Wabunge Dr. Slaa na Dr. Tarab wafanyiwa umafia!

Kama wameweza kuingia na kuweka vifaa hivyo je tuna uhakika gani kuwa Afya Dr. Slaa haijadhuriwa?. Ili Serikali ijitoe katika hili, Bunge Limgharamie Dr. Slaa na mwenzake kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya zao katika nchi ambazo wao wenyewe watazichagua kwa kuona kama wameisha wekewa "Slowly killing poison", vinginevyo serikali haitakwepa lawama yoyote ile endapo Dr. Slaa na mwenzake watapoteza maisha hata kwa malaria.

Watu wa usalama watakachofanya hapo ni kuja kuvichukua vitu na kuvirudisha store na kutoa taarifa kuwa ni toys etc. Hii ni kashfa kubwa kwa bunge na serikali yetu kwa kutotoa ulinzi wa kutosha kwa wabunge wetu. Nashauri serikali iwekee kipaumbele suala la hawa jamaa kuangaliwa afya zao nje ya nchi kama nilivyosema mwanzo ili kujisafisha na hii scam.
 
mtaambiwa kuwa "vyombo hivyo si vya kunasa sauti bali ni kwa ajili ya kuhakikisha joto la magodoro linabakia kuwa constant"! Atakayesema hivyo atakuwa Waziri Mkuu tena kwa uchungu wote na machozi yakimlenga "Dr. Slaa ni mtu muhimu sana, tumechoshwa kuona anatishiwa tishiwa hivyo kwa kutumia mbinu za kisasa tumemuongezea ulinzi na usalama. Sasa kama Watanzania wanafikiri sisi kumlinda Dr. Slaa ni kosa kubwa kulinganisha na yeye kuja kurudhika fine! Mungu atanisamehe na ninaomba mtusamehe"... atasema Waziri Mkuu..

Wabunge watasimama na kumpigia makofi. Vyombo vya habari vitaandika "Waziri Mkuu azikoga nyoyo za wabunge"

Mkulu Mwanakijiji, kama vile unatazama fikra zao, kwani nina uhakika maelezo yao hayatapishana sana na unachokisema. Tena bila aibu nakumbuka unga uliomwagwa bungeni na majibu yake yalikuwa na mwelekeo huohuo. Anyway, wananchi tukaze buti kitaeleweka tuu. Kuna jamaa kanirushia kijarida cha cheche nimesoma ingependezasana ukikiliki na hapa jamvini tuwe tunapata access nacho pia.
 
Hii kitu binafsi nilishaihisi.

Nimeongea na mtu wa karibu na Dr. Slaa kanihakikishia kuwa kitu hicho kimetokea na akaniambia kwa sasa Slaa hatoweza kuongea kwakuwa ni kitu ambacho hakutarajia angeweza kufanyiwa. Naambiwa alikuwa anapaamini sana chumbani kwake. Katibu wa Bunge yuko njiani kuelekea huko ili polisi na wana usalama wetu watekeleze wajibu wao.

This' Bongo!

Hao wanausalama wanaokwenda kuangalia na kufanya uchunguzi ndiyo wameviweka. Sasa sioni ni kwa nini waende kuchunguza huku tayari wakiwa wameshaumbuka. Mchezo baaaaado kabisa haujaanza, hilo ni jaramba tu la SISIEMU, wee subiri pale uchaguzi utakapokaribia mtaona makubwa zaidi ya hayo. Walishazoea Watanzania ni watu wa ku-react mara moja kisha wanasahau au kupuuzia.
 
Slaa hapa alifanya haraka. Alitakiwa kwenda navyo na kuviacha kwa Spika Sitta au PM Pinda. Hapo wangelitoana macho CCM wenyewe kwa wenyewe. Zima moto wanasema "fighting fire with fire". Duu, naona tunaelekea kweli kwenye siasa za Urusi kama Masha alivyosema kummaliza Mengi. Ila tu tofauti ni kuwa Putin anafanya juu chini kulinda maslahi ya Warusi na mali zao na sisi tunafanya kinyume. Ahhh, halafu mtu anasema Chama chetu CCM..... Ni kama Tyson, sasa wanauma na kunyofoa masikio.
 
Mimi nadhani pamoja na kuwa makundi yote yaliyotajwa wapo wasiompenda Dr Slaa, lakini bado ukweli unabaki kuwa masilahi ya hayo makundi hayako sana mashakani ukilinganisha na kundi kubwa la wasiopenda mabadiliko, na ambao bahati mbaya wengi wao wamo ndani ya mfumo. Hivyo waacheni watu wacheu, ukweli ukitoka, nao watapata nafasi ya kupima kulingana na yale waliyokuwa wanayahisi.

Lakini kubwa zaidi hapa, ni kupeana habari, na kumbuka kuwa habari zinasema kuwa Dr Slaa alipata habari za kuwepo vifaa hivyo kabla hata ya kufika chumbani, hivyo hawa hawa unaotaka wasiseme sasa, wapo wenye habari za uhakika na sio sahihi kuwasitisha wasitufikishie hapa jamvini! La msingi wenye taarifa za uhakika watumwagie hapa kama unavyotumwagia.

- Mkuu wangu huwezi toa hukumu bila facts, acha hisia ingawa ni maneno mazuri sana lakini bado ni hisia ngoja tupate ukweli, au dataz maana ndio sifa yetu JF, otherwise tupo pamoja sana.
 
Mbona wanatumia nguvu sana kunyamazisha sauti za wanyonge ? Kwa nini wasiende kutegesha mitego yao hiyo kwa waganga wanaoagiza viungo vya albino ?Tena wangewapata vizuri kweli.
Ni ajabu sana inapokuja kutetea WAKUBWA ndiyo tunaona kuwa kweli vyombo vyetu vya usalama vinafanya kazi. Sasa namuona Pinda ni mnafiki mkubwa sana. Eti mkiwashika waueni ! Ulipoenda kuwatembelea victims wa mauaji hayo kwa nini usibebe vinasa sauti hivyo kwenye ndege yako ukawape polisi wa huko ?
Inauma sana.
Nchi hii kweli si yetu tena, ni yao.
 
Mkulu unapiga Ikulu kabisa huogopi kitu hahahah umenifurahisha .....kikao cha bunge saa nane hahahahah haya mtu wangu tupo pamoja kwa hili. Ila waziri kijana ana hali mbaya kama ni mgonjwa anapumulia mashine
Masa

Mkuu tupo pamoja hapo, waziri ameharibu na inasikitisha sana hasa vijana wanapoharibu maaana wanaziba nafasi za vijana wengine,

- kati ya Masha na Charles Kajege, binafsi nimekua very disappointed, hawa niliwaaaminia sana, na ninakumbuka one time kuwaambia wote wawili kwamba vijana wengi wanawatumainia sana katika kuweka msingi kwa vijana wengine, lakini kweli mbuzi wa masikini hazai, maana huko mbele itakwua vigumu sana vijana kupewa madaraka makubwa.

Mkuu SHY, check PM.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu FMES vijana hawawezi kuwekwa kando kwasababu tu ya kina Masha...Kama that was the case basi based on where our country is rightnow, then tukitumia same reasoning tunaweza kusema wazee hawafai kwani ndio wametufikisha hapa...Naona maybe unasema hivyo ili vijana wasimkabe koo sana lau kwasababu wanaweza kufikiri ni sawa na kukata tawi ulokalia.

Anyways nilitaka pia nigusie posti yako moja iliyopita kwa kusema kuwa tusikimbilie ku judge kwasababu Dr Slaa anaweza kuwa na maadui nje ya ccm kwa maana hata ndani ya upinzani na hata chadema...Mimi mawazo yangu ni kwamba mwizi na mnunuaji wa mali ya wizi wote wana hatia...Kwani hata hao unaowaita wapinzani ambao hawampendi Slaa hizo habari watapeleka wapi zaidi ya ccm? Bottom line zitaenda ccm kwani ndiko kwenye dau kubwa la kuweza kununua data zilizopatikana through bugging...Nilitegemea mara baada ya maongezi ya marehemu Wangwe na Rostam kunaswa huko Kempiski basi na kina Slaa wange debugg maskani zao na kuwa extra carefull.

Slaa ni stable na sidhani kama ni mtu wa kufanya makosa madogo madogo...Ni wajibu wa Mbowe na Zitto kumpa ushirikiano wa kutosha maana saa nyingine kuna mambo yanaoitwa UTAIFA ambayo kimwelekeo wanapishana licha ya kwamba hawataki kuweka wazi...Lakini to what extent one is gonna be against each other in this political game is beyonf imagination...We cannot just have a clear and outright intelligence because ofcourse the intelligence is shared for the sake of the party.

I wish you guys well but please be carefull wanamapinduzi,na pia keep your friends closer,keep your enemy closer...If you don't know what they are doing then you are doomed to failure...Bob alisema pia your worst enemy could be your best friends and you best friend your worst enemy.
CHADEMA mjitahidi tunawategemea katika kuleta chachu ya maendeleo. Nakubaliana pia na maoni ya Kwame Nkrumah na Hofstede.
Ni hayo tu kwa sasa.
 
wanasihasa hao wanacheza pilitiki hakuna kitu hapo
Dr.tarab i know the dude personally was former biochemistry lecturer at muchs sasa leo sijui mbunge wa wapi manake sijamsikia popote akiongea chochote eti nae aje kuwa target ya mafisadi?
 
Duh!!! Pamoja na ufisadi sasa CCM imeamua kujiongezea sifa nyingine ya umafioso!!!! Inaelekea wanamuogopa sana Dr. Slaa kwa sababu anawaendesha puta kila kukicha sasa wamempania kumrekodi maongezi yake ili wammalize kisiasa!!!

Inabidi awe 007 kila anaposafiri awe na vifaa vinavyorekodi movements zote zinazofanywa chumbani kwake ili kuwanasa wahusika na hatimaye kuwapandisha kizimbani. Si ajabu CCM wameuanza mchezo huu kwa Dr siku nyingi tu na labda kuna wengine pia wanaofanyiwa uchafu huu.
 
Duh!!! Pamoja na ufisadi sasa CCM imeamua kujiongezea sifa nyingine ya umafioso!!!! Inaelekea wanamuogopa sana Dr. Slaa kwa sababu anawaendesha puta kila kukicha sasa wamempania kumrekodi maongezi yake ili wammalize kisiasa!!!

Inabidi awe 007 kila anaposafiri awe na vifaa vinavyorekodi movements zote zinazofanywa chumbani kwake ili kuwanasa wahusika na hatimaye kuwapandisha kizimbani. Si ajabu CCM wameuanza mchezo huu kwa Dr siku nyingi tu na labda kuna wengine pia wanaofanyiwa uchafu huu.

Bubu,
Umafioso wa CCM umeanza zamani. Hivi sasa unashamiri!
 
Duh! hii kali,
Yawezekana hii imeanza siku nyingi na wamekwisha kukusanya data fulani juu ya maongezi ya Dr. Slaa. Tukiweka kumbukumbu sahihi kuelekea uchaguzi wa 2010 tunaweza kupata mengi juu ya tabia hii ikiwa ni pamoja na waliyoweza ku-record si kwa Dr Slaa tu, hata kwa wengine.
 
mtaambiwa kuwa "vyombo hivyo si vya kunasa sauti bali ni kwa ajili ya kuhakikisha joto la magodoro linabakia kuwa constant"! Atakayesema hivyo atakuwa Waziri Mkuu tena kwa uchungu wote na machozi yakimlenga "Dr. Slaa ni mtu muhimu sana, tumechoshwa kuona anatishiwa tishiwa hivyo kwa kutumia mbinu za kisasa tumemuongezea ulinzi na usalama. Sasa kama Watanzania wanafikiri sisi kumlinda Dr. Slaa ni kosa kubwa kulinganisha na yeye kuja kurudhika fine! Mungu atanisamehe na ninaomba mtusamehe"... atasema Waziri Mkuu..

Wabunge watasimama na kumpigia makofi. Vyombo vya habari vitaandika "Waziri Mkuu azikoga nyoyo za wabunge"

Waziri mkuu anatokea wapi tena mkuu???
 
Wakuu Invisible na Mwanakijiji nina uhakika ninyi mna uwezo wa kuwasiliana na Dk.Slaa,kama vp fanyeni muwasiliane naye ili tupate uhakika wa taarifa hii ambayo mpaka dakika hii inaonekana kuwa ni tetesi hivyo kuwa vigumu kwa baadhi yetu kuchangia...Maana kilichopo ni kwamba baadhi ya watu wanaichukulia hii kama taarifa iliyothibitshwa na kuanza kuelekeza lawama sehemu mbalimbali kuwa zinahusika na tukio hili wengine mara CCM,mara wana Usalama,mara wapinzani wenzie,mara watuhumiwa wa ufisadi nk...So ni vema ifanyike jitihada ya kuwasiliana na Dk.Slaa atuthibitishie hili na atueleze anadhani ni kwa nini watu hawa wamemfanyia hivi(kama ni kweli tukio hili limetokea) hapo ndo tutapata mwanga wa nini kimetokea na tutapata wigo wa kuchangia kwa upana zaidi...
 
Mkuu FMES,

vipi zile Tshs. bn 2/= ambazo waziri kijana ndo anadaiwa kuzitia ndani kutoka Sagem?Naambiwa watu mpaka wana details za bank cheque an a/c no. za hiyo transaction.

By the way aligoma kuwagawia na kuwakatia "wenzake" nini?
 
Wakulu Heshima Mbele,

Mpaka sasa sijapata Taarifa ambazo zinridhisha kuamini Dr. Slaa aliwekewa vifaa vivyo vya kurekodi sauti.Mambo mawili ambayo nasikitika tumeingia kwa mkumbo kwa mawazo ya kulia tu ni haya.

1.Kwanini tunashikilia Dr. slaa ndiyo amewekewa vifaa hivyo na watu ambao hawatuwafahamu ili khali inawezekana kabisa Dr. Slaaa na CHADEMA wakawa wameweka vifaa hivi kama kujitafutia Umaarufu.Hilo Linawezekana na ni moja ya mbinu za kisiasa ili watu waendelee kuamini kuwa unaweza kuleta Mabadiliko. Tusubiri uchunguzi na iiwezekana Mzee Mwanakijiji na Bongo Radio any mahojiano na wale wahudumu wa ile Hotel.

2. Kuanza kuhisi kuwa ni Masha ndiyo kafanya jambo hili, ama waziri kijana. Huu ni upotoshaji tena kwa hoja kwamba Masha alilipuliwa na Dr. Slaa. Kama tumefika katika siasa za chuki kama alivyosema Mzee Mkapa basi 2010 uchaguzi utakuwa ni wa aina ya ajabu kutokea katika Nchi hii.

Mzee Mwanakijiji na wengine hasa Invisible tuwe waangalifu sana katika Masuala kama haya na tusipende kutoa maamuzi mapema sana. Mpaka sasa niko kwenye msimamo wangu kuwa vile vifaa havijawekwa na mtu yeyote na nitafanya jitihada za kuongea na Mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Dodoma kujua ukweli.!
 
Ebu tujiulize what was the outcome of investigation ya Chenge kumwaga unga wa miujiza bungeni? Sioni tofauti yoyote kati ya kuwaita wanausalama kuja chunguza ki-device hiki leo hii na ile story ya mwaka jana ya kumpatia tenda Mkemia mkuu wa Serikali achunguze unga uliomwagwa na Chenge bungeni. Hivi ni viini macho tu..... Tunapotezeana mida tu hapa, hamna chochote cha maana kitakachoelezewa baadaye. ##@8^0>,&^#
 
Habari hii inasikitishwa na inapaswa kulaaninwa na kila mtanzania mpenda maendeleo.

Aluta continua!
 
Wakuu

Ni kweli nimesikia kwenye Radio kwamba vitu kama Flash Disk vimekutwa kwa Dr Slaa Na Dr Taarab. Polisi wamesema wanachunguza ili waweze kutoa taarifa kamili.

Swali kwa Dr Slaa na mwenzake Tunataka kujua nani alimwambia kuwa kuna vitu vimewekwa kwenye vyumba vyao?

Kama ni kweli Haya mambo yanatisha?? Tusubiri tuone kinachofuata
 
Back
Top Bottom