHADEMA wakawa wameweka vifaa hivi kama kujitafutia Umaarufu.Hilo Linawezekana na ni moja ya mbinu za kisiasa ili watu waendelee kuamini kuwa unaweza kuleta Mabadiliko. Tusubiri uchunguzi na iiwezekana Mzee Mwanakijiji na Bongo Radio any mahojiano na wale wahudumu wa ile Hotel.

2. Kuanza kuhisi kuwa ni Masha ndiyo kafanya jambo hili, ama waziri kijana. Huu ni upotoshaji tena kwa hoja kwamba Masha alilipuliwa na Dr. Slaa. Kama tumefika katika siasa za chuki kama alivyosema Mzee Mkapa basi 2010 uchaguzi utakuwa ni wa aina ya ajabu kutokea katika Nchi hii.

Mzee Mwanakijiji na wengine hasa Invisible tuwe waangalifu sana katika Masuala kama haya na tusipende kutoa maamuzi mapema sana. Mpaka sasa niko kwenye msimamo wangu kuwa vile vifaa havijawekwa na mtu yeyote na nitafanya jitihada za kuongea na Mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Dodoma kujua ukweli.!

unapenda sana kutoa maagizo! Sijui kwanini!?
 
Kumbe wameekewa viua mbu vya kisasa vijulikanavyo kama VAPE au vifaa vya aina hiyo vinavyotumika kama Vaporizers ,na subirini kwa wataalam yaani hapa Slaa ndio ataumbuka ,saa ingine kujitafutia umaarufu kuna bei na hivyo unaweza ukakukosti na kuna faida na hasara ,hapa kuna mtu atapata hasara.
 
Lazima wanausalama waende kwenye hiyo hoteli ili waweze kuchukua vifaa vyao. Kwa vingine lingekuwa ni swala la kipolisi tu.

Cha kuogepesha ni uwezo wa mafisadi kumdhuru Dr. Slaa. Itabidi tumlilie Mungu amlinde kiongozi wetu shuavu.
 
Kuna taarifa zinatinga mezani kwetu zinadai kuwa kuna mchezo mchafu kafanyiwa mpambanaji Dr. Slaa kwa kuwekewa vinasa sauti chini ya godoro lake na tayari polisi wanaelekea chumbani kwake na watu wa usalama na kuthibitisha tukio hilo.

Jopo la waandishi wameelekea chumbani kwa Dr. Slaa na watatufahamisha kinachoendelea.

Hapo ni Dodoma - Hotel 56.

Ikiwa ni vyombo vya uslama ndo vimemfanyia hivi kwa nia ya kumtegea na kumshitaki kwa kashfa anazoibua bas nathubutu kusemahii ni aibu kubwa sana kwa Serikali ya CCM na Chama Tawala na Vyombo vya Usalama. Na kama wanadhani watakuwa wamemkomoa Dk Slaa basi litawageukia wao maana kuna mambo mengi ya kuyafanyia kazi kwenye nchi yetu kama vile kukamata wauaji wa Albino nk na si kuwasongasonga Wapambanaji. Pia ni kashfa kwa Serikali na vyombo vya uslama kwa kuwa inadhihirisha kuwa Usalama wa Wabunge na watu muhimu uko mashakani sana.

Mugabe alijitahidi kumtegea Askofu na kumchukua picha akifanya ngono na mke wa mtu lakini pamoja na kuchapisha kwenye vyombo vya habari havijamsaidia yeye na Serikali yake kupata nafuu yoyote na kinyume chake upinzani dhidi yake na Serikali ya Zimbabwe unaongezeka kila siku.
 
Hii ni kuwa mapambano bado yanaendelea. Mafisadi wana nguvu kubwa na na Slaa anaungaji mkono mkubwa, kwa hiyo sioni ajabu watu wa TISS wenyewe waliweka vidubwana hivyo kumdokeza Slaa. Nadhani sasa hivi inaonekana ni vigumu kumuua iliyobaki ni kutafuta namna ya kumblackmail.
Uchunguzi utakaofanya na polisi au idara yoyote ya ndani utakuwa danganya toto, itakuwa same story kama uchunguzi wa unga wa chenge. Issue hapa ni nini wamekipata cha kueza kumblackmail Slaa. Au ilikuwa ni attempt zao za kum-bug ili wajue mapema nini kitaenda kwenye kamati inayozungumzia suala la Masha?? Kama wahudumu wa hoteli wanashikiliwa na polisi hiyo ndio sahau kabisa, inawezekana hatutajua kitu na inawezekana wamepata kitu cha kumblackmail asigombee ubunge mwaka kesho.
 
Kumbe wameekewa viua mbu vya kisasa vijulikanavyo kama VAPE au vifaa vya aina hiyo vinavyotumika kama Vaporizers ,na subirini kwa wataalam yaani hapa Slaa ndio ataumbuka ,saa ingine kujitafutia umaarufu kuna bei na hivyo unaweza ukakukosti na kuna faida na hasara ,hapa kuna mtu atapata hasara.


I like this :)
Ama kweli Mwiba umenifurahisha sana, kwani hata simu za mkononi haziwezi kutumika kunasa sauti na picha for that matter. Yale yale ya Mwanahalisi kutumia yahoo.com kupitishia vimeseji vyake.

Mashikolo .. Doho Taabu ... wanasema watani zahu!

ZalendoHalisi
 
Lazima wanausalama waende kwenye hiyo hoteli ili waweze kuchukua vifaa vyao. Kwa vingine lingekuwa ni swala la kipolisi tu.
Cha kuogepesha ni uwezo wa mafisadi kumdhuru Dr. Slaa. Itabidi tumlilie Mungu amlinde kiongozi wetu shuavu.

Bado sijauona ushupavu wa Slaa kisiasa,mafanikio ya kisiasa ni pale mwanasiasa anapofanikiwa kuteka wananchi na kumchagua yeye au Chama chake kwa wingi nasikupapatua kashfa za serikali na mawaziri wake au jumuia zake huko kutakuwa hakuna tofauti na mtu anekosoa chama chake na ndivyo anavyoonekana Slaa na Zitto ni wakosoaji tu na wanashangiliwa na wananchi lakini kura zao hawazipeleki kwa Chama cha akina Slaa.

CUF imefanikiwa kuteka wananchi kule Zanzibar,CUF wana nguvu za Umma kule Zanzibar na zimeonekana katika uchaguzi uliopita wa 2005 kwenye majaribio ya mwanzo kuzijaribu nguvu hizo,hivyo viongozi wamejihakikishia kuwa nguvu zipo na zinatosha kabisa ikiwa wataamua kuzitumia kikamilifu.CUF imetumia matatizo ya kimaendeleo kuikabili Chama cha CCM na selikali yake na si kudungua kashfa au ufisadi mambo ambayo huyasikii kuzungumzwa sana au kuwa ndio bendera ya kuisakama CCM na serikali yake ,pia mikutano ndio iliyowapa nafasi ya kuwateka wananchi.

Hivyo akina Slaa na Zitto wasiwe na mori wa kuanika maovu ya serikali ni lazima kwanza wajipeke kwa wananchi kila wakati nasema kila wakati kwa sababu kamba hukata jiwe si kwa process ya siku moja ila ni ya kila siku ni lazima iwepo mikutano mingi mingi sana na wananchi ,hizi operesheni sangara hazitafua dafu kuwavutia wananchi ikiwa hazifuatiwi na mikutano mikubwa.

Kama nisemavyo kunahitajiwa mikutano ya nguvu kabisa tena ikihutubiwa na wenyewe viongozi wakuu na wakati mwengine iwepo safu kamili ya uongozi ,sio purukushani za kuwasakama mafisadi kwani agenda hizi ni za mpito ,baadae utakuwa huna jipya na ndivyo tuonavyo hivi sasa hawana jipya wanazunguluka palepale huku uchaguzi ukiwa umebakiza mwaka mmoja,nikiwauliza ni nini wamekipata tokea waanze kupigishana makelele na mafisadi jawabu hawana, na CCM nayo imesitukia na kuwabana kwa kuwawekeza katika mzunguluko huo wa mafisadi yaani inachelewesha kila kitu,hivyo kuwaweka akina Slaa katika pause ya mafisadi.

Kama mmegundua mtaona kuwa akina Slaa na Zitto hawaendi mbele wapo katika jambo moja tu la mafisadi ,kuna mambo kama Katiba ,tume ,hayo hawayapi kipaumbele ,mambo ambayo ndio muhimu kuliko yote, Hivyo hawana jipya kwa wananchi.

Ni lazima Serikali iwekwe bize isipate kutulia,inatakiwa hawajamaliza la mafisadi wanahamishiwa kwenye Katiba ,hawajamaliza kwenye Katiba wanahamishiwa kwenye Tume na huku mikutano ya nguvu inaendelea na huku mishen town zinaendelea ,misheni town ndio kama haya ya kutaka kuhujumiwa japo hayana ukweli lakini yananafasi katika kuwa kuwashawishi wananchi kwa kiasi chake.
Lakini kuganda hapohapo kwenye ufisadi itakuwa ngumu sana kufikia kwenye uchaguzi mkuu na dau hilo na yako mambo mengi ya kimaendeleo ambayo yanaweza kwa urahisi kabisa kubadilisha wananchi kiitikadi na kuwa na msimamo wa uyakinifu kuwa CCM haijawaletea maendeleo ya kweli.
 
Last edited:
mtaambiwa kuwa "vyombo hivyo si vya kunasa sauti bali ni kwa ajili ya kuhakikisha joto la magodoro linabakia kuwa constant"! Atakayesema hivyo atakuwa Waziri Mkuu tena kwa uchungu wote na machozi yakimlenga "Dr. Slaa ni mtu muhimu sana, tumechoshwa kuona anatishiwa tishiwa hivyo kwa kutumia mbinu za kisasa tumemuongezea ulinzi na usalama. Sasa kama Watanzania wanafikiri sisi kumlinda Dr. Slaa ni kosa kubwa kulinganisha na yeye kuja kurudhika fine! Mungu atanisamehe na ninaomba mtusamehe"... atasema Waziri Mkuu..

Wabunge watasimama na kumpigia makofi. Vyombo vya habari vitaandika "Waziri Mkuu azikoga nyoyo za wabunge"

Nadhani hii ni kashfa ambayo Wapinzani wasikubali Serikali na vyombo vyake vya usalama washughulikie suala hili. CAHEDAM na Wapnzani waiombe Scotland Yard waje kuvichunguza hivyo vifaa na nani wanahusika navyo na kwa kuanzia wasiruhusu vitunzwe na vyombo ya Serikali ni heri wakae navyo wenyewe (Dr Slaa na CHADEMA) hadi hapo hao Scotland Yard watakapofika.

Dk. Slaaa usikubali chochote hapo MAfisadi wamejiingize wenye kwenye kumi na nane yako. Waite Makachero wa Scotland Yard waje wachunguze suala hilo maana huenda uhai wako ukawa umeshapunguzwa kwa miaka kadhaa maana hatujie effects za vifaa hivyo.
 
Mkuu FMES vijana hawawezi kuwekwa kando kwasababu tu ya kina Masha...Kama that was the case basi based on where our country is rightnow, then tukitumia same reasoning tunaweza kusema wazee hawafai kwani ndio wametufikisha hapa...

- Vijana tumeharibu period, hiyo dhana ya vijana ni mufilisi sasa hivi mkuu wangu, wazee wameshika maisha yetu yote, hii ilikuwa ni mara ya kwanza kujaribishwa kuaniza rais mpaka chini, sisi vijana hatuna solution ya hili taifa na matatizo yake, sasa ni kuwaachia kina Mkuchika.

Naona maybe unasema hivyo ili vijana wasimkabe koo sana lau kwasababu wanaweza kufikiri ni sawa na kukata tawi ulokalia.

- Kumkaba koo kiongozi ni lazima uwe na ukweli mkuu wangu, tulizonazo ni habari nyingi za kusadikika maana kuna theory nyingi sana, mimi ninasema hivi Lau jina lameharibika sana hawezi kuwa na authority ya kuwa waziri baada ya haya yote, lakini ya kumkaba sijakukataza mkuu.
 
FDR ukweli uliosema hautaeleweka leo, lakini nakuhakikishia kuwa katika muda mfupi ujao utaeleweka.

Marsha pamoja na matatizo yake, kwenye hii issue ya IDs anatetea ukweli na kama waziri mhusika ni yeye mwenye dhamana hatimaye kuwajibika kwa lolote lile litakalotokea wala siyo Luhanjo. Tena la ajabu nu kuwa katibu mkuu wake ana amua makusudi kumwandikia CS kisirisiri bila ya kumhusisha waziri wake, na issue ambayo anailalamikia ni kwamba waziri hakukubaliani na double standards zilizotumika kuengua wazabuni wengine wakati huo huo kuna wengine waliokuwa na short-commings more serious waliopewa nafasi za kuzirekebisha. Anachotetea Marsha ni double-standards zilizotumiwa!

Waziri Marsha baada ya kutokubaliana na katibu mkuu wake (wa wakati huo) akatoa wao kuwa PPRA iliangalie hilo swala kwa undani na watoe uamuzi kama hiyo evaluation process ilikuwa fair kwa wazabuni wote. PPRA ndicho chombo cha juu kuliko vyote kisheria kwenye mambo ya zabuni. Katibu mkuu wake akalikwepa hilo na kumwandikia Luhanjo waraka ambao ulimfanya Marsha naye amwandikie bosi wake, waziri mkuu.

Kwenye hili swala FDR Jr. umegusa raw-nerve; hebu kumbuka ni nani alianzisha mchakato huu - Mungai! Mungai + Luhanjo = 1; Tena la kuchekesha ni kuwa huyo katibu mkuu aliyemwandikia Luhanjo barua sasa hivi hayupo tena wizarani hapo, ila bado ana watu wake ambao waliinyofoa barua hiyo na kumpa Slaa. Hili dili lilisukwa na Mungai na agents wake ambao bado wapo wizarani na hata wengine wao wapo kwenye idara yenyewe ya vitambulisho ya Mr. Dickson Mwaimu (mlarushwa ile mbaya) pamoja na IT expert wake aliyetimuliwa/demoted Immigration akapelekwa Mbeya baada ya kupokea rushwa kwenye tenda ya passport - baadaye akaenda Uingereza - Oxford - akasomea MSc na aliporudi Mungai akamhamishia kwenye hiyo agency. Kwenye hili wanaoomba Marsha lizwe wako kibao; payroll hiyo ni ndefu ingawa wengine wataambulia bia tu!



Marsha alichofanya cha kuuliza na kutoa option ya kuhusisha PPRA ni sawa. Motive zake za kufanya hilo, who knows ila la uhakika nitakalo lisema milele ni kuwa huu mradi ulisha sukwa mapema mno na walaji walishajiweka tayari na pesa wanazo, Marsha kachafua hali ya hewa. Kuna katibu mkuu mstaafu aliyeteuliwa kuwa consultant kwenye huo mradi hadi leo wamemweka kando kwa vile haeleweki eleweki!

La kuchekesha ni hilo kampuni la Sagem (nime-Google) mbona limepata matenda ya vitambulisho mengi tu Africa (over 15 projects) na hata huko Nigeria walikohonga eventual walipewa kazi. Hata huku majuu FBI, FBI certifies Sagem Sécurité's new MorphoTopTM biometric sensor - find BIOMETRICS , Secret Service, Interpol na idara nyingi nyeti ulimwenguni wanawatumia. Labda inawezekana kuwa wanazaipata kazi zote kwa kuhonga! Or they are just good technically kwa hivyo inawezekana wazabuni wenzao kwenye zabuni la vitambulisho bongo waliwashtukia na kuamua kuwaengua kimafya! Kama ni hivyo basi wamezidiwa kete kijanja na wangojee kwingine.

La mwisho ni kwamba kuna issue ya kutumia model ya Malaysia katika utoaji wa vitambulisho vyetu ambalo linzaungumziwa mara nyingi; hivi hawa wa Malaysia wa utaalamu kweli au ni madalali wa Sagem; Nimekumbana na article hii nikabaki mdomo wazi, inawezekana hao hao Sagem tukawa tunawakubali through the back door! Just a thought. Soma hili; ThirdFactor | Sagem Sécurité selected by Malaysia for new biometric ID system


ZalendoHalisi


- Mkuu wangu Mushi, tizama hii theory nayo unaionaje katika kumkaba jamaa? Ndio maana nimekuambia kuna thoery nyingi sana lakini tunasema jina limechafuka sana aondoke tu kwa amani na mapema.
 
mbinu za kizamani hizi, hazita zaa matunda kwa wakati huu.. Ni kikundi kidogo tu katika ccm ndicho kinacho haribu usalama wa nchi yetu.Huyu Masha kawekwa hapo na RA na swahiba wake mkuu EL kwa makusudi makuu ya kula rushwa ya vitmbulisho vya uraia.Wameona mpendwa wetu Dr Slaa kakomaa nao,wameanza kumuhujumu!Sauti ya wengi itasikika si muda mrefu.
 
Mpaka vifaa viwekwe chumbani kwa mtu, ina maana lazima mlango ulifunguliwa. Na wenye funguo ni wamiliki wa Hoteli, sasa kitu cha kwanza viongozi na wahudumu wa hiyo hoteli wanatakiwa kuisaidia polisi. Lakini kama ni watu wa usalama/serikali ndio walioweka hivyo vifaa, hata hao viongozi na wahudumu wa hiyo hoteli hawatatoa ushahidi utakaomsaidia Dk. Slaa.

Lakini pia kama tuna uchunguzi huru, hivyo vifaa vingeweza onesha alama za vidole (finger prints), ila huenda waliovitoa walivishika bila kutumia gloves.

Kwa kuwa siasa nao ni mchezo wa kuviziana, na kwakuwa Dk. Slaa alisema alitumiwa habari, na alipofika chumbani kwake aliomba na majirani zake waangalie vyumba vyao. Ikakutwa tena kwa Mbunge wa CUF kuna hicho kifaa. Yawezekana pia vifaa wameviweka wenyewe ili kuonesha wanafuatiliwa na wapate huruma toka kwa wananchi. Nakubaliana na Dk. Slaa na wapinzani kwa kazi wanayoifanya kwa Taifa letu, lakini bado siasa yaweza tumika vibaya.

Ingekuwa vyombo vyetu vya uchunguzi viko huru, tungejua mbaya ama mkweli nani?.

Mkubwa umechambua vizuri sana...nimekukubali mfumwa!
 
Back
Top Bottom