Wafuasi wa Muhamad wanakwambia Zabur alipewa Daudi. Huwa nashangaa sana nikisikia hizo story zao.
Pia kwao kuimba ni Haram lakini hawajui Mfalme Daudi alikuwa fundi wa muziki.
Zaidi wanadai Daidi ni Nabii...hivi Daudi siyo Mfalme tu?
Daudi huyu jamaa alikuwa hatari sana,alikuwa mbabe sana wa vita ,hajawahi kushindwa vita ,namfananisha na Netenyau ubishi wake ,anapenda sana vita
Jina Daudi Lina maana nyingine tofauti na ile ya kihebrania ,anaitwa pia man of War
Huyu jamaa alipendwa sana na Mungu sababu moja tu, hakuwa mnafiki ,
Mungu kampa Hadi mtaa huko mbinguni, ukisikia Sayuni ,basi huo ni mtaa wa Daudi huko mbinguni
Alikuwa nabii pia mfalme
Biblia inaonyesha Daudi kama Mfalme wa Israeli, lakini pia kama nabii kwa sababu Mungu alinena naye moja kwa moja na kupitia yeye akatoa unabii.
Yesu alimuita pia alimuita Daudi nabii
Yesu alisema
“Daudi mwenyewe alisema kwa Roho Mtakatifu…” (Marko 12:36)
Hii inaonyesha Daudi alinena kwa uongozi wa Roho wa Mungu, kitu kinachoonesha ni karama ya unabii.
Mitume pia walimwita Daudi nabii Petro alisema
“Ndugu, lazima itimie andiko ambalo Roho Mtakatifu alisema kabla kwa kinywa cha Daudi…” Matendo 1:16
“Kwa kuwa alikuwa nabii…” Matendo 2:30
Halafu Zaburi nyingi ni unabii
Daudi aliandika Zaburi nyingi ambazo ni unabii kuhusu Yesu ,kuhusu Israel,kuhusu matukio mengi sana , mfano
Zaburi 22 ni unabii wa mateso ya Yesu
Zaburi 110 ni unabii wa Masihi kukaa mkono wa kuume wa Mungu
Huyu jamaa naweza kumuelezea asubuhi mpaka jioni ,