Waandishi wa Habari Simiyu wamaliza tofauti zao na DC Simalenga

KwetuKwanza

Member
Mar 13, 2023
34
82
Kikao cha maridhiano kimefanyika na kumalizika kwa mafanikio Machi 9, 2024, kati ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Simiyu na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga.

Kikao kilifanyika kwa muda wa Saa nne na zaidi hivi, kikisimamiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, UTPC na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mr. Nawanda.

Kwa mujibu wa mmoja wa waandishi wa Habari ambaye nimezungumza naye, anasema maridhiano yalifikiwa lakini kila upande kwa ulipewa nafasi ya kutoa ya moyoni.

"....Sisi waandishi tulifunguka kweli kweli, kwanza tuliambiwa tufunguke bila ya kuogoa, tuseme nini kilifanya tufike uhamuzi ule wa kutangaza kutofanya kazi na huyo DC, waandishi walifunguka na kueleza mambo yote....

"...Kisha naye Mkuu wa Wilaya alipewa nafasi, alitumia muda kama wa nusu saa kutoa maelezo, na mwisho akasema yeye hana tatizo lolote na waandishi wa habari na angelipenda kuendelea kufanya nao kazi......"

Ingawa Waandishi wa Habari walionekana kutaka kugoma tena, na baadaye majadiliano yakafanyika na mwisho mambo yakaisha.
WhatsApp Image 2024-03-10 at 15.15.46_0aaa118d.jpg

WhatsApp Image 2024-03-10 at 15.16.56_e1590ae9.jpg
Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali iliwakilishwa na Msaidizi wake anaitwa Bi. Zamaradi, ndipo akawaomba Waandishi wa Habari kuondoa hizo tofauti na kurudi kufanya kazi kama kawaida na Mkuu wa Wilaya.

Zamaradi alionekana kugundua tatizo lilipo kwa upande wa Waandishi wa Habari pamoja na Mkuu huyo wa Wilaya na kutaka kusahau mambo yote kasha wote warudi kazi kwani wananchi wanataka haki yao ya kupata habari.

Naye Rais wa UTPC, Deo ambaye naye alikuwepo, aliwaomba Waandishi wa Habari kusamehe yote yaliyopita kwani kama ujumbe waliotaka kufikisha, ulifika vyema kwa wahusika na ni matumaini yao hakuna jambo ambalo litajirudia tena.

Nsokolo alieleza hakuna haja ya kuendelea kugombania fito, na badala yake warudi kufanya kazi kwa pamoja na kila upande kuheshimu mwingine ili kazi ya umma iweze kufanyika vyema.

Mkuu wa Mkoa akahitimisha kwa kuwaomba Waandishi wa Habari kuondoa mgomo huo, na kufanya kazi kwa pamoja huku akisisitiza ushirikiano, upendo na kujaliana.

Aidha, Klabu ya Waandishi wa Habari imetoa tamko likieleza wamemaliza tofauti zao, tamko limetolewa na Mwenyekiti wa Press Club yao, Frank Kasamwa.

Taarifa hiyo imesema hivi, nanukuu... “ Uongozi wa SMPC unatangaza kuwa kufuatia kikao hicho tumekubaliana kuondoa tofauti zilizokuwepo baina yetu na Mkuu wa Wilaya, tumekubaliana kushirikiana na kwamba kila upande utafanya kazi kwa kuzingatia mipaka ya kazi yake bila ya kuathiri upande mwingine kwa manufaa ya umma,”

Hivyo ni dhairi waandishi wa habari wamemaliza tofauti zao lakini ujumbe umefiika kwa wahusika.

WhatsApp Image 2024-03-10 at 15.16.55_57a63dd4.jpg

WhatsApp Image 2024-03-10 at 15.16.57_40a6856c.jpg

WhatsApp Image 2024-03-10 at 15.16.56_eaa0dc73.jpg
 
Back
Top Bottom