Oya sio poa ,Ujue ukimsoma Daudi na Sauli, mwenye madhambi mengi ni Daudi, Sauli kosa lake ilikuwa kwenda kwa mganga yule wa endori
Daudi alikuwa muhuni ,mtu wa totozi, halafu anajadiliana na Mungu kama rafiki yake ,alimfanya Mungu rafiki yake ,
Ukimsoma sana Utagundua kilichomfanya awe rafiki wa Mungu ,hakuwa mnafiki ,
Akikosea akiambiwa hatafuti visingizio ndicho kilichofanya apendwe sana ,
Alikuwa mwepesi sana wa kutubu
Alikuwa na vipaji vingi ,jamaa alizijua natural law vizuri sana ,alijua ili Mungu akukubali ufanye nini
Alikuwa jasusi ,aliwahi kukaa kwa wafilist kwa muda mrefu akiwapeleleza na hawakimjua
Kuhusu kutunga nyimbo alijua sana,kupiga ala za muziki alikuwa fundi
Napenda sehemu moja ,alipozini na mke wa Uria ,na kuua ,kafatwa na nabii Nathani, sasa Nathani kaanzia mbali kumwambia maana ilikuwa hatari sana kumwambia directly
Halafu Daudi anapojua ni yeye anasemwa wala habishi ,anakubali fasta ,anatubu anaandika Zaburi ya 51 ,
Sasa niliposhangaa jamaa alikuwa rafiki wa Mungu, wanajadili na Mungu adhabu ya kupewa
Mungu anampa option 3 ,jamaa anachagua kupigwa na Mungu anakwambia Mungu ni mwenye huruma ,atakuchapa ila atakuonea huruma tu 🤣
Kabla ya kufa anampa Suleiman list ya maadui zake ,anamwambia Suleiman awamalize
Kuna tukio lake moja nalipenda sana ,napenda sana watawala wa Leo wajifunze kwa Daudi aisee,
Kama unataka kuwa kiongoz Bora msome Daudi ,
Siku moja ndugu wa Sauli walikuwa wanamtukana sana Daudi akiwa na majemedari wake Wana wa Seruya ambao ni watoto wa dada yake
Wale majemedari( Wana wa Seruya) wakamwambia Daudi inakuwaje huyu mbwa anakutukana hivi, turuhusu tukakuletee vichwa vyao .
Daudi akawajibu " waache wanitukane maana huenda Mungu amewaruhusu kwa kufanya hivo Mungu atanilipia MEMA"
Kuna funzo kubwa sana hapo
Daudi mwana wa Yese Mbethelehem anabaki moja ya watu ambao Dunia iliwapata
View attachment 3536763