Waandishi wa Habari wa Tanzania jitahidini mlizingatie sana hili la TCU kuhusu PhD za Taaluma na zile za Heshima

Cognizant

JF-Expert Member
Aug 13, 2022
491
1,056
Kwa mujibu wa TCU ni kwamba Mtu yoyote ( hata awe ni nani Tanzania ) akiwa ametunukiwa PhD ya Heshima akiwa anatajwa ni lazima Kianze Cheo chake kisha Jina na Tuzo hiyo ya Heshima.

Kwa mfano Cognizant nikiwa labda ni Mkuu wa Wilaya na nimezawadiwa PhD ya Heshima na Chuo Kikuu chochote Waandishi wa Habari wote kwa Sheria za TCU wanatakiwa Wanitambulishe kama Mkuu wa Wilaya Cognizant a.k.a Adorable Angel Daktari wa Falsafa ya Heshima kisha ndipo Waendelee na Maelezo yao mengine.

Kwa mujibu wa TCU ni kwamba anayetakiwa kuanza Kutambulishwa kwa Hadhi ya Daktari wa Falsafa ni yule tu aliyekaa Darasani na kupata Taaluma na Kufaulu vyema Masomo yake hasa Tafiti zake mbalimbali.
 
Back
Top Bottom